SoC01 Mauaji yanayohusisha wivu wa kimapenzi yanaongezeka Tanzania. Sababu, madhara na suluhisho kupunguza na kutokomeza

Stories of Change - 2021 Competition

The patriotic

Member
Aug 7, 2021
25
22
Mauaji yanayohusisha wivu wa kimapenzi
Mauaji yanayohusisha Wivu wa kimapenzi ni jambo ambalo kwa Tanzania linaongezeka kwa Kasi katika mikoa yote ambapo lisipotafutiwa ufumbuzi litaweza kugharimu maisha ya vijana wengi ambao ndio wahanga wakubwa.Vyombo vingi vya habari vimekuwa vikiripoti Vifo Kila siku .Mfano jamii forum,Habari leo na ITV

Viashilia vinavyoonyesha ongezeko la mauaji yanayohusisha wivu wa kimapenzi

.Kamishina wa oparesheni na mafunzo wa jeshi amesema kwa kiasi kikubwa mauaji yaliyotokea hapa nchini mwaka 2020 yamesababishwa na wivu wa kimapenzi
Chanzo habari leo 22/11/2020
.Nchini Tanzânia LHRC ilikusanya matukio ya mauaji 14 ya ukatili wa kimwili dhidi ya wanawake hao 2019 Kati ya hao 12 ni wanawake
Chanzo http.human right.co.tz

Sababu zinazopelekea mauaji yanayohusisha wivu wa kimapenzi yanaongezeka Tanzânia

.Ukosefu wa elimu kuhusu mahusiano

Watu wengi hususa ni vijana wamekuwa wakiingia katika mahusiano bila kujua katika mahusiano zipo changamoto zake.Mfano usaliti na vipigo jambo linalopekea akikutana na changamoto suluhisho huwa ni kutekeleza mauaji

.Mapenzi katika umri mdogo
Vijana wengi hususa ni vijana wamekuwa wakijihusisha na mapenzi katika umri ambao sio sahihi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi na pia maadili ya kitanzania ,kwa hiyo huingia katika mapenzi bila kuwa na ukomavu

.Mila na tamaduni potofu
Baadhi ya mila Tanzania zimekuwa zikishawishi na kuwalazimisha au kuwachagulia wachumba vijana mwisho wa siku madhara yanatokea kwa sababu wanaingia katika mapenzi na mtu ambaye sio chaguo lake na ikitokea wamegombana suluhisho huwa ni kumuua.

Athali za utandawazi
Utandawazi unapelekea mauaji kwa sababu filamu nyingi zinazoingia nchini zimekuwa zikifanya vijana au jamii kuiga.Mfano mwanamke akiona kwenye filamu mwanaume aliyemkosea alichoma nyumba na yeye atamani aige vile vile mwisho wa siku anapata kesi ya mauaji na kifungo Cha maisha jela vile vile huchangia kuharibika kwa tamaduni za kitanzania.

Makundi yafuatayo yawajibike na yahusishwe ile kupata suluhisho kamili

Viongozi wa kidini

Jamia nyingi Tanzania na duniani kote viongozi wa kidini wamekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha tabia mbalimbali na mienendo ya waumini kwa kutoa mawaidha na maonyo kwa mienendo ambayo haikubaliki katika jamii kwa hiyo mashehe,wachungaji,mapadre,shemasi,imamu na maaskofu wanayo nafasi
Je wafanye Nini...…?
.Watoe elimu ya ndoa
.waandae makongamano ya vijana
.Wawe washauri sahihi kwa vijanapasipo chuki na unafiki

Viongozi wa kimila
Hii ni jamii ambayo inaishi na watu mtaani na raia wanayonafasi ya kutoa elimu vijijini kuhusu ndoa na mahusiano kwa vijana wadogo

Wanasaikolojia
Saikolojia ni sayansi inayohusu akili na mienendo ya watu ,kwa hiyo jamii nyingi za Tanzania hawajui umuhimu wa Hawa wataalamu.Serikali lazima iongeze nguvu kitengo Cha saikolojia ili kitoe elimu katika jamii kuhusiana na changamoto za mahusiano na suluhisho la matatizo ya mahusiano

Vyombo vya habari
Vyombo vya habari mfano jamii forum ,magazeti yote ,televisheni vina nafasi kubwa ya kutoa madhara, suluhisho pia kuikumbusha serikali kuhusu kutilia mkazo mkubwa suala la mauaji yanayohusisha wivu wa kimapenzi
Mfano:Jamii forum inaweza kuanzisha kitengo Cha elimu ya jinsia,ukatili wa kijinsia au tangazo linalocheza cheza ili jamii ijue madhara na suluhisho la matatizo ya mahusiano

Asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali
Katika jamii mashirika yasiyo ya kiserikali yaanzishe vitengo ambavyo vitakuwa na wanasaikolojia na team ya watu ambao watatoa elimu kwa wafanyakazi,pia waanzishe taasisi zitazoshughulikia ukatili unaohusiana na jinsia

Serikali ifanye Nini?

Sheria ya ndoa ipitiwe,Tanzania msichana akimaliza masomo shule ya msingi hata Kama Bado mdogo anaweza kuolewa Jambo ambalo linafanya vijana waolewe wakiwa hawajapevuka kuhusu mahusiano.Bunge Lina jukumu la kupitia sheria upya ya ndoa

Somo lá saikolojia lianzishe mashuleni na kupewa nguvu.
Katika jamii ya Tanzania asilimia kubwa watoto wanaenda shule katika elimu ya sekondari kuwe na somo na wataalamu wa saikolojia kwa sababu wanafunzi siku hizi wanahusika katika mapenzi tangu shuleni

Kitengo Cha elimu ya kijinsia na mahusiano ianzishwe na ipewe nguvu.
Ofisi ya Raisi na waziri mkuu kushilikisha na waziri wa afya,elimu jinsia na watoto kwa pamoja washirikiane kuanzisha kitengo na kukipa nguvu.

NB:(Life is full of conflict when you fail to rationalize those conflicts become stress ,try to rationalize those conflicts)

MUHIMU:Maisha yana migogoro mingi ukifeli kuwahusisha migogoro hiyo inakuwa msongo wa mawazo ,jaribu kupunguza migogoro hiyo
Binafsi ufanye Nini migogoro inayohusisha wivu wa kimapenzi ikikuandama
.Tafuta mwanasaikolojia
.Tafuta viongozi wa kidini
.Shirikisha rafiki unayemwamini
.Wazazi Kama wao sio chanzo.
.Viongozi wa kimila

Hitimisho
Mauaji yanayohusisha wivu wa kimapenzi yanaweza kupunguza na kuisha mimi na wewe kwa kushilikiana

Natanguliza shukrani za dhati kwenu wadau na jamii forum kwa ujumla Mungu awabariki

ASANTENI SANA KARIBUNI KWA MJADALA
 
Hapa kuna kitu hakiko sawa.............Ustawi wa Jamii..kila mwaka wanatoa wahitimu wa ngazi mbalimbali katika fani hii je hawa wanaisaidiaje jamii maana;
1. Rate ya divorce inaendelea kuongezeka kwa kasi (hata wanaojitajidi kuipunguza ni kina Dr. Chriss Mauki na wengineo - ambao wao wanaifanya kama njia ya kuongeza kipato kwa maisha yao - Ustawi wa Jamii si wapo wanaosomeshwa na mikopo itokanayo na Kodi za wananchi??) ---Upatikanaji wao ukoje? Kabla mie sijajifungia chumbani na kisha kufanya maamuzi magumu, ninawezaje kuwapata na kuyasemea yaliyomo moyoni mwangu?
2. Tunalalamikia wanaojiua kwa sababu ya kudhulumiwa mapenzi/hisia za mapenzi - Hivi anapoingia kwenye dimbwi hili anakuwa na uelewa wa nafasi yake katika hili? ........Yaani mume, mchumba, mpenzi.... anakuja na sweets words........unamkubalia tena pasipo kuwaza twice then anakutenda unaamua kujinyonga, kujiua, kuumia n.k. Alternatives anazijua?

Dah
 
Back
Top Bottom