maumivu wakati wa tendo la ndoa -part 1 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

maumivu wakati wa tendo la ndoa -part 1

Discussion in 'JF Doctor' started by Pdidy, Oct 14, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  [h=3]Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa[/h]

  [​IMG]Maumivu wakati wa tendo la ndoa au kuumia wakati mnafanya tendo la ndoa kwa mwanamke hujulikana kama Dyspareunia.
  Neno Dyspareunia tamka (dis-pa-roon-ia) linatokana na neno la kigiriki lenye maana ya shida katika kuingiliana wakati wa kufanya tendo la ndoa (difficulty mating au badly mated).

  Utafiti unaonesha kwamba kati ya wanawake watatu, wawili wamewahi au hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
  Imefika kwamba baadhi ya ndoa, mwanamke anapata maumivu kiasi cha kutokuwa na hamu tena ya tendo la ndoa na matokeo yake wamekuwa na wakati mgumu linapokuja suala la kufanya mapenzi na pia kila wakirudia kufanya tendo la ndoa, mambo ni yamekuwa ni yaleyale kwa mwanamke kuumia zaidi kuliko mara ya kwanza.

  Kawaida huwa haifurahishi kabisa na haina hata ladha kufanya tendo la ndoa huku mmoja kati yenu akiwa anapata maumivu makali au shida hiyo husababisha kutojishughulisha katika kuleta raha ya kweli na hatimaye kuridhishana kimapenzi wakati wa tendo la ndoa.
  Tendo la ndoa halikuwekwa ili kukupa shida au maumivu bali kukupa raha, furaha na kuridhishwa.
  Moja ya kanuni muhimu sana katika tendo la ndoa ni
  “ Kama unapata maumivu usifanye”
  Badala yake tafuta nini kimesababisha na tafuta jibu sahihi la kuondoa hiyo hali au muone daktari akusaidie.
  Na baada ya kupata tiba na kupona ndiyo unaruhusiwa kuendelea kufanya tendo la ndoa kwa kufurahia na kukupa raha zaidi, vinginevyo itakuwa ni kuleta maangamizi.

  Ni kweli kwamba kama moja wapo ya mahitaji ya msingi ya kihisia (emotions) kama hili la tendo la ndoa halipatikani katika ndoa linaweza kusababisha mmoja ya wanandoa kutokuwa mwaminifu kwa mwenzake na kutoka nje kwenda kutafuta mtu wa kumridhisha zaidi, hata hivyo kwa mwanamke kufanya tendo la ndoa huku anapata maumivu au kuumia kwa kuogopa kwamba asipompa Mume wake haki yake basi anaweza kutoka nje na kutokuwa mwaminifu hilo si sahihi kwani ni kutojiamini na kutojali si afya yako tu bali haki yako ya msingi ya kufanya tyendo la ndoa kwa kupata raha.
  Mnahitaji kujulishana na kuelezana ukweli ili muweze kupata dawa na hatimaye kurudi kwenye raha upya badala ya kuumizana.

  Kuna mambo mengi yanayosababisha mwanamke au hata mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa na inaweza kuwa ni wakati mwanaume anapoingia (penetrate) au wakati wa kitendo chenyewe au baada ya kitendo chenyewe.
  Inaweza kuwa ni maumivu makali sana au inaweza kuwa ni kuwashwa au inaweza kuwa ni maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida au inaweza kuwa ni maumivu ambayo unasikia kama moto unawaka vile ndani yako wakati wa tendo la ndoa.

  Naamini kufika mwisho wa hili soma utakuwa umefahamu si nini kinasababisha bali utafahamu jibu la hili Tatizo.   
 2. NG'ADA

  NG'ADA Senior Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  somo zuri kaka...saaana!!maana hata mm limenikuta hilo, kijana nahangaika mwisho wa siku ni kusumbuana tu na kukojolea mashavuni mwa "mma"!!!mbaya zaidi maandalizi yalikua yanachukua muda wa kutosha, ila ukitaka tu kubisha hodi..kesi!! ila KY inasaidia..
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  teeeteehhhhh ssoma part 2 kesho nakuja na 3 na 4 itusaidie
  hii ni special kwa nyerere day
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  heeeeeeeeeeeh!
   
 5. Emasaku

  Emasaku Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kaka hii kitu mpenzi wangu anayo. Wakati wa tendo yeye anasikia maumivu na wakati mwingine pana waka moto, kuna siku tulikutana kimwili na alipata hiyo hali lakin hakumia sana kivile, chakushangaza kesho yake alinipigia cmu nakudai anasikia maumivu makali na kumevimba! Kaka hii hali inatiba? Hebu nisaidie nisije nikapoteza kipenzi changu!
   
 6. Baba Erick

  Baba Erick JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimechoka ila niwape kiprofessional kidogo. Maumivu haya kwa wanawake yanatokana na
  i)STDs/STIs
  ii)FUNGI
  iii) Cancer.
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Baba erick
  sisemi muongo ila hizo zinachangia maumivu ..binafsi nikiwa na google nimeona mtu akiwa anaumia kweli ingwa katikati anaita tamu huku mwanzoni kaumia na tukapima zote hapo juu -NIL
  Tulichofanya nikuamini hayo ndio mapenzi tuliopewa na muumba mppaka akaja kuolewa ...ila ukiona mtu anaumia pls nenda pima hayo juu ukikuta akuna kitu basi hilo Neno yaani ndio mzigo wako
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Kila mwanamke kwenye uke wake kuna kiwango muhimu cha bacteria, fungus, yeast au protozoa na hawa viumbe hawana madhara yoyote katika mwili hadi hapo kiwango chake kikiathirika na mazingira yake kama matumizi ya antibiotics, kuwa na medication au madawa na uzazi wa mpango na ndipo matatizo hutokea na kupata haya matatizo si kuwa unaumwa magonjwa ya zinaa ni hali ya kawaida kitu muhimu lazima uhakikisha unapata dawa.[​IMG]Leo tumalizie na mambo yanayosababisha kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke.

  Maambukizo (vaginal infection)
  Mwanamke anaweza kupata maambukizi kutokana na bacteria, fungus, yeast na amoeba.
  Kawaida kwenye sehemu za siri za mwanamke kuna kiasi kikubwa cha bacteria, fungus, yeast au amoeba ambao hawana madhara yoyote hadi pale uwiano ukiwa tofauti kutokana na sababu mbalimbali kama vile madawa nk
  Maambukizi (infections) yanapotokea kawaida kunakuwa na mabadiliko yafuatayo
  Kubadilika rangi kwa majimaji yanayotoka sehemu za siri za mwanamke,
  Pia kutoa harufu mbaya baada ya tendo la ndoa,
  Kuvimba sehemu za siri,
  Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo,
  Kuumia wakati wa tendo la ndoa (maumivu ya kama kuchoma na kuwasha).

  Menopause
  Upo wakati mwanamke anafikia (miaka 48 - 52) muda ambao hawezi kuzalisha tena homoni za estrogen zinazosababisha kuzalishwa kwa yai kila mwezi.
  Kutokuwepo kwa hii homoni husababisha uke wake kuwa mkavu hata wakati wa tendo la ndoa.
  Uke kuwa mkavu husababisha kujisikia maumivu wakati wa tendo la ndoa na hasa kama hakuandliwa vizuri.

  Zipo sababu zingine kama vile hitilafu katika maumbile ya uke kutokana na operation au kubakwa n.k husababisha mwanamke kujisikia maumivu wakati wa tendo la ndoa.

  Je wanaume nao hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa?
  Ni kweli inawezekana kwa mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa ikiwa
  Amepata maambukizi ya bacteria, fungus au yeast kutoka kwa partner wake
  Kama ameambukizwa magonjwa ya zinaaa
  Kama hajatahiriwa na hasa kama ndo anaanza kufanya tendo la ndoa atajisikia maumivu kwa sababu ya gozi (foreskin) kugoma kujivuta nyuma.


   
 9. m

  mselem nation New Member

  #9
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KUACHA NI DHAMBI MAANA KILA KIUNGO CHA BINADAMU KIMEWEKWA KWA MAKUSUDI MAALUM.

  USHAURI WANGU
  1. Jichunguze wewe mume kwanza. Je, huna vimwana wasiojua kuoga na kusafisha nyeti zao kwa maji safi na salama?
  2. Uwe makini sana na utendaji kazi wako. Uzamishaji wa oil stick kwenye Engine sio sawa na urefu wa stick izame yote. Zamisha Stick kwa uangalifu na si lazoma uende mpaka Brake iwe ni Bulb zako.
  3. Uchanganyaji wa sera ya maandalizi ya mwenzi wako si mke tu anaye andaliwa bali hata mume huandaliwa sawa dada zangu. Mume huandaliwa ili ukali na vurugu ukiherehere wa kupanda gari wakati hujatiza maji yapo? oil imeshuka au lah? na je nyaya za betri ziko active?
  4. Dada zangu Ubinafsi wenu ndio unawafanya mnapata hayo maumivu makali maana nyie mnaona haki ni kwenu tu na wenzenu oooooh!!!!!!!
  5. Mwisho kama unayafanya haya yote na bado unasikia maumivu, Jaribu kumuona daktari mkiwa na mwenzi wako ili mpate ushauri kwani Conc. U.T.I inaweza kusababisha hayo muanza dozi wote.
  ZINGATIENI SANA HAYO.
   
 10. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Leo nimefarijika na somo hili. Kesho nitakuja na maswali yangu. Ngoja niandae kwanza. Asanteni sana kwa muda wentu kutuelimisha.

  CD
   
 11. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ila hua watu wengi wanaumia sana alafu mi hua nashangaa wanaume hawaumii hata loh! kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni..............hebu mie napita tu hapa maaaaana................
   
 12. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
   
 13. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  thanx kwa somo hii ndo faida ya jf jamn burudan na somo juu be blecd wajmn
   
Loading...