Mavazi ya Nyerere na kuiga kutoka China

Uzuri au ubaya wa Nyerere siyo mada ya thread hii, inalenga kuimarisha umuhimu wa watu kutumia rekodi sahihi za matukio mbalimbali bila kuyageuza kwa nia ya ama kumsifia au kumdhalilisha mtu yeyote kwa namna yoyote ile.

Thanks Kichuguu. Nimekuwa mara kadhaa nikijiuliza bila majibu, inakuwaje gazeti la watu makini kama Raia mwema kuchapisha makala mbofu mbofu za upotoshaji zinazoandikwa na huyu Mjengwa? Makala zake zinafaa sana kwenye vile vijarida vya Global publishers.
 
Asante Kichuguu kwa kunipa somo tena kuhusu mavazi ya mwanasiasa nguli tz, afrika na duniani (asiyewasifu wakwao ni mtumwa)..mimi sina shida hata mtu akishikilia kuwa Mlw. aliiga..ndiyo aliiga mambo mema kwa ajili ya watu wake na nchi yake, mbaya ni kuiga mambo yatakayowaangamiza watu wako...hata ktk habari ya uchumi wakati wa Mlw. kulianzishwa viwanda vingi tu nchini hasa viwanda vya nguo ambavyo tungekomaa navyo bila kukata tamaa yamkini tungekuwa tunazlisha nguo zetu na kwa soko la A. Mashariki, ndiyoo mbona bia yetu inatamba sasa..tungeyafanyia kazi mawazo ya Mlw. (yale mazuri) nina imani tusingekuwa hapa leo..
 
Kuna picha ya Nyerere akiwa na suti isiyo na kola kabla ya February 1965?

Watu wengine mnasomaje habari. Yaani ubongo wako unachagua ni habari ipi ya kusoma na ipi ya kuacha? Unataka kuniambia kuwa hukuiona picha hii hapa?

attachment.php
 
nyerere aliokuwa swahiba mkubwa wa MAO ... Nyerere ndiye raisi anayeongoza africa kwenda kukutana na MAO... nasikia waLIKUWA MASWAHIBA KIASI KWAMBA HADI WALITAKA WAFANYE PROJECT FLANI KUTENGENEZA KIZAZI REMIX MCHINA & MBONGO ....
 
...Yaani ubongo wako unachagua ni habari ipi ya kusoma na ipi ya kuacha? Unataka kuniambia kuwa hukuiona picha hii hapa?

attachment.php

Labda ni kweli ubongo wangu una matatizo. Nionavyo, Nyerere amevaa kaunda suti yenye kola.

Tuna kigezo kingine cha kuhitimisha kuwa Nyerere alikuwa anavaa suti hizo zisizo na kola kabla ya Februari, 1965?
 
Labda ni kweli ubongo wangu una matatizo. Nionavyo, Nyerere amevaa kaunda suti yenye kola.

Tuna kigezo kingine cha kuhitimisha kuwa Nyerere alikuwa anavaa suti hizo zisizo na kola kabla ya Februari, 1965?
Je wote hapo kwenye picha hiyo wamevaa mashati yenye kola au ni Nyerere tu mwenye kola
 
Je wote hapo kwenye picha hiyo wamevaa mashati yenye kola au ni Nyerere tu mwenye kola

Mkuu pamoja na kazi yote uliyofanya kuweka the recodz straight na some fact tena kwa picha bado hakieleweki!!!!!! Hivi kweli kuna siku taifa hili na sisi tutaenda kutalii in the outer space?
 
Ngua zile hazikuwa na uhusiano na China: si ujamaa wala TAZARA iliyosababisha nguo zile, ilikuwa staili iliyobuniwa hapo Magagoni tu

Mkuu,

I think Mjengwa might be misleading people by mention only the male dress that it was copied from China. He should have known that the collarless suit was designed together with Kitenge wraparound and headscarf for women. If Nyerere did copy the suit from China, then where did he copy the Kitenge wraparound and the headscarf? Did Chinese women used to wear Kitenge wraparound and the headscarf? Otherwise, his article is biased if not discriminatory. Look at Mama Maria Nyerere (right) dress in the photo below. Was this copied from China as well? If not where?

samora.jpg



Again, look at how Tanzanian women use dress during that period in the photo below. Full Kitenge wraparound and headscarf. Where were these copied. China?

ctc_04_img1072.jpg


And what about this one?

nye.jpg


Nyerere administration designed the both the male and female dress as an attempt to install a sense of cultural identity in Tanzania through a national dress. However, the colourful Kitenge wraparound and headscarf for women, and for men, a suit similar to the collarless one worn by the former Chinese Prime Minister Chou en-Lai, did not go down well with the people. Some have even said that some of both male and femele outfits had the national flag sown on the breast to symbolise Tanzania's national identity.

The designers were each awarded TSh1.5 million in prizes but even government and ruling party high officials seemed unexcited by the new outfits. Mkapa himself favoured Kaunda suit at home but Western suit when travelling abroad. Most of the rest of the male apparatchiks went for Western suits even under the hot sun. Interestingly, our current leaders have come up with a new suit: The East African: *- Magazine*|Have you seen the president
 
Mkuu Kichuguu Shikamoo kwanza, kila nikiona post yako lazima nitoke na kitu, Wazee wetu wa zamani msichoke kutujuza sisi vijana wa dotcom juu ya historia ya nchi yetu.
 
attachment.php



Je wote hapo kwenye picha hiyo wamevaa mashati yenye kola au ni Nyerere tu mwenye kola

Hayo mengine ya Kambona kavaa nini, Kawawa kavaa nini, si mada yetu kwa kweli, mwali wetu hapa ni mavazi ya Nyerere.

Lakini kwanza nikushukuru, Kaka, kwamba tumekubaliana kuwa Nyerere hajavaa suti ya kichina kwenye hii picha ya 1964. Kumbe ukweli ni kuwa tunamwona Nyerere na suti ya kichina wakati, na baada ya, safari ya Uchina.

Tuendelee na utafiti wetu, lakini kwanza, kama ilivyo ada ya muungwana, tumuombe msamaha Mjengwa kwa shutuma zako kwamba "JF imedanganywa na Mjengwa" na kuwa "hakusema ukweli." Tukipata vidhibiti vipya basi tutaenda kumhukumu.

Binafsi nikushukuru kwa dhati kwa kuvumilia matatizo yangu ya "ubongo" na kushindwa kusoma habari, lakini naamini kwa pamoja tutaweza kudadavua mchele ni upi na mchanga ni upi, au yupi.
 
Nadhani maelezo hayo yanasaidia kuulewesha umma hasa wa wale waliozaliwa miaka ya karibuni kutambua kuwa lile vazi lislokuwa na kola la Nyerere halikuigwa na wala halikuwa na uhusiano wowote na China. Hatujui nani aliyelibuni lakini kwa vyovyote ni vazi lililobuniwa hapa hapa Tanzania kwani hakuna sehemu nyingine duniani lilikowahi kuvaliwa.
Pole pole mkuu nadhani uzalendo unaweza kutufanya tukawa blind ......

In the early Beatle-mania years, The Beatles would occasionally wear black, and then later grey, Edwardian collarless suits.[SUP][9][/SUP][SUP][10][/SUP] This style of suit was adopted from the Mod youth cult, then at its peak in the UK.[SUP][11][/SUP] These suits (instead of leather trousers, plaid shirts, and slacks) became extremely common for new bands to wear after 1964.
Mkuu nadhani inabidi tuwape hawa jamaa credit ya collarless suits..., na sio invention iliyotokea Tanzania
beatles5990.jpg
 
Thanks Kichuguu. Nimekuwa mara kadhaa nikijiuliza bila majibu, inakuwaje gazeti la watu makini kama Raia mwema kuchapisha makala mbofu mbofu za upotoshaji zinazoandikwa na huyu Mjengwa? Makala zake zinafaa sana kwenye vile vijarida vya Global publishers.

Mkuu,
Kama unaliona raia mwema hivyo basi hakuna gazeti lingine makini.Bora Raia Mwema wanaandika makala wanakosea kuliko wale wanaojadili umbea na kupotosha.Raia Mwema lina wandishi mahiri sana kwa kweli.Nimesoma makala ya Jenerali ulimwengu juzi haina kifani

Tuendelee na mjadala.Kichuguu asante sana kwa kuweka record straight
 
Raia Mwema lina wandishi mahiri sana kwa kweli.Nimesoma makala ya Jenerali ulimwengu juzi haina kifani

Bw Ben,
Nakubaliana na wewe kuwa Raia mwema lina waandishi mahiri kama Ulimwengu, Mihangwa, Karugendo nk. Binafsi siamini kuwa Mjengwa ni miongoni mwa waandishi hao mahiri. Let's agree to disagree on this one.
 
Nyerere kuna mambo mengine zaidi ya mavazi ambayo ametohoa - natumia neno kutohoa kwa kutaka kutofautisha na kuiga- kutoka China. Vijiji vya Ujamaa na mbiu za "Zidumu Fikra bora za Mwenyekiti" ni mifano miwili tu.

Ukisoma habari zote za "Siasa Ni Kilimo" (how many read these?) halafu ukaangalia "The Great Leap Forward" (that laughingstock of the Chinese) unaona mzee anafuata nyayo zile zile za Mao. But to take this as an example that Nyerere was in the pocket of the Chinese would be a mistake. Nyerere was much more complex than that.

Wengine wanasema kachukua kwa Lenin. Tena kuna wanaodai aliiga kwa Stalin. Rejea maelezo haya kutoka kwenye mahojiano yake:

"In a conversation with...Nyerere, the present writer (having previously read his writings) drew his attention to this particular passage from Lenin and what Lenin was striving to teach far back as 1923. The African leader said that he did not know it - he had arrived at his conclusion by himself and with his people" - CLR James (1969) on A History of a Pan-African Revolt
 
attachment.php





Hayo mengine ya Kambona kavaa nini, Kawawa kavaa nini, si mada yetu kwa kweli, mwali wetu hapa ni mavazi ya Nyerere.

Lakini kwanza nikushukuru, Kaka, kwamba tumekubaliana kuwa Nyerere hajavaa suti ya kichina kwenye hii picha ya 1964. Kumbe ukweli ni kuwa tunamwona Nyerere na suti ya kichina wakati, na baada ya, safari ya Uchina.

Tuendelee na utafiti wetu, lakini kwanza, kama ilivyo ada ya muungwana, tumuombe msamaha Mjengwa kwa shutuma zako kwamba "JF imedanganywa na Mjengwa" na kuwa "hakusema ukweli." Tukipata vidhibiti vipya basi tutaenda kumhukumu.

Binafsi nikushukuru kwa dhati kwa kuvumilia matatizo yangu ya "ubongo" na kushindwa kusoma habari, lakini naamini kwa pamoja tutaweza kudadavua mchele ni upi na mchanga ni upi, au yupi.

Kwenye hii picha hata kama angekuwa amevaa shati lenye kola ndefu kama masikio ya sungura, bado itakuwa ni jambo la kutia wasiwasi anapotuambia eti Nyerere alianza kuvaa suti zisizo na kola mwaka 1965 baada ya kuiga kwa Mao; wakati picha ya 1964 inaonyesha akiwa amezungukwa na mawaziri wenye hizo suti. By the way ni nini kinachokufanya u-conclude kuwa aliiga Uchina na siyo kwa hao mawaziri waliomzunguka?
 
Back
Top Bottom