Mawakala wa M-Pesa wanaliibia Taifa na Vodacom

Team JPM

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,074
1,608
Kampuni za simu zilianzisha mfumo wa Malipo kwa njia ya simu ili

1. Kumwezesha Mteja kulipia huduma au bidhaa moja kwa moja kwa kutumia simu yake pasipo usumbufu wa kutembea na pesa Taslim

2. Kumwezesha mtoa huduma au muuzaji wa bidhaa kuhifadhi pesa katika simu kwaajili ya usalama

Nia njema ya Kampuni za simu imegeuzwa kichaka cha kukwepa kodi na kuhujumu mapato ya Taifa na kampuni.

Nimeshuhudia Mawakala wa M-Pesa wakiwaelekeza wateja wao kutoa pesa kwa kutumia namba ya malipo badala ya namba ya uwakala.

Ukishatumia namba hiyo, unakatwa ada ya kutolea pesa wakati umetumia namba ya malipo badala ya namba ya kutolea.
Athari zake:

1. Kampuni haipati mapato yatokanayo na huduma ya kutolea pesa kwakuwa mteja huelekezwa kulipia huduma badala ya kutoa pesa

2. Serikali haipati kodi kwakuwa kodi hukatwa kwa kupitia miamala ya kutoa pesa na sio kwa kulipia huduma au bidhaa kwa njia ya simu

Ushauri:

1. Mawakala wa M-Pesa wasiruhusiwe kuwa na namba za kulipia huduma

2. Wafanyabiashara na watoa huduma namba zao zihakikiwe upya
NB: Vita vya Kiuchumi vinahitaji Uzalendo
 
Kuna kitu kimaitwa loophole. Sasa kama ulikuwa hujui hiyo ndiyo moja wapo sasa. All and all hakuna muamala unaofanywa bila ya kulipia kodi.

Makampuni na wso wizi pia. Wanatoza shilingi 300 kwa kutowa Tsh1. Ndio nina maana Ths moja. Yaani ukitoa 9,999 unakatwa 1050 lets say lakini ukiengeza Tsh1 na ukatowa Tsh 10,000 unakatwa Tshs1350. Thats insane!

Sasa hapa.loophole ni kutowa.Tshs 9950 na ukampa wakala Tsh50 akupe Tsh10000 kamilli na uta save Tsh299.
 
Sijui kama unajua mfumo wa M pesa unafanyeje kazi...

Hata hivyo hongera kwa uzalendo.
 
Itoshe tu kusema mleta mada ni mjinga mbobezi. Hakuna ajuacho.
 
Ushauri:

1. Mawakala wa M-Pesa wasiruhusiwe kuwa na namba za kulipia huduma

2. Wafanyabiashara na watoa huduma namba zao zihakikiwe upya
NB: Vita vya Kiuchumi vinahitaji Uzalendo

Unafikiri tatizo ni mawakala tu; mfumo mzima wa simu za mkononi Tanzania ni wizi wa aina fulani hivi...
 
Kuna kitu kimaitwa loophole. Sasa kama ulikuwa hujui hiyo ndiyo moja wapo sasa. All and all hakuna muamala unaofanywa bila ya kulipia kodi.

Makampuni na wso wizi pia. Wanatoza shilingi 300 kwa kutowa Tsh1. Ndio nina maana Ths moja. Yaani ukitoa 9,999 unakatwa 1050 lets say lakini ukiengeza Tsh1 na ukatowa Tsh 10,000 unakatwa Tshs1350. Thats insane!

Sasa hapa.loophole ni kutowa.Tshs 9950 na ukampa wakala Tsh50 akupe Tsh10000 kamilli na uta save Tsh2999.
Eeh bwanaaaa
 
Nimeipenda hii mkuu, thanks sana
 
Huyo wakala mwizi mwizi hivyo na msaliti kwa taifa lazima atakuwa Chadema tu.
Wenye tabia hii ni maccm na wewe ndiye kungwi wao
tapatalk_1564893878930.jpeg
 
Back
Top Bottom