maumivu wakati wa tendo la ndoa -part 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

maumivu wakati wa tendo la ndoa -part 2

Discussion in 'JF Doctor' started by Pdidy, Oct 14, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  [h=3]Maumivu wakati wa tendo la ndoa - 2-[/h]

  Kichwani (brain & mind) ndiyo kiungo kikubwa cha tendo la ndoa, jinsi unavyojiweka kwenye akili zako inaweza kusababisha raha au maumivu ya tendo la ndoa[​IMG](Picha kwa hisani ya clearingfiles)
  Kwa nini ujisikie maumivu.Maumivu wakati wa tendo la ndoa husababishwa au hutokana na sababu za kihisia na za pia (physical and emotional)
  Ili kujua kwa nini maumivu kutokea ni vizuri kujua nini hutokea kwa mwili wa mwanamke wakati wa tendo la ndoa (sex)
  Mwili wa mwanamke hupitia hatua nne (4) muhimu kukamilisha tendo la ndoa.

  HAMU (dedire)
  Hapa mwanamke hujisikia anataka kufanya tendo la ndoa
  KUSISIMKA (arousal)
  Hapa mwili husisimka kwa sehemu zake za siri (vagina) hutanuka urefu na upana pia hutoa majimaji yanayorahisisha mwanaume kuingia (penis penetration), kisimi hudinda na kuongezeka ukubwa, chuchu husimama na kusisimka, uterus hupanda juu nk
  KUFIKA KILELENI (orgasm)
  Hapa ni kilele cha mwitikio wa tendo la ndoa, misuli hujikusanya (contradict) na kumpa hisia kubwa za raha na utamu wa tendo lenyewe.
  SULUHISHO (resolution)
  Viungo vyote vinavyohusika na tendo la ndoa hurudi kwenye hali ya kawaida

  Aina za maumivu na sehemu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke zinaweza kutokea kwenye katika sehemu zifuatazoSehemu ya nje ya vagina, yaani vulva na huumia wakati inaguswa au kuwasha hata unapotumia baadhi ya sabuni na wakati mwingine kusababisha makovu au utando unaonesha kuna cheese.sehemu ya tundu la kuingia kwenye vagina na sehemu ya ndani ya Vagina unayoungan na uterus.

  Je ni kawaida mwanamke kupata maumivu hata kama hajaambukizwa magonjwa ya zinaa?
  Kawaida kila mwanamke ana aina ya chachu au hamila (yeast) kwenye sehemu za siri zake za siri, na hii yeast ikiongezeka sana inaweza kusababisha kuwasha au maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida na pia husababisha kutoa majimaji meupe mithili ya maziwa na hii hutokea kama mwanamke anatumia antibiotics au medication inayosababisha kuua bacteria wanaofanya hiyo yeast kutoleta madhala yoyote. Hivyo ni jambo la kawaida kwa mwanamke kujisikia maumivu mara chache wakati wa tendo la ndoa ingawa maumivu yakizidi inabidi uchukue hatua inayotakiwa ili kupata tiba kamili.

  Vitu gani vinavyosababisha kuumia wakati wa tendo la ndoa?
  Kukaza kwa misuli ya vagina (Vaginismus) (tamka vaj-uh-niz-muh s)Ni kukaza kwa misuli ya vagina bila hiari (involuntary) na kusababisha tendo la ndoa kuwa gumu au kutofanyika kabisa. Mwanamke mwenyewe anaweza asijue kwamba misuli inayozunguka vagina umekaza na kusababisha maumivu wakati mwanaume anaingiza penis.
  Hii hali hutokana na hofu na mashaka aliyonayo mwanamke kuhusiana na suala la tendo la ndoa kwamba anaweza kuumia (kisaikolojia).
  Pia wanawake wengi wenye vaginismus hawajawahi pata furaha ya tendo la ndoa maishani mwao na wengi ni waoga sana hata kwenda kwa madaktari kuhofia daktari anaweza kuchokonoa vagina zao hivyo kuongeza tatizo zaidi.

  Ni nini husababisha hiyo hofu na mashaka?
  Malezi aliyofundishwa kwamba tendo la ndoa ni chafu na baya na dhambia na hata akiolewa anafahamu kwamba tendo la ndoa ni chafu na baya.
  Malezi aliyolelewa kwa kuambiwa kwamba vagina ni nyembamba sana na hivyo tendo la ndoa husababisha mwanamke kuumia.
  Kama amewahi kudhalilishwa kimapenzi kama kubakwa anaweza kuwa na hofu na tendo la ndoa kwa sababu aliumizwa.
  Kama amewahi kupata magonjwa ya zinaa yaliyokuwa yanamuumiza sana na kumpa shida pia anaweza kuwa anahisia za kuumia wakati wa tendo la ndoa.
  Wanawake wengi wa aina hii hupata raha sana wakati wa foreplay na utamu wa mahaba huwaisha pale tu penetration ikianza.Kitu cha msingi ni kwamba ili tendo la ndoa liwe tamu na zuri hali ya akili na ubongo ni muhimu sana kwani hisia zote za utamu wa tendo hutafsiriwa kwenye ubongo na ubongo ukipata pollution ya mawazo mabaya basi kila kitu kitaenda kombo.Tutaendelea na somo kuangalia vitu vingine vinavyosababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.......​
   
 2. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Embu ukate kate huu uzi ni mrefu sana...
   
 3. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160


  Huelewi sababu ya urefu wa uzi?
  au wakusumbua?
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Haya tunakusubiria ndg.
   
 5. Emasaku

  Emasaku Member

  #5
  Oct 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asante kwa elimu yako mkubwa kwani mpenzi wangu analo hili tatizo, bora nitafute tiba mapema!
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Asante kwa Ujumbe Pidy... ila siku nyingine ukitaka kweli members tusome don't put picha inachkua kama more than five minutes kuingalia...lol
   
 7. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,368
  Trophy Points: 280
  Somo zuri. Pia hiyo picha nimeipenda.
   
Loading...