Mauaji yanayofanywa na Polisi: Chadema yataka JK aingilie kati

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Chadema imetoa taarifa kuwa haina imani na tume inayoundwa na Waziri Nchimbi kuhusu mauaji ya raia huko Morogoro kutokana na polisi kutoa maelezo yanayojikanganya na yale ya wananchi.

Hivyo chadema imemtaka Rais Kikwete kuingilia kati na kuunda tume itakayofanya uchunguzi wa matukio yote ya mauaji yanayofanywa na Polisi kwa raia wasio na hatia na kutoa tamko la kukomeshwa kwa vitendo hivyo vya polisi.

Taarifa ya Chadema imetoewa leo na John Mnyika katika mkutano wake na wanahabari.
 
Hata ww unaweza ukawa na imani na haya mapoliCCM?Upumbavu mtupu.Mbona 2015 kama inachelewa......
 
Chadema ndo hapo huwa wananiudhi!mtamwombaje JK afuatilie vifo vya makamnda aliowatuma?kama angekuwa hajafurahishwa angeshawafukuza kazi kitambo sana.Tafadhali chadema msianze kutuudhi bana!

Hivi hivi kashfa za madini eti mkampeleka Zitto kwenye kamati ya mwenye kashfa,mlitegemea nini?saa nyingine ni kama mnajipiga risasi ya mguu!
 
Si jk wala pinda anaeaminika labda wajukuu zao. Hao tuwatose tu.
c5fa40c1-1c66-51af.jpg
 
Leo ntatofautiana na CDM kumuomba dhaifu aunde "tume"? hivi toka aingie madarakani alishaunda "tume" ngapi na matokeo yake yalikuwaje? na kwa rekodi toka tupate "uhuru" hatuna records ya tume iliofanya vizuri ama mapendekezo yake yakafanyiwa kazi na watawala, ok toka kipindi cha JK...anzia tume ya Zombe ambaye ilimpatia umaarufu, tume ya madini na mpaka ya sasa ya tume ya katiba kuna jipya? naungana na MMM, CHEDEMA watumie nguvu ya UMMA kumuong'oa SAID MWEMA, tume kupoteza pesa na itakuwa yale yale ya Dr.Slaa -kesi ya nyani kumpa ngedere-
 
Kikwete asipounda tume huru atakuwa amedhihirishia Watanzania kuwa yeye ndio kinara wa mauaji na mkandamizaji wa katiba na haki za binadamu
 
Mwana Mpotevu hii rangi ya maandishi inashout sana na macho yetu wengine duh!....JK ni mtuhumiwa no 1 kama Mungi alivyosema maana serikali yake ndiyo inayofanya hayo
Yes!rangi nyekundu inaashiria hatari lakini siyo nzuri kwa kusomea hata mie naumia macho, I dont know kama anaweza badilisha coz inaumiza macho!
 
Mwana Mpotevu hii rangi ya maandishi inashout sana na macho yetu wengine duh!....JK ni mtuhumiwa no 1 kama Mungi alivyosema maana serikali yake ndiyo inayofanya hayo

Asante Prishaz nimejirekebisha kuanzia sasa
 
Leo ntatofautiana na CDM kumuomba dhaifu aunde "tume"? hivi toka aingie madarakani alishaunda "tume" ngapi na matokeo yake yalikuwaje? na kwa rekodi toka tupate "uhuru" hatuna records ya tume iliofanya vizuri ama mapendekezo yake yakafanyiwa kazi na watawala, ok toka kipindi cha JK...anzia tume ya Zombe ambaye ilimpatia umaarufu, tume ya madini na mpaka ya sasa ya tume ya katiba kuna jipya? naungana na MMM, CHEDEMA watumie nguvu ya UMMA kumuong'oa SAID MWEMA, tume kupoteza pesa na itakuwa yale yale ya Dr.Slaa -kesi ya nyani kumpa ngedere-

Mkuu, huyohuyo aliyesema JK dhaifu, ndio huyohuyo anamtaka JK aingilie kati leo
 
Back
Top Bottom