Mauti yaliosababishwa na mke

Jiwedogo

JF-Expert Member
May 23, 2017
2,811
4,084
FB_IMG_1510474834547.jpg

Pichani ni gari lillilopatwa na mkasa wa ajali nzito na habari yake inaanza kama ifuatavyo.
Kijana Joseph ambaye sasa ni marehemu enzi za uhai wake alibahatika kuwa na kazi nzuri kabla ya kuoa.
Baada ya kuoa miaka mitano ya kwanza akabahatika kuwa na watoto mapacha wa kike na wa kiume na mke wake aliishi kwa furaha akifurahia baraka ambazo Mungu aliwapa familia ile.
Mke hakuwa na kazi na mme akaona ni vyema amsaidie kwa kumsajilia kampuni na mama yule akawa na kampuni ya mitindo na ikafana sana na kupata umaarufu katika eneo lile.
Miaka michache baadae baadae mme akapatwa na matatizo kazini na kusimamiswa kazi na kwa kuwa alikuwa daktari basi na leseni yake ya udaktari ikafungiwa na hakutakiwa kufanya kazi yoyote.
Mpango huo ulisukwa na wenzake pale kazini kwa kuwa alisifiwa sana kwa utendaji wa kazi zake na kupinga vitendo vya rushwa.
Maisha yakazidi kuwa mabaya pale nyumbani kwani miaka ilivyosogea hakupata tena wala kuliona lile penzi la mkewe, kwani mke akawa ni mtu wa kumchukia mmewe mara mme akihitaji fedha apewe kwa masimango na mbaya zaidi hata watoto wakaanza kufundishwa na mama yao kumchukia baba yao.
Hali ile ilimpa mzee yule wakati mgumu na ikafikia kipindi akaanza kudhohofika mwili kwa mawazo ingawa akajitahidi sana kutoyaonhesha hayo machoni pa matu na majirani.
Baada ya muda akapatwa na homa na akawa akijiuguza lakini baada ya muda akashauriwa aende akapimwe na kugundulika kuwa alikuwa na tatizo katika moyo wake lililosababishwa na msongamano wa mawazo.
Akamfuata mkeweofisini kwake na kumwambia anatyatizo la moyo na ilihitajika apate msaada wa fedha kiasi cha laki tano (500,000) kwa thamani ya fedha za kitanzania ili afanyiwe upasuaji wa haraka na kujiokoa katika hali hiyo hatarishi kwa maisha yake.
Mke alimjibu, " Sidhani kama nina hela ya kuchezea kwa kukupa mwanaume usiye na faida kwa familia yako... yaani mpaka chuni nikununulie mimi?Wanaume wenzako wanfanya kazi na sio kama wewe ulivyo sasa"
Baba alinyanyuka na kuufuata mlango bila ya kusema nen machozi yakimtoka na akikumbuka jinsi alivyoijenga familia yake kwa upendo na amani akiwapa mahitaji yote na jinsi alivyotumia mpaka tone lake la mwisho la fedha, muda na hata jasho kuinyanyua biashara ya mkewe ambayo ni kwa ajili ya familia.
Akawasha gari na kuondoka kuelekea nyumbani akiwa na mawazo huku akiona jinsi mtu umpendaye anayoweza kubadilika kiasi cha kukuombea ufe kwa kuwa ni kero kisa huna kazi na kumfananisha na wale wote.
Huku nyuma mke akaingiwa na roho ya ubinadamu na na kujilaumu kwa kauli ile na kuanza kuumia kisha akajaribu kumpigia simu mzee ikawa haipokelewi na kumka kuliwasha gari na kuanza kumfuata mzee
Kilomita chache mbele akaona kuna mkusanyiko mkubwa wa watu akapaki gari na kuuliza kuna nini? wakamwambia kuna ajali ya gari kuna mzee alikuwa anataka kuingia upande wa kushoto bila kuona kama kuna gari.
Kusogea pale hakuamini kuona mwili wa mme wake ukiwa umefunikwa alinianza kutokwa na machozi kabla ya kuingia kwenye gari na kuona kuna kadi nzuri ikiwa kwenye bahasha akaifungua na kuisoma.
Kilio kikubwa kilimtoka baada ya kugundua kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku za kuzaliwa ya baba huyo na hakuna aliyekumbuka zaidi ya yeye mzee kununua kadi iliyoandkiwa " NAKUSHUKURU MUNGU KWA KUNIFIKISHA MWAKA HUU MPYA PAMOJA NA CHANGAMOTO NINAZOZIPITI NAAMINI KUNA SOMO WATAKA KUIPA JAMII KUPITIA MIMI. UHIMIDIWE BWANA.. HAPPY BIRTH DAY TO ME"
Mama yule aliomboleza na mpaka sasa anazidi kuomboleza na hana amani tena hata faida ya ile biashara haioni tena na hajui nani atamsamehe.
Je unapitia mapito gani sasa katika mahusiano yako?
Je unayamudu vipi matatizo ya mahusiano yako?
Je unafikiria nini kama siku ukiamka na kuona wewe ndio chanzo cha kifo, kilema au chanzo msongamano wa mawazo kwa mwenza wako kutokana na tabia zako za ubinafsi?
Ndugu una kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kukupa mwenza huyo na kuamini kuwa katika kila mnalolipitia ni jaribu la kuwafanya muwe na sababu ya kuonyeshana upendo vyema zaidi ya ule wa mwanzo;
Nimeumia sana mpaka nimefikiria sana mahusiano yangu na watu wanaonizunguka nikajiona nina kila sababu ya kusema R.I.P Joseph ni kupitia wewe umenipa somo la upendo na uvumilivu na kuzishinda stress za dunia hii.
 
Ubalikiwe mleta uzi binafsi nina ushuuda mwingi kwenye hili wanawake tulionao majumbani 98% naamini wako sawa na uyu mke wa marehemu km ndani mwako unaona kunaupendo omba sana usiishiwe pesa kwa kipindi rulichopo tambua kua upendo unaouna ni pesa yako ulionayo sku ukiyumba utashangaa .
 
Ubalikiwe mleta uzi binafsi nina ushuuda mwingi kwenye hili wanawake tulionao majumbani 98% naamini wako sawa na uyu mke wa marehemu km ndani mwako unaona kunaupendo omba sana usiishiwe pesa kwa kipindi rulichopo tambua kua upendo unaouna ni pesa yako ulionayo sku ukiyumba utashangaa .
Naomba niunge mkono hoja
 
Hakupaswa kulaumu hivyo sababu alishawafahamu walimwengu.
Huyo mkewe yupo ktk hali gani sasa?
Mungu nijalie hekima kama nisiyumbishwe na walimwengu bali niwe mwema kwako Mola.

Huyo mke ana roho mbaya sana sijui hata anaishie now
 
Hakupaswa kulaumu hivyo sababu alishawafahamu walimwengu.
Huyo mkewe yupo ktk hali gani sasa?
Mungu nijalie hekima kama nisiyumbishwe na walimwengu bali niwe mwema kwako Mola.

Huyo mke ana roho mbaya sana sijui hata anaishie now

Matatizo gani yalisababishwa kufukuzwa kazi? Mkewe hakuweza kumsaidia?
Ana roho ya mnyama huyo.
So sad...inauma R.I.P sote tunapita
Wahenga waliwahi kusema......
Dunia tambala bovu
 

Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom