Mavazi ya Nyerere na kuiga kutoka China | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mavazi ya Nyerere na kuiga kutoka China

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Jul 8, 2011.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hii thread siyo ya siasa sana bali ni katika kueleimishana; ninarekebisha jambo mojawapo ambalo haliliweki vizuri miongoni mwetu. Kama kuna anayeweza kunyoosha zaidi maelezo yangu kwa kujaza habari nisizofahamu, basi atujulishe zaidi.


  Maneno haya hapa chini niliyonukuu, nimeyasoma katika article moja ya Mjengwa anayoelezea mfarakano baina ya Nyerere na Kambona. Kwa vile hajamaliza mfululizo wa makala hizo, niliahidi kuwa akishamaliza mfululizo wake, mimi pia nitatoa mfululizo wangu kulingana na record zilizopo, siyo maoni yangu. Nilifanya utafiti wa kutosha kuhusu uhusiano baina ya Nyerere na Kambona baada ya mjadala fulani tulioufanya hapa mwaka 2007 ila sikuwahi kuiandika, na naona hii itakuwa nafasi nzuri kuweka rekodi hiyo hapa.

  Ninalotaka kuongelea leo ni hii tabia yetu ya kuchukua hisia zetu na kuzifanya kama ndiyo historia kamili badala ya kufuata rekodi sahihi. Huyu mwandishi mkongwe Mjengwa hakuandika ukweli hapo nilipowekea rangi kuhusu Nyerere kubadilisha mavazi na kuwa kama ya Mao Tse-Tung! Ninajua kuwa Mjengwa ni msomaji wa jamvi hili na hatakosa kusoma hii critique yangu. Hata hivyo nitaitumia nafasi hii pia kuwafahamisha wana JF ambao wanaweza kuwa wamedanganywa na hiyo article ya Mjengwa. Iwapo kuna mapungufu katika maelezo yangu, naomba mwenye kujua zaidi asaidie katika kunyoosha rekodi.

  Nyerere alipoanza kuvaa zile nguo zisizokuwa na kola yaani neckless shirts, hakukuwa na uhusiano wowote na ziara yake ya China ya February mwaka 1965, na wala hakuiga kutoka kwa Mao kama ambavyo wengi walidhania. Miaka hiyo kulikuwa na effort ya kutafuta vazi ambalo ni identity ya waafrika, na wanasiasa ndio walikuwa msitali wa mbele katika ubunifu. Vazi la kwanza kubuniwa na wanasiasa wetu lilikuwa ni blanket la kujifunika kama ambalo linaonekana kwenye official portrait ya Nyerere ya wakati huo kwenye picha ya hapa chini. Wanasiasa wengi barani Afrika walijifunika mablanketi hayo, ambayo nadhani muasisi wake alikuwa Kwame Nkurumah au Ahmed Sekou Toure. Zaidi ya Nyerere wanasiasa kadhaa wa Tanzania pia walijifunga mablanketi hayo, kwa mfano Nyerere, Kambona Lusinde, n.k

  [​IMG]

  Nyerere.png


  Pamoja na kuvaa hayo mablanketi, miaka mitano ya kwanza ya Nyerere madarakani alikuwa akichanganya mavazi ikiwamo business suit pamoja na hayo mablanketi hayo kulingana na mazingira. Kwa mfano picha ya cabinet yake ya kwanza ya mwaka 1962 na ile ya state visit yake Marekani mwaka 1963 alikuwa amevaa business suit kama zinavyoonekana hapa.
  [​IMG]
  Nyerere1962.jpg
  [​IMG]
  nyerere_in_usa_1963-1_.jpg

  Ingawa siku ya Muungano bado alivaa business suit wakati wa kumkribisha Karume na wakati wa kubadilishana hati za Muungano kama inavyoonekana hapa chini, ni katika kipindi hicho hicho cha muungano ndipo alipoanza kuvaa hayo mashati ya neckelss kama inavyoonekana kwenye picha ya cabinet yake ya kwanza ya mwaka 1964 hapa chini kabisa

  Official portrait ya Rais Nyerere iliyotolewa wakati huo huo inamwonyesha wazi akiwa amevaa hicho kineckless kama invyoonekana hapa chini. Hata Kawawa na Karume pia walikuwa wamevaa hizo neckless shirts kwenye official portarits zao za mwaka 1964.

  [​IMG]

  president_julius_nyerere.jpg  Kipindi hicho cha mwaka 1964 matumizi ya mablanketi kama nguo ya kiafrika yalianza kupungua sana na viongozi wengi wa Afrika ya Magharabi, ambayo ilitangulia kupata uhuru walikuwa wakivaa zaidi aina fulani ya kanzu ambazo ni kama jadi yao, na leo hii kanzu hizo zimekuwa maarufu sana kama nguo za kiafrika. Kanzu hizo hazikuwa na kola ( neckeless), kwa mfano nguo alizovaa Sekou Toure, Tafawa Balewa na Azikiwe kama ilivyo hapa chini hazina kola.

  [​IMG]

  sekou toure6.jpg
  Sekou Toure


  [​IMG]

  _48919961_balewagetty.jpg
  Tafawa Balewa

  [​IMG]

  Azikiwe.JPG
  Nnandi Azikiwe.


  Kwa hiyo, ingawa hatujui ni lini Nyerere na viongozi wenzake wa Tanzania walianza kuvaa hizo nguo za neckless, ni wazi kuwa alianza kuzitumia kabla au mara tu baada ya Muungano, April 1964 lakini ikiwa kabla hajasafiri kwenda China mwaka 1965. Kuna uhusiano wa karibu sana katika uamuzi huo wa kuvaa mashati neckless na zile kanzu neckless walizokuwa wakivaa "wanamapinduzi wa Afrika wakati huo", ambao wengi wao walikuwa huko Afrika ya Magharibi.

  Wakati Nyerere anatembelea China mwezi Februari mwaka 1965, tayari alikuwa amevaa shati hilo neckless kama anavyoonekana hapa wakati wa kusalimiana na Mao. Utamwona Nyerere alikuwa bado ni kijana lakini amevaa hicho ki-neckless chake.

  [​IMG]

  Nyerere+Mao-1965.jpg


  Na hata kwenye picha aliyopiga na Charles De-gaule mwezi June mwaka huo huo 1965 hapa chini, unamwona Nyerere amevaa kineckess chake. Baada ya Nyerere kutoka China, sinema iliyohusu ziara yake huko China haikutoka mpaka mpaka mwishoni mwa mwaka 1965 akiwa tayari amesharudi kutoka ziara nyingine ikiwamo hii ya Ufaransa.

  [​IMG]

  nyerere_with_de_gaule_1965.jpg


  Aliendelea kutumia nguo hizi za neckless mpaka mwanzoni wa miaka ya sabini ambapo alianza kuvaa nguo zenye kola ambazo zilijulikana katika kipindi fulani kama Nyerere suit (kama kushindana na Kaunda suit za wakati huo.) Kuanzia hapo Nyerere akawa anachanganya hizo neckless suits, na hizo Nyerere suits zake. Mfano wake ni kama ionekanavyo hapa chini.  Nimeshindwa kupata official portrait ya Nyerere baada ya kupunguza matumizi ya neckless suits (yaani kwenye website ya ikulu hakuna kumbukumbu yoyote inayohusu maraisi wa zamani wa Tanzania. Afadhali website ya waziri Mkuu ina rekodi za mawaziri wakuu wa nyuma wote, lakini Ukulu dah!!) Portrait hiyo inafanana na hiyo picha iliyochorwa juu ya lango la kaburi lake hapa chini


  [​IMG]

  0002bsdx.jpg


  Aliendelea kuchanganya matumizi ya hizo Nyerere suits na Neckless suits hadi mwishoni wa maisha yake.


  Mao alikuwa havai mashati yasiyokuwa na kola. Nguo za Mao pamoja na viongozi wote wa china zilikuwa zimeshonwa kuwa kama za kijeshi kama anavyoonekana hapo chini zikiwa na kola kubwa ya kutosha au ndogo ndogo lakini inayoweza kuwekwa nembo za kijeshi ikiwa lazima, kama anavyoonekana hapa chini.

  [​IMG]

  Mao.jpg

  [​IMG]

  mao-tse-tung.jpg


  Hata waziri wake mkuu, Chou En-Lai ambaye jina lake lilitumika kuziita hizo nguo neckless za Nyerere, pia alikuwa akivaa nguo zenye kola tu, kama anavyoonekana hapa chini.

  [​IMG]

  Chou-en-lai.jpg  Unaweza kuona tena katika ile picha ambayo Mao aliyopiga na Nyerere mwaka 1965 hapo na juu na ile aliyopiga naye tena mwaka 1972 pia hapa chini kuwa Mao alivaa shati lenye kola wakati Nyerere akiwa na shati lislokuwa na kola.

  [​IMG]

  Nyerere+Mao-1974.jpg


  Ukiangalia tena kwa karibu zaidi, utaona kuwa kuna tofauti kubwa sana baina ya Neckless za Nyerere na zile nguo za wachina kama inavyoonekana katika hii picha ya Sokoine akiwa na waziri mkuu wa China.

  [​IMG]

  Sokoine.JPG

  Nadhani wanasiasa wengi wakongwe Tanzania kama akina Mzee Malecela na Msuya ambao wamekuwa wakiendelea kuyavaa mashati yao neckeless freeely bila kuyaonea haya kwa vile nadhani wanajua wazi kuwa hawakuyakopi kwa Mao.

  [​IMG]


  MALECELA.jpg
  Nadhani maelezo hayo yanasaidia kuulewesha umma hasa wa wale waliozaliwa miaka ya karibuni kutambua kuwa lile vazi lislokuwa na kola la Nyerere halikuigwa na wala halikuwa na uhusiano wowote na China. Hatujui nani aliyelibuni lakini kwa vyovyote ni vazi lililobuniwa hapa hapa Tanzania kwani hakuna sehemu nyingine duniani lilikowahi kuvaliwa. Watu walioiga mavazi ya China kwa hapa Afrika labda ni pamoja na kwame Nkurumah, na Mengistu Haire Mariam kama wanavyoonekana hapa chini.


  [​IMG]
  in_zachary11_ph.jpg
  [​IMG]
  Mengistu_Haile_Maria_29605t.jpg

   
 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Mbona sijamwona Malecela maana naamini naye ni mwanzilishi wa kaunda suti zisizo na kola.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu kichuguu naona umetoa elimu swafi kabisa kuhusu hii myth! I am just wondering kwa nini uongo ule ume-exist for decades kwamba baada ya JFK kufariki, Nyerere akaenda China aliporudi ndiyo akaja na hizo neckless suits na siasa ya ujamaa na kujitegemea.

  Thanks again for setting the records straight!
   
 4. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good Job!
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Si lazima u copy tena habari yote hasa ikiwa ndefu.
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nimeupdate post na kuongeza ya Melecela!!
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kichunguu

  Unasema Mzee Malecela na Msuya wanaendelea kuyavaa bila ya kuyaonea haya kwa kuwa wanaelewa hayajakopiwa kutoka China. Hivi yangekopiwa kutoka China kungekuwa na sababu ya kuyaonea haya?
   
 8. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Nimeona mkuu maana hao ndio wahafidhina wa siasa za Mao Tse Tung walikopi vijiji vya ujamaa hadi mavazi.
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Kichuguu hilo vazi halikubuniwa Tanzania limekopiwa kutoka China na Korea.
   
 10. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kichuguu katoa maelezo wazi na yanayojitosheleza kwa mifano halisi. Nashukuru sana kwa elimu yake hiyo. Sasa wewe ndugu yangu kama unaona vinginevyo toa pia nawe uthibitisho wako-ndo kazi ya great thinkers. Leo nimeelimishwa sana na maelezo ya Kichuguu juu ya mavazi haya.
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Sawa katoa maelezo mazuri je yanajitoshereza kwa asilimia ngapi hata yeye kasema hajui aliyelibuni
  kama hajui aliyelibuni kuna wanaojua yeye kaongelea mavazi ya China hajaongelea mavazi ya Korea na Japan kwa wakati ule.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Korea ipi? ni vizuri kuonesha japo mfano...
   
 13. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #13
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hapana, hilo siyo vazi la wachina wala la wakorea! Korea ya kusini, kama ilivyo Japan wao wamekuwa wakivaa business suit tangu baada ya vita ya dunia. Korea ya kaskazini wenyewe wamekuwa wakivaa kama wachina kutokana na ukomunist wao, ingawa huwa wanachanganya  na business suit pia. Nguo traditional za watu wote wa eneo hilo ni ile aina inayojulikana kama kimono katika kijapani, na haifanani kabisa na hizo neckless suits za Nyerere. Kimono ni kama nguo ambazo umeona wanavaa wanafunzi wa Karate, za aina ya Goju Ryu na Kae Kwon Do.
  [​IMG]

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Baada ya ujamaa kuzikwa nadhani asingependa kuyavaa kulingana na nadharia kuwa ujamaa na mavazi yale yaliigwa kutoka China
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Duh!!!!! hii picha ya chini unaweza kusema ni photoshop from the myths that have been around!!!!!! Mkuu kichuguu nakupa tena kudos!
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,103
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kichuguu,

  ..asante sana. kwa kweli umetufumbua macho wengi.

  ..hii imenikumbusha post yako nyingine iliyohusu sarafu zilizowahi kutumika hapa kwetu.
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Nyerere kuna mambo mengine zaidi ya mavazi ambayo ametohoa - natumia neno kutohoa kwa kutaka kutofautisha na kuiga- kutoka China. Vijiji vya Ujamaa na mbiu za "Zidumu Fikra bora za Mwenyekiti" ni mifano miwili tu.

  Ukisoma habari zote za "Siasa Ni Kilimo" (how many read these?) halafu ukaangalia "The Great Leap Forward" (that laughingstock of the Chinese) unaona mzee anafuata nyayo zile zile za Mao. But to take this as an example that Nyerere was in the pocket of the Chinese would be a mistake. Nyerere was much more complex than that.

  Zaidi ya hayo - on the subject of kuiga/ kutohoa-, Nyerere, pamoja na uzuri wake wote. Alikuwa na tabia ya kutoa mambo kwa watu na kuya present kama yake.

  Katika hotuba ya Tangazo la Vita dhidi ya Iddi Amin pale Diamond Jubilee Hall kwa mfano, sehemu inayokumbukwa sana ni pale aliposema "Nia tunayo, uwezo tunao, sababu tunayo" etc. Watu wengi wanafikiri haya ni maneno ya Nyerere originally, actually haya ni maneno ya bendi moja ya Kiingereza wakati wa vuguvugu la Uingereza kutaka kuingia vitani dhidi ya Hitler.

  But some would say this is retrospective judging, using a different yardstick influenced by our zeitgeist.

  While others would say Nyerere was learned and that he should have known better than to pose as the originator, and that scholastic/ statesman's accreditation is not a thing of our zeitgeist.

  Bottom line, Nyerere was much more complex person than to be pigeonholed according to his dress. While he was left leaning, he was also an influential leader of the Non-Alignment Movement, a patron of the Dar-es-salaam Buddhist Temple, devout Catholic, and a great friend of JFK and Chairman of the South-to-South Commission.

  So if you inferr that Nyerere was a Communist or Communist influenced because of his dress, some could equally say that Nyerere was working with the Kennedy administration to contain the spread of communism in Zanzibar (Karume was very much influenced by Communism, just look at the names of Zanzibari Schools and Hospitals) and that was part of the original reasons for "Muungano" and why "Makomredi" walitimuliwa.

  Nyerere was more influenced by his African upbringing and Scottish/ Fabian society Socialism while at Edinburgh than any Eastern type of communism. Why do you think he kept Joan Wickens at Ikulu for all those years ?
   
 18. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Maneno mengine ya kuiga ya nyerere ni haya: Tanzania haitakuwa huru mpaka Africa nzima iwe huru. Haya ni maneno ya Raisi wa marekani mwaka 1963 JF Kened alipokuwa nawatetea haki za wamarekani weusi. American can not be free not until all black people are free. Halafu maneno kama Nitaona haya kumuonea haya mzebe na mzululaji. Haya aliyakopi kutoka mao Tsedong wakati alipokuwa nawakama kamata wazururaji mijini na kuwafunga mashambani kama watumwa. Jamani mano mtetea nYerer tuambieni ni mafanikio gani kiuchumi katuletea ambayo kamshinda hata kenyatta? utaona hakuna ila yeyey ni jina kubwa Non alignmnet na South South commissio, au siyo?
   
 19. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Umetupa ufafanuzi wa kutosha, asiye elewa ni mgumu wa kuelewa na mwepesi wa kusahau.
  Je watanzania watajifunza au wataiga nini toka kwa JK wa sasa?
   
 20. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kweli JF ni kisima cha maaarifa... Thanks kwa research on this subject, maana wengi walisha lishwa sumu for decades.
   
Loading...