Mawakili Kutetea Mafisadi na Uzalendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawakili Kutetea Mafisadi na Uzalendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana wa Mungu, Apr 28, 2009.

 1. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Jamani, hivi kwanini watz wengine hawaonekani kuwapinga mafisadi? nikianza na Game theory aliyeko humu ndani, nakuja kwa sophia simba yule anayejifanya kusali makanisa ya kilokole kumbe anawaaibisha walokole bure, mkuchika na kikwete?

  Nikianza na kikwete, kwanini anapata kigugumizi kuwashughulikia mafisadi papa?

  sophia simba, ana nini cha kutuambia, au kwasababu ana mwili mkubwa?hahaha, akili nazo ni kubwa? anafikiri wao kama wanakaa masaki sisi sote tunakaa masaki?

  wengine ni wengi, lakini hivi kwanini watz wengine hadi sasa hawajafunguka tu kuwapinga hawa mafisadi hata tukaandamana mtaani kuwalaani na kuwashinikiza wakamatwe watiwe pingu? hivi kama Game theory hivi, si anatia hasira zaidi jamani, watu hawa wanaongeza hasira kwa watz masikini, kwasababu ukweli upo na unajilikana ya kwamba KUNA MAFISADI WANAOTUMIA HELA ZETU KUTUTESA NA KUWAWINDA WATZ WENZETU. tukubali hii vita mafisadi washinde? watumie hela yetu sisiwenyewe walioiba ili kutunyamazisha na kutupiga changa la macho, kukodi majambazi kuwaua wapigania haki? tukubali kushindwa? kwanini? sasa kwanini watz wengine hasa wenye rungu, wanaonekana wana kigugumizi? hii inatia hasira, ngojeni mwakani wakati wa kampeni, patachimbika.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuna hatari kuwa hii nchi imeshatekwa si uliwasikia wakisema kuwa ni hatari na maneno kibao ikiwa utaamua kudili ,naogopa isije kuwa woga huu kuna watu wameshatishwa si bure maana ushahidi uliopo si wa kushitaki mtu ni wa kumpeleka jela moja kwa moja masuali na majibu yatapatikana akiwepo jela ila tuonavyo mambo ni mwendo wa kobe ukichanganyika na umbo la kinyonga.
   
 3. M

  MchungajiMakini Senior Member

  #3
  Apr 28, 2009
  Joined: Apr 4, 2008
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  noma hiyo!

  ali hassani mwinyi kachezea kibano.
  na hao waumini walipoona mzee kapewa kibano wakampa huyo muislam mwenye imani kali na ya haki wakampa pia kibano

  sasa munataka na kikwete nye pia apingwe vibao?
  sasa kuna hatari kama wewe ni ccm ukiwapa vibano viongozi wako kwa haki basi hao hao ccm wenzako watakupa kibano.

  serikali zote duniani haziendi kwa haki ila mfalme wa katoliki tu rome (italia)
   
 4. B

  Bull JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Nani kakwambia Wakatoliki inendeshwa kihaki? ill informed!!! watoto kibao wa kiume wamelawitiwa na mapadre, bado mfalme wao anawatetea na kuwalinda, Rome haina tafauti na CCM mafisadi wanalindwa, wanalindana kwa taarifa yako
   
 5. j

  jibabaz Member

  #5
  Apr 28, 2009
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MWANA WA MUNGU..Heshima mbele! Mbona jibu la swali lako ni rahisi, Ni kwamba PESA ndio inatutawala kwa hio kwanini upinge ufisadi wakati ndokula yako?
  Pili, watu kuandamana sahau maana hii jamii yetu ambayo "imeridhika" kama huna kitu mfukoni ukimbomu mtu anakupa kwa hio amani yetu iko mifukoni mwetu. Na pia hatujui haki zetu, mfano wazee wetu wa East Africa walivyoandamana basi ikaonekana kuwa wazee hawana cha kufanya wakati hawajui maandamano yametoa marais kadhaa kutoka kwenye uongozi na kuwafanya waachie ngazi.
   
 6. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wanaogopa tambi itakatwa kama jk mwenyewe anavyosema!
   
 7. N

  Nibo Member

  #7
  Apr 29, 2009
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wote ni walewale. Hakuna wa kumnyoshea kidole mwenzake.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wengine wanategemea mafisadi hata michango yao hapa tunaiona!
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mbali na kutegemea mafisadi ni kwamba humu humu mafisadi wamo wanaona mnatishia maslahi yao. Ndiyo maana wanakuwa mbogo!
   
 10. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwana wa Mungu...ubarikiwe kwanza!

  First, unaowaona wakiwatetea mafisadi hapan jamvini ni either vibaraka wa mafisadi au ni mafisadi wenyewe, kumbuka ID zetu wengi wetu zimefichwa, laiti kila moja wetu angeweza weka real ID yake ungeona ukweli huo!

  Second, wale wanaotetea mafisadi huko mitaani, hao kula yao or maisha yao yapo mikononi mwa mafisadi i.e they indirectly benefit from ufisadi, kama vile wapambe wa karibu, washirika wa kibiashara, family members, politicians ambao wakichacha huwapiga simu hawa mafisadi na kupewa chochote ...the likes of Mtikila (kama mnakumbuka issue yake)

  Third, kuna wanafiki ambao wanaujua ukweli halisi lakini kwa sababu za kisiasa wanaogopa kuutetea ukweli huo kwa kuogopa kutoswa na wenzao hasa kwenye vyama vyao ambavyo pia hufadhiliwa na mafisadi hao e.g CCM ambayo imeshapoke michango mingi sana toka kwa watu kama Somaiya...hivyo watu kama kina Simba, Mkuchika, wanasali sana wasiombwe kucomment juu ya issues za kifisadi, lakini inapotokea wakatakiwa kufanya hivyo huwa hawana option nyingine bali kuwa wanafiki na kusema kitu wasicho maanisha.....hawa dawa yao ni wananchi kwenye majimbo yao!

  Fourth, watanzania wengi sana hawashabikii sana hizi issues za kifisadi ni kutokana na the fact that, most of them ni mambumbumbu wa kutupwa kuhusu elimu ya uraia na haki zao za msingi. Hawa wanashindwa kabisa kuhusianisha (kurelate) ufisadi na umasikini na ujinga walio nao, laiti watz hawa wangepata kujua uhusiano wa ufisadi na umasikini wao...basi mitaa yote tz isingekalika! Viongozi wanaofurahia ufisadi huo, basi ujinga wa watz ni mtaji wao mkubwa sana katika chaguzi mbali mbali, na kamwe serikali itakayoundwa na viongozi hao haiwezi kupigana kuuondoa ujinga na umasikini wa watanzania kwa sababu huo ndio mtaji wao mkubwa!
   
 11. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  a bullet dont lie.... am a professional sniper...with only 5 bullets i can resolve this MAFISADI PAPA watano tu...

  watu 40million wanateseka.....sijui usalama wa taifa wapo wapi na wanafanya nini?..enzi za mwalimu alitokea giriki akaropoka kuwa kaiweka serikali ya mwl mfukoni...you know what nyerere did?....USALAMA WA TAIFA UPO KWELI?...NA KAMA UPO UNAFANYA NINI NA KWA MASLAHI YA NANI?...MAFISADI??...AU MENGI NDIO AWE KIONGOZI WA USALAMA WA TAIFA....maana hawa jamaa wanawezaa hata kumwondoa rais wetu na tunachekelea kuwa usalama wa taifa wapo...f***ck everything..usalama wa taifa my...***ss. wadau hii ni hasira na chuki yangu dhidi ya mafisadi papa wa5 tu...we dare to talk openly and xpress our inner feelings.
   
 12. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Sasa wewe unaleta utani kwenye jasmbo ambalo is so serious. Mfalme wa Rome yupi? Benedict ndiye mwenye haki?
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hebu chukua mshahara wa mafanyakazi wa serikali amabaye ndiye pengine ana kipatao kikubwa ukilinganisha na wakulima of course ondoa baadhi ya wafanyabishara. Umpigie hesabu ya matumizi kwa mwezi uone anavyoteseka. Wahindi na akina RA wanalijua hilo.

  Wanajua gap iko wapi ndio maana wanaitumia ipasavyo. Wataanzia kwa viongozi wao ambao wana vyeo vikumbwa lakini tamaa ya fedha au njaa ya kweli inawaua. Watapewa hata milioni moja tu then uone matokeo yake. Watawatumika kama miungu vile .Waswahili husema watawalamba hata***********ko.

  hili ndilo jibu. Usishangae ukiwaona akina Sophia simba wakibwatuka hivyo hovyo , huko ndiko kutumikia kafiri Mzee. Hapo ndipo wanajiafanya hawaoni hezo fedha wanazitoa wapi , kumbe ndio huko kwenye ufisadi. Hata wakijua fika , hawatakubaliana na ukweli. Wataendelea kulamaba ********ko yao hadi kiama . Hiyo ndiyo power of poverty against development.
   
 14. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Who cares? ......I do care when few people (fisadis) make the life of more than 40 Tanzanians a living hell!

  Naungana na wewe, hawa UWT kazi yao na naona ni kulinda maslahi ya mafisadi na vibaraka wao na sio kulinda maslahi ya Taifa...ngoja tuanzishe thread ya kujadili kazi na umuhimu wa UWT kwa Taifa letu!
   
 15. w

  wajinga Senior Member

  #15
  Apr 29, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao wanaotetea mafisadi wasome barua ya Salva kwa fisadi wake na waone kama ukitetea fisadi akifanikiwa atakukumbuka. Fisadi ni fisi aktakula mpaka atapike na ale matapishi yake na atapike tena.
   
 16. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii barua ilishawekwa hapa JF? if not tuwekee basi, nami sijaiona pia!
   
 17. Companero

  Companero Platinum Member

  #17
  Apr 29, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mtanzania Utajipingaje?
   
 18. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Mwana wa Mungu!

  Naona umeleta hoja nzuri jamvini na next level amehitimisha barabara! big five!

  Ni ukweli usiopingika kwamba watawala wameshikilia ujinga na umaskini wa Watz walio wengi above 80%( This figure is equal to the percentage of the fake landslide victory by JMK in 2005) kama mtaji wao wa kuishi and this will take a long time!!! Indicators zipo JMK as the wrong driver wanajenga vyumba badala ya shule what do you expect at the end of the day it's making a lot of wajinga who can't analyse.

  That is why at the beginning of the saga ufisadi ulionekana kama porojo za wapinzani and CCM is rest assured of another landslide victory next year come what may!

  Kwa IQ ndogo ya Mustapha Mkullo na Jakaya Mrisho Kikwete walidiriki kusema pesa za EPA sio za serikali na wote tulikaa kimya = tulikubali badala ya kuwatoa baruti shame on Watanzania ni watu wa ajabu kwenye hii karne ya 21 you know why 95% wajinga period!

  Changamoto watu wote wenye access na hii forum the majority wanatumia mitandao ya makazini kwao (huu ni ufisadi in the first level) and very few like myself seldom buy airtime via data cards from Zantel or Voda ,Tigo and Zain or TTCL mobile to air their views hapa jamii forums!!! Wote wanakua na kigugumizi cha kukemea ufisadi cause mnakosa moral justfication! I said it!!!

  The way forward let us wage a crusade ili TACRA the corrupt regulator aamke ili kufanya internet free as long as you are connected through your phone like in other countries au at least iwe affordable(low cost). Tuachane na hii tabia ya kushabikia kupunguza nauli ya daladala while forgetting to control bei ya kaunga(sembe) au hata maziwa na madaftari ya vitoto vya bush school!!

  Otherwise katika list ya wanaofaidika na ufisadi asiwe CCM;serikali na RA peke yake tuwaingize kwanza wanajamii forum wote hata kwa majina yao ya bandia(aka)

  Lastly don't forget the President(leader) is the mirror image of the people he is leading! Kama unamtabua JMK kama rais wako basi ujue he is your reflection!! Kama hufanyi hivyo as per the katiba you ara subject to treason !!
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  1.True, a bullet dont lie but it may not be the ultimate solution to the Ufisadi biz.Ukiwaua hao watano bado kuna wengi tu wataendelea kufaidika...we need a practical solution.

  2.Just a caution katika kutumia takwimu ..... nadhani siyo sahihi kusema kuwa watu 40m wanateseka.....idadi ya watu TZ inakadiriwa kuwa about 40m, humohumo kuna mafisadi pia.Mafisadi hao na wanaowategemea kwa namna moja au nyingi hawamo kati ya watu wenye kuumizwa na ufisadi bali wanafaidika na ufisadi.Labda tuseme kuwa majority ya Watanzania hasa wa vijijiji ambao ni asilimia kama 80% ndiyo wanaoteseka.Najua ni kitu kidogo lakini tunahitaji umakini ili tuonekane tunajenga hoja nzito zisizojaa jazba tu.
   
  Last edited: Apr 29, 2009
 20. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mafisadi wana fedha nyingi walizoiba hivyo wanazitumia kuwaziba midomo wazalendo na kujisafisha kwa njia mbalimbali.
   
Loading...