Mawakili watajwa kuchangia migogoro mingi ya ardhi kutopata utatuzi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka mawakili kuharakisha kesi za ardhi zaidi ya 2,000 ambazo zina Mawakili wanaosimamia kwa niaba ya wateja wao.

Waziri Angella Mabula amsemea: “Katika mashauri 3000 yaliyochukua zaidi ya miaka miwili, 2,000 kati yao ni yale ambayo yanasimamiwa na Mawakili wanaowakilisha wateja wao.

Baadhi ya mawakili hawaweki nia ya dhati ya kuwezesha umalizaji wa mashauri hayo kwa wakati na hayo ndiyo yanayochelewa, tunatakiwa kujiuliza kuna nini hapo.

Katibu Mkuu naomba uangalize kwa jicho la tatu mabaraza yote ya Dar es Salaam kwa kuwa ndiko kuna migogoro mingi ya ardhi.

Chanzo: Azam TV
 
Mama Mabula, wewe kama wewe uje na plan za kumaliza tatizo. Huyo unayempa wajibu huo inawezekana uwezo wake wa kufikiri kutatua hilo ni mdogo. Katika management tunafundishwa kuwa kazi kubwa ya Manager or for that matter CEO, wa kampuni or any institution ni ku formulate policies so that the objectives of the institution are met! Lukuvi alikaribia sana kutimiza wajibu wa manager. He was coming with a solution na si matamko.
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka mawakili kuharakisha kesi za ardhi zaidi ya 2,000 ambazo zina Mawakili wanaosimamia kwa niaba ya wateja wao.

Waziri Angella Mabula amsemea: “Katika mashauri 3000 yaliyochukua zaidi ya miaka miwili, 2,000 kati yao ni yale ambayo yanasimamiwa na Mawakili wanaowakilisha wateja wao.

Baadhi ya mawakili hawaweki nia ya dhati ya kuwezesha umalizaji wa mashauri hayo kwa wakati na hayo ndiyo yanayochelewa, tunatakiwa kujiuliza kuna nini hapo.

Katibu Mkuu naomba uangalize kwa jicho la tatu mabaraza yote ya Dar es Salaam kwa kuwa ndiko kuna migogoro mingi ya ardhi.

Chanzo: Azam TV
Nikweli, kesi nyingi zinawekwa mahakamani na mawakiri.
 
Mheshimiwa Waziri umelishwa matango pori na wasaidizi wako nawe umeyabugia. Mbona judiciary hawalalamiki mawakili wanachelewesha kesi!!!! Kama mahakama za ardhi zimewashinda kuziendesha mzirudishe Judiciary badala ya kuwatesa wananchi!! Ukienda mahakama za kawaida Resident au District Courts kesi mwaka mmoja tu haufiki na mawakili wapo, primary court miezi 6 tu kesi inaisha. Wizara yako kesi hadi miaka 10. Mbaazi ukikosa maua husingizia jua. Unakuta mkoa mzima una Wenyeviti wawili au watatu wakati mahakama za kawaida mkoani tu mahakimu wa mkoani hawapungui 10 bado huko wilayani na mahakama za mwanzo, hao wenyeviti wawili wanalipua kesi zinarudishwa na mahakama kuu zisikilizwe upya miaka nenda rudi. Kazi imewashinda msiwasingizie mawakili.
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka mawakili kuharakisha kesi za ardhi zaidi ya 2,000 ambazo zina Mawakili wanaosimamia kwa niaba ya wateja wao.

Waziri Angella Mabula amsemea: “Katika mashauri 3000 yaliyochukua zaidi ya miaka miwili, 2,000 kati yao ni yale ambayo yanasimamiwa na Mawakili wanaowakilisha wateja wao.

Baadhi ya mawakili hawaweki nia ya dhati ya kuwezesha umalizaji wa mashauri hayo kwa wakati na hayo ndiyo yanayochelewa, tunatakiwa kujiuliza kuna nini hapo.

Katibu Mkuu naomba uangalize kwa jicho la tatu mabaraza yote ya Dar es Salaam kwa kuwa ndiko kuna migogoro mingi ya ardhi.

Chanzo: Azam TV
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , ukitaka ufanikiwe kwa hili badili mahakama za mabaraza ya ardhi wilaya ziwe mahakama kamili na ziwe na mahakimu kamili.
Zinachangia rushwa, uwonevu na ucheleweshaji wa kesi .
 
Back
Top Bottom