Mawakili: Je, katika sheria mnafundishwa kuhusu Physiology ya Jaji? Na kama ukiijua inasaidia nini?

MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
353
1,000
Mimi si mwanasheria lakini marafiki zangu wengi ni wanasheria na nimeshuhudia mijadala mingi ya wanasheria.

Lakini nilichogundua katika practice (siyo fani) ya wanasheria ni kwamba huwa inafika mahala wanaongea kuhusu tabia ya Jaji fulani, physichology ya Jaji fulani. Kwa maana hiyo ni kama vile unatakiwa kuwajua majaji.

Mfano mtu anasema Jaji fulani hapendi hiki wakati jaji mwingine hana tatizo na hicho anachokataa huyo mwenzake. Nilipogundua hivyo tatizo langu hapa likawa ni hili.

Kwa maana hiyo majadiliano mengi wanajadili hivi vitu. Yaani ukitaka kujua tabia za majaji, siyo katika mambo binafsi au vituko, bali katika uendeshaji wa kesi basi kaa na wanasheria.

Sasa hapa likaja tatizo sijui kama ni ujinga wangu kuhusu sheria au la. Kabla ya urafiki na wanasehria nilikuwa ninadhani kwamba kule University au Law School wanasheria walifundishwa sheria zinavyosema. Nikadhani ukijua provision (vifungu) vya sheria basi utatamba kifua mbele kwamba kesi inayoendana na vifungu hivyo utaishinda maadamu hata utaratibu wa kuifikisha (technicality) mahakamani umeufuata.

Hivyo, hata mjinga wa sheria kama mimi, ukijua vifungu vya jambo fulani na utaratibu wake basi una uhakika wa kushinda hiyo kesi. Na kwa kweli hivyo ndivyo ilitakiwa, tuvijue vifungu, tukiviheshimu hatushindwi kesi na anayetushitaki, tukivikiuka tunashinda kesi tunapowashitaki waliovikuka dhidii yetu.

Niliamini hivyo kwa sababu sheria zinatungwa kwa kwa ajili yetu wote na si kwa ajili ya mawakili au wanasheria ambao siyo lazima uwatumie kama huna hela au huwahitaji.

Na mazoea yangu na wanasheria nilidhani nitaokota mengi kuhusu vifungu kwani nilitarajia wanasheria wabishane vifungu kwamba kifungu hiki kinasema hivi na mwingine anabisha nasema kifungu kile kinasema hivi.

Kumbe sivyo! Ukikaa na wanasheria utasikia wanasema jaji huyu yuko hivi na yule yuko vile. Nilipogundua hilo nikasema hebu nililete humu mitandaoni na ikibidi humu JF.

Kama wanachokifanya wanasheria hawa ni kweli huko mahakamani basi nchi yetu iko katika hatari kubwa na mhimili huu wa mahakama. Tunadhani vifungu vya sheria ulivyosoma chuoni au hata sisi mtaani vinatosha kumbe unatakiwa kumsoma na Jaji jambo ambalo mwanasheria hakulisoma chuoni!

Kama mimi ndiye ninakosea kudhani hivi, basi ninatakiwa nirekebishwe lakini hili nimeliona mara nyingi na ninaiona hatari hii. Wengi wengi tu hufungua kesi zao hawana fedha za kuweka mwanasheria anayejua tabia ya jaji.

Hivyo sisi kazi yetu ni kujua vifungu na kamwe hatutahangaika na kupekenyua tabia za Jaji au Hakimu.

Wasalaam katika mjadala mwema.

Ni mimi MdogoWenu
 
Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,032
2,000
MdogoWenu , au Mdogo Wetu, hakika ulichokisema kina ukweli mkubwa ndani yake. Majaji, kama walivyo binadamu wengine, wanayo mihemuko yao, na zaidi ya hapo wanazo chuki binafsi, ukiachilia mbali chuki za kisiasa. Katika kufanya kazi zangu na majaji, kuna mambo mengi nimejifunza. Moja wapo ni hili unalolisema, na ndio maana wanasheria wana msemo wao mmoja wanasema: Know your Judge, yaani mfahamu jaji wako. Huu msemo una maana kubwa kwenye practice ya sheria.

Yafuatayo ni mapungufu au matatizo ya majaji (au mihemko, bila kujali faida na hasara zake) ambayo yako sana kwa majaji wetu. Nitatoa na majina ya majaji wahusika inapobidi, maana hili ni jukwaa huru.
 1. Kuna wanaopenda wakili au mtoa hoja mahakamani aweke na vigezo (authority) kwa kila anachosema, na wanafurahishwa sana na tabia hii na inamsaidia sana wakili au mdaawa kushinda kesi au shauri lake, mfano ni Jaji Rutakangwa na Jaji Mziray.
 2. Kuna wasiopenda maneno mengi, unaweza ukawa unaongea lakini yeye anakuangalia tu haweki maneno yako katika maandishi (record) -hawapendi maneno mengi, wanataka point tena in short. Hawa mara nyingi kuwashawishi kwa kuongea tu haiwezekani, utawashawishi kwa kuongea point. Mfano ni Jaji Ndika.
 3. Wapo majaji wanaopenda kusikiliza shauli kwa maandishi (writtten submission), yaani hata kitu kidogo tu mahakama itaahirishwa ili wadaawa au mawakili walete hoja zao kwa maandishi. Hawa asili yao ni uvivu, wazito kufikiri na wapenda kutafuniwa. Hapa sitawataja kwa majina.
 4. Wapo wasiopenda kuandika maamuzi (hukumu) ndani ya mda muafaka. maamuzi yanaweza kusubiriwa hata kwa mwaka au zaidi, wakati kesi ilishasikilizwa, lakini kutoa hukumu ni kazi. Hawa mara nyingi hawajiamini, eitha kwa kutokujua sheria au kwa sababu ya ubadhirifu (rushwa), lakini wengi ni sababu ya ukilaza. Hapa pia sitatoa majina, ni aibu sana.
 5. Wapo wanaopenda stori katika mahakama. Hata kama mahakama inaendelea mdaawa au wakili akichomekea stori basi jaji atafurahi sana na kuendeleza soga. Hawa siku zote ni wacheshi, na ni rahisi sana kushinda kesi iliyoko katika mikono yao. Ni kumfahamu tu, kuwa nae karibu. Mfano mzuri ni Jaji Mgeta.
 6. Wapo wasiopenda ujuaji. Hata kama ni wakili msomi hutakiwa kuonesha kuwa unajua sheria. Kila kitu omba mahakama itende hekima na haki. Hawapendi hata uingie umevaa vizuri (mavazi ya gharama kama suti (assorted) na saa na simu za kisasa. Ushamba na upole wako ndio mafanikio yako katika kesi. Mmoja wapo katika kundi hili ni Jaji Rugazia.
 7. Majaji wengine ni pro-goverment, yaani wameelemea sana upande wa serikali na huwaambii kitu dhidi ya serikali. na ole wako ajue wewe ni mpinzani au unatetea sana kesi za wapinzani. Siku zote utapoteza kesi kama atafahamu wewe ni mpinzani au mpenda upinzani. Mmoja wapo ni Jaji Rweyememu.
 8. Majaji wengine ni majanga. Yuko radhi muanze kuongea umbea na udaku mahakamani, hapo atakupenda na kesi zako utashinda sana tu. Kosa ujioneshe wewe ni zaidi ya yeye katika nyanja yeyote ile. Ukitaka uende nae sawa msifie - sifia mavazi yake, hukumu zake na hata tembea yake, utafaidi. Mmoja wapo ni jaji Mutungi (Beatrice Mutungi)
 9. Wapo majaji wanaotoa hukumu kufuatana na wenye kesi (wadaawa) au mawakili wamesema nini. Ni rahisi sana kumshawishi jaji kama huyu, hata kama si msimamo wa sheria ili mradi tu ujitahidi kumfafanulia. Mfano ni jaji Awadh.
 10. Wapo Majaji wasipenda kushobokeana, kesi ni kesi tu na hakuna mjadala mwingine. Always be serios, utam-win. Huyu ni Jaji Mansoor -so smart indeed.
 11. Kuna wasipenda kunyanyaswa au kudharauliwa, atalia sana na kukuwekea chuki zisizo na msingi, so epuka kumkwaza. Mfano ni Jaji Abood.
 12. Wapo majaji wanaoamua kesi kufuatana na hali halisi, yani anaangalia mdaawa/mshtakiwa ana nini au anahitaji nini. kwao ni hekima kwanza kabla ya sheria. Tena huruma zaidi kabla ya maneno maneno. Ukitaka kushinda kesi kwake onesha huruma au unyonge kwa mteja wako au kwa wewe mwenyewe. Mfano ni jaji Ngwala.
 13. Wapo majaji wasiojitambua. Sijui kwa sababu gani. Ni rahisi sana kuwaendesha kadri mnavyotaka ninyi. Kwa kifupi ni dhaifu na/au hawajiamini. Mfano ni Jaji Chikoyo.
 14. Pia wapo majaji wanaopenda kuzingatia kalenda na mda, mambo ya kuahirisha ahirisha kesi hawataki na siku zoto usipende kuomba udhuru kwao, Hawa ni kazi tu. Mfano ni jaji Ndika. Nasikia pia Jaji Nyalali (alistaafu mini niko shule) alikuwa kwenye hili kundi.
 15. wapo majaji wenye chuki. kama hakupendi hakupendi tu na mara zote kesi zako utapigwa chini tu hata kama ziko wazi. Ni majaji wa kuepukwa sana. Sitaji jina la mheshimiwa yeyote hapa, sipendi chuki.
 16. Wapo majaji wasiopenda ulevi. Kamwe usiende kwake (mahakamani) unanuka pombe au sigara. Tena hata asisikie wewe ni cha pombe, utapoteza tu. Maskini nikifuatilia wengine sio hata walokole sijui mambo haya wameyatoa wapi. Mwingine namfahamu anatumia pombe (Alhamundulillah nilishakunywa nae mara kadhaa) lakini hapendi kabisa mawakili walevi.
 17. Kuna majaji wapenda majigambo tu, Sijui hawaamini kama wamekuwa majaji! kwao ni kujifanya wajua kila kitu. Kama una kesi kwao wewe tulia tu wala asikufahamu, maana haitasaidia sanasana atakuharibia kesi yako bure. Kwa kifupi hawasomeki, wanaendeshwa na mihemuko yao ya kibinafsi na majigambo. Mfano ni jaji Bongole na jaji Mwambegele.
 18. Wapo majaji wasiopenda ushauri na kujiona ni high classic na wanajua sana, Yaani kwao hata kama unaona anakosea chuna tu, usimshauri utaharibu kesi. Mfano ni jaji Luand na jaji Twaib.
 19. Wapo majaji wasiojua kuwa hawajui, tena hawaombi hata ushauri kwa mawakili wasomi pindi wanapotatizwa na jambo, au hata kwa majaji wenzao. Ukitaka kum-win mpotezee tu, kuwa serios na kesi yako na ikiwezekana hata usimsalimie atakuheshimu. Mfano ni Jaji Fereshi.

Wapo wengine wengi, kwa leo niishie hapa Kwa kifupi hapa bongo kuna mawakili wanashinda kesi kwa kuwasoma majaji tu, wengine wanapigwa chini kwa kutowafahamu majaji wao.
 
Kaka Dragon,

Nashukuru sana kwa kutujulisha hayo unayoyasema. Sasa tatizo ni kwa watu wa kawaida ambao huingia mahakamani kwa ajili ya kesi moja tu tena ya Jaji mmoja tu na huumjuia. Hapo iko shida maana mtu kama huyo anachojua ni kutafuta haki tu hata sheria ikibidi hajui.
 
.
Uko sahihi. Wapo wengi wanapoteza haki zao kisa "hawamfahamu jaji" Tena kuna mawakili wana bahati mbaya sana na majaji, sio kwa sababu hawajui sheria, la hasha!

Pia wapo wanaokesea kutaka kuwahonga majaji, Kuna wanaopokea rushwa ndio, tena wengi tu. Lakini wapo ambao rushwa kwao ni mwiko, ukijaribu kufanya huu mchezo atakuchukia na matokea yake kesi zako nyingi (kwa mawakili) utashindwa sana.
 
permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
5,036

Mkuu pamoja na hoja nzuri hapo juu, ni namna gani mazingira au hali inayomzunguka judge inavyoathiri ufanyaji wa maamuzi vinaelezwa vizuri na American School of jurisprudence I.e American Realism
 
MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
353
1,000
Mkuu pamoja na hoja nzuri hapo juu, ni namna gani mazingira au hali inayomzunguka judge inavyoathiri ufanyaji wa maamuzi vinaelezwa vizuri na American School of jurisprudence I.e American Realism

Asanteni sana wakuu mnaoendelea kutujuza. Sikujua kwamba kumbe haya mambo yanajulikana na yako sehemu nyingi na mnayasoma hadi vyuoni na yameandikiwa vitabu.
 
MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
353
1,000
Asanteni sana wakuu mnaoendelea kutujuza. Sikujua kwamba kumbe haya mambo yanajulikana na yako sehemu nyingi na mnayasoma hadi vyuoni na yameandikiwa vitabu.
 
kson m

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
5,704
2,000
Physiology/physichology...yana maana gani kama alivyoandika mtoa mada?
 
Stanley Mitchell

JF-Expert Member
Jan 2, 2014
4,589
2,000
MdogoWenu , au Mdogo Wetu, hakika ulichokisema kina ukweli mkubwa ndani yake. Majaji, kama walivyo binadamu wengine, wanayo mihemuko yao, na zaidi ya hapo wanazo chuki binafsi, ukiachilia mbali chuki za kisiasa. Katika kufanya kazi zangu na majaji, kuna mambo mengi nimejifunza. Moja wapo ni hili unalolisema, na ndio maana wanasheria wana msemo wao mmoja wanasema: Know your Judge, yaani mfahamu jaji wako. Huu msemo una maana kubwa kwenye practice ya sheria.

Yafuatayo ni mapungufu au matatizo ya majaji (au mihemko, bila kujali faida na hasara zake) ambayo yako sana kwa majaji wetu. Nitatoa na majina ya majaji wahusika inapobidi, maana hili ni jukwaa huru.
 1. Kuna wanaopenda wakili au mtoa hoja mahakamani aweke na vigezo (authority) kwa kila anachosema, na wanafurahishwa sana na tabia hii na inamsaidia sana wakili au mdaawa kushinda kesi au shauri lake, mfano ni Jaji Rutakangwa na Jaji Mziray.
 2. Kuna wasiopenda maneno mengi, unaweza ukawa unaongea lakini yeye anakuangalia tu haweki maneno yako katika maandishi (record) -hawapendi maneno mengi, wanataka point tena in short. Hawa mara nyingi kuwashawishi kwa kuongea tu haiwezekani, utawashawishi kwa kuongea point. Mfano ni Jaji Ndika.
 3. Wapo majaji wanaopenda kusikiliza shauli kwa maandishi (writtten submission), yaani hata kitu kidogo tu mahakama itaahirishwa ili wadaawa au mawakili walete hoja zao kwa maandishi. Hawa asili yao ni uvivu, wazito kufikiri na wapenda kutafuniwa. Hapa sitawataja kwa majina.
 4. Wapo wasiopenda kuandika maamuzi (hukumu) ndani ya mda muafaka. maamuzi yanaweza kusubiriwa hata kwa mwaka au zaidi, wakati kesi ilishasikilizwa, lakini kutoa hukumu ni kazi. Hawa mara nyingi hawajiamini, eitha kwa kutokujua sheria au kwa sababu ya ubadhirifu (rushwa), lakini wengi ni sababu ya ukilaza. Hapa pia sitatoa majina, ni aibu sana.
 5. Wapo wanaopenda stori katika mahakama. Hata kama mahakama inaendelea mdaawa au wakili akichomekea stori basi jaji atafurahi sana na kuendeleza soga. Hawa siku zote ni wacheshi, na ni rahisi sana kushinda kesi iliyoko katika mikono yao. Ni kumfahamu tu, kuwa nae karibu. Mfano mzuri ni Jaji Mgeta.
 6. Wapo wasiopenda ujuaji. Hata kama ni wakili msomi hutakiwa kuonesha kuwa unajua sheria. Kila kitu omba mahakama itende hekima na haki. Hawapendi hata uingie umevaa vizuri (mavazi ya gharama kama suti (assorted) na saa na simu za kisasa. Ushamba na upole wako ndio mafanikio yako katika kesi. Mmoja wapo katika kundi hili ni Jaji Rugazia.
 7. Majaji wengine ni pro-goverment, yaani wameelemea sana upande wa serikali na huwaambii kitu dhidi ya serikali. na ole wako ajue wewe ni mpinzani au unatetea sana kesi za wapinzani. Siku zote utapoteza kesi kama atafahamu wewe ni mpinzani au mpenda upinzani. Mmoja wapo ni Jaji Rweyememu.
 8. Majaji wengine ni majanga. Yuko radhi muanze kuongea umbea na udaku mahakamani, hapo atakupenda na kesi zako utashinda sana tu. Kosa ujioneshe wewe ni zaidi ya yeye katika nyanja yeyote ile. Ukitaka uende nae sawa msifie - sifia mavazi yake, hukumu zake na hata tembea yake, utafaidi. Mmoja wapo ni jaji Mutungi (Beatrice Mutungi)
 9. Wapo majaji wanaotoa hukumu kufuatana na wenye kesi (wadaawa) au mawakili wamesema nini. Ni rahisi sana kumshawishi jaji kama huyu, hata kama si msimamo wa sheria ili mradi tu ujitahidi kumfafanulia. Mfano ni jaji Awadh.
 10. Wapo Majaji wasipenda kushobokeana, kesi ni kesi tu na hakuna mjadala mwingine. Always be serios, utam-win. Huyu ni Jaji Mansoor -so smart indeed.
 11. Kuna wasipenda kunyanyaswa au kudharauliwa, atalia sana na kukuwekea chuki zisizo na msingi, so epuka kumkwaza. Mfano ni Jaji Abood.
 12. Wapo majaji wanaoamua kesi kufuatana na hali halisi, yani anaangalia mdaawa/mshtakiwa ana nini au anahitaji nini. kwao ni hekima kwanza kabla ya sheria. Tena huruma zaidi kabla ya maneno maneno. Ukitaka kushinda kesi kwake onesha huruma au unyonge kwa mteja wako au kwa wewe mwenyewe. Mfano ni jaji Ngwala.
 13. Wapo majaji wasiojitambua. Sijui kwa sababu gani. Ni rahisi sana kuwaendesha kadri mnavyotaka ninyi. Kwa kifupi ni dhaifu na/au hawajiamini. Mfano ni Jaji Chikoyo.
 14. Pia wapo majaji wanaopenda kuzingatia kalenda na mda, mambo ya kuahirisha ahirisha kesi hawataki na siku zoto usipende kuomba udhuru kwao, Hawa ni kazi tu. Mfano ni jaji Ndika. Nasikia pia Jaji Nyalali (alistaafu mini niko shule) alikuwa kwenye hili kundi.
 15. wapo majaji wenye chuki. kama hakupendi hakupendi tu na mara zote kesi zako utapigwa chini tu hata kama ziko wazi. Ni majaji wa kuepukwa sana. Sitaji jina la mheshimiwa yeyote hapa, sipendi chuki.
 16. Wapo majaji wasiopenda ulevi. Kamwe usiende kwake (mahakamani) unanuka pombe au sigara. Tena hata asisikie wewe ni cha pombe, utapoteza tu. Maskini nikifuatilia wengine sio hata walokole sijui mambo haya wameyatoa wapi. Mwingine namfahamu anatumia pombe (Alhamundulillah nilishakunywa nae mara kadhaa) lakini hapendi kabisa mawakili walevi.
 17. Kuna majaji wapenda majigambo tu, Sijui hawaamini kama wamekuwa majaji! kwao ni kujifanya wajua kila kitu. Kama una kesi kwao wewe tulia tu wala asikufahamu, maana haitasaidia sanasana atakuharibia kesi yako bure. Kwa kifupi hawasomeki, wanaendeshwa na mihemuko yao ya kibinafsi na majigambo. Mfano ni jaji Bongole na jaji Mwambegele.
 18. Wapo majaji wasiopenda ushauri na kujiona ni high classic na wanajua sana, Yaani kwao hata kama unaona anakosea chuna tu, usimshauri utaharibu kesi. Mfano ni jaji Luand na jaji Twaib.
 19. Wapo majaji wasiojua kuwa hawajui, tena hawaombi hata ushauri kwa mawakili wasomi pindi wanapotatizwa na jambo, au hata kwa majaji wenzao. Ukitaka kum-win mpotezee tu, kuwa serios na kesi yako na ikiwezekana hata usimsalimie atakuheshimu. Mfano ni Jaji Fereshi.

Wapo wengine wengi, kwa leo niishie hapa Kwa kifupi hapa bongo kuna mawakili wanashinda kesi kwa kuwasoma majaji tu, wengine wanapigwa chini kwa kutowafahamu majaji wao.
Mkuu umeelezea vizuri sana muelezee na George Masaju basi na yeye si aliteuliwa kua judge
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom