Chembe ya moyo ni nini na hutokana na nini?

Chukua Kutunguu swaumu,Tangawizi visage chukua kipande cha limao kamulia kwenye huo mchanganyiko...baada ya hapo utachukua Asali mbichi kijiko kimoja weka kwenye huo mchanganyo then koroga mpka upate ujiuji mzito then kamua upate maji maji ya huo mchanganyo wako......unywe vijiko viwil kutwa mara tatu....(asbh..mchana..jion...) Ndani ya siku tatu Lete majibu hapa....me cyo dokta ila huu mchangnyiko n dawa tosha kwa wale wanasumbuliwa na kifua sugu
 
Mimi sio daktari;
Maumivu ya namna hiyo yanaweza kuwa ama ni chembo moyo,kiungulia au ni dalili za mwanzo za vidonda vya tumbo.Pia inaweza kuwa pneumonia au angina.Kwa kwaida pneumonia huwa inkuwa na homa pia.Kama hupati homa basi jaribu kufikiria kama unaweza kuwa na vidunda vya tumbo anagali kama mamumivu hayo yanatokea unapokula vyakula vya ina fulani hasa vyakula vichachu.Kama ni kiungulia pia angalia kama kuna vyakula vina sababisha hiyo kama nic chembe ya moyo angalia kama unapokuwa na mshtuko maumivu yanakuwa makali zaidi.Pembeni ya tiba ya pneumonia unaweza tafuta tiba za tumbo kama dawa za antacid/antiflatulent.Ni vizuri umeona daktari wako kabla ya kufanyia ushauri huu kazi
Hii ina ukweli nimekuwa na tatizo kama lako toka 2003 nikafanyiwa xray temeke, amana na muhimbili hakuna tatizo nikapigwa masindano ya kutosha christapen na powercef, nikatumia kila aina ya dawa, nikapiga CT scan ya kichwa na kifua hakuna tatizo mpaka mwaka 2012 nilienda TMJ nikakutana na daktari wa kihindi nikamuelezea historia na vipimo nilivyopitia na ninavyojiskia mpaka leo akasema hebu tuangalie mfumo wako wa chakula maana kifua kuuma na nyuma ya mgongo inaweza kuwa ni mfumo wa chakula pia, nikapigwa endoscopy na tatizo likaoneka ni GERD grade 1 bahati mbaya hakuna tiba ya uhakika hata opersheni ukifanyiwa wanasema success rate ni 50% so nikashauriwa tu kubadili mtindo wa maisha na kutumia dawa ila nimateso makubwa.
 
mkuu hakuna kitu kinaitwa chembe ya moyo. hayo ni maumivu yanatokea chini ya kifua mithili kama unachomwa na kitu chenye ncha kali.
hivyo ni vidonnda vya tumbo(peptic ulcers au duodenum ulcers) mara nyingi husababisha maumivu makali chini ya kifua ambayo watu wengi huita chembe ya moyo.
nakushauri uwahi haraka hospitalini ukapime vidonda vya tumbo kabla havijawa chronic. kwani hiyo unayoita chembe ya moyo ni moja ya dalili za mwanzo.
Ni kweli kiongozi ila sasa kwangu imefikia hata ukikandamiza kifua huwa kinauma na kiungulia kimepanda mpaka kwenye koo
 
wahi hospitali mweleze Dk lakini ni dalili kuwa acid inazalishwa kwa wingi tumboni mwako jaribu kuepuka kula kwa wingi vitu vyenye asili ya acid na pia jitahidi kunywa maji kwa wingi
Hebu niorodheshee hivyo vyakula vya acid tuvijue mkuu
 
Aisee mimi nina hili tatizo serious kabisa.
Maumivu yangu cku za nyuma yalianza kiuno yakapanda na mgongo karibu na mabega. Sasa yamehamia kifuan upande wa kushoto na napata na gesi wakat mwingine. Halafu kuna wakat kichwa kinauma upande mmoja huu huu wa kushoto mpaka jicho linaniuma. Nilijaribu kwenda sana hospital wao wananiambia hawaon kitu so ninachojaribu kufanya ni mazoez. Nikifanya mazoez hii kitu inapungua. Cjawah kutumia dawa za mitishamba toka nitoke kijijin miaka ile 90 bibi yetu alikuwa anatuleteaga dawa za kimasai. Nimesona ushaur wenu ngoja tena nikachek na Dr kesho nimsikilizie.
 
Nina jirani yangu anateseka kila usiku, ukimuliza anasema ana "chembe ya moyo"

Sijui ni ugonjwa gani mwenye idea na solution yake.

Hospitali alienda wakampa dawa lakini naona panadol n.k
 
Mwambie apunguze mawazo kwa jambo ambalo ameshindwa kulipatia ufumbuzi, hiyo ni dalili ya vidonda vya tumbo na maumivu yake huitwa kitaalamu kama epigastric pain.
 
Wadau hivi majuzi nilishikwa na kama kichomi fulani hapa juu ya tumbo yani katikati ya tumbo na kifua sikulala kabisa usiku wake.

Sikuwahi kutokewa na hali hii hiyo ndiyo ilikua mara ya kwanza.

Hata hivyo sikuweza kwenda hospitali kwa sababu nilikua na safari ya muhimu sana. Nilijaribu kuwauliza watu mbali mbali wakawa wananiambia ni chembe ya moyo lakini mimi sijui chochote kuhusu hiyo chembe ya moyo yenyewe.

Naombeni msaada wenu wadau.
=======

w0rM anasema:
Chembe ya moyo(Angina Pectoris) ni tatizo linalowasumbua watu wengi sana kwa sasa na hutokea pale moyo unapopata hewa ya oxygen kidogo tofauti na mahitaje yake

Hali hiyo inaweza kusababishwa na aidha kuziba kwa mishipa ya damu inayopeleka damu moyoni na kusababisha misuli ya moyo isipate damu ya kutosha inayobeba oxygen

Sababu nyingine ni pale moyo unapofanya kazi kubwa sana ya kusukuma damu kiasi kwamba kiwango cha oxygen ambacho moyo huo unapata kinakua hakitoshi

Inaelezwa kuwa Watu waliopo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo ni; Wanaovuta sigara, Wanene kupita kiasi na wenye ugonjwa wa kisukari

DALILI ZA CHEMBE YA MOYO
Dalili kubwa ni maumivu katikati ya kifua yanayokua kuelekea kwenye mkono wa kushoto

MATIBABU YAKE
Kuna dawa nyingi zinazo weza kutumika kutibu tatizo hili, baadhi ya dawa hizo ni Nitroglycerine(Glyceryl Nitrtrate), Nifedipine na Atenolol

Aidha, ikigundulika mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye misuli ya moyo imeziba mgonjwa atakiwa kufanyiwa upasuaji ili kuizibua
AHSANTE SANAMKUU SIJALALA MAJIRAN WANANGALIA ANAVYOHANGAIKA JORAN UNALIA KABISAA AISEE UGONJWA WA HATAREE SANA
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom