Mavazi mabaya kwa mabinti na unywaji wa pombe

Guled Omary

Member
Nov 29, 2015
6
1
Uvaaji wa mavazi mavazi mabaya kwa mabinti na akina mama pamoja na unywaji wa pombe ndio chanzo kikuu cha maambukizi ya UKIMWI.

Serikali haikuwa na haja ya kufanya kampeni ya uvaaji mipira na kuwa na mpenzi mmoja bali ingetosha kusisimamia vyema mavazi ya hekima kwa jinsi zote pamoja na unywaji pombe kwani pombe ndio funguo ya maasi yote.

Ujumbe huu unaunga mkono kauli ya mama Samia kupiga marufuku mavazi yaliyo kinyume na maadili ya jamii hususani akina dada na akina kaka.
 
mavazi na ukimwi??
kishawishi cha kwanza ni pale macho yanapoangalia umbile la mtu jinsi lilivyochongwa kwa kubanwa na mavazi aliyovaa, hivyo kutokana na ushawishi huo fikra huanza kujengeka na matamanio hupatikana hatima yake ni zinaa inachukua mkondo wake.. lakini endapo mtu atajiweka mbali na mavazi yasiyo onesha maumbile yake atakuwa amejiweka mbali na kumshawishi mtu mwingine na kuwa sababu ya kupunguza kama si kutokomeza maambukizi ya ukimwi....
 
mavazi na ukimwi??


NDIO! SANASANA MAVAZI YANAOONYESHA NUSU YA MWILI UCHI !..

UNAWEZA UKABAKWA NA MTU MWENYE VIRUSI HUTOPATA UKIMWI ?

ATAKUJA MTU ATASEMA MBONA WAOVAA VIZURI WANABAKWA ..

JIBU NDIO..

LAKINI TUANGALIE STATISTICS ...
 
Jamani tuache kutafuta vijisababu. Nguo kama vazi havitazuia mtu kungonoka. Tokeni nje mkang'aenga'e macho kwingineko. Dunia sasa kijiji hata mngewavika baibui wote. Kama tamaa zako unaziachia tu na hazifugiki baasi ngono ni lazima.
Badiliko la fikra litatusaidia zaidi. Hebu fikiri, madaktari wangebaka wangapi? Tubadili fikra zetu ndo usalama wetu. Si kila mwanamke akipita mbele yako, tiyari mpango wa kungonoka unaanza kichwani. Tutaangusha wangapi?
Sereekali inapoteza fedha za kigeni kuagiza kondom, sasa walioltewa wanasema ati hakuna raha ukivaa. Badilini fikra, wazeni kujenga taifa na haswa familia. Fikiria, watoto wako umewaachaje, weye na umri mdogo hivyo?
 
Hivi wabongo tunaweza kweli kuishi majuu? Ama kweli Trump ni nabii. Nilikuwa nawaza tu!
 
Back
Top Bottom