Mauzo ya katani yanauzwa kwa tani au kwa kilo?

Remmy Nkwera

New Member
Sep 6, 2016
3
6
Wanajamii naomba kuuliza, mauzo ya katani yanauzwa kwa tone au kwa kilo? Na kwa sasa hivi zao la katani linalipa?

Naomba msaada wenu.

======

Inauzwa kwa tani, inafungwa katika marobota ya kilo 100 au 200 au 250. Kwa sasa inauzwa kwa Tsh 2,600,000/= hadi millon 3. Kwa sasa upatikanaji si mkubwa sana, unahitaji kusubiri wakukusanyie. Kuna wakulima wadogo unaweza kupata tani moja hadi tani 5. Wakulima wakubwa wanaweza kukupaTani zaidi kulingana na mahitaji na bei yako. Wakulima wakubwa unapata Pangani, Mkinga, Korogwe, Hata hapa Tanga Mjini.

Mashamba mengi sana yametelekezwa sema sasa hivi, kama utahitaji shamba ulime unanda TSB au katani LTD wao wanakupa utaratibu unaofaa na wakati mwengine ukibahatika unapewa shamba bure ulime.

Changamoto za hili zao ni ugonjwa unajulikana kama KLF au kwa kirefu ni Korogwe leaf spot

Kama umewahi kuyachunguza majani ya mkonge, utaona mostly yana kama ugonjwa flani hivi either wa maduara au jani linakua na mabaka mabaka ndio hiyo inajulikana kama korogwe leaf spot huu ugonjwa ni changamoto kwa wakulima wengi sana maana ukikata jani lenye huu ugonjwa likienda kuchakatwa kwenye korona hayo mabaka yanajishika na nyuzi.
 
Wanajamii naomba kuuliza, mauzo ya kkatani yanauzwa kwa tone au kwa kkilo? na kwa sasa hivi zao la katani linalipa?Naomba msaada wenu.
Sijui wanapimaje ila linalipa balaa, soko lake hata hapa Tanzania na Kenya lipo pia wanauza Japan, India, Yemen, Spain, Ethiopia, German, Italy, Belgium, Holland na France

- Mo Dewji ana mashamba makubwa sana ya mkonge huko Tanga na pia ana kiwanda cha katani ( Nyuzi Moshi ), 21 CENTURY HOLDINGS LIMITED
 
Remmy Nkwera naomba nikusaidie kidogo palipobakia mwengine atajazia

inauzwa kwa tani. Inafungwa katika marobota ya kilo 100 au 200 au 250. kwa sasa inauzwa kw sh 2,600,000/= hadi millon 3. kwa sasa upatikanaji si mkubwa sana, unahitaji kusubiri wakukusanyie. kuna wakulima wadogo unawez kupata tani moja hadi tani 5. wakulima wakubwa wanaweza kukupaTani zaidi kulingana na mahitaji na bei yako.
wakulima wakubwa unapata Pangani, Mkinga, Korogwe, Hata hapa Tanga Mjini
 
ila daily mizigo yake bandari ya tanga inapigwa stop order labda wawe wamejirekebisha this time
(namsemea mo dewji)

mashamba yapo mengi sana kuna amboni plantation na amboni spinning mills, kuna sagera estates, mohammed enterprises, katani ltd, d.d. ruhinda & compnqy ltd, amboni ndo wapo pangani huko mwera sakura hayo n baadhi mkuu na n zao zuri linastahmili ukame hakihitaji kupandwa sehem yenye kutuama maji kama vile mpunga au sehem inayotiririsha maji , baada ya miaka yako mitatu had mitatu na nusu unavuna kama atahitaj anicheki nimuunganishe na tanzania sisal board wampe somo kabisa
 
Huwa naona Moro kuna mashamba makubwa ya mkonge yametelekezwa, sijui ni kwanini.
- Changamoto za hicho kilimo ni nini ?
 
unajua mkuu sio morogoro peke yake mashamba mengi sana yametelekezwa sema sasa hivi kama utahitaji shamba ulime unanda tsb au katani ltd wao wanakupa utaratibu unaofaa na wakati mwengine ukibahatika unapewa shamba bure ulime

changamoto za hili zao ni ugonjwa unajulikana kama klf au kwa kirefu ni korogwe leaf spot

kama umewah kuyachunguza majani ya mkonge, utaona mostly yana kama ugonjwa flani hivi either wa maduara au jani linakua na mabaka mabaka ndio hiyo inajulikana kama korogwe leaf spot huu ugonjwa n changamoto kwa wakulima wengi sana maana ukikata jani lenye huu ugonjwa likienda kuchakatwa kwenye korona hayo mabaka yanajishika na nyuzi
 
Dah, hauna tiba ?
 
Dah, hauna tiba ?
kuhusu tiba sana sana kuna dawa ya kupulizia mkuu na changamoto nyengine hawa tumbili sometimes nguruwe pori hua wana mtindo wa kuukata shina la mkonge na kulitafuna japo sio lote na kuna wadudu flani huvutiwa na ile nta inayopatikana kwenyebshina la mkonge lenye ladha ya asali so hua mara nyingi wanashambulia na inashauriwa pia kuna njia ya kienyeji me hua nasema hivo, unatafta shina ambalo halina kazi tena shambani yan limevunwa kiasi kwamba haliwez kutoa tena majani, unalipasua kati kati unalilaza pembezoni au mpakani mwa shamba karibu shamba zima usambaze kila hekta hawa wadudu watahama kutoka kwenye shina lemye uhai kuja hili jipya n kama mtego hivi so unalilaza kwa mda (sikumbuki vizuri almost kwa muda gani) ukimalizika muda huo unaligeuza tu na wadudu wote wanakua wamekufa)
 
Okay. Mambo yanaenda kumbe kama mtu akiamua kufanya kilimo hicho. Na ishtoshe soko lipo
 
Kilimo cha katani kilivyoangukani kielelezo cha Ujamaa kushindwa.

Kabla ya Azimio la Arusha, Tanzania ilishika nafasi ya kwanza kwa uzalishaji wa katani kama sikosei, tulifikisha mpaka tani robo milioni.

Baada ya Nyerere kutaifisha mashamba uzalishaji ulishuka sana.

Nyerere mwenyewe kuna siku alihojiwa,akaulizwa kamakuna vitu anajutia na angefanya tofauti,akasema utaifishaji wa mashamba, hususan katani,ulikuwa si uamuzi mzuri.

Wiki ya katani Tanzania ipo hapa Sisal production in Tanzania - Wikipedia
 
Okay. Mambo yanaenda kumbe kama mtu akiamua kufanya kilimo hicho. Na ishtoshe soko lipo
naomba nikutoe mashaka kabisa soko lipo tena bas ikiwa unataka kupanda hili zao, unaonana na washauri husika wanapatikana hapo tsb au katani ltd wapo tanga wote hawa na ofisi zao n jengo moja then kwa tsb ukienda huko watakupa elimu ndefu nzuri tu tuseme mathalani weww una shamba lako unataka kupanda sisal, utaenda tsb utapata ushauri ukibahatika kama shamba lako lipo tanga watakuja had shambani kwako watachek sample ya udongo wa shamba lako then tuseme ardhi yako haina shida utawaza nitapata wapi mbegu napo unarudi tsb (nikusaidie mbegu zipo za aina mbili kuna bullbills na suckers au maotea, bullbills ni mbegu zinazopatikana kwenye lile lingoti la mkonge hayabmaotea n yale yanayojiotea pembezoni mwa shina la mkonge, sasa ukiamua mm natumia maotea ya mkonge unaweza kuja pata hasara hapa utakuta maotea mengine makubwa karefu mengine madogo machanga so unakuta kwenye shamba lako muda wa mkonge n mfupi lakini tayar lingoti liko juu ujue maotea uliyotumia yalishapevuka na mkonge hukaa shamba hata zaidi ya miaka nane bullbills ndio mbegu bora mana huota kwa pamoja na shida ya hiz bullbils utakapotikisa lingoti mbegu zimwagike unatakiwa uandae kitalu pembeni had kwa muda flani ndio uhamishe shambani) haya umeshapanda mkonge wako miaka mitatu na nusu umelitunza shamba na mkonge wako unahaha soko unakuja tsb wao wanakupeleka mikononi mwa wanunuzi mnaelewana bei hapo n mkulima wa chini asiye na uwezo wa kuweka korona na kulisha korona yake sjui nimeeleweka?
na uzuri wa hili zao unaweza kupanda na mazao mengine kama mahindi
 
naomba nikutoe mashaka kabisa soko lipo tena bas ikiwa unataka kupanda hili zao, unaonana na washauri husika wanapatikana hapo tsb au katani ltd wapo tanga wote hawa na ofisi zao n jengo moja then kwa tsb ukienda huko watakupa elimu ndefu nzuri tu tuseme mathalani weww una shamba lako unataka kupanda sisal, utaenda tsb utapata ushauri ukibahatika kama shamba lako lipo tanga watakuja had shambani kwako watachek sample ya udongo wa shamba lako then tuseme ardhi yako haina shida utawaza nitapata wapi mbegu napo unarudi tsb (nikusaidie mbegu zipo za aina mbili kuna bullbills na suckers au maotea, bullbills ni mbegu zinazopatikana kwenye lile lingoti la mkonge hayabmaotea n yale yanayojiotea pembezoni mwa shina la mkonge, sasa ukiamua mm natumia maotea ya mkonge unaweza kuja pata hasara hapa utakuta maotea mengine makubwa karefu mengine madogo machanga
Shukhrani sana Madame S
 
Shukhrani sana Madame S
asante tupo pamoja

na kuna kitu nilitakankusahau kwenye changamoto za mkonge

upatikanji wa mashine za kuchakata mkonge na kifunga hasa kwa wakulim wadogo.
umeme wa uhakika au gharama za dizeli katika kusindika.
tija ndogo ya mkonge kutokana na kutofuata kanuni za kilimo,kodi mbalimbali z halmashauri na mamlaka zingine
 
Kwa Morogoro, tatizo hiki kilimo kimehodhiwa na wakulima wakubwa tu, nadhani ingetungwa sera ktk kila kwenye shamba kubwa, wananchi waruhusiwe kuzalisha makwao kwa ukulima mdogo,hawa wakubwa wanunue mazao yao toka mashambani na kwenda kuyachakata viwandani mwao, Kilombero sugar inafanya hivyo.
 
asante tupo pamoja

na kuna kitu nilitakankusahau kwenye changamoto za mkonge

upatikanji wa mashine za kuchakata mkonge na kifunga hasa kwa wakulim wadogo.
umeme wa uhakika au gharama za dizeli katika kusindika.
tija ndogo ya mkonge kutokana na kutofuata kanuni za kilimo,kodi mbalimbali z halmashauri na mamlaka zingine
Changamoto hizi zingemalizwa kwa wakulima wakubwa kuyanunua mazao toka mashambani mwa wakulima wadogo.
 
Uzi bora kabisa wachangiaji wanafunguka na watu wanauliza maswali yenye tija hongereni wote.
Uzi umejaa maarifa sio utoto wa watu wasio jitambua
 
Remmy Nkwera naomba nikusaidie kidogo palipobakia mwengine atajazia

inauzwa kwa tani. Inafungwa katika marobota ya kilo 100 au 200 au 250. kwa sasa inauzwa kw sh 2,600,000/= hadi millon 3. kwa sasa upatikanaji si mkubwa sana, unahitaji kusubiri wakukusanyie. kuna wakulima wadogo unawez kupata tani moja hadi tani 5. wakulima wakubwa wanaweza kukupaTani zaidi kulingana na mahitaji na bei yako.
wakulima wakubwa unapata Pangani, Mkinga, Korogwe, Hata hapa Tanga Mjini
hawa wakulima wadogo ni organised farmers au ndio kila mtu na lake....?
 
unajua mkuu sio morogoro peke yake mashamba mengi sana yametelekezwa sema sasa hivi kama utahitaji shamba ulime unanda tsb au katani ltd wao wanakupa utaratibu unaofaa na wakati mwengine ukibahatika unapewa shamba bure ulime

changamoto za hili zao ni ugonjwa unajulikana kama klf au kwa kirefu ni korogwe leaf spot

kama umewah kuyachunguza majani ya mkonge, utaona mostly yana kama ugonjwa flani hivi either wa maduara au jani linakua na mabaka mabaka ndio hiyo inajulikana kama korogwe leaf spot huu ugonjwa n changamoto kwa wakulima wengi sana maana ukikata jani lenye huu ugonjwa likienda kuchakatwa kwenye korona hayo mabaka yanajishika na nyuzi
haijagundulika dawa ya huu ugonjwa....?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom