Wanabodi,
Naomba tujadili hii mada. Mawakili mabwana Medium Mwale na Loom Ojare ni maarufu sana mjini Arusha hasa katika kutetea majambazi mahakamani, tena wana ujasiri wa kutosha sana wa kuwatetea majambazi wanaokamatwa kwenye tukio. Hawa ndio waliosimamia rufaa ya Bw Nyari hadi akafutiwa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kufuatia kupatikana na hatia ya ujambazi wa kutumia silaha.
Hawa hawa Ojare na Mwale ndio wanaowatetea wale majambazi wawili waliopambana na polisi kwa masaa 6 katika nyumba ya Bw Chonjo kule Njiro walikokuwa wamejificha baada ya kupora na kuua kwenye benki ya NMB Mwanga. Hawa pia wamewatetea majambazi waliopora sh bil 4 NBC Moshi mwaka 2004. Na katika tukio moja mtuhumiwa mmoja wa ujambazi sugu aliyekuwa anatafutwa na polisi aliwahi kukamatwa akiwa nyumbani kwa mmoja wa mawakili hawa, wakili alipobanwa na polisi akadai ni mpangaji wake.
Na zipo kesi nyingine nyingi tu za watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha katika mahakama kuu kanda ya Moshi na katika mahakama za hakimu Mkazi Moshi na Arusha ambazo mawakili hawa wanasimamia. Ukisikia kuna tukio la ujambazi wa kutumia silaha na majambazi wamekamatwa Moshi au Arusha, kama ni majambazi sugu wale wanaofahamika hata na wenyeji, fuatilia utasikia pia kuwa mawakili wao ni Loom Ojare na Medium Mwale.
Ukisikia benki imevamiwa Moshi na kuporwa mabilioni, fuatilia nani wakili wa watuhumiwa mara wakamatwapo; Loom Ojare na Medium Mwale. Sijui kama wana kesi nyingine za wasiotuhumiwa ujambazi. Je kuna uhusiano wowote (zaidi ya umahiri katika sheria) kati ya mawakili hawa na majambazi wauaji? Je hawa jamaa nao pia ni majambazi au washirika wao?
Hebu naomba tujadili hii mada maana kuna watu wameshaanza kupoteza imani si tu na mawakili hawa, bali pia na mfumo wetu wa sheria kwa ujumla. Naelewa katika nchi zilizoendelea kuna mawakili ambao wamejikita katika aina fulani za kesi na kuwa mahiri na wa kutumainiwa kwa mfano katika kesi za murder, fraud, divorce, blasphemy, n.k, ambapo yeyote mwenye kesi ya namna hiyo huwafuata mawakili hao. Je ni hivyo kwa hawa Mwale na Ojare au kuna zaidi?
Nafahamu pia huu usemi: "A bright lawyer knows the law (might be LL.B Hons first class) but a smart lawyer knows the judge" (might have passed his law degree very poorly and by sheer luck, but wins cases by all means!) Hawa jamaa wako upande upi hapa?
Naomba tujadili, mwenye ushahidi wowote hata wa kimazingira atuwekee hapa. Asanteni.