Maumivu kama kuchomwa na msumari mguuni,tatizo nini?

Domy

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
4,698
Points
1,195

Domy

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
4,698 1,195
Salaam wanabodi.

Kwa wiki kama ya tatu sasa nimekuwa nahisi maumivu mara kwa mara kama vile kitu kimenichoma katika mguu wa kulia upande wa kulia wa mguu huo kwa chini.maumivu hayo yanapoanza yanagonga mpaka kichwani lakini hayadumu sana hata dakika moja haifiki.

Yamekuwa yanatokea mara nyingi kama natembea,nimekaa wakati mwingine nikiwa nimelala.Naomba kwa anayejua ni tatizo gani na nini tiba yake anijuze tafadhali.!
 

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined
Sep 1, 2011
Messages
3,232
Points
1,195

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined Sep 1, 2011
3,232 1,195
Upo dar? karibuni nitaandaa video ya mazoezi kwa ajili ya watu wa aina yako maana ishakuwa ishu kwa watu wengi, matatizo ya miguu yanawasumbuwa sana watu wanaotumia muda mwingi kukaa au kusimama katika siku. Lazima kuwe na balanzi, hutakiwi ukae muda mrefu au usimame muda mrefu, lasivyo damu inajikusanya sehemu moja na kutengeneza taka za asidi ambazo ni sumu. Kwa sasa tafuta matunda uanze kuyala na ongeza mboga za majani katika mlo wako, nitakuandikia vizuri usiku mazoezi gani utapaswa kufanya.
 

Forum statistics

Threads 1,390,122
Members 528,091
Posts 34,043,135
Top