Chembe ya moyo ni nini na hutokana na nini?

OSAM

Member
May 14, 2011
31
2
Wadau hivi majuzi nilishikwa na kama kichomi fulani hapa juu ya tumbo yani katikati ya tumbo na kifua sikulala kabisa usiku wake.

Sikuwahi kutokewa na hali hii hiyo ndiyo ilikua mara ya kwanza.

Hata hivyo sikuweza kwenda hospitali kwa sababu nilikua na safari ya muhimu sana. Nilijaribu kuwauliza watu mbali mbali wakawa wananiambia ni chembe ya moyo lakini mimi sijui chochote kuhusu hiyo chembe ya moyo yenyewe.

Naombeni msaada wenu wadau.
=======

w0rM anasema:
Chembe ya moyo(Angina Pectoris) ni tatizo linalowasumbua watu wengi sana kwa sasa na hutokea pale moyo unapopata hewa ya oxygen kidogo tofauti na mahitaje yake

Hali hiyo inaweza kusababishwa na aidha kuziba kwa mishipa ya damu inayopeleka damu moyoni na kusababisha misuli ya moyo isipate damu ya kutosha inayobeba oxygen

Sababu nyingine ni pale moyo unapofanya kazi kubwa sana ya kusukuma damu kiasi kwamba kiwango cha oxygen ambacho moyo huo unapata kinakua hakitoshi

Inaelezwa kuwa Watu waliopo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo ni; Wanaovuta sigara, Wanene kupita kiasi na wenye ugonjwa wa kisukari

DALILI ZA CHEMBE YA MOYO
Dalili kubwa ni maumivu katikati ya kifua yanayokua kuelekea kwenye mkono wa kushoto

MATIBABU YAKE
Kuna dawa nyingi zinazo weza kutumika kutibu tatizo hili, baadhi ya dawa hizo ni Nitroglycerine(Glyceryl Nitrtrate), Nifedipine na Atenolol

Aidha, ikigundulika mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye misuli ya moyo imeziba mgonjwa atakiwa kufanyiwa upasuaji ili kuizibua
 
Maumivu hayo ni makali mfano wa nini? Maumivu yalichukua muda gani? Unafikiri ni nini kilipelekea maumivu kupotea?
 
chembe ya moyo ni sharp pain chini ya sternum (hapo mbavu zinapoishia kuungana na tumbo kuanzia,panabonyezeka).inasababishwa na acid indigestion,ni kama dalili za mwanzo za ulcers. lakini kama maumivu ni chini ya titi la kushoto maybe uonane na daktari,inaweza kuwa shida ya moyo (broken heart hahaha)
 
Nimekuwa nikisumbuliwa na chembe ya moyo takribani wiki moja sasa.
kwa anayejua anisaidie jamani.
 
Mkuu hakuna kitu kinaitwa chembe ya moyo. hayo ni maumivu yanatokea chini ya kifua mithili kama unachomwa na kitu chenye ncha kali.

Hivyo ni vidonnda vya tumbo(peptic ulcers au duodenum ulcers) mara nyingi husababisha maumivu makali chini ya kifua ambayo watu wengi huita chembe ya moyo.

Nakushauri uwahi haraka hospitalini ukapime vidonda vya tumbo kabla havijawa chronic. kwani hiyo unayoita chembe ya moyo ni moja ya dalili za mwanzo.
 
Tedo yuko sahihi, hiyo ni dalili ya mwanzo kabisa ya ulcers. Stage inaitwa 'acid indigestion'. Epuka kula vyakula vyenye acid nyingi kama ndimu na nyanya. Wahi hospitali, ukipata matibabu mapema itaisha kabisa na utaepuka dhahma ya vidonda vya tumbo.
 
Tedo yuko sahihi, hiyo ni dalili ya mwanzo kabisa ya ulcers. Stage inaitwa 'acid indigestion'. Epuka kula vyakula vyenye acid nyingi kama ndimu na nyanya. Wahi hospitali, ukipata matibabu mapema itaisha kabisa na utaepuka dhahma ya vidonda vya tumbo.
Usemayo ni sahihi kabisa. Chembe ya moyo ni lugha inayoweza kumisslead mtu lakini ukweli ni kwamba hiyo ni mojawapo ya dalili za ulcers. Suluhisho ni kwenda hospitali haraka ili kupima na hatimaye kupata tiba sahihi.
 
Tafadhali nenda hospital na usingojee hilo tatizo likawa kubwa litakusmbua.muone dr na upate dawa na tumai utapona haraka kwa uwezo mungu
 
mkuu hakuna kitu kinaitwa chembe ya moyo. hayo ni maumivu yanatokea chini ya kifua mithili kama unachomwa na kitu chenye ncha kali.
hivyo ni vidonnda vya tumbo(peptic ulcers au duodenum ulcers) mara nyingi husababisha maumivu makali chini ya kifua ambayo watu wengi huita chembe ya moyo.
nakushauri uwahi haraka hospitalini ukapime vidonda vya tumbo kabla havijawa chronic. kwani hiyo unayoita chembe ya moyo ni moja ya dalili za mwanzo.

ahsante mkuu kwa ushauri mzuri
 
salaam ndugu zanguni wana jf naombeni mnisaidie na ushauri wa nini nile, ninywe, au nifanyeje niondokane na hili tatizo nilonalo la kuumwa na chembe ya moyo nateseka sana ndugu zangu nashindwa hata kufanya kazi vizuri! msaada tafadhali.
 
Mkuu hivyo ni vidonda vya tumbo, nenda kafanye vipimo na utapewa dawa kulingana na vipimo
 
salaam ndugu zanguni wana jf naombeni mnisaidie na ushauri wa nini nile, ninywe, au nifanyeje niondokane na hili tatizo nilonalo la kuumwa na chembe ya moyo nateseka sana ndugu zangu nashindwa hata kufanya kazi vizuri! msaada tafadhali.
sijui maana ya chembe moyo, nieelezee dalili zake au jinsi unavyo umia!
 
wahi hospitali mweleze Dk lakini ni dalili kuwa acid inazalishwa kwa wingi tumboni mwako jaribu kuepuka kula kwa wingi vitu vyenye asili ya acid na pia jitahidi kunywa maji kwa wingi
 
JF doctor's naombeni kujulishwa dawa ya kutibu huu ugonjwa wa wenye maumivu chini ya kifua uitwao chembe maana wengi wanadai kwab:A S confused:paka uchanjwe (kibantu zaidi) inamaana huu ugonjwa ni wa sisi wabantu tu.
 
Kuchanjwa ni Imani, nenda hospitali wakupime na wajue tatizo ni nini ili upate matibabu.
 
Back
Top Bottom