Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,624
- 218,047
Nimeona niliweke hili wazi ili kuwakumbusha wanaJF,
Kulikuwa na makubaliano ya UKAWA kutoka nje ya bunge ili kuonyesha kupinga kwa vitendo kusiginwa kwa katiba ya Tanzania kuhusu namna majina ya mfukoni mwa Lipumba yalivyoletwa na kuapishwa bungeni
Huku kukiwa na kesi Mahakamani kuhusiana na wabunge hao, Mtulia aliamua kubaki ndani ya bunge, huu ulikuwa usaliti wa wazi na wote wenye macho matatu tulianza kumtilia shaka.
Tetesi zinadokeza kwamba bwana Maulid ameahidiwa kununuliwa kwa kulipwa mafao yote na mshahara pamoja na stahili zingine ambazo angepata katika kipindi cha miaka mitano, ikiwemo hela inayoitwa ya usumbufu.
Hii ndio namna hela ya makinikia inavyotumika! Unamuungaje mkono mtu aliyezuia demokrasia ambayo ndio uliitumia kupata ubunge? Katiba inavunjwa makusudi bila haya, hakuna ajira, hakuna maendeleo, maisha ni magumu kuliko enzi ya ukoloni, mikopo ya wanafunzi ni chini ya 50% , inahitaji akili ya kichaa kuunga mkono mambo haya.
Kitendo alichokifanya Mtulia si tu kwamba ni matusi makubwa kwa wana Kinondoni waliompigania kufa na kupona ili apate ubunge, bali ni kufuru kubwa sana kwa Mwenyezi Mungu ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuumbwa kwake, hakika laana ya jambo hili haitamuacha salama.
Tunamtakia kila la heri katika maisha yake mapya ya usaliti.