Mawakala wa Kutoa/Kuweka Pesa Walivyo wezi wa Pesa za Wateja

Jamaa ni muongo au tuseme anatia mashaka, kwa kutumia APP ni kweli inawezekana lakini kila baada ya muda fulani ukifungua APP (TigoPesa) huwa kuna CODE inatumwa kwenye namba (LINE) iliyotumika wakati wa kuinstall hiyo APP.

Ikiwa haipo kwenye simu hiyo basi huwezi kuipata hiyo code na hivyo huwezi kuendelea.

Huyu anayedai miamala takribani 25 ni NGUMU SANA kumwamini hapa.
Mkuu siko Hapa Kukuaminisha ww na hata kama unaamini ninakudanganya basi elewa ninajidanganya Mwenyewe.

Nimeleta huu uzi ili nipate mawazo ambayo ni way forward ila unani attack personally

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashindwa kuwaelewa hawa Airtel, nimewaomba Airtel wanisaidie printing out ya money transaction kutoka kwenye namba ya Mama kwenda kwa hyo namba ya hyo jamaa Wananiambia hawawezi Kutoa, kwamba ni siri za wateja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unakuane wa kizamani mkuu? Chamsingi na wewe download hio app weka kwenye smartphone kuna sehemu za kupata details hata za zaidi ya mwaka mzima unaona hela ilipotumwa na vice versa
 
Pale Mlimani City mwananchi alisahau password akaenda airtel kupata huduma ya password wakamwambia atembee Madukani kisha arudi kuwaona baada ya nusu saa pale ofisini kwa huduma zaidi.

Basi yule mwananchi akatoka kuzunguuka Madukani kama alivyoambiwa na mfanyakazi wa airtel baada ya dakika chache akapigiwa simu na mtu akajitambulisha kama mfanyakazi wa airtel akamwambia jinsi ya kurekebisha password yako fanya yafuatayo akafanya kumbe ndio anaibiwa hela zake nyingi.

Anafika ndani ofisini anaambiwa huyo tapeli amekuibia.

Sasa Je alijuaje kuwa anatatizo la password na kwamba alikuwa hapo ofisi ya airtel Mlimani city?

Inamaana wafanyakazi wanashirikiana na wezi.

Mtapata tabu sana kwa huo wizi wenu.

Tangu muanze kuibia watu mmefanya yepi ya maana?!
 
Ingia hela kwenye airtel money tu wanakupigia simu wakijitambulisha kuwa wafanyakazi wa artel na kukuuliza maswali ya kupuuzi na kujifanya wanataka kukupa bonus kumbe wana test zari ili kama vipi utaingia mkenge wakuibie.

Artel kuna baadhi ya wafanyakazi wasio waadilifu wanashirikiana na wezi matapeli kuibia wananchi.
 
Kwani kuomba print out za miamala ni lazima uwe mjini?

Niliongea nao kupitia namba ya huduma kwa wateja nikawaomba wanisaidie hyo print out wakagoma kwamba sio utaratibu sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app

Huko kijijini kuna ofisi ya airtel?

Au wakuprintie kisha unazipataje, bila kufika ofisini huwezi kupata huduma hiyo hata kama inawezekana…. unaongea na watu tofauti tofauti hapa hivyo jitahidi kuzingatia hilo.
 
With ict, anything is possible, niseme tu kuwa security zilizoko kwenye hizi app, ziwe za simu au hata za benki ni ndogo kwa mtu anayejua kucheza na hayo mambo, kitendo cha mama kumwachia dogo password ni kosa kubwa sana maana kumpa mtu password ni kama kumpa access ya pesa zako.
Kama kweli mama ameibiwa kwa staili hiyo, anzia police, pata rb, dogo akamatwe, akiwekwa ndani atasema hela zote alizoiba.
Kama utapenda kuendelea na kesi, hizo meseji zilizo kwenye simu ya mama cana be a starting point
 
Huko kijijini kuna ofisi ya airtel?

Au wakuprintie kisha unazipataje, bila kufika ofisini huwezi kupata huduma hiyo hata kama inawezekana…. unaongea na watu tofauti tofauti hapa hivyo jitahidi kuzingatia hilo.
Kijijini kwetu sio mbali na mjini, ni mwendo wa nauli ya 1500/= so kama wangeniambia wananitumia niende Airtel Shop ningeenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Badilisha password, na umwambie mama yako akienda kufanya muamala asitoe password
 
With ict, anything is possible, niseme tu kuwa security zilizoko kwenye hizi app, ziwe za simu au hata za benki ni ndogo kwa mtu anayejua kucheza na hayo mambo, kitendo cha mama kumwachia dogo password ni kosa kubwa sana maana kumpa mtu password ni kama kumpa access ya pesa zako.
Kama kweli mama ameibiwa kwa staili hiyo, anzia police, pata rb, dogo akamatwe, akiwekwa ndani atasema hela zote alizoiba.
Kama utapenda kuendelea na kesi, hizo meseji zilizo kwenye simu ya mama cana be a starting point
Thanks dude maana Kwa hali ya SSa chochote kinatokea.

Mkuu sio mama tu Hapa, kuna wazee wamemwamini Kijana na wanafika wanampa simu hyo chalii ndio anafanya process zote na anakupa hela na simu yako wala hakwambii Salio lililobaki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila umuadabishe huyo wakala asije kurudia tena
Nimejaribu kufuatilia Tena ni kwamba hawa wazee wakienda kutoa pesa hawapi namba ya Till ya Airtel money, yeye anajitumia kwenye simu yake then mlengwa anapewa pesa na kuondoka.

So ninajiuliza anakuwaje wakala wa Airtel wakati Till ya Airtel Hana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejaribu kufuatilia Tena ni kwamba hawa wazee wakienda kutoa pesa hawapi namba ya Till ya Airtel money, yeye anajitumia kwenye simu yake then mlengwa anapewa pesa na kuondoka.

So ninajiuliza anakuwaje wakala wa Airtel wakati Till ya Airtel Hana?

Sent using Jamii Forums mobile app

Inamaana akijitumia anatuma na ya kutolea still anapata faida
 
Mkuu siko Hapa Kukuaminisha ww na hata kama unaamini ninakudanganya basi elewa ninajidanganya Mwenyewe.

Nimeleta huu uzi ili nipate mawazo ambayo ni way forward ila unani attack personally

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakuna personal attacks hapa, kama kweli unataka way forward basi tunakupa uzoefu kwenye hizo APPs ambazo wewe huzitumii unahisi tu.

Binafsi nimekupa mfano kwa TigoPesa, sijui huko kwingineko huenda inawezekana…. usichague cha kushauriwa mkuu ila mwisho utaamua mwenyewe.
 
Hivi unajielewa kweli wewe....
Kwanza ningekua mimi ndio moods nishakupiga ban ya wiki mbili ili akili ikukae sawa.
Watu wenye akili mgando kama wewe ndio wanao chelewesha mabadiliko ya hiki chama cha kijani kutoka madarakani.
Yaani hadi ushahidi unao, jamaa alitakiwa saizi yupo ICU na pingu mkononi anasubiri kuzindika tu ajikute mahakamani hata kama ni jumapili.
Mama amesema vijana TUCHAKARIKE

Ampe kichapo heavy sio
 
Wakuu Habari ya Mchana.

Niko Likizo ya Sikuukuu za Mwisho Wa Mwaka Huku Kijijini Kwetu.

Mama yangu Mzazi Anaishi Huku Kwetu Kijijini na Ni Mtu mwenye umri wa takriban miaka 90.

Watoto wake Uwaga tunakawaida ya Kutuma Hela Za Matumizi kwa ajili yake na Matumizi ya Nyumbani Kwa Ujumla.

Hapa Nyumbani Kijijini kwetu anaishi Mama, Mtoto wa Marehemu Kaka ana miaka 12, na Msaidizi wa Ndani.

Mama yetu licha ya Kuwa na umri huo Bado anatembea na anaona Vzr.

Kwa hyo Hapa Kijijini Kuna Kijana anafanya Issue za Mpesa, Airtel Money Nk kwa maana ya Money Transaction.

Kwa hyo Wazee wenye Umri wa Mama wanaenda Hapo Kupata huduma ya Kutoa Fedha so Kwa Umri wake na Hawezi kufanya process ya Kutoa pesa.

So Wazee Wetu wakifika Hapo kibandani kwa hyo mwamba wanatabia ya Kumpa Simu Ili Awasaidie kutoa kiasi wanachokihitaji so huyo Jamaa anajua Namba za Siri Za Kutolea pesa za hawa wazee wetu Hapa Vijijini.

Sasa Juzi Niko Na Mama Tumekaa mida Ya Sa12 jioni Ikaingia Meseji ya Airtel money Kwamba Mama amefanya muamala wa 145000/=kwenda kwa hyo Wakala kwa namba yake binafsi.

Nikamuuliza Mama leo umeenda kutoa pesa kwa hyo Wakala wa hapa kijijini, Mama akaniambia sijaenda huko na hata kama nikienda siwezi kutoa hela yote hyo na natumaje hela kwa namba yake binafsi badala ya kutoa kwenye Till # ya Wakala.

Sasa huyu Mtoto wa Braza akanaMbia kama week hivi ilikuja meseji Kwamba mama amemtumia hyo kijana tena 18500/=

So ikabidi nifuatilie kwa Kupiga Namba ya Huduma kwa Wateja Ya Airtel, Wakaniambia kwamba ni kweli Muamala huo umefanyika na ipo miamala mingine takribani 25 ambayo mama yako ametuma kwa hyo kijana.

Ikabidi nimuulize hyo mtaalamu wa Airtel kwamba inakuwaje anaamisha pesa kutoka kwenye simu ya Mama na Simu wakati anayo Mama?

Wakanijibu Kwamba yawezekana huyo Wakala ana Smartphone ambayo ame download apps ya Airtel money So Ndio anatumia kutoa hyo pesa hata kama hana simu.

Wakaniambia Mtu akiwa na hyo Apps yoyote ya hizi huduma za kifedha na akawa na namba yako ya simu na akawa na namba yako ya Siri anauwezo wa kutoa au kuangalia Salio lako bila ww mwenye simu kujua.

Wakuu niko njia panda naombeni ushauri wenu jinsi ya kudeal na huyu Mtu Kabla Sijarudi mjini maana atakuwa ameshawaumiza Sana Wazee Wetu Hapa Kijijini.

Nawasilisha Wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani kwenye simu ya Bibi yetu Kuna hela nyingi Sana kiasi kwamba anaibiwa hivyo na Bado nyie wote mnaomtumia na anayetumiwa hamjui hell zilizomo Ni sh?
 
Laiti ningekuwa mimi aisee directly proportional to.... Ningechukua hatua mikononi ningempa kichapo kimoja hatari sana hadi ajinyee na kujikojolea hapohapo
 
Aaaah ana zari sana huyo kijana kufanya masihara na pesa za watu kutoka familia yenye vinasaba vya uyesu
Mleta mada inaonekana huwa hamtumii yeye izo pesa mama yake. Hivyo hazimuumi kwa sababu wanaotuma ni wengine ndo maana saivi Yuko huko kijijini anakenua tu.
 
Back
Top Bottom