Mawakili waliopo Mjini Kigali Rwanda Wamelaani Vikali Kitendo cha Tundu Lissu Kukamatwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mawakili waliopo mjini Kigali huko Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Mawakili Afrika ya Mashariki (EALS) wamelaani vikali kitendo cha kukamatwa Rais wa (TLS) Chama cha Wanasheria wa Tanganyika Tundu Lissu.

Baadhi ya Mawakili jijini humo, wamekosoa kitendo cha Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar Es Salaam cha kumkamata Rais wa TLS Tundu Lissu ambaye alikuwa njiani kuelekea jijini humo kuhudhuria Mkutano wao.

Baadhi ya Mawakili na Wanasheria waliozungumza na kituo cha utangazaji cha BBC wamesema kuwa, kitendo hicho wanakihusisha na Mkakati wa siri uliokuwa umepangwa na Serikali ya Tanzania ili kumdhibiti Tundu Lissu asifanikiwe kufika kwenye Mkutano huo kwa sababu angeweza kueleza uhalisia wa kilichopo Nchini Tanzania kwa sasa.

"Ni kitendo kibaya sana kimefanywa na Serikali ya Tanzania kupitia vyombo vyake vya Usalama, Tanzania inaweza kukosa mwakilishi kwenye Mkutano huu muhimu, na hili halina shaka tena kuwa, huu ulikuwa ni mpango wa siri wa Serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa Rais wa TLS hafiki hapa Rwanda ili kuficha uhalisia wa kile kinachoendelea Nchini Tanzania kwa sasa, hasa uvunjwaji wa Sheria za Tanzania na Haki za Binadamu kwa ujumla, ingawa mambo haya ya Tanzania naamini tutayazungumza kwa upana wake kupitia huu Mkutano wetu". Alifafanua Wakili kutoka Nchini Kenya aliyeko Kigali, Rwanda ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Tundu Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), amekamatwa leo Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) alipokuwa safarini kuelekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.

Aidha, kwa upande wake Wakili wa kujitegemea Rwebangiza Kiondo kutoka Tanzania amesema kuwa, huu ulikuwa ni mpango tu wa kumdhoofisha Tundu Lissu, na akahoji ni kwa nini hawakumkamata jana yake.

”Huu ni mpango wa kumdhoofisha, kwanini asingekamatwa jana?”

Wakili Rwebangiza ameiambia BBC, kuwa Polisi wanatumia nguvu nyingi kupambana na Mwanasheria huyo ambaye alikuwa akitekeleza wajibu wake.

”Unamkamata Wakili akiwa katika pilika za kutekeleza wajibu wake, tena kwa kumshtukiza utafikiri ni jambazi anayetafutwa, sikatai kwamba huenda pana hoja lakini kwanini umshtukize, mtu ambaye ni mbunge?”

Wakili mwingine ambaye hakutaka kuandikwa jina lake hadharani amesema kuwa Polisi haijaonesha weledi kwa kumkamata mtu ambaye hakuwa na kosa la Jinai.

”Wakati anagombea urais wa TLS (Chama cha Mawakili wa Tanganyika) walimvizia wamkamate lakini baadaye alikamatwa na kuachiwa, binafsi naona huu ni uonevu na mwendelezo wa kuizoofisha taaluma ya Mawakili” amesema Wakili huyo.

Wakili Msemo Aljebra anasema Tundu Lissu alikuwa kesho Julai 21 awasilishe mada ambayo ni muhimu katika mkutano huo.

”Siyo kila wakati nguvu inatumika, kwa hili busara ilipaswa kutumika zaidi, na kumuachia kiongozi huyo, binafsi sikuona sababu ya kumvizia, na ilihali alipaswa kuwasilisha mada amesema Msemo.

Wakili wa CHADEMA, Peter Kibatala amesema kuwa, kama Polisi wamemkamata Lissu, wakamilishe taratibu zao wampeleke mahakamani ili wakutane huko
 
Ni sahihi tu. Tanzania haiko kwenye kisiwa cha peke yake. Iko katika dunia yenye mataifa mengi, ni afadhali wajue kilichoko ili watupongeze na kujifunza kwetu ama kujenga ushirkiano bora wenye manufaa na sisi. Tukipongezwa na kupewa fursa za kimaendeleo, tushangilie na kufurahi kwa pamoja, tukipongezana na kuchakarika kuzitumia hizo fursa.

Tunapofanya manyanga, pia watushangae, kutukandia, kutudharau, kutubagua na kutudhihaki. Inapokuwa hivi, ni pia ni vyema tukapokea hizo dhihaka na laana kwa mioyo na mikono yote. Tuone kama kkuna maendeleo katika kuzomewa na dunia nzima. Kama tukiona haina tija, tujibadilike. Duniani hapa ubabe hauna tija. Hakuna mtu anaweza kuishi maisha yote peke yake asihitaji watu wengine. Hakuna!. Labda sisi tutakuwa wa kwanza.
 
Huyo wakili aliyoyaongea unaishia kujiuliza hata kama alisoma kwa kubebwa kufika alipofika...
Kweli akili za kusoma sio za kuishi... inaonyesha walivyo mawakili wa nchini hapa kuropoka tu na kutosimamia kesi za watu vizuri halafu watalalamikia serikali. akayatamka kabisa kwa kujiona kaongea duh!! Kwa hiyo sababu mtu ana kazi zake basi atende maovu tu na kuendelea... eeeh kimbieni saa nane usiku mkayapate hukoooo
 
Message sent; Mission accomplished!
Hao mawakili nao ni mufilisi kwanza wangeuliza kulikoni polisi kumkamata ana kosa lipi kwani Lissu ni rais wa dunia kiasi kwamba akienda kwenye mkutano asikamatwe hata kama ana makosa? Na wao pia wakija hapa waje kwa heshima wakileta matusi nao pia korokoroni. Tumechoka na lugha za kejeli na dharau
 
Huko Rwanda kwenyewe walikuwa wanamtegea

Binafsi nilikuwa napenda asikamatwe hapa DAR ili akateme pumba zake Rwanda zihusuzo uchaguzi then Kagame amdake, aozee huko huko
 
Back
Top Bottom