Mawaziri acheni kumsifia Mama Samia kupitiliza, chapeni kazi!

Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,703
3,304
Leo huko Misungwi kulikuwa na tukio la kitaifa mbashara karibu vyombo vyote. Inasikitisha sana mnatumia muda mwingi kumpamba Rais katika hotuba zenu.

Kazi tunajua mnafanya vizuri lakini mnaboa sana kumpamba mkubwa hadi mnatoka nje ya tukio. Aweso punguza mbwembwe na kuinua misuli na mifano ya kujirudiarudia mbele ya Rais. Sikiliza hotuba za Mabalozi na wadau, Waziri mwenye dhamana andaa neno zito kijibu hotuba zao kuunga mkono mchango wao kwa nchi.

Leo huku Misungwi mmetia aibu kutokuonesha kuunga mkono hata neno la ASANTE mmeshindwa. Hotuba zenu zimejaa mbwembwe na kumsifia Mama too much.

Punguzeni mazulia mekundu huko kwenye miradi hadi kwenye mitambo, ni matumizi mabaya ya fedha. Aliyeandaliwa mwishowe akawa anakanyaga kusiko na zulia.

Gharama za mazulia hayo huko porini mngekuwa mmenunua pipe ziende kwa vitongoji mama azindue watu wakiwa wanachota maji ingekuwa heshima sana. Yaani mnapewa msaada halafu mnanunua zulia kuweka kwenye mradi. Nini heshima ya zulia jekundu?

Tunakupenda Aweso, unachapa kazi, ila acha mbwembwe kwa bosi wake Tulia na Balozi wa Ufaranza na mwakilishi wake hamjamtendea haki.

Muda wa kampeni bado, fanyeni kazi bila kumsifia sana aliyeko juu, kazi yako itamsifu kupitia wewe.
 
Ulianza vizuri suala la kusifia kupitiliza.
Wengi hao ni watu walizoea sana au kubebwa na Jiwe... sasa wanatumia kila nafasi in public kujikomba kwa Mama.

Ila kuhusu mazulia hayo ni ya Ikulu sio ya mradi. Logistic team ni sehemu ya misafara ya wakubwa nje ya Ikulu.
Sijui kama jana uliona pia kiti, kale kameza kadogo na podium vinavishwa special cover na kuwahishwa BOT kwa ajili ya next tukio baada ya uzinduzi wa kiwanda cha kuchakatua dhahabu
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom