Mauaji yanayoendelea tanzania na kisa cha mtego wa panya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji yanayoendelea tanzania na kisa cha mtego wa panya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chona, Sep 5, 2012.

 1. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Kisa hiki si kigeni masikioni pa wengi lakini pia nishikuru ndugu yetu Majjid Mjengwa kwa kukiweka katika maandishi nami nimetumia maandishi yake kuwakumbushia watu.

  Ndugu zangu,  Kuna kisa cha mtego wa panya uliosababisha madhara hata kwa wasio panya.

  Panya kwenye nyumba aliubaini mtego wa panya uliowekwa uvunguni mwa kitanda na mwenye nyumba.


  Panya yule akamwendea jogoo wa mwenye nyumba. Akamwambia; " Ewe jogoo, kuna mtego umewekwa uvunguni mwa kitanda. Tusaidiane namna ya kuutegua kabla haujatudhuru wote".


  Jogoo akajibu; " Ondoka zako, mie mtego wa panya unanihusu nini wakati sina kawaida ya kufika uvunguni mwa kitanda!"


  Panya yule akaenda hadi kwa mbuzi wa mwenye nyumba. Akamwambia; " Ewe mbuzi mwema, unajua kuna mtego wa panya uvunguni mwa kitanda cha mwenye nyumba. Tusaidiane mawazo ya kuutegua kabla haujatudhuru sote".


  Mbuzi akajibu; " Hivi tangu lini ukaniona nikiingia chumbani kwa mwenye nyumba? Mtego huo wa panya haunihusu mie mbuzi".


  Panya akaenda hadi kwa ng'ombe wa mwenye nyumba. Akamwambia; " Ewe ng'ombe wa bwana, kuna mtego wa panya umewekwa uvunguni mwa kitanda. Tusaidiane mawazo namna ya kuutegua kabla haujatuletea madhara"


  Ngombe akajibu akionyesha mshangao;
  " Sijapata kusikia jambo la ajabu kama hilo. Yaani, mie ng'ombe nidhurike na mtego wa panya ulio uvunguni mwa kitanda! Hilo halinihusu."


  Basi, ikatokea siku moja, nyoka akaingia chumbani kwa mwenye nyumba. Katika kutambaa kwake uvunguni mwa kitanda, mkia wa nyoka ukanasa mtegoni. Kishindo kilisikika.


  Mwenye nyumba alikwenda kwa furaha akiamini hatimaye panya aliyekuwa akimsumbua sasa amenaswa. Hapana, ni nyoka aliyenaswa mkia. Na ni mwenye hasira pia. Akamng'ata mguu mwenye nyumba. Sumu kali akamwachia. Mwenye nyumba akafa.


  Jirani wakafika msibani. Siku ya kwanza watu walikuwa wachache. Wakahitaji kitoweo . Akakamatwa jogoo wa mwenye nyumba achinjwe.


  Siku ya pili watu wakaongezeka. Kilihitajika kitoweo pia. Akakamatwa mbuzi wa mwenye nyumba ili achinjwe.


  Na siku ya maziko watu wakawa wengi zaidi. Akakamatwa ng'ombe wa mwenye nyumba ili achinjwe.  Ni jogoo, mbuzi na ng'ombe wa mwenye nyumba walioamini kuwa madhara ya mtego ule wa panya yasingewahusu wao. Walikosea. Panya alikuwa sahihi, na wala mtego haukumdhuru panya!

  Mtazamo wangu

  Watanzania tumekuwa ni watu wakupokea habari mbaya za matukio ya mauaji ya kutisha. Matukio haya hayajaanza leo wala jana lakini tumekuwa ni watu wa kukaa kimya bila kuchukua hatua. Kuna visa vingi sana vimetokea ambavyo vilitakiwa kutuamsha watanzania na kupiga kelele kupinga mauaji, mateso na vurugu zinazoendelea nchini. Tatizo tumekuwa wabinafsi kama ule ubinafsi uliooneshwa na Jogoo, Mbuzi na Ng'ombe kwenye kisa hiki. Tumekuwa tukidhani kuwa labda mambo hayo hayatuhusu. Lakini legea kisa hicho kitakufungua macho. Janga la mwenzio ni janga lako.
  Miaka kadhaa iliyopita kulitokea mauaji Arusha kwasababu ya wananchi wasiokuwa na silaha kuandamana. Wengine wakadhani hayawahusu kwa sababu wao si wapenzi wa siasa. Lakini wakasahau kuwa kuandamana ni haki ya kila mmoja. Walichokuwa wanakidai kilikuwa ni haki yao ya msingi. Lakini je tulifanya nini kuhakikisha kitu hicho hakijirudii!!!!! Watanzania Kimya!!!

  Baada ya hapo kukatokea vurugu huko Mwanza hata wabunge wakakatwa mapanga. Tumekuwa tukisiakai mauaji yaliyofanywa kule kwenye machimbo ya Nyamongo tumekaa kimya. Yametokea mauaji Songea, Morogoro na sasa Iringa tumekaa kimya.

  Madaktari wakaja na kilio chao amabacho kingeponya huzuni yetu, tena kikiwa na mikakati ya kusaidia kuboresha huduma za afya nchini kwetu. Wamejaribu kwa uwezo wao, sisi watanzania tumekaa kimya tukidanganyika na propaganda za "hao wanataka mishahara mikubwa" lakini hawazungumzii vipi kuhusu vitendea kazi vyao. Watanzania tumebaki kimya kama watazamaji. Huku wale wanafunzi waliokuwa wanafanya internship wakiwa mitaani. Walifanya hivyo ili watusaidie sisi watanzania. Ni mara ngapi unafika hospitali unafanyiwa vipimo unaambiwa vipimo vingine nenda hospitali za private ambazo zinatoza hela nyingi. Unaandikiwa dawa unaambiwa dawa zimeisha kanunue pharmacy.

  Kimekuja kisa cha Dr Stev Ulimboka na mabwepande. Namwombea Mungu azidi kumpa ulinzi na afya njema. Yeye alikuwa ni kiongozi tu, mtumishi mwaminifu kwa watu wake. Akasimamia kile walichokiamua na wenzake bila usaliti. Maono yao makubwa ni kuona sekta ya afya inaimarika, kwamba hata kama huna hela unaweza kupata huduma bora kwenye hospitali zetu za serikali. Unaweza kufanyiwa vipimo bila daktari anaye kuhudumia kupata vikwazo vya vifaa duni. Lakini pia daktari anafanya kazi yake bila manunguniko. Kilichotokea kila mmoja anajua na Dr Ulimboka kabla ya kwenda South Africa alituambia kila kitu na Gazeti la Mwanahalisi likadadavua kila kilichokuwa kimebaki na shaka. Sasa sisi wananchi tumechukua hatua gani? Tumekuwa watu wa kunungunika bila kuchukua hatua. Wengine wanataka Dr Ulimboka ajitokeze aeleze kila kitu, najiuliza ni kitu gani ambacho hatujui mpaka sasa. Tunahitaji kujua nini zaidi ili tuchukue hatua? Tumefanyiaje kazi taarifa za awali. Ni wapi tumekwama ili atupatie taarifa za kusonga mbele.

  Mifano ipo mingi sana, lakini yoyote inarudisha majibu kwetu, kwamba ni wajibu wetu kuwajibika. Wale tuliotegemea watusemehe hawasemi, na hata wanaposema hawasemi ukweli. Wamekuwa watumwa wa wakubwa zao na si sisi wananchi. Wamebaki kulamba viatu vya wakubwa na kuwapamba. Huku hali inazidi kuwa mbaya wao wanasema uchumi wa nchi unakuwa na maisha bora kwa wananchi yamepatika. Wakati tunaambiwa serikali haina hela ya kutosha kuboresha huduma ya afya tunashuhudia wagari ya kifahari kama VX yakizidi kununuliwa kwa ajili ya watendaji wa serikali.

  Inasikitisha zaidi kuona polisi wanaotakiwa kuwalinda raia wangeuka na kuwa wauhaji wa raia. Hii halikubaliki hata kidogo. Sasa tuseme hapana kwa mauaji, majina yao tunayajua. Mahali wanapo ishi tunapajua. Wawe kwenye magwanda hao kwenye nguo za kiraia tutawafikia. Wapo wengine wanaodhani wapo salama kwa kuwa wanakubaliana na kuwatumika wenye dola. Kumbuka huu ni mtego wa panya. Leo kwa wengine kesho kwao. Nao tunawajua kwa majina, mahali wanapoishi na kwa kila hali. Hawapo salama pia. Hasira za watu waliochoka kuonewa na kukandamizwa ni mbaya sana.

  Natoa mwito tuanze kuwatambua kwa majina wahusika wote wa mauaji yote. Tukiacha yaendelee, basi, yeyote yule, bila kujali dini, rangi, itikadi au hata wadhifa wake, anaweza kuwa mhanga wa maovu haya. Wakati wao wanadhani sisi ni wanyonge, hatuna dola wala silaha watakuja kugundua kuwa kumbe dola na silaha zao si chochote mbele ya wananchi waliokata tamaa ya jinsi mambo yanavyokwenda. Tujinasue kwenye mtego wa panya kwa kutafuta ufumbuzi mapema, tusidhani yanayoendelea hayatuhusu. Mauaji haya si ya watu flani au kikundi flani. Yanaweza kukukuta wakati wowote wahali popote. Hii ni vita na vita haina macho.

  Shime tuungane na tuache woga, Tanzania tunayoitaka ipo mikononi mwetu


   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mabwepande wameshika mpini sisi raia tumeshika makali! tukianza kuvutana nani ataumia??
  Watawala wamejisahau kabisa as if watatawala milele.Ukiua raia utatawala wanyama?? Newton's third law of motion states that for every action there must reaction which acting in opposite direction in order to balance that action.
   
Loading...