WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Gone are the days when the legal profession stood out as "the noble profession".Ilikuwa ni fahari sana kwa mtu kuwa mwanasheria hasa wakili wa kujitegemea maana ilikuwa inaaminika kuwa hawa ndiyo watu pekee waliosoma/kuelimika ( learned fellows!) nadhani kutokana na jinsi taaluma hiyo ilivyokuwa conservative ikishikilia miiko ya kitaaluma na kuwa na mifumo ya kuwaadhibu wale walioenda kinyume na maadili kupitia siyo tu chama cha mawakili bali hata jaji mkuu aliwachukulia hatua wale walioonekana na utovu wa nidhamu na kuwa strike out of the advocates roll.
Tuangalie historia kidogo ili tuweze kuelewa tatizo linakotokea:
Miaka ya nyuma ilikuwa kazi kwelikweli hadi kuingia katika uwakili wa kujitegemea na wakati wa Nyerere ilikuwa ndiyo kabisaaa mawakili wa kujitegemea wenye kufanya kazi kibinafsi ni kama " haikuruhusiwa!" it was kind of restricted.Mawakili wengi wakujitegemea walikuwa wale wa enzi za ukoloni na wengi walikuwa wahindi na wachache wazungu. Kulikuwa na shirika la sheria Tanzania Legal Corporation ambalo kama shirika la umma liliajiri mawakili kusimamia kesi za mashirika na kwa kiasi kidogo kusimamia mashauri ya watu binafsi.Nidhamu ilikuwa juu!
Polepole mawakili binafsi wazalendo wakaanza kusajiliwa lakini ilibidi kufanya usahili maalum ( bar exam) na mchujo ulifanyika ikiwa ni pamoja na kutaka maoni kuhusiana na credibility/conduct ya muombaji na kama alionekana hana maadili ilikuwa kigezo tosha kumnyima uwakili.
Miaka kama mitano sasa, usajili wa mawakili umekuwa kama umerahisishwa zaidi na idadi kubwa sana ya mawakili wamesajiliwa ikiwemo hata watu wasiokuwa na maadili.Wengi wao wamekuwa watu wakujali sana kujilimbikizia mali zaidi ya kutoa huduma.Hizi mbio za kusaka utajiri harakahara kumekuwa kunawaumiza watu kwa namna mbalimbali ambazo labda wachangiaji wanaweza kuchangia. Ndiyo tunaona na kusikia mawakili wakiwaibia na kuwadhulumu wateja wao kama ilivyotokea hapa karibuni ambapo wakili ametiwa mbaroni kwa kumuibia mteja kiasi kikubwa cha pesa ( about 400 million) na mpaka sasa yuko rumande.Zamani mawakili walikuwa wakijiheshimu na kuchunga mienendo yao hata in public. Not anymore! Ndiyo tunaona mawakili kama Magai wakipigana hadharani!
Maswali ya kujiuliza ni:
1. Je code of conduct ya mawakili imetupiliwa mbali na hivyo kuwafanya kuwa huru ku behave kama wahuni?
2. Je tatizo ni mchakato wa kuwasajili au ni mfumo wa kuwamulika mienendo yao?
3. TLS na Council of Legal education hawaoni iko haja kujizatiti na kuionyesha jamii kuwa nidhamu ni sifa moja wapo ya kuwa wakili na si kule kujua sheria tu?
4. Can we compromise on discipline hadi fani hii idharaulike na kuonekana ya wahuni?
5.Jamii inaweza vipi kuwawajibisha hawa watu?
Naomba kutoa hoja ili ijadiliwa kwa undani zaidi