MAKOLE
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 618
- 280
Wadau, naomba msaada wenu. Nimengoa jino na leo tar 26/7 nna siku ya nne. Jino lenyewe ni namba 7 kwa sababu nimewasikia madaktari wakilitaja. Lilikatika wakati wakiling'oa na ikasababisha watumie nguvu ya ziada kungoa mizizi. Nilipata maumivu sana kiasi kwamba hadi leo naumwa.
Waliniandikia kumeza Paracetamol, Cloxaxiline na Metronidazole(flagile), Pia wamenishauri nisukutue maji ya uvuguvugu yenye chumvi. Yote nimeyafanya lakini mara kwa mara maumivu yanarudi. Madaktari naomba mnipatie msaada wa dawa ya uhakika kama ipo na pia mnieleze ni mpaka siku ngapi fizi inaweza ikapona?