Mauzo ya apartments Dar

MpendaTz

JF-Expert Member
May 15, 2009
2,185
884
Naomba ushauri maana nimetangaziwa Apartments zinauzwa na kampuni inaitwa Proin hapo Dar. Meneja wa Kampuni inasemekana ni mtajwa wa EPA. sasa ninawasiwasi wa kunigizwa mjini. Ushauri tafadhali kwa wale wenye kujua haya mambo. Apartments zenyewe ziko Tabata nazo ni former Sigara apartments.
Natanguliza shukrani zangu.
 
Mkuu hilo la kuingizwa mjini sijui lakini huyo jamaa najua alizinunua kihalali kabisa sasa suala la kuingizwa mjini labda uangalie na contract yenyewe
 
watembelee hapa www.prointz.com its OK lakini hakuna info za kutosha yaani kama kawaida ya biashara na kazi zinazofanywa na wabongo bado ni kulipua lipua tuu,hawa watu kabla ya kutaka mamilioni ya watu wafanye biashara wangeongeza quality ya kazi yao lakini mtu yeyote serious na pesa yake ni ngumu sana kufanya kazi na walipuaji kama hawa...yaaani huu ubabaishaji sijui utaisha lini,inabidi wajifunze au watafute mtalam wa website anayejua awafanyie kazi inayoeleweka,mimi binafsi siwezi fanya nao biashara naona ni wababishaji tuu!
 
Be careful!! Huyu Jonson Lukaza ndiye owner wa hizo apartment na alizinunua kipindi cha wakati wa EPA na sasa. Na mali zote za watuhumiwa zilizopatikana between EPA and now ziko under guarantee. Search vya kutosha kuhakikisha kuwa hazimo kwenye mzozo. Pia kumbuka kuwa Johnson alikataa kabisa kurejesha pesa ya EPA (wengine walirejesa zote na wengine kiasi) hivyo kama atapigwa chini na kutakiwa kulipa basi watanadi vitega uchumi vyake kama atashindwa kurejesha fedha taslim.

Ni mawazo yangu tuu mkuu. Wengine sijui mnashauri vipi.
 
Back
Top Bottom