Maumivu kwenye nyonga, kibofu na korodani.

Samireal

Member
Aug 16, 2015
88
22
Salaam, naomba msaada
Huwa nafanya mazoezi ya kukimbia, kucheza mpira pamoja na mazoezi mengine lakini niliacha kwa muda wa wiki tatu au nne nafikiri,

Jana nilienda uwanjani nikafanya mazoezi ya kukimbia pamoja na kucheza mpira wa miguu kidogo lakini imenitokea hali ambayo sio ya kawaida nahisi maumivu kwenye kibofu, korodani (Mapumbu) na nyonga za ndani. Je inawezekana ikawa ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesho nenda hospitali mkuu, ukapime tu.

Mimi nakumbuka kuna siku nilienda kufanya zoezi la kupanda ngazi na kushuka ngazi,

Nakwambie usiku yake tu malaria ikachukua nafasi yake, kesho nikaamkia hospitali na kuandikiwa dawa za malaria

Sasa huwenda na wew ndio ugonjwa umeanza na zoezi ulilopiga leo limechochea taarifa hzo za kuumwa kuanza mapema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kila kitu ni ugonjwa mkuu, mazoezi siku zote hayaitaji kupumzika kwa muda mrefu kias hicho, unapofanya consecutively mwili unabadilika na kuendana na aina ya mazoezi hayo, pale pindi unapoacha tu kwa muda mrefu, mwili huanza kurudi katika hali yake ya mwanzo, yaani misuli, mishipa na hapa joints zinarudi normal. Kosa kubwa ulilofanya ni kuacha mazoezi kwa muda mrefu kisha kuanza kufanya tena, lazima maeneo fulani ya mwili yapate hali ya tofauti ili kurudi katika ile hali ya mwanzoni kabla ya kuacha mazoezi, so elewa hayo ni mabadiliko ambayo lengo kuu ni kuweka mwili sawa ili kurudi katika hali ya kuzoea mazoezi kama ilivyokuwa mwanzo.
Huwezi pasha maji moto halafu ukaacha kuchochea moto mkuu lazima maji yatapoa, so ili yaendelee kuwa ya moto ni lazima kuendelea kuchochea moto mkuu ili kubalance joto lake. So cha kufanya si kuacha wala kujenga dhana tofauti na ya kimazoezi mkuu, cha msingi fanya maamuzi kuendelea kufanya mazoezi kama ilivyokuwa mwanzo basi hata angalau mara tatu au nne kwa wiki, hiyo hali itapotea na mwili utarudi normal kabisa na hayo maumivu hutoyasikia, kukimbilia dawa za mseto hiyo inaonyesha dhahiri uamini katika mazoezi kama dawa ya magonjwa mengi sana mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungeanza taratibu mazoez kuliko kurudi na kasi ileile.

Chagua kusuka au kunyoa
 
Kesho nenda hospitali mkuu, ukapime tu.

Mimi nakumbuka kuna siku nilienda kufanya zoezi la kupanda ngazi na kushuka ngazi,

Nakwambie usiku yake tu malaria ikachukua nafasi yake, kesho nikaamkia hospitali na kuandikiwa dawa za malaria

Sasa huwenda na wew ndio ugonjwa umeanza na zoezi ulilopiga leo limechochea taarifa hzo za kuumwa kuanza mapema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kila kitu ni ugonjwa mkuu, mazoezi siku zote hayaitaji kupumzika kwa muda mrefu kias hicho, unapofanya consecutively mwili unabadilika na kuendana na aina ya mazoezi hayo, pale pindi unapoacha tu kwa muda mrefu, mwili huanza kurudi katika hali yake ya mwanzo, yaani misuli, mishipa na hapa joints zinarudi normal. Kosa kubwa ulilofanya ni kuacha mazoezi kwa muda mrefu kisha kuanza kufanya tena, lazima maeneo fulani ya mwili yapate hali ya tofauti ili kurudi katika ile hali ya mwanzoni kabla ya kuacha mazoezi, so elewa hayo ni mabadiliko ambayo lengo kuu ni kuweka mwili sawa ili kurudi katika hali ya kuzoea mazoezi kama ilivyokuwa mwanzo.
Huwezi pasha maji moto halafu ukaacha kuchochea moto mkuu lazima maji yatapoa, so ili yaendelee kuwa ya moto ni lazima kuendelea kuchochea moto mkuu ili kubalance joto lake. So cha kufanya si kuacha wala kujenga dhana tofauti na ya kimazoezi mkuu, cha msingi fanya maamuzi kuendelea kufanya mazoezi kama ilivyokuwa mwanzo basi hata angalau mara tatu au nne kwa wiki, hiyo hali itapotea na mwili utarudi normal kabisa na hayo maumivu hutoyasikia, kukimbilia dawa za mseto hiyo inaonyesha dhahiri uamini katika mazoezi kama dawa ya magonjwa mengi sana mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom