Maumbo ya wanawake wakimbizi yabomoa ndoa za watu Kigoma

Samweli Mathayo

JF-Expert Member
Aug 1, 2017
1,577
1,700
Maumbo ya wanawake wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burundi huko mkoani Kigoma yamezua gumzo baada ya akina Baba kuzitelekeza familia zao na kuoa wanawake hao wakirundi


Baadhi ya Wanaume katika wilaya ya Kakonko wanadaiwa kutelekeza ndoa zao na kwenda kuoa wanawake hao wa Kirundi huku sababu ikiwa ni uzuri maumbo yao.

Hayo yameelezwa na wanawake wa kijiji cha Kaziramihunda, kilichopo kata ya Kasanda wilayani Kakonko mkoani Kigoma mbele ya Mkuu wa wilaya hiyo, Kanali Hosea Ndagala.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa kijiji hicho Bi. Tabu Kiuliko amesema anamuomba Mkuu wa Wilaya kuingilia kati suala hilo la kutelekezwa na wanaume zao kwani limekuwa sugu na limerudisha nyuma maendeleo ya baadhi ya familia.

Wanawake wengi wameachiwa jukumu la ulezi wa familia baada ya waume zao kuwatelekeza wake zao na kuoa wakimbizi , tunaomba serikali iingilie kati suala hilo,“amesema Bi. Tabu.

Hata hivyo, Afisa Mtendaji wa kata ya Kasanda, Motoni Borutu ameunga mkono taarifa hiyo kwa kukiri kuwa Ofisi yake imepokea malalamiko hayo na kuahidi kuyafanyia kazi.

Kwa upande mwingine, Afisa Uhamiaji wa wilaya ya Kakonko, Christopher Mlemeta ambaye alikuwa kwenye msafara huo wa mkuu wa wilaya, amesema ni kosa kisheria kwa mtu kuoa au kuolewa na mkimbizi na kuishi naye nchini bila kupata kibali maalumu kutoka serikalini.

Chanzo:Mwananchi
 
Mbona hao wanawake wa kirundi hawana tofauti na waha wenyewe? wanafanana karibia kila kitu kwanza wengi wao hua hawana shape..ukiacha wale wenye asili ya kitutsi wenyewe ni weusi warefu na pua kuchongoka..ila ni kama waha tu kimsingi...cc nyarubanda...
 
Mi mwenyewe na mpango wa kuelekea huko Kigoma,nijitafutie mkimbizi nianzishe maisha rasmi na Mtoto wa Kitutsi
 
Mbona hao warundi ni kama waha tu. Au labda watutsi nao wanakimbilia Kigoma badala ya kukimbilia Rwanda ?Wanawake wa kiha hawajui mapenzi ama ? Ila wana heshima kweli kweli.
 
Back
Top Bottom