Mawakili Medium Mwale na Loom Ojare ni majambazi?

Wanabodi,

Naomba tujadili hii mada. Mawakili mabwana Medium Mwale na Loom Ojare ni maarufu sana mjini Arusha hasa katika kutetea majambazi mahakamani, tena wana ujasiri wa kutosha sana wa kuwatetea majambazi wanaokamatwa kwenye tukio. Hawa ndio waliosimamia rufaa ya Bw Nyari hadi akafutiwa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kufuatia kupatikana na hatia ya ujambazi wa kutumia silaha.

Hawa hawa Ojare na Mwale ndio wanaowatetea wale majambazi wawili waliopambana na polisi kwa masaa 6 katika nyumba ya Bw Chonjo kule Njiro walikokuwa wamejificha baada ya kupora na kuua kwenye benki ya NMB Mwanga. Hawa pia wamewatetea majambazi waliopora sh bil 4 NBC Moshi mwaka 2004. Na katika tukio moja mtuhumiwa mmoja wa ujambazi sugu aliyekuwa anatafutwa na polisi aliwahi kukamatwa akiwa nyumbani kwa mmoja wa mawakili hawa, wakili alipobanwa na polisi akadai ni mpangaji wake.

Na zipo kesi nyingine nyingi tu za watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha katika mahakama kuu kanda ya Moshi na katika mahakama za hakimu Mkazi Moshi na Arusha ambazo mawakili hawa wanasimamia. Ukisikia kuna tukio la ujambazi wa kutumia silaha na majambazi wamekamatwa Moshi au Arusha, kama ni majambazi sugu wale wanaofahamika hata na wenyeji, fuatilia utasikia pia kuwa mawakili wao ni Loom Ojare na Medium Mwale.

Ukisikia benki imevamiwa Moshi na kuporwa mabilioni, fuatilia nani wakili wa watuhumiwa mara wakamatwapo; Loom Ojare na Medium Mwale. Sijui kama wana kesi nyingine za wasiotuhumiwa ujambazi. Je kuna uhusiano wowote (zaidi ya umahiri katika sheria) kati ya mawakili hawa na majambazi wauaji? Je hawa jamaa nao pia ni majambazi au washirika wao?

Hebu naomba tujadili hii mada maana kuna watu wameshaanza kupoteza imani si tu na mawakili hawa, bali pia na mfumo wetu wa sheria kwa ujumla. Naelewa katika nchi zilizoendelea kuna mawakili ambao wamejikita katika aina fulani za kesi na kuwa mahiri na wa kutumainiwa kwa mfano katika kesi za murder, fraud, divorce, blasphemy, n.k, ambapo yeyote mwenye kesi ya namna hiyo huwafuata mawakili hao. Je ni hivyo kwa hawa Mwale na Ojare au kuna zaidi?

Nafahamu pia huu usemi: "A bright lawyer knows the law (might be LL.B Hons first class) but a smart lawyer knows the judge" (might have passed his law degree very poorly and by sheer luck, but wins cases by all means!) Hawa jamaa wako upande upi hapa?

Naomba tujadili, mwenye ushahidi wowote hata wa kimazingira atuwekee hapa. Asanteni.
Mkuu, kwa kua imani imeanza toweka kuhusu hawa watu, nashauri wauwawe kwa mwano tu,
 
Mleta Uzi nakushauri ukiwa na kesi au una ndugu yako ana kesi kawatafute hawa jamaa wawili. Hapa umetufumbua macho wengine tuanze kuwatumia hawa watu.

These guys are smart lawyer's.. Huo ujinga wa kusema eti na wao in majambazi unapotoka, kama ni majambazi wangeshakamatwa kitambo. Wanaitumia shule yao ya sheria ipasavyo.

Hongera sana kwao

Akawatafute wapi au aende nae gerezani kisongo? Hawa mawakili nao wapo gerezani toka mwaka 2011 kama sikosei walikuwa wanatafutwa na interpol.
 
Mleta Uzi nakushauri ukiwa na kesi au una ndugu yako ana kesi kawatafute hawa jamaa wawili. Hapa umetufumbua macho wengine tuanze kuwatumia hawa watu.

These guys are smart lawyer's.. Huo ujinga wa kusema eti na wao in majambazi unapotoka, kama ni majambazi wangeshakamatwa kitambo. Wanaitumia shule yao ya sheria ipasavyo.

Hongera sana kwao
Mwale yupo ndani (mahabusu) kitambo.....na dalili ya kutoka hakuna! Toka enzi ya JK.
 
Hii post ni ya miaka 11 iliyopita, yaani ya mwaka 2007,..., why here today? Nini kimejiri?
Labda ni kwa sababu hawa mawakili; sina uhakika wote wawili lakini nina uhakika na Mwale walikuja kukamatwa baadaye na hadi sasa wapo mahabusu. Mambo ni hayohayo aliyoleta mleta mwaka 2007 na ni order kutoka US nasikia...ugaidi. Ogopa watu wa humu JF!
 
Ugaidi ni Nomaa Kesi yake

Ova
 
Sheria gani nchini inasema jambazi ,mwizi kibaka haruhusiwi kutetewa?

Everyone has a right to be represented, hqta uwe shetani haki yako haipotei.

Wao kama mawakili wanatimiza wajibu wao tuuu wa kuwakilisha wateja wao, sasa wewe ukisema ni majambazi uende mahakamani ukathibitishe
 
leo mwizi akiwa anatafutwa na polisi baada ya kufanya wizi sehemu na akakutwa kajificha kwako, huko unakuchukulia kama kukutana kwa kawaida? iko wazi lema anawatetea hawa maana walikuwa ni watetezi wa majambazi na lema mwenyewe akiwemo maana kazi yake inajulikana alikuwa jambazi, wewe tulia maana hujui lolote.
Sikujui ila majibu yako unajidhalilisha....sio lazima kila kitu ujibu watu wanaweza judge uwezo wako ulivyomdogo kureason
 
Mleta Uzi nakushauri ukiwa na kesi au una ndugu yako ana kesi kawatafute hawa jamaa wawili. Hapa umetufumbua macho wengine tuanze kuwatumia hawa watu.

These guys are smart lawyer's.. Huo ujinga wa kusema eti na wao in majambazi unapotoka, kama ni majambazi wangeshakamatwa kitambo. Wanaitumia shule yao ya sheria ipasavyo.

Hongera sana kwao
Wanaitumia wapi hio shule ya sheria?Wapo ndani mwaka wa 7 sasa
 
Wana JF,

Tunaishiwa jamani, sheria inasema everybody is innocent until proven guilty in the court of LAW.

Hata kama umerusha risasi, inawezekana ulikuwa unajitetea, kani polisi nao si ni watu?

Hamkuona wale wananchi wema waliouwawa na ZOMBE? kama wangekuwa na bastola/bunduki wasingejitetea? kwahiyo wangejitetea wangeitwa majambazi na hakuna wakili ambaye angestahili kuwatetea!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1

This is very low of US!
Wonderful tackle, majic
 
Mleta Uzi nakushauri ukiwa na kesi au una ndugu yako ana kesi kawatafute hawa jamaa wawili. Hapa umetufumbua macho wengine tuanze kuwatumia hawa watu.

These guys are smart lawyer's.. Huo ujinga wa kusema eti na wao in majambazi unapotoka, kama ni majambazi wangeshakamatwa kitambo. Wanaitumia shule yao ya sheria ipasavyo.

Hongera sana kwao
Hao wawili akina nani?,kwani mwale alishatoka ndani na kesi yake ya utakatishaji?
 
leo mwizi akiwa anatafutwa na polisi baada ya kufanya wizi sehemu na akakutwa kajificha kwako, huko unakuchukulia kama kukutana kwa kawaida? iko wazi lema anawatetea hawa maana walikuwa ni watetezi wa majambazi na lema mwenyewe akiwemo maana kazi yake inajulikana alikuwa jambazi, wewe tulia maana hujui lolote.
Kafanya uhalifu kakutwa kwa mwanasheria??? Kwani nani aliyeprove kuwa uhalifu umefanyika ilihali hajahukumiwa au kukutwa na hatia?? Kwahiyo hata mimi nikikaribisha mgeni alafu kumbe katoka kuiba akikamatwa kwangu basi automatically na mimi nageuka kuwa Jambazi???

Deo deo deo naona umefilisika kimawazo.... Hii reasoning ya wapi hii?? Jambazi ana haki ya kusikilizwa ili apate hukumu anayostahili kwa maana hata hao unaowaita majambazi wangekosa wakili bado serikali ingetakiwa iwatafutie wanasheria je ina maana serikali nayo inasupport ujambazi kisa inawapa wanasheria wauaji na majambazi???

Anyway Esther anakusalimia anasema 2020 anakusubiri tena :D:D:D
 
Kwahiyo sheria inakataza mtuhumiwa kukutana na mwanasheria wake nje ya ofisi??? Kwahyo pale magufuli anapokutana na watu nyumbani kwake chato huwa hakutani nao kama Rais ila kama mwananchi wa kawaida kisa tu hayupo ofisini ikulu ??? Kazi kwelikweli

Huo ni utetezi wa ajabu sana kutoka kwa kijana msomi kama wewe maana hata nikikuuliza sheria gani inasema hivo huna jibu...... Pia pale anakuwa mtuhumiwa au anayehisiwa ila sio jambazi akisha kuwa declared ni jambazi of course hawezi kuwa uraiani unless katimiza kifungo sasa kwanini unaforce eti JAMBAZI kakutwa kwake?? Unaweza thibitisha nani ni jambazi kisheria kabla hajahukumiwa na mahakama ??

Naona toka uambulie kura 300 jimbo zima umeacha kureason kama deo wa mwaka 2013
Mkuu unatoka kwenye mada unaanza personal attack,hayo ya kura 300 yametoka wapi kwenye hii thread?,tujikite kwenye mada iliyopo hapa
 
Kafanya uhalifu kakutwa kwa mwanasheria??? Kwani nani aliyeprove kuwa uhalifu umefanyika ilihali hajahukumiwa au kukutwa na hatia?? Kwahiyo hata mimi nikikaribisha mgeni alafu kumbe katoka kuiba akikamatwa kwangu basi automatically na mimi nageuka kuwa Jambazi???

Deo deo deo naona umefilisika kimawazo.... Hii reasoning ya wapi hii?? Jambazi ana haki ya kusikilizwa ili apate hukumu anayostahili kwa maana hata hao unaowaita majambazi wangekosa wakili bado serikali ingetakiwa iwatafutie wanasheria je ina maana serikali nayo inasupport ujambazi kisa inawapa wanasheria wauaji na majambazi???

Anyway Esther anakusalimia anasema 2020 anakusubiri tena :D:D:D
Hivi facts Za Kesi Yao au mazingira ya kushikwa kwao unayajua???
Zaidi ya hapo wao ni wanasheria na Kwa vyovyote vile wanawanasheria, je umewasikia wao au wanasheria wao kulalamika kuhusu kushikwa kwao au wao kuwa kisongo Kwa kipindi chote ???
 
Nafikiri unaenda nje ya mada au hujaelewa nachomjibu deo..... Yeye anadai ni kosa mtuhumiwa kukamatwa nyumbani kwa mwanasheria ndio najiuliza ni sheria ipi inayolazimisha mwanasheria asikutane na mteja wake nyumbani??? Hilo ndio ninalopinga hayo ya wao kukamatwa kma ni halali au lah mahakama itaamua maana mimi sio jaji ila hoja ya kusema mtetea majambazi mahakamani ni jambazi simply because huwa anakutana nao nyumbani kwake ni utetezi wa ajabu sana
 
Msingi wa point Yangu au zangu ni hizi , hujui hao watuhumiwa Kama wapo wa ujambazi walikutwa katika mazingira yapi nyumbani Kwa hao mawakili juu ya Dari , store chumbani , n.k na Kama walikuwa wanatafutwa , halafu wakakutwa nyumbani Kwa wakili inaweza kuchukuliwa Kama ni kosa kwani sehemu ya shughuli Za wakili ni ofisini kwake . Jingine ni ushahidi wa mawasuliano Kati ya majambazi na Mali zao na mawakili wao .
 
Back
Top Bottom