Maumivu ya Mgongo/ mbavu, naomba msaada

Heisenberg

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
1,683
2,906
Habari za muda huu.

Napata maumivu sana ninapovuta hewa ndani ( Breath in) kuna maumivu kama kichomi nayapata kwa upande wa mgongoni lakini ni kwa ndani nadhani ni mbavuni upande wa kulia. Yamedumu sasa kwa muda kama miezi 3. Sina historia ya kuumia au kupata ajali.

Naomba kujua kabla ya sijaenda Hosp kama kuna Inputs zozote
 
Pole mkuu! Ila kwanini unadumu na maumivu mda wote huo ? Ungeenda hospital ili kama ni shida itatuliwe mapema. Pole
 
Mkuu wewe si ulisema kwamba ulitema kitu(Tonsil Stones) mdomoni? Huenda hivyo vitu bado vipo ndio vinakuletea maumivu.
 
Habari za muda huu.

Napata maumivu sana ninapovuta hewa ndani ( Breath in) kuna maumivu kama kichomi nayapata kwa upande wa mgongoni lakini ni kwa ndani nadhani ni mbavuni upande wa kulia. Yamedumu sasa kwa muda kama miezi 3. Sina historia ya kuumia au kupata ajali.

Naomba kujua kabla ya sijaenda Hosp kama kuna Inputs zozote

Si rahisi sana kupata uhalisia wa eneo husika kwa mgongoni sehemu inayouma hasa. Pia, suala la umri na aina ya kazi unazofanya. Ila mambo haya yanaweza kuhusika:
1: Maumivu toka kwenye pingili za mgongo na mishipa yake ya fahamu.
2: Maumivu toka kwenye figo ie. Mawe kwenye figo
3: Maumivu toka kwenye mapafu, hasa upande wa chini

Fika hospitali ili usikilizwe na ufanyiwe vipimo zaidi.
 
Habari za muda huu.

Napata maumivu sana ninapovuta hewa ndani ( Breath in) kuna maumivu kama kichomi nayapata kwa upande wa mgongoni lakini ni kwa ndani nadhani ni mbavuni upande wa kulia. Yamedumu sasa kwa muda kama miezi 3. Sina historia ya kuumia au kupata ajali.

Naomba kujua kabla ya sijaenda Hosp kama kuna Inputs zozote
Mkuu nenda Hospitali ukapime na utumie dawa.Usipo pona na dawa za kizungu tuone sisi tunaotibu kwa dawa za asili ili tuweze kukutibia maradhi yako upate kupona uguwa pole.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom