Maumivu ya kuachwa katika mapenzi hayana mfano

Alexjohn1

Member
Aug 4, 2021
8
18
Siku zote maumivu ya mapenzi, huwa ni zaidi ya maumivu ya kitu kingine chochote kile... Yaani haya ni zaidi ya maumivu... Ama kwa hakika... Kwani haya ni maumivu ambayo huja wakati ambao tayari umekwisha mpoteza mtu umpendae kwa dhati... Pengine... Zaidi hata ya neno lenyewe nakupenda,,, Lakini kama haitoshi,,, maumivu haya ya mapenzi huja wakati ambao wewe na moyo wako kwa pamoja hamkutarajia ujio huo... Labda ni kwa sababu umependa sana... Kana kwamba,,, ujio huo umekuja mithili ya ujio wa Tsunami kisha kuharibu kila ulichokuwa umekiweka katika ustaarabu wake...

Inauma sana,,,tena sana,,, inauma kweli kweli na inauma moyoni... Jaribu kufikiria ni maumivu kiasi unayopata pale mtu uliyemwamini na kumthamini zaidi ya kitu chochote,,, ama pengine zaidi ya mtu yeyote yule... Anapoamua kuondoka mtu huyo na kukuacha kisha akaenda zake mbali... Hakika pasipo huruma nyuma anakuachia maumivu yasiyoweza kuelezeka ama kupozwa kwa urahisi... Maumivu haya wazungu wanasema ni more than pain.. Lakini pia kitu kinachoumiza zaidi,,, ni pale ambapo aliyekuacha hawezi kugeuka nyuma kamwe walau ashuhudie machozi yako jinsi yanavyotiririka,,, pengine anaweza akabadili maamuzi... Lakini hapana bali yeye anaamua kogongelea misumari ili kuzidisha kiwango cha maumivu moyoni mwako na kukuacha ukiwaza,,, ukifikiria na kulia kwa ajili yake,,, tena pasipo kupata faraja yoyote ama kuambulia patupu...

Kuondoka kwake kunaacha jeraha la mapenzi moyoni mwako... Jeraha ambalo hata kama likipona daima halitofutika bali litaacha alama moyoni mwako... Alama ya kovu ambalo pengine hutopenda mtu aliguse ukihisi unaweza pata maumivu ya mapenzi kwa mara nyingine... Mara kadhaa unateseka na kunyanyasika kwa kumbukumbu za upendo uliowahi kuwa nao juu ya mtu yule... Unawaza kama utaweza kupata mwingine utakayempenda kama ulivyompenda yule... pengine alikuwa na kila ulichokuwa unakihitaji katika mapenzi... Lakini unabaki tu ukilia na kuumia moyoni na usimwamini tena mtu yeyote yule...

NINI CHA KUFANYA

Ninachotaka kusema ni kuwa hayo ni maumivu ya mapenzi... Si maumivu ya kawaida... Mtangulize Mungu pale unapohitaji kujiingiza katika ulimwengu wa mapenzi... Mwambie Mungu akupatie unachostahili na sio kile unachotaka wewe... Lakini kama wewe umeshaumizwa tayari,,, basi huna haja ya kukata tamaa... Bali tumia maumivu hayo ulionayo kufikiria ulipokosea ili wakati mwingine liwe funzo... Utakaporejea kwenye mahusiano uwe imara na uweze kujua nini unapaswa kufanya na usichopaswa kufanya...

Ahsante
By Alex mambi...

1628666687229.png
 
Jina lako limenishitua kidogo maana Kuna mtu katika jina hilohilo yupo katika masahibu hayo..😀

Dunia ya mapenzi unaenda kukutana na watu wenye tabia mbalimbali,Kuna wenye dharau,kejeli na kujiona n.k
Kuna vitu vyengine mtu hawezi viona vya thamani kwako mpk siku akakutane na masokomoko huko ndo ataelewa wewe ulikuwa nani..!!

Wengine hawajui walitakalo ama hajui anataka fedha au mapenzi,hivi viwili vinauhusiano lakini kila kimoja kinanafasi yake. Mkuu maumivu ya mapenzi hayaelezeki yanauma na kuutafuna wewe yako.
 
Kupenda mtu raha sana ila akitoka kwenye maisha yako ni moja ya painful experience.
 
Back
Top Bottom