Mavazi ya wasanii kwenye video sio tatizo, tatizo ni ushamba wa viongozi wetu

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
MAVAZI YA WASANII KWENYE VIDEO SIO TATIZO, TATIZO NI USHAMBA WA VIONGOZI WETU.

Majuzi nimewasikia Naibu Waziri Habari na Rais Magufuli wakikemea kuvaa nguo za utupu kwenye Video. Ukiwa Mshamba ni mshamba tu hata ungekuwa na cheo Ikulu, hata kama ungekuwa Profesa.

Nchini Swaziland kwa King Mswati mavazi wanayovaa ni nusu uchi kabisa tena mbele ya Mfalme wao mpaka matiti yakiwa nje na huo ndio utamaduni wa Mwafrika tangu kale, wazungu wamechukua kwetu na Leo mnafikiri tunawaiga wao. Mwanamke mvuto bila mwanamke kwenye kazi ya Sana'a mambo haya nogi na ndio maana ukiwa na mke unatamani awe mtupu muda wote ule maisha ya mahaba lakini utupu wa kwenye video ni wa maigizo tu kuvuta watazamaji na ndio maana hawaachii kila kitu.

Mziki ni mvuto na inategemea unafanya mziki wa aina gani na una lenga jamii gani, Mziki wa bongofleva ni mziki unaofikisha ujumbe kwa vijana na mavazi lazima yaendane na ujana, kama ni nyimbo za asili nazo zina mavazi yao na aina yake ya watazamaji, na ndio maana kuna vipindi tofauti redioni kulingana na rika, kama tunataka mziki wa kuuza uswahilini basi tusikilize ushamba lakini kama tunataka mziki wa kimataifa basi lazima twende na wakati na mazingira ya Globolaizesheni.

Kazi njema Viongozi wa Awamu ya Tano.

Deogratius Nalimi Kisandu.
25 Desemba 2017.
 
usasa mbona hamtembelei mikono badala ya miguu!! Kongole kwa raisi magufuri kwa kupiga vita picha za uchi ...vijana wangapi Leo hii wamekuwa mateja wa puli na kujichua kutokana na hiyo mnayoita "globalization" kwa nini mwanamke awe ni kiumbe dhwalili ktk huu uso wa dunia? hivi na waislamu pia mtampinga raisi kwa hili? Wallah Mimi ni muislamu wa kwanza kusema hadharani na kumuunga mkono raisi wetu ktk hii vita ....mtu anaangalia mziki sijui ndo diamond Mara kamshika kiuno mwanamke aliyevaa chupi tu sa ndo nini? maadili kwanza siasa baadae
 
Ukiwa mjinga ni mjinga tu. Rejea utamaduni wa mwafrika kabla ya Ukoloni.
 
Nimeamini kuna watu wamejipanga kupinga kila kitu toka kwa jpm.Sikuwahi waza mtu kuja kuwatetea wasanii wanaovaa vibaya kwenye video.Kama huo ni utamaduni wa mwafrika kwanini utamaduni huo hawaudumishi mitaani?Ni kweli Great thinker anaweza andika upuuzi ka huu wa mtoa mada?dah
 
Wewe bado kinda sana, fatilia Afrika ndio utajua ukweli halisi.
 
Hivi mnaosema kuvaa nusu uchi ni utamaduni wa Mwafrica hamuoni hayo yalitokea kwa sababu ya uduni wa teknolojia.......kama ndivyo basi tungeacha kuiga elimu,dini,sanaa nw vitu vingi tu toka kwa wazungu tukabakia na vyetu mkaendelea kusisitiza eti ni utamaduni acheni uzwazwa usiokuwa na maana!!
 
Back
Top Bottom