Mawakili wa Lengai Ole Sabaya waangukia pua kesi ya Uhujumu uchumi, pingamizi lao latupwa

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mawakili wanaomtetea aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ,Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wameangukia pua katika kesi ya uhujumu uchumi mara baada ya mahakama ya hakimu mkazi Arusha,kutupilia mbali pingamizi waliloweka wakipinga baadhi vielelezo vya ushahidi visipokelewe.

Shahidi wa tisa katika kesi hiyo Mary Mayoka(40) ambaye ni Meneja wa Bank ya CRDB Tawi la kwa Morombo Jijini Arusha aliiomba mahakama kupokea vielelezo hivyo kama sehemu ya ushahidi katika kesi huyo,lakini Wakili Mosses Mahuna anayemtetea mshitakiwa Sabaya alipinga vielelezo hivyo visipokelewe kwa kuwa sio halisia.

Vielelezo hivyo ni pamoja na Nakala ya Barua kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa TAKUKURU} Mkoa wa Arusha iliyokuwa ikienda kwa Meneja wa Tawi la CRDB Kwa Mrombo, ikimtaka kutoa CCTV Camera{video sita} vya tukio la januari 22 mwaka huu,karatasi ya benki ya iliyotolea fedha ya Francis Mrosso ya januari 22 mwaka huu na taarifa ya akaunti ya benki ya Mrosso ya kuanzia januari mosi mwaka huu hadi januari 31 mwaka huu.

Baada ya mabishano ya kisheria jana yaliyochukua takribani dakika 90 katika mahakama hiyo chini ya hakimu Patricia Kisinda alikubaliana na hoja za upande wa Waendesha mashitaka wa serikali wakiongozwa na Tacila Asenga.

Hakimu Kisinda baada ya kuvikubali vielelezo hivyo katika kesi hiyo Shahidi Mayoka aliendelea kutoa Ushahidi wake na aliieleza mahakama hiyo kuwa yeye aliidhinisha kiasi cha shilingi Milioni 90 baada mteja wa Benki hiyo Francis Mrosso kutaka kiasi hicho na alichukua fedha hizo na kumwekea katika Boks wakiwa na kijana ambaye hamjui na kutoka nje ya Benk na kwenda katika gari na kuondoka eneo la benki.

Shahidi alida kuwa hawezi kushitakiwa kwa kosa la Utakatishaji Fedha Haramu na utoaji Rushwa kwani alikuwa akiwajibika katika nafasi yake ya kazi kama Meneja.

Alidai kuwa alimwambia Mrosso kwa nini huyo anayekudai asilipwe kiasi hicho kikubwa kwa njia ya Benki lakini Mfanyabiashara huyo Alisema kuwa anahitaji fedha taslimu na aliomba msaada wa kuongea naye na alifanya hivyo lakini kijana huyo ambaye hamfahamu aligoma kufungua akaunti kwa siku hiyo ya januari 22 mwaka huu na alisema atafanya hivyo wakati mwingine akienda katika benki hiyo

Mbali na Sabaya washtakiwa wengine, katika shauri hilo ni Silvester Nyengu(26), Enock Togolani(41), Watson Mwahomange(27), John Odemba, Jackson Macha(29) na Nathan Msuya(31).

Kesi hiyo ya uhukumu uchumi inaendelea kusikilizwa mfururizo katika mahakama hiyo huku idadi ndogo ya ndugu na jamaa wa washtakiwa wakihudhulia mahakani hapo .

Sabaya na Silvester Nyegu ni wafungwa wanaotumikia kifungo cha miaka 30 jela Mara baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha,hata hivyo sabaya na wenzake wawili akiwemo Daniel Mbura tayari wamekata rufaa mahakama kuu ya Tanzania na rufaa yao ikitazamiwa kuanza kusikilizwa desemba 13 mwaka huu mbele ya jaji Philip Butamo.

Ends...
 
Mawakili wanaomtetea aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ,Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wameangukia pua katika kesi ya uhujumu uchumi mara baada ya mahakama ya hakimu mkazi ,Arusha,kutupilia mbali pingamizi waliloweka wakipinga baadhi vielelezo vya ushahidi visipokelewe.

Shahidi wa tisa katika kesi hiyo Mary Mayoka(40) ambaye ni Meneja wa Bank ya CRDB Tawi la kwa Morombo Jijini Arusha aliiomba mahakama kupokea vielelezo hivyo kama sehemu ya ushahidi katika kesi huyo,lakini Wakili Mosses Mahuna anayemtetea mshitakiwa Sabaya alipinga vielelezo hivyo visipokelewe kwa kuwa sio halisia.

Vielelezo hivyo ni pamoja na Nakala ya Barua kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa TAKUKURU} Mkoa wa Arusha iliyokuwa ikienda kwa Meneja wa Tawi la CRDB Kwa Mrombo, ikimtaka kutoa CCTV Camera{video sita} vya tukio la januari 22 mwaka huu,karatasi ya benki ya iliyotolea fedha ya Francis Mrosso ya januari 22 mwaka huu na taarifa ya akaunti ya benki ya Mrosso ya kuanzia januari mosi mwaka huu hadi januari 31 mwaka huu.

Baada ya mabishano ya kisheria jana yaliyochukua takribani dakika 90 katika mahakama hiyo chini ya hakimu Patricia Kisinda alikubaliana na hoja za upande wa Waendesha mashitaka wa serikali wakiongozwa na Tacila Asenga.

Hakimu Kisinda baada ya kuvikubali vielelezo hivyo katika kesi hiyo Shahidi Mayoka aliendelea kutoa Ushahidi wake na aliieleza mahakama hiyo kuwa yeye aliidhinisha kiasi cha shilingi Milioni 90 baada mteja wa Benki hiyo Francis Mrosso kutaka kiasi hicho na alichukua fedha hizo na kumwekea katika Boks wakiwa na kijana ambaye hamjui na kutoka nje ya Benk na kwenda katika gari na kuondoka eneo la benki.

Shahidi alida kuwa hawezi kushitakiwa kwa kosa la Utakatishaji Fedha Haramu na utoaji Rushwa kwani alikuwa akiwajibika katika nafasi yake ya kazi kama Meneja.

Alidai kuwa alimwambia Mrosso kwa nini huyo anayekudai asilipwe kiasi hicho kikubwa kwa njia ya Benki lakini Mfanyabiashara huyo Alisema kuwa anahitaji fedha taslimu na aliomba msaada wa kuongea naye na alifanya hivyo lakini kijana huyo ambaye hamfahamu aligoma kufungua akaunti kwa siku hiyo ya januari 22 mwaka huu na alisema atafanya hivyo wakati mwingine akienda katika benki hiyo.

Mbali na Sabaya washtakiwa wengine, katika shauri hilo ni Silvester Nyengu(26), Enock Togolani(41), Watson Mwahomange(27), John Odemba, Jackson Macha(29) na Nathan Msuya(31).

Kesi hiyo ya uhukumu uchumi inaendelea kusikilizwa mfururizo katika mahakama hiyo huku idadi ndogo ya ndugu na jamaa wa washtakiwa wakihudhulia mahakani hapo.

Sabaya na Silvester Nyegu ni wafungwa wanaotumikia kifungo cha miaka 30 jela Mara baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha,hata hivyo sabaya na wenzake wawili akiwemo Daniel Mbura tayari wamekata rufaa mahakama kuu ya Tanzania na rufaa yao ikitazamiwa kuanza kusikilizwa desemba 13 mwaka huu mbele ya jaji Philip Butamo.

Ends...
 
Unakuta Sabaya anachukua hizo 90 m then anawapa mgao wapambe wake kila mtu wastani wa 5 m.....

Na unakwenda jela miaka 30 sawa na Sabaya aliyekuwa anachukua pesa zaidi ya 90%
 
Hii case itamfunga Sabaya miaka mingine 30 jela..

Atamaliza jela miaka 60 ijayo.
Upandacho ndio uvunacho.
 
Unakuta Sabaya anachukua hizo 90 m then anawapa mgao wapambe wake kila mtu wastani wa 5 m.....

Na unakwenda jela miaka 30 sawa na Sabaya aliyekuwa anachukua pesa zaidi ya 90%
Walikua wanakula raha na kupewa vichenchi tu
 
Back
Top Bottom