Mauwaji yaendelea 5 wauwawa mara na bastola, 8 wajeruhiwa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,722
21,775
Watu wasemekeanao majambazi wamevamia harusi moja kwa
kuingia na kuwaua watu watano na kuendelea kuwasha moto kwa wengine waliokuwa wakitafutwa,..habari zaiidi zinasema walipoingia walikuwa kama wana harusi ndipo baada ya wanaharusi kuingina wakaanza kuwasha bastola kama njugu
harusi iliishia hapo baada ya bibi harusi kula kona na huku bwana harusi akiachwa kama mmoja wa majeruhi

wachungaji wameomba watu waliouwawa jamanai chonde msirudishe kisassi mtamaliza mara yetu tunaomba...
Mmoja wa wana mara amesema kama wananchi tunashirikiana na polisi sidhai kama tutaacha kuwakamata lakini kama tukishindwa basi tuwaageukie mapolisi
 
We waache wamaliazane tukachukue yale mashamba ya bangi kule yanayowafanya wawe na kiburi
 
WATU watano jana wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika waliokuwa na silaha wakati wakisherehekea harusi katika Kijiji cha Kimusi, wilayani Tarime mkoani Mara.
DC Uhahula, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Constantine Masawe na viongozi wengine waandamizi wa ulinzi walikimbilia eneo la tukio na kutumia muda mwingi kuchunguza mazingira ya mauaji hayo.
"Tunawaomba wanakijiji cha Kimusi, msilipize kisasi, vyombo vya Dola vimechukua tahadhari na pia kulaani mauaji haya, tumetoa namba zetu za simu kwa wananchi ili watupatie taarifa ambazo zitatusaidia kuwakamata wauaji hawa," alisema DC Uhahula alipozungumza na waandishi wa habari.
Tayari waliokufa katika tukio hilo wameshatambulika kuwa ni Wangwe Wambura, Mwita Mathias, Matoka Sokoni, Magaiwa Makindi na Marwa Munyoro wote ni wakulima katika Tarafa ya Ingwe wilayani hapa.
Tembelea Http://lukwangule.blogspot.com
 
Mauwaji yaendelea 5 wauwawa

mara
Ukisema Mara watu wanakuwa hawakuelewe bora ungesema Musoma.

Hivi hawa ndugu zetu wana matatizo gani kila kukicha wanauana tu, pia jeshi la Polisi Mkoa wa Mara naona kazi yao imewashika kama wananchi wanauana hivi na wao wanashindwa kuzibiti mauaji haya.
 
Watu wa kutoka mkoa huu, nadhani wanafaa kugombea urais wa nchi yetu...maana dawa ya mafisadi ingekuwa tayari inajulikana..mtu anavyokula rushwa au kufisadi hela za serikali prescription ingekuwa tayari inajulikana...I will vote for any presidential candidate from Mara if that chance comes!
 
Mama Mia, Avatar yako ina niweka njia panda mwenzio napata taabu na Avatar yako i wish ningekuwa garimoshi nione kinacho endelea hapo.
 
Sasa subirini revenge ya walokimbia ndo mtawajua hawa Wamara. nadhani kama hawakuiba chochote basi labda walikuwa na ugomvi na mmoja wa wanaharusi. Ni kuomba amani tu na hawa jamaa wasilipe kisasi!
 
Sasa subirini revenge ya walokimbia ndo mtawajua hawa Wamara. nadhani kama hawakuiba chochote basi labda walikuwa na ugomvi na mmoja wa wanaharusi. Ni kuomba amani tu na hawa jamaa wasilipe kisasi!

weee unaambiwa mkuu wa wilaya mwenyewe kaomba aongezewe ulinzi na akisikia wameshauana anazima kwanza huku anatumia simu nyingine kuulizia imeishaje??yaani hao jamaa noma...badhi wameomba jeshi la polisi lipewe kazi ya kuulinda nikasikitika sana katika jeshi lislo na nidhamu ya bastola ni la tanzania mtasikia kila siku wameuwa mia ,80 awana heshima akabisa na bastola
 
Natamani waletwe dar kwa muda adabu ingekuwepo
 
Watu wasemekeanao majambazi wamevamia harusi moja kwa
kuingia na kuwaua watu watano na kuendelea kuwasha moto kwa wengine waliokuwa wakitafutwa,..habari zaiidi zinasema walipoingia walikuwa kama wana harusi ndipo baada ya wanaharusi kuingina wakaanza kuwasha bastola kama njugu
harusi iliishia hapo baada ya bibi harusi kula kona na huku bwana harusi akiachwa kama mmoja wa majeruhi

wachungaji wameomba watu waliouwawa jamanai chonde msirudishe kisassi mtamaliza mara yetu tunaomba...
Mmoja wa wana mara amesema kama wananchi tunashirikiana na polisi sidhai kama tutaacha kuwakamata lakini kama tukishindwa basi tuwaageukie mapolisi

Mh, Mama Mia kweli jamani? Waliouwawa watarudishaje kisasi?

Poleni sana wafiwa
 
Jamani kwanza nitoe pole kwa waliokumbwa na mauaji haya huko mara.PIli niliombe jeshi la polisi lifanye kazi yake maana kama hawa wauaji waliingia kama wageni waalikwa ni kwamba watu wanaweza kuwatambua maana walikaa kwa muda hapo ukumbini.kwa kweli niliposikia habari hii ITV nilipatwa na mshituko.Hawa watu watatufanya tuogope kwenda makwetu jamani
 
Back
Top Bottom