Maumivu chini ya tumbo wakati wa mimba

Peace92

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
261
55
Habari wakuu! Mimi nina ujauzito wa miezi minne lakini tumbo chini ya kitovu limekuwa linaniuma sana hasa nikiwa nainama! Nimeenda hospitali wakasema ni kawaida tu.

Naombeni ushauri wenu je nifanye nini.
 
Habari wakuu! Mim Nina ujauzito wa miezi minne lakini tumbo chini ya kitovu limekuwa linaniuma sana hasa nikiwa nainama ! Nimeenda hospital wakasema ni kawaida tu . Naombeni ushauri wenu je nifanye nin
Habari,
Pole kwa madhila.
Ni kweli kwamba wakati mwingine maumivu chini ya tumbo huwa yanatokea hasa kuanzia wiki ya 12 (yaani miezi minne). Hii hutokana na kutanuka kwa nyonga kulingana na mabadiliko ya vichocheo na pressure/ mgandamizo wa mtoto wakati anaendelea kukua.
Maumivu haya huwa si makali sana ili kwa wengine huitaji kuchukua dawa ya kutuliza maumivu/paracetamol pale unapoona yanakuwa makali zaidi.

Pia, ni mhimu kujiridhisha kuwa maumivu unayopata hayana chanzo kingine kama maambukizi kwenye njia ya mkoji. Hivyo ni vyema pia kwenda kuwaona wataalamu zaidi ili tathimini ya hali yako iwe imefanyika kwa ufasaha. Hii ni kama ulipofika kwa mtaalamu wako wa mwanzo hakujaribu kuangalia chanzo kingine cha maumivu zaidi ya kusema ni kawaida.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom