Mawaziri 5 walioboronga zaidi mwaka 2016

Quarteman

Senior Member
Jul 31, 2016
104
250
Katika kumalizia mwaka huu, tunahitimisha kwa kufanya tathmini ya mambo mbalimbali yaliyofanyika ndani ya nchi hii katika serikali yetu, lengo ni kujua wapi tulipofanya vibaya ili tuanze na kufanya vizuri mwaka unaoanza!

Sasa tuwajue ni mawaziri gani ambao walionekana kutokufanya vizuri kwenye wizara zao ili waweze kujijua na hatimaye kurekebisha yale madhaifu yao ili kuleta ufanisi zaidi!!
 
Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
3,963
2,000
Katika kumalizia mwaka huu, tunahitimisha kwa kufanya tathmini ya mambo mbalimbali yaliyofanyikakani ya nchi hii katika serikali yetu, lengo ni kujua wapi tulipofanya vibaya ili tuanze na kufanya vizuri mwaka unaoanz!
Sasa tuwajue ni mawaziri gani ambao walionekana kutokufanya vizuri kwenye wizara zao ili waweze kujijua na hatimaye kurekebisha yale madhaifu yao ili kuleta ufanisi zaidi!!
Mbona we hujamtaja hata mmoja? Anza wewe ndipo sisi tufuatie. Wote wameboronga sana,hakuna aliyefanya kazi kwa kiwango kizuri. Kiwango cha kufanya kazi kwa Waziri ni katika kumshawishi Mh Rais katika mambo mazito yanayoigusa jamii.

Kama wamekuwa wazito alafu Rais anajiamulia chochote maana yake Mawaziri wamechangia katika mambo hayo mabovu kupitiliza.
 
Quarteman

Senior Member
Jul 31, 2016
104
250
Mbona we hujamtaja hata mmoja? Anza wewe ndipo sisi tufuatie. Wote wameboronga sana,hakuna aliyefanya kazi kwa kiwango kizuri. Kiwango cha kufanya kazi kwa Waziri ni katika kumshawishi Mh Rais katika mambo mazito yanayoigusa jamii.

Kama wamekuwa wazito alafu Rais anajiamulia chochote maana yake Mawaziri wamechangia katika mambo hayo mabovu kupitiliza.
Will update!!..
Tushirikiane tuwajue kila mtu ana mtazamo wake..
 
darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,070
2,000
Mawaziri hawajaboronga ila faru John ndio amekufa..kuna haja ya kumpima vinasaba (DNA) kuona kama ana asili ya kwetu.Na hao watoto ishirini na kitu nao wachunguzwe maana hawaeleweki
Lazima tulinde mbuga zetu.
 
kinumi

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
1,025
2,000
Mawaziri wanacheza ngoma anayopiga mkuu wa kaya hatuwezi kuwahukumu kwa mapungufu yao wakati wanafanya kazi na mtu anayejua kila kitu kasoro siku yake ya kufa
 
Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,130
2,000
Waziri kivuli lema ameboronga maana kutwa yeye kesi,waziri kivuli wa ajira,waziri kivuli wa mambo ya ndani ki ufupi baraza kivuli limeboronga
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom