Mavazi ya taifa hutengenezwa kwa kamati au ni utamaduni wa jamii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mavazi ya taifa hutengenezwa kwa kamati au ni utamaduni wa jamii?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JOE58, Jan 28, 2012.

 1. J

  JOE58 Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mavazi kama ilivyo ngoma,vyakula,lugha mila na desturi nk ni moja ya tamaduni za taifa au jamii yoyote.Huzuka kutegemea maendeleo ya kiuchumi, kimazingira,kijamii. hayatungwi wala hayapangwi. ukomavu wa taifa ndio hukomaza utamaduni wa jamii.Jamii changa kama tanzania yenye miaka 50 huwezi kulinganisha na jamii zilizo sheheni karne nyingi.vazi la taifa sio jezi ya timu ya taifa wala bendera, kwamba wala hukaa na kubuni(design), jinsi utakavyokuwa. leo kichekesho tunavamia mambo eti kamati ya kubuni vazi la taifa WAPI IMEWAHI KUTOKEA.nani alitunga lubega, kanzu hijab,baibui, kente, tartan, suti? nielewesheni au ndio kutafuvumbuzi mpya? au lula hela ?:lol::lol:
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  hata wanakamati ni sehemu ya utamaduni. Pia kamati inaratibu tu lakini maoni ni ya wananchi. Hata hivyo haimaanishi kuwa nawaunga mkono
   
 3. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Aah, fomula ya maisha imebadilika ndugu yangu. Itafikia siku ukitaka kuoa italazimu upigiwe kura. Au umesahau juzi hapa tuliambiwa tuupigie kura mlima wa wachaga uwe wa ajabu?!
   
 4. m

  macinkus JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  sisi ni wa kwanza duniani kuunda kamati ya vazi la taifa. Pia ni njia moja wapo ya kugawiwa posho kwa wateuliwa wa hiyo kamati.

  macinkus
   
 5. mshana org

  mshana org JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 2,102
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  taifa la tanzania kila siku kutafutiana ugali yani ccm niwabovu mpaka kufikiria.vazitu limeundiwa tume na wameanza mchakato tangu 2004 mpaka leo hawazi mambo ya msingi eti wanawaza vazi la taifa
   
 6. R

  RIZIKI JUMATATU Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vazi la taifa sio kitu cha kufungia watu ndani ili wabuni watanzania tutokeje! Kama tunataka kutambulika kama watanzania tunapokuwa katika viwanja vya kimataifa kuna vitu vingi tu vinaweza kututambulisha na sio nguo ulizovaa mf: Utawala bora na wa kidemokrasia, kuzingatia haki za binadamu, kupinga rushwa na ufisadi(Pagumu hapo) kupunguza zigo la umasikini na njaa vinavyotuandama nk. Mi nawaambieni tunaweza kupata hilo vazi na watu wasilivae aidha kwa kuona aibu kwa kutoka nchi yenye sifa mbovu ua kukosa uzalendo.
  Halafu nimesikia kamati inakaribisha mawazo na ubunifu kutoka kwa wadau mbalimbali kwa sharti kwamba ubunifu wako uwe na rangi ya Bendera ya Taifa. Sasa mimi nashindwa kushangaa nini kazi ya bendera ya taifa? na kama tutakua tumeivaa kama shati au bilauzi hapo tutakua tumevaa vazi la taifa au bendera ya taifa?
  Mimi naona tujitazame upya na tuanze kutafuta mambo ya msingi kama vile ni jinsi gani tutamkomboa mwananchi na maadui watatu wa Mwalimu Nyerere na sio kutafuta vazi la taifa ambalo kwa sasa linatugharimu rasilimali zetu nyingi bila faida yoyote.
  Kama vazi la taifa lilikua la msingi na maana kwa nini lingoje mpaka tumefikisha miaka 50? Pili mavazi ni kiungo kimojawapo kinachoelezea utamaduni wa taifa husika sasa hili vazi tunalotaka kulitunga sasa hivi litaelezea utamaduni upi? Tatu kama tulishindwa kitu kidogo cha kuhamishia makao makuu ya serekali Dodoma tutawezaje kuwalazimisha viongozi wetu waache kunyonga suti zao za bei ghali walizonunua kwa fedha za ufisadi na rushwa wavae nguo yenye marangi rangi mengi?​
   
 7. terabojo

  terabojo JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Binafsi ninashauri watanzania waruhusiwe kujitambulisha kwa kutumia bendera ya taifa kupiti sakafu/vitambaa/pin za kubandika katika nguo waizovaa.
   
 8. S

  Stv Mkn JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 237
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hili suala la vazi la taifa kuundiwa kamati,nafikiri kuna mapungufu mengi hapa.
   
 9. f

  freakshow Member

  #9
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Inaonesha uwezo mdogo wa kufikiria wa waziri aliyeanzisha mchakato,culture ndio inatoa mambo kama mavazi n.k na you develop your culture through everyday living that eventualy you see vazi flani is acceptable on a very involuntary basis by the whole comunity!unles huyu waziri is one among many who we can consider 'dumb',this thing is a failure all along!embu tuelekezeni resources zetu kwenye mambo yenye tija kiutamaduni wetu,na sio this peace of rotten idea!
   
Loading...