Mauaji yaliyojaa utata

NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA

Sehemu ya Sita.

“Tunahitaji kukulipa kiasi cha dola milioni moja kwa kutufanyia kazi moja tu, yaani kazi moja tu,” alisema Dragon mara baada ya kumrudia Benjamin.
“Kazi gani?”
“Najua ushaijua, tunataka huyu Carter kuuawa haraka sana!” alisema Dragon.
“Carter kuuawa?”
“Ndiyo! Na tumeona hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya hivyo zaidi yako!” alisema Dragon huku akimwangalia Benjamin usoni.
“Kwa nini mimi?”
“Kwa sababu una akili! Benjamin, kati ya vijana wote hapa Marekani, hakuna mwenye akili zaidi yako! Tumeamua kukupa kazi hii kwa kuwa tunaamini utaifanya kiakili na isigundulike kabisa,” alisema Dragon.
“Hapana! Siwezi kuua!”
“Benjamin! Umesahau tulichokwambia! Unataka Vivian auawe?” aliuliza Dragon. Benjamin akabaki kimya.
Siku hiyo, Benjamin hakukubali kabisa kufanya mauaji hayo, hakutaka kuona akitenda dhambi ya kuua, kwake, alikuwa tayari kufanya kitu chochote lakini si kuua.
Hakuumficha Dragon, alimwambia kweli kwamba hakutaka kuua na wala hakutegemea kufanya kitu kama hicho maishani mwake. Jibu hilo lilimkera Dragon, akachukua simu yake na kwenda pembeni, huko, akampigia simu bosi wake, Bwana Seppy na kumwambia kwamba Benjamin alikataa kufanya walichomtaka kukifanya.
“Una uhakika amekataa?”
“Ndiyo bosi! Amekataa katakata!”
“Kamtekeni Vivian, hakuna zaidi ya hilo,” aliagiza Bwana Seppy na kisha kukata simu.
Hayo yalikuwa maagizo ambayo yalitakiwa kufanyika haraka sana. Alichokifanya Dragon ni kuwapigia simu vijana wengine na kuwaambia kile kilichotakiwa kufanyika. Walimfahamu Vivian hivyo walichokifanya ni kuahidi kwamba msichana huyo angetekwa haraka iwezekanavyo!
****
Japokuwa alibembelezwa sana lakini Benjamin hakutaka kukubaliana nao hata kidogo, hakuwa radhi kumuua mtu yeyote yule kwa kipindi hicho. Mbali na hiyo yote, hakutaka kuamini kama watu hao wangeweza kumteka mpenzi wake.
Dragon hakutaka kuzungumza naye sana, akamruhusu kuondoka huku akimtakia maisha mema. Benjamin akasimama na kutoka nje ya chumba kile, alipofika nje, akakuta gari likiwa linamsubiri na hivyo kuamriwa kuingia, alipoingia tu, akafunikwa macho yake kwa kutumia kitambaa na kisha safari kuanza upya.
Safari hiyo ilichukua dakika arobaini, gari likasimama na kisha kuteremshwa. Sehemu aliyoteremshiwa ilikuwa kwenye uwanja uleule ambao alikula baga na kisha kupoteza fahamu, baada ya kushushwa, watu hao hawakutaka kusubiri, wakaondoka zao.
Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya Benjamin ni kuchukua simu yake na kisha kumpigia mpenzi wake, Vivian, alitaka kusikia kama alikuwa salama lakini pia alitaka kumwambia kuwa ni lazima kuondoka kuelekea Los Angeles kwani hapo Washington DC walipokuwa hakukuwa salama kabisa.
Simu ikaanza kuita, iliita na kuita lakini haikuwa ikipokelewa. Hali hiyo ikamtia hofu Benjamin kwa kuhisi kwamba inawezekana mpenzi wake huyo tayari alitekwa na watu hao. Hofu ikamjaa moyoni mwake lakini huku akiwa anafikiria mambo hayo yote, mara simu hiyo ikapokelewa.
“Upo wapi mpenzi? Unanitia wasiwasi mwenzio?” aliuliza Vivian kwenye simu.
“Kuna sehemu nipo, nimekuwa na hofu sana, upo salama hapo nyumbani?” aliuliza Benjamin.
“Ndiyo!”
“Kweli?”
“Ndiyo! Kuna nini kwani?”
“Hakuna mtu aliyekuja hapo nyumbani?”
“Hakuna! Kwani kuna nini?”
“Subiri! Nakuja!”
“Unanitia wasiwasi mpenzi!”
“Usijali! Nakuja!”
Benjamin akakata simu, akashusha pumzi nzito, kidogo moyo wake ukawa katika hali ya kawaida, kumsikia mpenzi wake akiwa mzima wa afya, kwake ilikuwa ni furaha tele.
Alichokifanya ni kukikodi taksi na kisha kuanza kuelekea mahali alipokuwa akiishi, kwenye apartment ambazo hazikuwa mbali sana kutoka mahali hapo alipokuwa.
Ndani ya gari alionekana kuwa na mawazo mengi, kichwa chake kilichanganyikiwa, maneno aliyoambiwa na mwanaume yule aliyemfuata pale chumbani yalimchanganya sana, hakuamini kama kweli kulikuwa na watu waliokuwa wakifanya mpango wa kumuua msanii Carter ambaye kwa kipindi hicho, yeye ndiye alikuwa top.
Kutokana na foleni za hapa na pale, teksi ilichukua dakika ishirini ndipo ikaingia katika eneo lililokuwa na apartment alizokuwa amepanga. Kwa harakaharaka akateremka kutoka ndani ya teksi ile na kuanza kuelekea ndani.
Kitu ambacho kilikuwa akilini mwake kwa wakati huo ni kumwambia mpenzi wake kwamba walitakiwa kuondoka kwani mahali hapo hakukuwa salama tena.
Baada ya kupandisha ngazi, akaufuata mlango wa chumba chake, kitu kilichomshtua ni pale alipoukuta mlango ukiwa wazi. Kwanza akashtuka, mapigo ya moyo yakaanza kudunda kwa kasi, hakuamini alichokuwa akikiona, hapohapo akaufuata mlango na kuingia ndani.
Mito ya makochi ilikuwa chini, sebule ilikuwa shaghalabaghala, akaanza kumuita Vivian lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyeitikia. Hakuishia hapo sebuleni, akaenda chumbani, bafuni mpaka jikoni, kote huko mpenzi wake hakuwepo.
“Vivian...Vivian...” aliita kila hatua lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyeitikia.
Benjamin akatoka ndani ya vyumba hivyo na kuelekea nje kabisa, alizunguka katika eneo zima lililokuwa likizunguka apartment hiyo, tena huku akimuita mpenzii wake lakini hakuitikiwa, msichana huyo hakuwepo kabisa.
Alichokifanya ni kuchukua simu yake na kuanza kumpigia tena, simu haikuwa ikipatikana kabisa kitu kilichomchanganya kupita kawaida. Hakuwa na jinsi, akapiga polisi na kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea.
“Where are you?” (Upo wapi?) ilisikika sauti ya polisi kutoka upande wa pili.
“West Mania Street, block number 45,” (Mtaa wa West Mania, nyumba namba 45) alijibu Benjamin.
“We are on our way,” (Tupo njiani)
Ndani ya dakika sita tu, tayari polisi wakafika mahali hapo na kuanza kumuuliza Benjamin juu ya kile kilichokuwa kimetokea. Aliwaelezea vizuri lakini katika maelezo yake yote hakutaka kuwataja watu waliokuwa wamemteka.
“Wewe ulikwenda wapi?” aliuliza polisi mmoja.
“Kununua vyakula...”
“Ulichukua muda gani kwa kwenda mpaka kurudi?”
“Nusu saa tu!”
“Na mara ya mwisho kuzungumza naye?”
“Kama dakika ishirini kabla ya kufika nyumbani!”
“Alikwambiaje?”
“Hakuna chochote, alikuwa akinisubiri tu,” alijibu.
Polisi wale walikuwa wakimuuliza huku macho yao yakiangalia huku na kule, walichokifanya nao ni kupiga simu kituoni na kutoa taarifa kwa kifupi juu ya kile kilichokuwa kimetokea kisha kuondoka mahali hapo.
Usiku haukuwa na amani tena, muda wote Benjamin alikuwa akimfikiria mpenzi wake, alikosa furaha, kuna kipindi alikuwa akiona kama alifanya kosa kukataa kufanya kile alichoambiwa akifanye lakini kuna kipindi aliona ni bora alivyokataa kwani moyo wake haukuwa radhi kabisa kuua.
Alijilaza kitandani huku akiwa na mawazo tele, muda mwingi polisi walikuwa wakimpigia simu na kuzungumza naye, walitaka kufahamu nini kilikuwa kikiendelea.
Ilipofika saa tano usiku, simu yake ikaanza kuita, harakaharaka akaipokea na kuanza kuongea na mtu wa upande wa pili.
“Upo tayari?” lilikuwa swali aliloulizwa mara baada ya simu kupokelewa, kwa mbali akaanza kusikia sauti ya mpenzi wake, alikuwa akilia huku akiomba msaada.
“Mpenzi wangu yupo wapi?” aliuliza Benjamin.
“Yupo salama, hajapigwa wala kujeruhiwa. Upo tayari au tumuue?” aliuliza mtu huyo aliyekuwa akizungumza kwenye simu.
Benjamin hakujibu kitu, alibaki kimya huku simu yake ikiwa sikioni mwake. Alichanganyikiwa, alimpenda sana mpenzi wake lakini kwa upande wa pili, hakuwa tayari kuua, hakutaka kudaiwa damu ya mtu mikononi mwake.
“Tunakupa dakika ishirini za kujifikiria, baada ya hapo, tutajua nini kinachofuata,” alisema mwanaume huyo na kisha kukata simu huku akiahidi kupiga tena baada ya dakika ishirini. Benjamin akashusha pumzi nzito.
Benjamini alibaki kimya chumbani kwake, hakuamini kwamba mwanzo wa kila kitu ungekuwa namna ile, alibaki akiiangalia saa yake ya mkononi, muda ulikuwa ukikimbia mno, tena zaidi ya siku nyingine.
Alitamani kuwapigia simu polisi na kuwaambia kilichokuwa kikiendelea lakini hakutaka kufanya hivyo kwani watu ambao alitaka kuwapa taarifa polisi kuhusu wao tayari walikuwa na mpenzi wake, hivyo alitakiwa kubaki kimya huku akiwa na muda wa kufikiria nini cha kufanya.
Hakujua sababu ya watu hao kutaka kumuua Carter, kwake, kijana huyo alionekana kuwa mpambanaji, alipambana katika maisha yake yote ili apate umaarufu na hatimaye atengeneze pesa, sasa iweje aje amuue mtu kama huyo na wakati kulikuwa na watu ambao walikuwa wakila kwa mgongo wake? Moyo wake ukamhukumu, hakutakiwa kufanya hivyo ila kila alipofikiria kwamba mkewe alishikiliwa mateka, hakujua nini alitakiwa kufanya.
Baada ya kujifikiria kwa muda, kichwani mwake likaja wazo moja kwamba ni lazima alifanye haraka iwezekanavyo na hatimaye kukimbia. Dakika ishirini zilipofika tu, akasikia simu yake ikianza kuita, hapohapo akaipokea.
“Umefikiria nini?” aliuliza mwanaume aliyekuwa upande wa pili.
“Nitamuua kwa ajili ya mpenzi wangu! Ila nitajuaje kama mpenzi wangu atakuwa salama baada ya kufanya kazi yenu?” aliuliza Benjamin.
“Usijali, hatuwezi kukusaliti katika hilo!”
Benjamin alijiamini, watu hao waliamua kumtafuta kwa kuwa walimuona kuwa na akili mno hivyo naye akataka kulidhirisha hilo, alitaka kuwaonyeshea kwamba yeye alikuwa na akili hata zaidi yao.
Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya ni kumpigia simu rafiki yake, David Belshaaz, Musraeli aliyekuwa akisoma naye, yeye alikuwa akichukua masomo ya kompyuta, na alikuwa mtu hatari sana.
“Vipi?” aliuliza David.
“Naweza kukutana nawe sehemu fulani kuongea?” aliuliza Benjamin.
“Ngoja niangalie ratiba yangu ya kesho!”
“Si kesho, nataka tuonane sasa hivi tuzungumze,” alisema benjamin.
“Kuna nini tena?”
“Naomba tuonane David, kuna kitu.
“kipi?”
“Wewe tuonane kwanza!”
“Mbona unanitisha?”
“Usijali!”
“Kuna usalama?”
“Ndiyo! Wewe tuonane!”
“Sawa!”
Baada ya kukubaliana kwamba wangeonana usiku wa siku hiyo, simu ikakatwa. Benjamin bado alikuwa na mawazo tele, hakujua kama katika kipindi hicho mpenzi wake alikuwa salama au la.
Baada ya dakika ishirini, akapigiwa simu na David na kumwambia kwamba alikuwa katika mgahawa wa KFC ambao haukuwa mbali kutoka katika apartment alizokuwa amepanga Benjamin, hiivyo akatoka na kwenda kuonana naye.
“Kuna nini?”
“Yaani nimechanganyikiwa!”
“Kuna nini?”
Hapo ndipo Benjamin alipoanza kumuhadithia David kile kilichokuwa kimetokea, wakati wote wa kusimulia alionekana kuwa na majonzi tele, kitendo cha mpenzi wake kutekwa kilimuumiza sana moyoni mwake.
Hakutaka kuficha kitu chochote kile, alimwambia wazi David ili kama kusaidiwa, asaidiwe kutokana na tatizo lililokuwa mbele yake. David alimsikiliza kwa makini, suala hilo lilikuwa kubwa kwani aligundua kwamba mtandao ambao ulimteka Vivian ulikuwa mkubwa na wenye watu wengi, hivyo walitakiwa kuwa makini.
“Itawezekana kweli kumpata Vivian?” aliuliza Benjamin.
“Kama tukiungana, tutampata tu. Ninataka unisaidie!”
David alikuwa mtaalamu wa mambo ya kompyuta, alijua kucheza nazo, alisomea mpaka pale alipopata PhD. Hakuipenda kompyuta alipokuwa mkubwa, tangu alipokuwa mdogo, alikuwa mtundu na hivyo kumfanya kugundua mambo mengi katika kompyuta.
Yeye ndiye alitengeneza virusi vilivyojulikana kama Y2K ambavyo viliaminika kuzima kompyuta zote duniani mwaka 2000, yeye ndiye aliyekuwa akiingia kwenye system za Urusi, anaiba data na kuwapa Wamarekani. Yeye ndiye aliyewaambia Wamarekani kwamba Iraq ilikuwa ikitengeneza mabomu ya nyuklia, kipindi cha kwanza walikataa lakini baada ya kuwaonyeshea data alizoziiba kwenye komyuta zao, wote wakaamini.
Alikuwa mtaalamu sana, sasa kitu ambacho Benjamin alikitaka ni kujua mahali alipokuwa mpenzi wake na vilevile kumgundua mtu aliyekuwa akihusika katika mpango wa kumuua Carter.
“Don’t worry, this is tracking issues, I will let you know, give me the damn number,” (Usijali, haya ni mambo ya kutraki, nitakutaarifu, naomba hiyo namba) alisema David na Benjamin kumpa namba hiyo.
Baada ya kukubaliana kwamba kazi ingefanyika, kila mmoja akaondoka huku Benjamin akiwa na uhakika kwamba rafiki yake huyo angefanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba mpenzi wake anajulikana mahali alipokuwa na hata mtu aliyekuwa nyuma ya mchezo mzima anajulikana.
Usiku mzima Benjamin hakulala, alikuwa na mawazo tele, bado alichanganyikiwa, alimpenda sana mpenzi wake lakini hakuwa tayari kuona akiua, tena kumuua mtu kama Carter.
“Nitafanya ujanja, subiri...” alijisemea Benjamin.
Ilipofika asubuhi, akapigiwa simu na kuulizwa kama alikuwa tayari, akampa taarifa kwamba alikuwa tayari kitu kilichohitajika ni kuambiwa namna ambayo ingefanikisha kumpata huyo Carter.
“Unakumbuka nilikwambia nini?” aliuliza mwanaume aliyekuwa akizungumza naye kwenye simu.
“Nini?”
“Una akili sana!”
“Nimekumbuka, kwa hiyo?”
“Wewe unajua ni jinsi gani unaweza kumpata Carter, naomba ufanye hivyo, hakikisha anapatikana na unamuua...au unataka tumuue Vivian?” aliuliza mwanaume huyo kwa sauti ya mkwara.
“Hapana mkuu! Naomba usifanye hivyo!”
“Basi fanya kazi yako!”
Kilichokuwa kikihitajika ni kuonana, Benjamin hakutaka kutumia kiasi chake cha fedha hivyo ilikuwa ni lazima apewe kiasi cha pesa ambacho ndicho angekitumia katika harakati zake za kumuua Carter.
Hilo wala halikuwa tatizo hata kidogo, akaonana na mwanaume mmoja ambaye akamgawia kiasi cha dola laki tano ambacho angekitumia katika kumuua Carter au vinginevyo kuuawa yeye.
Alipozipata hizo fedha, kitu cha kwanza ni kuanza kufuatilia ratiba ya Carter ilisemaje. Katika ufuatiliaji wake huo akagundua kwamba baada ya wiki moja msanii huyo angekwenda Miami kwa ajili ya kupiga shoo na angefikia katika Hoteli ya Samson And Delilah, hivyo naye akaenda huko haraka sana kwa ajili ya kukamilisha mchakato wake, baada ya hapo, mpenzi wake angeachiwa huru.
****
Carter hakuwa mtu wa kutulia, kila siku ilikuwa ni kwenda huku na kule akifanya shoo. Alichoka sana lakini hakutaka kuacha, ilikuwa ni lazima kufanya hivyo kwani maisha yake ndivyo yalivyotaka kufanya hivyo. Kuna kipindi alikuwa akionekana mgonjwa, alipoteza hamu ya kula na alipokwenda hospitali, daktari alimwambia kwamba alichoka.
Watu walimuonea huruma Carter lakini hakukuwa na mtu aliyemwambia asubiri, asiende sehemu kupiga shoo na wakati kila mtu alikuwa na hamu ya kumuona.
Kila siku alipokea shoo mbalimbali, tena nchini Marekani na hata nje ya nchi hiyo. Baada ya kuzunguka kwa kipindi kirefu, akaamua kupumzika nyumbani kwake jijini New York kabla ya kuanza tena ziara zake kama kawaida.
Katika kipindi hicho cha mapumziko ndipo alipopokea mwaliko wa kwenda kufanya shoo katika shule yake aliyosoma kipindi cha nyuma iliyokuwa huko Miami. Kwanza alichoka, hakutaka kwenda huko lakini kila alipotaka kuwaambia, hakuona kama lingekuwa jambo jema.
Hakutaka kulipwa kiasi chochote kama sehemu nyingine, Shule ya St. Peter ilikuwa ni kama yake, alipendwa sana huko na kila mwanafunzi alijisikia fahari kusoma shule ambayo Carter alisoma hivyo kwenda huko, hata kama alikuwa amechoka hakuwa na jinsi, ila wao walitakiwa kuingia gharama, hasa hoteli ya kufikia.
“Nataka nifikie kwenye hoteli nzuri tu ambayo itakuwa na ulinzi hasa kwa mashabiki zangu,” alisema Carter.
“Hakuna tatizo! Samson And Delilah itafaa?”
“Ndiyo! Hakuna tatizo!”
Baada ya siku mbili, alikuwa ndani ya ndege yake binafsi akielekea Miami. Ndani ya ndege alikuwa na meneja wake na marafiki zake watatu, hakutaka kwenda na mpenzi wake kwani msichana huyo hakuwa mpenzi wa safari na alijua kwamba kama angekwenda huko, basi angeumia moyo wake kutokana na wanawake kumpapatikia sana mpenzi wake.
Hawakuchukua muda mrefu angani wakawa wamekwishafika Miami ambapo wakateremka na kisha kutoka nje ya uwanja huo. Watu wengi walikuwa wamejazana nje, walimsubiria tangu asubuhi mpaka mchana wa siku hiyo.
Mikononi walikuwa na mabango yaliyoonyesha kumkaribisha ndani ya Miami. Moyo wake ukafarijika sana, hakuamini kama kweli wale waliokuwa wamejitokeza walitoka katika shule ambayo alisomea.
Wengi wakamsogelea na kuanza kupiga naye picha, si wao tu bali hata wasafiri wengine waliokuwa na safari zao, walimfuata, wakampiga picha na kisha kujipiga pamoja naye.
Baada ya shamrashamra za hapo kumalizika, safari ya kuelekea hotelini ikaanza. Ulinzi wa magari ulikuwa mkubwa, wengi hawakuamini kama kweli Carter alifika hapo Miami na alikuwa tayari kwa kufanya shoo moja kubwa jijini hapo.
Hotelini, watu wengi walikusanyika, kila mmoja alitaka kumuona Carter, wengine waliposikia kwamba mtu huyo alikuwa katika hoteli hiyo, hawakutaka kupitwa, nao harakaharaka wakasogea na kutaka kuingia ndani ya hoteli hiyo.
“Subiri! Tukutane kesho uwanjani...” alisema mpambe wake huku akiwaangalia.
“Hatuondoki, kama kubaki, ngoja tubaki, tunataka kumlinda Carter wetu,” alisikika mwanaume mmoja mwenye mwili mkubwa, wengine nao wakamsapoti, hawakutaka kuondoka, walikuwa radhi kulala hapohapo nje, kama kupigwa na baridi, walikuwa tayari lakini si kuondoka mahali hapo.
Wakati hayo yote yakiendelea, tayari Benjamin alikuwa amekwishafika ndani ya hoteli hiyo, alikuwa mteja ambaye alifanya juu chini kuzoeana na dada wa mapokezi pamoja na msafisha vyumba.
Alikuwa mzungumzaji sana, mcheshi ambapo watu hao wawili walimsifia sana na muda mwingi walitamani kuwa karibu naye. Katika kipindi cha wiki moja alichokaa katika hoteli hiyo, alizoeleka sana.
“Unajua u msichana mzuri sana Rose,” alimwambia dada a mapokezi.
“Nani? Mimi?”
“Ndiyo! Una tabasamu zuri sana, macho ya goroli, umbo namba nane, hakika namuonea wivu sana shemeji,” alisema Benjamin huku akimwangalia msichana huyo wa mapokezi.
“Hahaha! Usitake nicheke! Kwenye wazuri na mimi nipo!”
“Ndiyo hivyo! Hebu subiri nikupige picha,” alisema Benjamin, hapohapo akatoa simu na kumpiga picha kisha akamgawia.
“Hebu itazame hiyo picha, ushawahi kukutana na msichana mrembo kama huyo?” aliuliza Benjamin huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
“Jamani! Unanionea hivyo!”
“Kweli! Natamani siku nijikute nikiwa nawe...yaani ghafla tuwe chumbani, hakika hautojuta, nitakufanya uhisi kama siku hiyo ni siku yako ya kuzaliwa!” alisema Benjamin.
“Kweli?”
“Huwa sitanii! Utani kwangu dhambi!”
Walibaki wakicheka kwa dakika kadhaa kisha kuondoka kuelekea chumbani kwake. Wakati amefika katika korido, akakutana na msichana Mercy, msichana wa usafi aliyekuwa amezoeana naye kama ilivyokuwa kwa Rose.
“Kwa mbali namuona mrembo wangu...” alisema kwa sauti huku uso akiwa ameuachia kwa tabasamu pana.
“Hahah! Umeanza!”
“Kweli tena! Unajua sana kufanya usafi, ningekuwa na msichana kama wewe, hakika ningejiona kuwa mtu mwenye bahati sana,” alisema Benjamin huku akiwa amemsogelea msichana huyo.
“Mmh!”
“Ndiyo hivyo! Una ngozi nzuri sana, nywele ndefu, unanukia sana, hivi unatumia manukato gani?” aliuliza Benjamin.
“The Prince!”
“Waoo!”
Kama kawaida yake alitafuta uhuru, alitaka kufanya mambo yake huku akiaminiwa kwa asilimia mia moja. Baada ya kumsifia sana Mercy, akaingia ndani ya chumba chake na kutulia.
Chumbani alikuwa na mawazo tele, kitu kilichobaki mbele yake kilikuwa kimoja tu, kumuua Benjamin na kisha kuendelea na mambo yake likiwepo la kumpata mchumba wake na kuondoka naye.
Siku hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kusuka mipango yake, alitaka kuhakikisha siku inayofuata anamuua Carter na kuondoka zake. Hilo lilionekana kuwa kazi kubwa lakini alikuwa na uhakika kwamba angefanikiwa kama kawaida. Alipokuwa kwenye mawazo hayo, mara simu yake ikaanza kuita.
“Vipi?” alikutana na swali hata kabla ya salamu!
“Nimefanikiwa kufika, na yeye amefika!”
“Umemuona?”
“Ndiyo!”
“Kwa hiyo unakamilisha lini mchakato huo?” aliuliza mwanaume huyo.
“Nafikiri kesho baada ya shoo!”
“Sawa! Fanya hivyo Bwana, ukishindwa, kama kawaida tunamuua huyu!”
“Msijali, nitafanikisha. Ila baada ya kumuua, nitampata Vivian kwa muda gani?” aliuliza Benjamin.
“Baada ya kifo chake kutangazwa.”
“Basi hakuna tatizo! Kesho namuua...” alisema Benjamin, hapohapo simu ikakatwa.
***
“Umefikia wapi David?” aliuliza Benjamin kwenye simu.
“Nilisahau, ila hilo si tatizo kaka, muda wowote ule nitalifanyia kazi,” alijibu David.
“Umejisahau sana kaka, wanataka kumuua Vivian,” alisema Benjamin.
“Unasemaje?”
“Ndiyo hivyo, ninataka kujua alipo kwa sasa na ndiyo maana nikakwambia lile jambo linatakiwa kufanyika kwa haraka sana,” alisema Benjamin.
“Basi sawa, nipe saa moja tu.”
Simu zikakatwa, Benjamin akatulia kitandani huku akionekana kuwa na mawazo tele, bado kichwa chake kilichanganyikiwa mno, hakuamini kilichokuwa kikiendelea maishani mwake.
Wakati mwingine aliwaza kutoroka lakini hilo lisingekuwa suluhisho hata kidogo, ilikuwa ni lazima kama kuondoka, aondoke na Vivian lakini si kumuacha.
Kumuua Carter lilikuwa jambo gumu sana lakini mpaka kufikia kipindi hicho, hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kumuua ili aweze kuyaokoa maisha ya mpenzi wake ambaye mpaka kipindi hicho bado alikuwa mateka.
Watu hawakupungua hotelini hapo, walilala huku kila mmoja akitaka kumuona Carter ambaye ndiye alikuwa gumzo duniani kwa kipindi hicho. Benjamin akasimama dirishani na kisha kuchungulia nje, watu waliolala pale nje ya hoteli ile walimfanya kuwa na huruma kumuua Carter, alijua ni kwa namna gani angewaumiza watu hao, si wao tu bali hata watu wengine duniani kote, hakika yangekuwa maumivu makubwa sana mioyoni mwao.
Kwa hatua aliyofikia, hakutakiwa kujali kitu chochote kile, kama alivyoambiwa kwamba asipofanikisha kumuua Carter basi mpenzi wake angeuawa, hivyo alitakiwa kupambana mpaka mwisho wa siku kuhakikisha kwamba mtu huyo anauawa.
Siku iliyofuata ilikuwa ni ya kihistoria hapo Miami, watu walikusanyika katika Ukumbi wa Carthebian uliokuwa katika ufukwe wa Salvador hapohapo Miami kwa ajili ya kuangalia shoo iliyoandaliwa na wanafunzi waliowahi kusoma na Carter.
Shoo ilikuwa nzuri, watu waliifurahia sana tena wengine wakichukua nafasi hiyo kupiga picha na msanii huyo huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha mno.
Wakati shoo hiyo ikiendelea huko, huku hotelini Benjamin alikuwa bize, alitamani sana kuingia chumbani kwa Carter lakini hakujua ni kwa namna gani angeweza kuingia.
Milango yote haikuwa ikitumia ufunguo, kulikuwa na kadi maalumu ambayo ulitakiwa kuichukua na mlangoni kulikuwa na sehemu ya kupitishia kadi hiyo na hatimaye mlango kufunguka.
Alichokihitaji kilikuwa ni kadi malaya ambayo angeweza kufungua kila chumba na kufanya kile alichotaka kufanya. Kabla ya kuitafuta, akaandaa sindano yake iliyokuwa na sumu ambayo aliiona kufaa sana kuchomwa Carter, baada ya kuiweka vizuri, akaanza mishemishe za kumtafuta msichanaMercy kwa kuamini kwamba alikuwa na kadi ya kufungulia milango yote kwani ndiye msichana aliyekuwa akifanya usafi wakati wageni hawapo vyumbani mwao.
Huyo ndiye alikuwa mtu muhimu, ilikuwa ni lazima kumtafuta, alichokifanya, akatoka chumbani humo na kuanza kumtafuta Mercy. Hakumuona na hakujua alikuwa wapi. Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, aliamini kwamba msichana wa mapokezi, Rose alikuwa akifahamu msichana huyo alipokuwa, hivyo akaenda huko kumuuliza.
“Mercy yupo wapi?” alimuuliza Rose.
“Wewe wa nini?” aliuliza Rose huku akionekana kuona wivu, kwa kifupi alishaanza kumpenda Benjamin.
“Nataka nimuone tu.”
“Kuna nini?”
“Kwani si kumuona tu jamani, au kuna tatizo?” aliuliza Benjamin.
“So ili mkeo nijue jamani,” alisema msichana huyo, Benjamin akamwangalia kwa macho makini, uzuri wake yeye mwenyewe ulimchanganya, ila hakutaka kujionyesha kama alipagawa.
“Kumbe tatizo lipo wapi? Si nataka kumuona shemeji wangu,” alisema Benjamin.
Rose akashusha pumzi, alimwangalia Benjamin kwa umakini, alimpenda mwanaume huyo na hakujua alikuwa akiishi wapi na alifika mahali hapo kufanya nini.
Kwa sababu kwa maneno ya Benjamin alionekana kama kukubaliana naye, akamwambia kwamba inawezekana Mercy alikuwa katika chumba cha usafi akifua mashuka kwa mashine pamoja na vitu vingine. Chumba hicho kilikuwa ghorofa ya sita, hakutaka kusubiri, akaelekea huko.
Alipandisha ngazi, hakutaka kutumia lifti kwa kuhisi kwamba angeweza kukutana naye hata kwenye korido za ghorofa nyingine. Alipofika katika ghorofa hiyo aliyoambiwa, akaelekea katika chumba kilichoandikwa laundry mlangoni, akafungua.
Mbele yake kulikuwa na mashuka mengi yakiwa yameanikwa, yalikuwa zaidi ya mia moja. Kumuona mtu wa upande mwingine ilikuwa ngumu sana hivyo alichokifanya Benjamin ni kuanza kuita.
“Mercy...Mercy...” aliita mwanaume huyo.
“Helo...” aliita msichana huyo.
Benjamin akaenda huko alipoitikiwa, alipofika, akamkuta Mercy akiwa peke yake, alikuwa akitoa mashuka kutoka kwenye tenga na kuweka kwenye mashine moja ya kufulia, hapohapo akamsogelea.
“What are you doing here?” (Unafanya nini hapa?) aliuliza Mercy huku akimwangalia mwanaume huyo machoni.
“I am here to see you baby! Is anyone here?” (Nipo hapa kukuona! Kuna mwingine hapa?) alijibu Benjamin na kuuliza.
“Nobody...” (Hakuna mtu)
Kabla ya kufanya kitu chochote kile alitakiwa kutafuta mahali kadi ilipokuwa, kwenye kuangalia huku na kule, pembeni akauona mkoba wa Mercy, akajua kwamba ni lazima ndani ya mkoba huo kulikuwa na hiyo kadi, hivyo akamchukua msichana huyo na kumpeleka kule kulipokuwa na mokoba ule.
“Kuna nini?” aliuliza msichana huyo.
“Nataka nikuone jinsi ulivyo, umezishtua hisia zangu,” alisema Benjamin huku akijifanya kuhema juujuu kimahaba.
“Jamani ndiyo unataka hapa?”
“Kwani kuna tatizo? Kuna mtu anatuona?” aliuliza Benjamin huku tayari mikono yake ikiwa imeanza kazi ya kufungua vifungo vya blauzi ya Mercy.
“Aishiiii...” alianza kutoa kelele za mahaba.
Akili ya Benjamin ilikuwa kwenye ule mkoba tu, aliihitaji kadi iliyokuwa katika mkoba ule na hakukuwa na njia nyingine ya kuipata kadi ile zaidi ya kufanya kile alichokuwa akikifanya.
Akaanza kumvua msichana huyo suruali ya jinzi aliyokuwa ameivaa na kubaki na nguo ya ndani tu, akaanza kuutalii mwili wake kwa kupanda huku na kule, kwa jinsi Mercy alivyochanganyikiwa, akaanza kufumba macho kimahaba, alichanganyikiwa mno.
“Unanukia vizuri sana...” alisema Benjamin kwa sauti ya chini karibu na sikio la Mercy.
“As..an..t..e..” aliitikia msichana huyo, mwili wake ulikuwa hoi.
Kitendo cha kufumba macho tu, Benjamin hakutaka kuchelewa, hapohapo akaupeleka mkono ule kisiri tena huku kichwa chake kuyaficha macho ya msichana huyo.
“Hii hapa...” alijisemea moyoni mara baada ya kuigusa kadi hiyo mkobani, alichokifanya ni kuichukua, akaiingiza mfukoni kisiri, kilichofuata ni kufanya mapenzi na msichana huyo ndani ya chumba hichohicho cha kufulia.

JE,nini kitaendelea?
Tukutane Jumatano.
 
NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA

Sehemu ya Pili.

“You are a killer,” (Wewe ni muuaji)
“No! I am not a killer officer, I am not,” (Hapana! Mimi si muuaji ofisa, mimi si muuaji)
“You killed them, why? Why did you kill them? Why?” (Umewaua, kwa nini? Kwa nini umewaua? Kwa nini?)
“I killed nobody officer,” (sijamuua yeyote ofisa)
Yalikuwa ni mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ndani ya chumba kimoja katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini New York. Ndani ya chumba kile, kulikuwa na kijana mmoja, kwa kumwangalia, alikuwa na miaka isiyozidi ishirini na tano, alikuwa mtu mwenye mchanganyiko wa rangi, mama yake alikuwa Mzungu na baba yake alikuwa mtu mweusi.
Polisi wanne waliovalia makoti makubwa ambayo nyuma yaliandikwa NYPD yaani New York Police Department walikuwa wakifanya naye mahojiano kwa sauti kubwa, walimuuliza maswali na kumwambia kwamba yeye alikuwa muuaji lakini alikataa, alikataa katakata lakini polisi hawakuacha, waliendelea kumwambia kwamba alifanya mauaji.
Polisi hao walizungumza naye kwa zaidi ya dakika arobaini, neno lao lilikuwa lilelile kwamba mtu huyo alikuwa muuaji. Kijana huyo aliyeitwa Benjamin Saunders hakukubali, aliwaambia wazi kwamba hakuwa amemuua mtu yeyote na katika maisha yake hakuwahi kuua hata siku moja.
Polisi hawakuridhika, waliendelea kumwambia hivyohivyo mpaka baada ya dakika kadhaa walipotoka ndani ya chumba hicho. Benjamin alikuwa kimya, pingu zilikuwa mikononi mwake, alilia, kila alipokiangalia kile chumba, moyo wake ulimuuma mno, hakuwahi kufikiria kwamba kuna siku angeitwa ndani ya jumba hilo kubwa la polisi na kuambiwa kwamba aliua.
Wakati akiwa humo huku akilia, mara mlango ukafunguliwa, wanaume wawili waliovalia suti nyeusi wakaingia ndani, mmoja alikuwa na begi dogo, wakachukua viti na kukaa mbele yake.
Hawakuzungumza kitu kwanza, walibaki wakimwangalia kwa muda, waliporidhika, wakachukua vitambulisho vyao na kumuonyeshea Benjamini, walikuwa ni maofisa kutoka katika Shirika la Kijasusi la FBI(Federal Bureau of Investigation).
“Naitwa Brett Phillip,” alisema mwanaume mmoja.
“Naitwa Ryan Cashman,” alisema mwingine na kunyamaza.
Benjamin akawaangalia wanaume hao usoni, walionekana kuwa makini na kazi yao. Walipoona kijana huyo ameangalia vitambulisho vyao na kujiridhisha kwamba wao walikuwa maofisa kutoka FBI, wakavirudisha vitambulisho vyao mifukoni.
“Tunajua kwamba hukuua, tunajua hilo Benjamin,” alisema Brett huku akimwangalia Benjamin usoni.
“Ndiyo! Sijaua, sijawahi kuua, na kamwe sitoua,” alisema Benjamin kwa sauti ya chini huku akijifuta machozi.
“Ila alama zote zinaonyesha kwamba uliua,” alisema Brett.
“Sijajua nini kilitokea ila sijamuua mtu yeyote,” alisema Benjamin.
“Kweli?”
“Ndiyo! Sijamuua yeyote yule.”
Alichokifanya Brett ni kuchukua begi lake aliloingia nalo humo ndani, akalifungua na kutoa karatasi fulani kisha kuiweka mezani huku akimtaka Benjamin aichukue na iangalie.
“Mungu wangu!” alisema Benjamin huku akianza kulia.
“Kweli mpaka hapo unasema hujaua?”
Benjamin akabaki kimya, kile alichokiona kwenye karatasi ile hakuamini, hakujua kitu gani kilitokea, mbele yake aliona giza na kuona maisha yake yakienda kuisha gerezani kama si kuchomwa sindano ya sumu au kunyongwa.
Mdomo wake ulikuwa mzito mno, hakuamini alichokuwa akikiangalia katika karatasi ile, akawaangalia maofisa waliokuwa mbele yake, walionekana kuwa makini na kazi zao, mtazamo waliokuwa wakiutumia kumwangalia Benjamin, ulionyesha walikuwa na uhakika kwamba kijana huyo alikuwa amefanya mauaji waliyokuwa wakimshuku.
“Una lolote la kujitetea kabla hatujakwenda mahakamani?” aliuliza Brett.
“Sikuwahi kufanya mauaji, sijui nini kilitokea...”
“Lakini alama zako zimekutwa kama ushahidi.”
“Najua, ila sijafanya mauaji......ninaanza kukumbuka, ninaweza kuwatajia aliyefanya mauaji haya, ila si mimi. Nakumbuka niliambiwa nifanye mauaji haya, nikakataa, nililazimishwa sana, niliendelea kukataa, nikaambiwa kwamba kama ninakataa, basi kuna mtu atafanya mauaji, baada ya hapo, nitaonekana mimi ndiye nimefanya mauaji. Mungu wangu! Kwanza mchumba wangu Vivian yupo wapi? Walimuua, kwa nini walimuua msichana ninayempenda?” aliuliza Benjamini huku akilia.
Maofisa wale walibaki wakimwangalia, alionekana kukumbuka kitu, kwa jinsi alivyokuwa akijitetea, hata muonekano wake ulionyesha kabisa kwamba hakuwa amefanya mauaji. Kitendo cha kusema kwamba alimfahamu muuaji, kwa maofisa hao kilionekana kuwa nafuu kwao, hicho ndicho kitu walichokuwa wakikihitaji kwani kwa jinsi mauaji yalivyokuwa yamefanyika, ilikuwa ni vigumu kumgundua muuaji.
“Sawa! Sasa muuaji ni nani?” aliuliza Brett huku yeye na mwenzake wakimwangalia Benjamin usoni.
****
Julai 4, 2010
Washington DC
Zaidi ya watu elfu tatu walikuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya Ikulu ya Marekani, White House kwa ajili ya kusikiliza hotuba kutoka kwa rais wa nchi hiyo, Barack Obama ambaye ndiye alikuwa akitimiza mwaka wa pili tangu aingie madarakani na kuwa rais wa nchi hiyo.
Watu wote waliokuwa hapo, walikuwa na bendera za nchi yao, waliipenda, waliitukuza na kuiona kuwa na thamani kuliko nchi zote duniani.
Siku hiyo ya kusherehekea Uhuru wa nchi yao tangu mwaka 1776 ambapo George Washington aliuchukua kutoka kwa Waingereza, ndiyo siku ambayo Wamarekani wote duniani huithamini kuliko siku yoyote ile.
Wanafunzi hawakwenda shuleni, wanachuo hawakwenda vyuoni, wafanyakazi hawakwenda kazini, yaani kila mtu alitakiwa kukaa nyumbani kwake, kwa wale waliokuwa mbali na Jiji la Washington, walitakiwa kubaki nyumbani na kuangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea huko kupitia runinga zao ila kwa waliokuwa Washington tena waliokuwa na nafasi, walitakia kufika katika uwanja wa Ikulu ya Marekani, White House.
Miongoni mwa watu wengi waliokuwa katika eneo la uwanja wa Ikulu hiyo alikuwepo kijana msomi kutoka katika Chuo Kikuu cha Harvard, Benjamin Saunders ambaye alibakiza mwaka mmoja kabla ya kuhitimu masomo yake.
Benjamin hakuwa peke yake, alikuwa na mpenzi wake, Vivian ambaye alisafiri kutoka Los Angeles mpaka hapo Washington kwa ajili ya kumsikiliza rais wao mweusi ambaye alitaka kuzungumza na Wamarekani wote duniani.
Kama walivyokuwa wengine, hata na wao walikuwa na bendera za nchi hiyo mikononi mwao. Muda wote walikuwa wakishangilia, walionekana kuwa na furaha mno huku wakati mwingine wakikumbatiana, hakukuwa na kitu kilichowapa furaha kama kuwa wote katika kipindi kama hicho.
Walipendana mno, hakukuwa na kitu ambacho kingeweza kuwatenganisha. Japokuwa walikuwa kwenye mafarakano ya mara kwa mara lakini muda mwingi walionekana kuwa na furaha kana kwamba hakukuwa na kitu kibaya kilichokuwa kikiendelea.
“Tukitoka hapa?” aliuliza Vivian.
“Twende nyumbani!”
“Kwako?”
“Kwani unaogopa nini?”
“Siogopi chochote, ila naweza kuchelewa masomo,” alijibu Vivian.
“Wala usijali, utawahi tu,” alisema Benjamin.
Benjamin alikuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Harvard kilichokuwa jijini Cambridge ndani ya Jimbo la Boston hapohapo nchini Marekani, mbali na kutoka katika familia iliyokuwa na fedha, Benjamin alikuwa na uwezo mkubwa chuoni. Alikuwa akichukua masomo ya uuguzi, ndoto yake kubwa iliyokuwa mbele yake ni kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini Marekani.
Hiyo ilikuwa ndoto yake, hakutaka kuiona ikipotea, katika maisha yake, alimuahidi mama yake kwamba kuna siku angekuwa daktari mkubwa wa magonjwa ya moyo nchini Marekani, baba yake alikufa kwa ugonjwa wa moyo, hakutaka kuona watu wengine wakifa na ndiyo maana alisoma sana kufanikisha ndoto hiyo aliyojiwekea.
Mpenzi wake alikuwa akisomea masomo ya uandishi wa habari katika Chuo cha UCLA (University of California, huko Los Angeles). Kama alivyokuwa Benjamin, hata naye Vivian alikuwa na uwezo mkubwa darasani, aliwaongoza wanachuo wenzake na kuonekana kufanya mambo makubwa hapo baadaye kupitia uandishi aliokuwa akiusomea.
“Ngriii...ngriii...ngriii...” ulisikika mlio wa simu ukiita, mbali na kuita, simu hiyo ilikuwa katika mtetemo.
Mlio wa simu hiyo waliusikia kwa mbali kutoka na kelele zilizokuwa mahali hapo lakini baada ya Benjamin kuhisi mtetemo huo kutoka mfukoni mwake, harakaharaka akaichukua simu hiyo.
Alishangaa, haikuwa simu yake lakini aliikuta katika mfuko wa koti lake, si yeye tu aliyeshangaa, hata msichana wake, Vivian alishangaa pia. Walibaki wakiangaliana kwa sekunde kadhaa, hawakujua ni nani aliiweka simu ile katika koti lake na wala hawakujua lengo la huyo mwekaji lilikuwa nini.
“Hiyo simu umeitoa wapi?” aliuliza MMMHHHVivian.
“Sijui, ndiyo kwanza nimeikuta mfukoni mwangu!”
“Nani amekuwekea?”
“Sijui pia.”
“Hebu pokea.”
Alichokifanya Benjamin ni kuipokea simu ile na kuita. Japokuwa mtu wa upande wa pili alikuwa akizungumza lakini Benjamin hakuweza kumsikia kutokana na kelele zilizokuwa mahali pale.
Wakati akiwa na simu hiyo sikioni, mara wanaume wawili waliovalia suti wakamsogelea, wakaanza kumwangalia na kumshika mkono huku wakimtaka wamfuate.
“Kuna nini?”
“Wewe twende tu,” alisema mwanaume mmoja, Benjamin hakuwa na wasiwasi, akaanza kuwafuata kama alivyoambiwa, hata Vivian naye hakutaka kubaki mahali hapo, naye akaanza kuwafuata huku akionekana kuwa na hofu kubwa, kichwa chake kikaanza kujiuliza mambo mengi kuhusu watu wale, walikuwa wakina nani? Akakosa jibu.

JE, nini kitaendelea?
MMMHH

Hhii ni stori ya maisha ya kweli au za kutunga
 
Madame S twendelee basi
NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA

Sehemu ya Saba

.Walichukua dakika arobaini na tano mpaka kumaliza. Mercy alikuwa hoi, hakuamini kama angeweza kukutana na mwanaume anayeweza kufanya mapenzi kama ilivyokuwa kwa Benjamin.
Hapohapo wakaanza kuvaa nguo zao na kisha kubaki wakiangaliana tu. Hakukuwa na mtu aliyesema chochote kile zaidi ya kusogeleana na kukumbatiana tu.
“Ninakupenda...” alisema Benjamin.
“Nakupenda pia.”
Benjamin hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka kurudi chumbani kwake huku tayari akiwa na kadi ile mfukoni mwake, alipofika, akaingia chumbani na kutulia.
Mpango aliokuwa nao ilikuwa ni lazima akalale chumbani kwa Carter usiku huohuo ili iwe rahisi kwake kukamilisha mpango wake. Muda ulizidi kwenda mbele, kuna kipindi alihisi kwamba angeweza kuchelewa, hivyo akaamka, akachukua kitambaa kilichokuwa na dawa za usingizi na kisha kutoka mule huku mfukoni akiwa na bomba la sindano.
Kwenye korido, hakukuwa na kamera za CCTV hivyo ilikuwa ni rahisi kwake kuingia humo ndani. Akachukua kadi yake na kuipachika katika kimashine kidogo, zikawaka taa nyekundu kwa zamu kisha kubadilika na kuwa za kijani, mlango ukafunguka.
Akaingia chumbani mule, hakikuonekana kuwa tofauti na chumba chake, vyote vilikuwa vya bei kubwa, alibaki akizungukazunguka mule, aliporidhika, akakifuata kitandani, kwa sababu kilikuwa na uvungu mkubwa kidog uliomuwezesha kupenya japo kwa tabu, akaingia humu huku akiwa na bomba la sindano na kitambaa ambacho alikiwekea dawa za usingizi.
“Ngoja nisubiri...Mungu, sifanyi hivi kwa kupenda, nimelazimishwa kwa ajili ya mpenzi wangu,” alisema Benjamin kwa sauti ndogo huku akivaa glovu mikono mwake.
Hakulala hata kidogo, alikuwa macho huku akiendelea kumsubiri Carter ambaye aliamini hakuwa mbali mpaka kufika mahali hapo. Huko uvunguni, alizima simu yake, hakutaka kufanya kosa lolote lile na kuonekana kabla hajakamilisha mpango wake.
Muda ulizidi kwenda mbele, ilipofika saa kumi alfajiri, akasikia sauti za watu nje, kwa kukadiria zilikuwa kama za watu sita, watu wale wakasogea mpaka mlangoni na kisha kuufungua.
Alikuwa Carter na wapambe wake, wakaingia ndani huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha. Muda ulikuwa umekwenda sana na hawakuwa na muda wa kupoteza, Carter akaenda bafuni, akaoga na kisha kurudi chumbani pale.
Wakapiga stori, nyingi walizozipiga hapo zilikuwa ni za kumsifia Carter kwamba alifanya kazi nzuri sana, aliwaonyeshea watu yeye alikuwa nani. Walikaa kwa dakika kadhaa mpaka muda ule ambao wengine wakaenda kulala na yeye kutulia kitandani ambapo baada ya dakika chache, akapitiwa na usingizi.
Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi kwa Benjamin kumuua Carter, hakutaka kuchelewa kule uvunguni, harakaharaka akatoka na kisha kumwangalia Carter kitandani pale, alichokifanya ni kuchukua kitambaa kile kilichokuwa na dawa ya usingizi na kisha kumkandamiza Carter kitandani pale huku kitambaa kile kikiwa usoni mwake.
Carter hakukubali, alijitahidi kuhangaika huku na kule ili kujinasua lakini ilishindikana kabisa, alikandamizwa kitandani pale na kadiri alivyovuta pumzi na ndivyo alivyokuwa akiivuta dawa ile na sekunde chache mbele, akatulia kitandani pale.
“Kazi imekwisha...” alisema Benjamin.
Mara baada ya kufanikiwa kumlevya kwa yale madawa yaliyokuwa kwenye kitambaa kile akachukua bomba la sindano aliyokuwa nayo na kisha kumchoma katika mshipa mmoja mkononi mwake ili aweze kumuua kitandani pale.
Alipohakikisha sumu ile imeingia vilivyo mwilini mwake, akachukua fedha ambazo aliambiwa aziweke ikiwepo euro, dola, yen na paundi kisha kuanza kufanya mikakati ya kutoka ndani ya chumba kile.
Hakukuwa na shida kwenye kutoka, akaufungua mlango ule na kutoka. Hakutaka kuingia chumbani kwake, akaelekea katika chumba kile cha kufanyia usafi kwa kufua mashuka na nguo kisha akaitupa ile kadi chini, pembenipembeni na kisha kurudia chumbani kwake, akavuta shuka na kutulia.
****
“Umenionea kadi yangu?” aliuliza msichana Mercy huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Kadi gani?”
“Ya milango!”
“Hapana! Kwani wewe uliiweka wapi?”
“Niliiweka kwenye huu mkoba.”
“Sasa iko wapi?”
“Ndiyo siioni.”
“Umeangalia vizuri?”
“Ndiyo! Hakuna!”
Mercy alichanganyikiwa, alikumbuka vilivyo kwamba aliiweka kadi ndani ya mkoba wake, lakini katika kipindi hicho alipokuwa akiitafuta, hakuwa akiiona. Akaondoka mahali hapo na kwenda sehemu zote alizopita lakini huko hakuona kitu.
Mercy alizidi kuchanganyikiwa, hakukumbuka kama aliuacha mkoba ule sehemu yoyote ile, mtu pekee na wa mwisho kumjia kichwani mwake alikuwa Benjamin.
“Inawezekana anajua...”
Alichokifanya Mercy ni kumpigia simu ya mezani chumbani kwake, kitu kilichomshtua ni kwamba simu iliita lakini haikupatikana. Mercy hakutaka kukata tamaa, aliendelea kupiga zaidi na zaidi lakini majibu wala hayakubadilika, bado simu ile haikupokelewa kitu kilichomtia wasiwasi mwingi.
“Au ameshaondoka?” alijiuliza.
Akaondoka na kuelekea mapokezini na kumuuliza dada aliyekuwepo hapo, hakuwa Rose, yeye aliondoka na kumuacha msichana mwingine, akamuuliza kama mteja aliyepanga chumba namba tisini na mbili alikuwa ameondoka.
“Hapana! Bado yupo,” alijibu msichana huyo.
“Mbona nampigia simu simpati?”
“Sijui! Inawezekana amelala, ila hapa inaonyesha yupo, hajaondoka,” aliongeza msichana huyo.
Mercy hakutaka kusubiri, alichokifanya ni kwenda wenyewe mpaka katika chumba kile, alipoufikia mlango, akaanza kugonga kwa nguvu, aligonga zaidi na zaidi lakini mpango wala haukufunguliwa kitu kilichoendelea kumpa maswali mengi.
“Mmh! Mbona naanza kuwa na wasiwasi...” alisema msichana huyo, akahisi akichoka, kilichobaki mbele yake kilikuwa ni kufukuzwa kazi tu, hakukuwa na kitu kingine zaidi ya hicho kwani kupoteza kadi, tena ile masta kabisa lilikuwa kosa kubwa mno.
Akaondoka na kuelekea nyumbani kwake, hakuwa na raha, alipanga siku inayofuata kuwa asubuhiasubuhi kuzungumza na Benjamin kwani bado moyo wake ulimwambia kwamba mwanaume huyo aliiona ile kadi aliyokuwa akiitafuta.
***
Asubuhiasubuhi msichana Mercy akafika hotelini hapo, bado akili yake haikuwa sawa hata kidogo, alikuwa na mawazo mengi, kadi ambayo aliipoteza usiku uliopita ilimchanganya mno.
Alipofika hotelini, hata kabla ya kufanya kitu chochote ilikuwa ni kwenda katika chumba cha Benjamin ili aonane naye na kumuuliza kuhusu kadi hiyo. Alipofika, akagonga mlango ambapo baada ya sekunde kadhaa, mlango ukafunguliwa, mwanaume aliyesimama mbele yake alikuwa Benjamin.
“Kumbe wewe...karibu mpenzi,” alisema Benjamin huku akimkaribisha msichana huyo huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
“Ahsante! Nimekuja kukuuliza kitu,” alisema msichana huyo.
“Kitu gani?”
“Nilipoteza kadi jana!”
“Kadi gani?”
Alijifanya kutokufahamu chochote kile, hata macho yake yalionyesha kabisa kwamba hakujua kilichokuwa kikiendelea. Mercy akaanza kumwambia kuhusu kadi ile ambayo aliipoteza katika mazingira ya kutatanisha huku muda wote huo akionekana kuwa na majonzi tele usoni mwake.
“Pole sana, ila umeangalia vizuri kwenye kile chumba?” aliuliza Benjamin.
“Nimeangalia kila kona.”
“Umetoa nguo zote na kuangalia vizuri?”
“Ndiyo!”
“Mmh! Sasa iweje isionekane?” aliuliza Benjamin.
“Ndiyo nashangaa!”
Alichokifanya Benjamin ni kumwambia waende kwenye kile chumba cha kufanyia usafi, alikuwa na uhakika kwamba kadi ile ilikuwa mule kwani alfajiri ya siku hiyo aliirudisha na kurudi chumbani kwake.
Mercy alikuwa na uhakika kwamba kadi hiyo haikuwepo huko, aliangalia kila kona, alitoa nguo zote na kuzirudisha lakini hakufanikiwa kuiona kadi hiyo. Benjamin alipomaliza kujiandaa, wakaelekea katika chumba hicho na kuanza kuitafuta kadi hiyo.
Kwanza Benjamin hakutaka waende kwenye ule upande alioiweka kadi ile, alimwambia Mercy waende kwenye upande mwingine kitu ambacho kikafanyika kikamilifu. Walipokosa na ndipo walipokwenda kwenye ule upande uliokuwa na kadi, kweli wakaikuta.
“Ni hii hapa,” alisema Mercy huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
“Wewe si ulisema umeikosa?”
“Ndiyo! Nilitafuta sana, nafikiri huku sikuja,” alisema msichana huyo.
Wakabaki wakiangalia tu, tayari miili yao ikaanza kuwasiliana mahali hapo, walikuwa wawili tu kama jana na kila mtu alionekana kumtamani mwenzake. Wakiwa wanaangalia kama mbuzi, wakaanza kusikia mlango mmoja huko nje ukigongwa, uligongwa huku sauti za watu zikisikika mahali hapo.
Kwanza wakashtuka, haikuwa kawaida kabisa, wakatoka chumbani humo na kwenda kwenye korido, marafiki zake Carter walikuwa katika mlango wa chumba alichochukua Carter na kuanza kugonga huku wakitaka wafunguliwe.
“Jamani, si jana amechelewa kulala, ataweza kuamka muda huu?” aliuliza Mercy huku akionekana kuwashangaa.
“Hatuna muda, tunatakiwa kuondoka sasa hivi,” alijibu jamaa mmoja.
Alichokifanya Mercy ni kwenda mapokezini ambapo huko akaanza kupiga simu ya mezani ndani ya kile chumba cha Carter, alipiga simu, iliita na kuita lakini haiupokelewa.
Hilohilo ndilo lililotokea kwa Benjamin usiku wa jana, hata naye alipojaribu kupigiwa simu hakuipokea. Wote wakaanza kushikwa na wasiwasi, wafanyakazi wa hoteli hiyo hawakutulia, wakaanza kupandisha juu mpaka kwenye korido iliyokuwa na chumba kile na kuanza kugonga.
Wakati huo Benjamin alikuwa chumbani kwake, alifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea, hakutaka kutoka nje, alitaka kuona kitu gani kingeendelea.
Mara akasikia mlango ukianzakupigwa, watu hao waligonga na kugonga, mlango haukufunguliwa na hivyo kuanza kuuvunja. Ilikuwa kazi kubwa, mlango ulikuwa imara sana, walifanya hivyo kwa zaidi ya dakika nne, mlango ukafunguka na kuingia ndani.
Picha waliyoiona, hakukuwa na mtu yeyote aliyeiamini, Carter alikuwa juu ya kitanda chake, sindano iliyokuwa na madawa ilikuwa katika mkono wake, tena ikiwa imechoma katika mshipa wake, kwa jinsi picha ilivyoonekana ilionyesha kabisa kwamba mtu huyo alikuwa amejidunga madawa ya kulevya.
“What the https://jamii.app/JFUserGuide is this?” (Ndiyo nini hiki?) aliuliza jamaa mmoja huku akionekana kushtuka.
Wakamsogelea kitandani pale, wanawake waliomuona Carter wakaanza kupiga kelele, waliokuwa wamelala katika vyumba vyao wakaamka na kwenda chumbani humo kushuhudia ni kitu gani kilikuwa kimetokea.
Mbali na mwili huo, pembeni yake kulikuwa na fedha za noti, dola, yeni, euro na paundi. Hilo wala halikuwafanya kuhisi chochote kile kwani kwa mtu kama Carter, kuwa na fedha mbalimbali lilikuwa jambo la kawaida sana.
“Was he cocaine addicted?” (Alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya?) aliuliza jamaa mmoja huku akimwangalia Carter pale kitandani.
Marafiki zake walibaki wakiashangaa, hawakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, rafiki yao wa muda mrefu, Carter eti alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya.
Hawakutaka kuamini hilo, pale kitandani alipokuwa, alikuwa kimya kabisa na hata mapigo yake ya moyo hayakuwa yakidunda hali iliyoonyesha kwamba alikuwa amekufa.
Walichokifanya ni kupiga simu polisi ambapo baada ya dakika ishirini walikuwa mahali hapo. Moja kwa moja wakaenda mpaka katika chumba hicho huku wakiwataka watu wote watoke nje na wao kufanya kazi yao.
Tayari mpiga picha wa polisi pamoja na mchoraji walifika mahali hapo na kuanza kuuangalia mwili wa Carter, alionekana kutumia kiasi kikubwa cha madawa mpaka kufariki pale kitandani.
Si marafiki zake walioshangaa tu bali hata polisi wenyewe nao walishangaa. Walimfahamu Carter, alikuwa mmoja wa wanamuziki wadogo ambao walitumika hata na kampuni mbalimbali kutokomeza utumiaji wa madawa ya kulevya, sasa iweje mtu huyo leo afe kwa kuzidisha utumiaji wa madawa hayo? Kila walichojiuliza, walikosa jibu.
Stori juu ya kifo chake zikaanza kusambazwa kwa kasi, hakukuwa na mtu aliyeamini kwamba mwanamuziki aliyekuwa na jina kubwa, Carter alikuwa amefariki dunia tena kwa kujidunga madawa ya kulevya kwa kiasi kikubwa.
Kila mtu aliyesikia taarifa hizo alibaki akishangaa, wengi wakajiuliza na mwisho wa siku kuja na majibu kwamba Carter alifanya siri utumiaji wa madawa ya kulevya.
Ulikuwa msiba mkubwa, kijana huyo, mwanamuziki huyo alikuwa na jina kuubwa, alikuwa kipenzi cha watuu wengi kitendo cha kusikia kwamba alikuwa amekufa ndani ya chumba hicho, hakika yalikuwa majonzi makubwa mno kwa kila mtu.
Taarifa hizo ziliendelea kuwekwa katika mitandao ya kijamii, kila aliyeziona, hakuamini, ndani ya saa moja tu, dunia nzima ilijua kile kilichokuwa kimetokea nchini Marekani huko Miami.
Watu walilia sana, wengine walijiuliza maswali mengi juu ya sababu iliyomfanya Carter kutumia madawa ya kulevya kwa kiwango kikubwa hicho mpaka kufa ndani ya chumba hicho.
Kila mtu alilaumu, wengine wakamuonea huruma. Mpaka mwili wake unaingizwa katika Hospitali ya St. Martin Luther King, tayari watu wengi walikusanyika hospitalini hapo, walitaka kusikia kile kilichokuwa kikiendelea, walitaka kuamini kama kweli msanii huyo alikufa baada ya kutumia madawa ya kulevya kupita kiasi.
***
“Nimefanya mlichotaka nikifanye, naomba mmuachie mpenzi wangu,” alisema Benjamin, alikuwa akizungumza na mtu fulani katika simu.
“Sawa! Tumeona, umefanya kazi nzuri sana...” ilisikika sauti upande wa pili.
“Kwa hiyo?”
“Kuhusu?”
“Mpenzi wangu! Si tayari nimekwishafanya kazi yenu, muachieni sasa,” alisema Benjamin.
Alikuwa akizungumza na mwanaume wa upande wa pili, alikuwa akimpa taarifa kwamba kazi aliyokuwa amepewa tayari ilikuwa imefanyika na hivyo alitaka mpenzi wake aachiwe huru kama yalivyokuwa makubaliano yao kabla.
Kwanza mwanaume huyo alikataa, kwa jinsi ilivyoonekana, alitaka kumuongezea kazi nyingine, ila alipotaka kufanya hivyo, aliona haikuwa sahihi kwani makubaliano ambayo waliwekeana mwanzo yalikuwa ni kumuua Carter na hakukuwa na jingine.
Walichokifanya huko walipokuwa ni kumfunga kitambaa cheusi Vivian na kumpakiza ndani ya gari, wakaanza kuondoka naye huku waliomsindikiza wakiwa wanaume wawili, waliokuwa na miili iliyojazia.
Njiani, Vivian alikuwa akilia, moyoni mwake aliumia mno, hakujua sababu iliyomfanya kutekwa na watu hao, kila alipouliza, hakupewa jibu bali aliambiwa asubiri mpaka atakapokutana na mpenzi wake.
Safari hiyo iliendelea mpaka walipofika katika kituo cha mafuta cha Total ambapo hapo ndipo walipomkabidhi Benjamin msichana Vivian ambaye hakuonekana kuwa sawa kabisa, kila wakati alikuwa akilia tu.
“Wamekufanya nini? Wamekupiga?” aliuliza Carter.
“Hapana! Kwa nini wamefanya hivi?” aliuliza Vivian.
“Sijajua! Acha tuondoke,” alisema Benjamin huku akionekana kutokujiamini.
“Benjamin, bosi amesema uchukue hii simu,” alisema mwanaume huyo huku akimpa simu aina ya iPhone 7.
“Ya nini?” aliuliza Benjamin huku akiichukua simu hiyo.
“Kama zawadi yako!”
“Nashukuru!” alisema Benjamin na kisha kumrudishia mwanaume huyo kwani alihisi kwamba simu hiyo ilikuwa na kifaa cha GPS ambacho kingemfanya kuonekana kila alipokuwa.
“Basi hakuna tatizo!”
Hawakutaka kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuingia ndani ya gari na kuanza kuondoka mahali hapo. Alichokifikiria Benjamin ni kuondoka na mpenzi wake kwenda mbali kabisa kujificha, hakutaka kuonekana kwani kile alichokuwa amekifanya chumbani kwa Carter, alikuwa na uhakika kwamba watu hao wangemtafuta na kumuua tu.
Walipofika katika apartment waliyokuwa wakiishi, Benjamin akamwambia Vivian wachukue kila kitu chao na kuondoka mahali hapo, kweli wakafanya hivyo.
“Ila kwa nini?” aliuliza Vivian.
“Wewe tuondoke, watatutafuta hawa.”
“Kisa?”
“Nimewachezea mchezo!”
“Mchezo gani?”
“Usijali, nitakwambia nini kilitokea,” alisema Benjamin huku akiendesha gari kwa kasi ya ajabu, alikuwa katika barabara ya St. Johnson ya magari yaendayo kasi kwa zaidi ya 180, ilikuwa ni lazima waondoke na kuelekea Alexandria, mji uliokuwa pembeni mwa jiji hilo la Washington DC.

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Jumamosi.
 
NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA

Sehemu ya Nane.

Madaktari waliendelea na tiba yao kama kawaida, mwili wa Carter uliwekwa kitandani huku ukiwa umetundikwa na dripu kadhaa. Japokuwa taarifa za awali zilisema kwamba mwanamuziki huyo alikuwa amekufa lakini walipomchunguza, wakagundua kwamba hakuwa amekufa bali mwili wake uliwekewa dawa Declophine, dawa ambayo mtu akiwekewa katika mishipa yake husimamisha mapigo ya moyo kwa muda.
Madaktari walikuwa wakiingia kwa zamu, walikuwa bize wakiendelea kumpa matibabu mwanamuziki huyo kwa kumwekea dawa iitwayo Anti-Declophine ambayo ndiyo ilikuwa na uwezo wa kuyarudisha mapigo ya moyo ya Carter.
Mpenzi wake alifika hospitalini hapo, muda wote alikuwa mtu wa kulia tu, hakuamini kama kweli siku ile aliyoagana naye na kwenda Miami ndiyo ingekuwa siku ya mwisho kuonana naye.
Ndugu zake ndiyo waliokuwa msaada, walimshika huku na kule, kila alipotaka kufanya jambo baya, walimzuia kwani walijua kabisa kwamba katika kipindi kama hicho angeweza kufanya jambo lolote baya.
Kama dunia ilivyokuwa ikishangaa, hata naye alikuwa akishangaa, mpenzi wake kufa huku akiwa amejidunga madawa ya kulevya ilimshangaza sana. Alikuwa naye kwa kipindi kirefu, walifanya mambo mengi walizoeana sana lakini hakukuwa hata na siku moja ambayo alimuona mpenzi wake akitumia madawa ya kulevya, si kutumia tu, hata kumuona akiyasifia madawa hayo, hakuwahi kusikia kitu kama hicho.
Kazi ilikuwa kubwa, kiasi cha dawa hiyo ambacho alipewa Carter ilionyesha kwamba angechukua saa arobaini na ndipo angerudiwa na fahamu hivyo. Nje ya hospitali hiyo, kulikuwa na watu wengi wakiwemo waandishi wa habari, kila mtu alitaka kusikia madaktari wangesemaje kuhusu afya ya Carter ambayo ilikuwa tata sana.
Madaktari hawakutaka kuzungumzia chochote kile, walikwishajua kile kilichokuwa kimetokea lakini hawakutaka kumwambia mtu yeyote kwa kuhisi kwamba kama wangefanya hivyo basi amtu aliyekuwa amemchoma sindano hiyo angeweza kumrudia hapo hospitalini na kufanikisha mpango wake.
Saa ziliendelea kusonga mbele, saa arobaini zilipofika, Carter akaanza kutingisha viungo vyake pale kitandani alipokuwa. Kiungo cha kwanza kabisa alichokitingisha kilikuwa ni vidole kisha kuyafumbua macho yake.
“He is back...” (Amerudi...) alisema Dk Phinias.
Kila mmoja akaonyesha tabasamu pana, kitendo cha Carter kurudiwa na fahamu kiliwafurahisha mno na hivyo kuwasiliana na wazazi wake ambao walikuwa nje na kuwapa taarifa juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
“Unasemaje?” aliuliza baba yake huku akionekana kutokuamini.
“Carter amerudiwa na fahamu!” alijibu Dk. Phinias.
“Inawezekana vipi?”
“Subirini kwanza, tunahitaji kuzungumza na polisi!”
Kila mmoja aliyesikia jibu la daktari alibaki akiwa na furaha mno, hawakuamini kile walichokisikia kwamba Carter alikuwa amerudiwa na fahamu. Ilikuwaje arudiwe na fahamu na wakati ukweli ulijulikana kwamba alikufa baada ya kujidunda madawa ya kulevya hotelini?
Hawakuamini hivyo wakataka kumuona. Kutokana na furaha walizokuwa nazo, wakashindwa kuvumilia na hivyo kuwataarifu watu wengine, hapo ndipo stori zilipoanza kuvuma kwamba kumbe Carter hakufa bali alikuwa amezimia.
“Sasa kwa nini polisi walisema kwamba alikufa? Kama alikufa si inamaana walisikiliza mapigo ya moyo lakini hayakuwa yakidunda, kama hayakuwa yakidunda, kwa nini yupo hai?” yalikuwa maswali kadhaa waliyojiuliza watu mitaani, maswali yalikuwa mengi mengi lakini hakukuwa na aliyepata jibu.
****
Bwana David Seppy alikasirika, hakuamini kile alichokisoma kwamba mtu aliyetaka afe, hakuwa amekufa, alichukuliwa kutoka hotelini na kupelekwa hospitalini na madaktari wakamtibu na hatimaye kupona.
Hakujua ni kitu gani kilitokea, hapo ndipo alipogundua kwamba Benjamin hakuwa mtu wa kawaida, alitumia ujanja ambao mpaka wao wenyewe hawakuuelewa ulikuwa ujanja upi ambao ulivizuga mpaka vyombo vya habari na kuripoti kwamba Benjamin alikuwa amekufa.
Hapohapo akawapigia simu vijana wake, kwa jinsi walivyomuona siku hiyo, hakuonekana kuwa katika hali ya kawaida hata kidogo, alionekana kuwa na hasira sana na hata alivyokuwa akizungumza alionekana kuwa mtu ambaye hakuleta utani hata mara moja.
Aliwaangalia vijana hao kwa zamu, aliwalaumu kwa kuwa walipewa taarifa kwamba Carter alikufa, hawakutaka kujiridhisha, wakakubaliana na Benjamin kwamba kijana huyo alikufa.
“Nani ana uhakika kwamba Carter amekufa?” alianza kwa kuuliza swali huku akiwaangalia vijana hao watatu kwa zamu, wote wakanyoosha mikono juu.
“Mna uhakika kwamba amekufa?” aliuliza Bwana Seppy.
“Ndiyo bosi!”
“Umesikia wapi?”
“Kwenye vyombo vya habari, na hata wewe tulikuja kukwambia kwamba kijana huyo amekufa, ukatuambia tumeona wapi, tukakuonyesha picha katika mitandao, ilionyesha kabisa kwamba alikufa, ukakubaliana nasi,” alisema kijana mmoja huku akimwangalia Bwana Seppy usoni.
Mzee huyo hakutaka kuzungumza kitu, akabaki kimya, ni kweli alikumbuka kwamba aliwaambia vijana hao maneno hayo kwamba mtu huyo alikuwa ameuawa, lakini kwa nini naye alikubaliana moja kwa moja kwamba mtu huyo alikuwa ameuawa, kila alipojiuliza, akakosa jibu.
“Sasa sikilizeni, ninataka muhakikishe kwamba hawa watu wawili wanauawa haraka iwezekanavyo,” alisema Bwana Seppy huku akiwaangalia vijana wake hao kwa zamu.
“Wawili tena?”
“Ndiyo! Carter na Benjamin, hakikisheni kabla mwezi huu haujakwisha, wanauawa wote,” alisema mzee huyo.
“Sawa mkuu!”
****
Maofisa wa upelelezi nchini Marekani, FBI (Federal Bureau Investigation) walitaka kufuatilia kuona ni kitu gani kilitokea mpaka hali iliyomkuta Carter imkute huku ulimwengu mzima ukijua kwamba mwanamuziki huyo alikufa hotelini baada ya kujiovadozi madawa ya kulevya.
Walitaka kupata ripoti kamili kutoka kwa madaktari, walikuwa na uhakika kwamba walijua kuwa mtu huyo alikufa kutokana na mapigo yake ya moyo kusimama, sasa ilikuwaje mpaka awe hai kipindi hicho, wakahisi kwamba kulikuwa na kitu kilitokea ambacho nao walitaka kukifahamu.
Harakaharaka wakawasiliana na uongozi wa Hospitali ya Martin Luther King na kutaka kuzungumza na daktari mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Terry. Walitaka kusikia kila kitu, walijua kwamba piga ua madaktari walifahamu ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka hali hiyo kuwa hivyo.
Hawakutaka kuchelewa, wakawatuma maofisa wawili ambao walikwenda moja kwa moja mpaka katika hospitali hiyo na kukutana na Dk. Terry ambaye mara baada ya kuambiwa dhumuni la maofisa hao kufika hospitalini hapo, akaahidi kutoa ushirikiano wote.
“Tunahitaji kufahamu kuhusu Carter,” alisema ofisa mmoja.
“Hakuna tatizo! Kipi mngependa kufahamu?” aliuliza Dk. Terry.
“Kuhusu kile kilichotokea, kuna ripoti yake?”
“Ndiyo! Ila bado sijaletewa ofisini!”
“Tunahitaji kuiona, na tunataka kujua nini kilitokea, ikiwezekana tuzungumze na madakatri wa kwanza ambao waliupokea mwili wake,” alisema ofisa mmoja.
Hilo wala halikuwa tatizo, alichokifanya daktari huyo ni kuwasiliana na daktari mmoja miongoni mwa madaktari waliompokea Carter na kumuhitaji ndani ya ofisi yake huku akiwa na ripoti kamili mara baada ya mwili wake kuchunguzwa na madaktari wa hospitali hiyo.
Ni ndani ya dakika kumi tu, mlango wa ofisi hiyo ukaanza kugongwa, Dk. Terry akamkaribisha mgongaji, mwanamke mmoja wa makamo akaingia ndani ya ofisi hiyo huku akiwa amevalia koti refu jeupe, shingoni alining’iniza mashine ya kusikilizia mapigo ya moyo, alipoingia ndani ya ofisi hiyo, akasalimia na kisha kumpa ripoti ile Dk. Terry ambaye akaanza kuiangalia.
“Mmh!” aliguna Dk. Terry.
“Kuna nini?” aliuliza ofisa mmoja.
“Ripoti inaonyesha kwamba alichomwa sindano iliyokuwa na Declophine, hii ni dawa ya kusimamisha mapigo ya moyo kwa muda,” alisema daktari huyo, maofisa wale wakajiweka vizuri vitini.
“Declophine! Ina maana alichomwa?”
“Hatuna uhakika, inawezekana alijichoma pia, hatuwezi kufahamu hilo,” alijibu daktari huyo.
“Kuna kingine?”
“Ndiyo! Sasa hapa nimepata uhakika kwamba alichomwa kwa sababu ripoti inaonyesha kwamba puani alipuliziwa dawa kali ya usingizi,” alisema daktari huyo.
“Na nani?”
“Hilo hatufahamu! Limetokea huko hotelini!’
“Kwa hiyo kulikuwa na mtu alitaka kumuua?”
“Sijajua! Mpaka hapa ripoti inashangaza! Hivi kweli mtu ambaye alitaka kumuua angeweza kumchoma sindano yenye Declophine?” aliuliza daktari huyo.
Hakukuwa na mtu aliyejibu swali hilo, kila mmoja alikuwa kimya. Swali alilouliza Dk. Terry lilikuwa kweli kabisa, kama kulikuwa na mtu aliyekuwa ameingia ndani ya chumba hicho kwa ajili ya kumuua, asingeweza kumchoma sindano iliyokuwa na Declophine, kama kweli alidhamiria kuua, basi angemuua kwa kumchoma sindano yenye sumu kali.
“Kwa nini huyo mtu alifanya hivi?” aliuliza ofisa mmoja.
“Hatujui!”
“Au Carter mwenye alitaka kutengeneza jina zaidi?”
“Nalo hatujui!”
“Ni lazima tufanye naye mahojiano, nadhani kuna jambo kubwa limejificha nyuma ya pazia,” alisema ofisa huyo, hawakutaka kubaki ofisini humo, wakaondoka zao kurudi makao makuu huku wakiwa na kopi ya ripoti hiyo.
“Hapana! Haiwezi kuwa hivi!” alisema mkuu wa upelelezi kitengo cha FBI.
“Hiyo ndiyo ripoti tuliyopewa!”
“Yaani mtu atokee tu na kumchoma sindano yenye Declophine, hivi inawezekana kweli? Ausimamishe moyo ili iweje? Kama angetaka kumuua si angemuua tu!” alisema mkuu huyo.
Ripoti hiyo ikaanzisha maswali mengi vichwani mwa FBI hao, kila mmoja alijiuliza sababu ya mvamizi kutumia sindano yenye Declophine lakini wakakosa jibu kabisa.
Walijua kwamba inawezekana mvamizi huyo alikuwa akimfuatilia Carter tangu kitambo lakini swali kubwa lilikuwa ni sababu gani ilimfanya kutumia Declophine kuusimamisha moyo wake na wakati alikuwa na uwezo mkubwa wa kumuua?
Hapo ndipo wakapata jibu kwamba wamfuate Carter hospitali na kuzungumza naye, awahadithie ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka kuchomwa sindano iliyokuwa na Declophine.
FBI hao hawakutaka kuchelewa, harakaharaka wakaondoka na kwenda hospitalini huko, walipofika, kwa kuwa tayari Carter alikuwa akijisikia nafuu, wakaruhusiwa kwenda kuzungumza nao, Carter alipowaona tu, akashtuka.
“Unaweza kutuambia nini kilitokea ndani ya chumba kile cha hotelini?” aliuliza ofisa mmoja mara baada ya salamu, muda huo, macho yake yalikuwa usoni mwa Carter tu.
“Naweza!”
“Nini kilitokea?” aliuliza ofisa huyo na Carter kuanza kuelezea kila kitu kilichotokea siku hiyo, mpaka aliporudi hotelini, alipolala na kisha kushtukia akiwa ameshikwa na mtu na kuanza kuvutishwa madawa ya usingizi, baada ya hapo, hakujua kitu gani kiliendelea kwani alipofumbua macho, alijikuta akiwa hospitalini.
****
Carter akaanza kuhadithia kila kitu kilichotokea hotelini katika usiku ambao alimaliza shoo yake na kurudi huko. Hakutaka kuficha, yeye mwenye alibaki akishangaa mara baada ya watu kumwambia kwamba alikufa, alikufa vipi na wakati alipewa tu madawa ya uzsingizi?
Wakati akisimulia hivyo, maofisa wa FBI walikuwa kimya wakimsikiliza, simulizi yake ilisema kwamba alivamiwa chumbani na mtu ambaye alikuwa na uhakika alikuwa ndani ya chumba hicho, baada ya kumvamia kitandani, akamkamata vilivyo na kumnusisha kitambaa kilichokuwa na madawa, baada ya hapo, hakujua nini kiliendelea zaidi ya kujikuta akiwa hospitali.
“Kwa hiyo hukumuona kabisa huyo mtu?” aliuliza ofisa mmoja wa FBI.
“Kwa kweli sijamuona.”
“Kuna nini kilitokea kabla, kuna ugomvi wowote, labda na mtu yeyote unayemuhisi?” aliuliza ofisa huyo.
“Hapana! Sina ugomvi na mtu yeyote yule, nina urafiki mkubwa na kila mtu, sijui kama kuna mtu niligombana naye, kilichotokea, inawezekana ikawa wivu tu wa watu wengine,” alijibu Carter.
Huo ndiyo ulikuwa ukweli, Carter alikuwa mtu wa watu, alipendwa na kila mtu, hakuwa mgomvi, watu wengi walimheshimu kwa kuwa hakuwa mbaguzi kama watu wengine.
Kila kona jina lake lilisikika na ndiyo maana hata taarifa za kifo zake zilipoanza kusikika kila kona, kila mtu alikuwa na huzuni tele. Aliendelea kubaki hospitalini hapo, hakuwa mzima kiafya na alitakiwa kusubiri kwa siku tano na ndipo arudi nyumbani.
Watu waliendelea kumiminika hospitalini hapo, wengine walileta maua, kadi na vitu vingine huku wakimpa pole kwa kila kitu kilichotokea.Mpenzi wake, kila siku ilikuwa ni lazima afike hospitalini hapo, alimpenda sana carter na hakuwa tayari akimuona akipitia katika kipindi kigumu peke yake, alimpenda na kumthamini zaidi ya mtu yeyote yule.

JE, nini kitaendelea?
 
NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA

Sehemu ya Tisa,

Bwana Seppy alituli chumbani kwake, alionekana kukasirika mno, mchezo aliofanyiwa na Benjamin ulimfanya kujona hana akili, kuwaona vijana wake hawakuwa siriazi kwa kazi kubwa aliyokuwa amewapa.
Alichotaka kuona ni Carter anakufa, tena hapohapo hospitalini kwani kama angeendelea kubaki hai ilimaanisha kuwa kuna siku angekuja kugundulika kwani huyo Carter angesema kilichotokea na hatimaye kufungwa pingu na kupelekwa jela.
“Ni lazima auawe hapohapo kitandani,” alijisemea.
Tayari aliwaambia vijana wake kwamba kitu hicho kilitakiw akufanywa haraka iwezekanavyo, ila alitaka kuwasisitizia kwamba kifo cha Carter kilikuwa muhimu sana kwa wakati huo kuliko kitu chochote kile. Hata alipowapigia simu, aliwasisitizia kwamba jambo hilo lilitakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo, hata kama lingehitaji kiasi kikubwa cha fedha, bado lilitakiwa kufanyika.
Vijana hao, watatu wakajiandaa, iliwapasa waingie ndani ya hospitali hiyo na kujifanya madaktari, wajifanye wanakwenda katika chumba alicholazwa Carter na hatimaye kumuua, hivyo ndivyo walivyotakiwa kufanya.
Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kununua makoti makubwa ya kidaktari, mashine za kupimia mapigo ya moyo na mafaili ambayo yangewafanya kuonekana kama madaktari na kuingia ndani ya chumba hicho kirahisi.
Wakafanikiwa kupata vitu vyote na hivyo kufanya kile walichotaka kukifanya. Kabla ya kwenda hospitalini huko kutekeleza kile walichotaka kukifanya, kwanza wakampigia simu Bwana Seppy.
“Ndiyo tunakwenda kiongozi, kuna lolote?” aliuliza kijana mmoja, huyu alijiita Dracula, kijana mwenye roho mbaya, mwanaume mwenye kuua watu kama alivyoua panzi.
“Kwa sababu huyu Benjamin alijifanya mjanja, sasa inabidi mkimuua muhakikishe mnaacha alama za vidole vyake, mmenielewa?” alisema na kuuliza.
“Ndiyo mkuu!”
Suala la kupata alama za vidole vya Benjamin wala halikuwa tatizo, walikuwa nazo katika kinailoni kidogo. Walizichukua alama hizo kipindi kile walipomkabidhi mpenzi wake kwake, walimpa simu aina ya iPhone 7, alipoishika, alama za vidole vyake zilibaki katika kioo cha simu.
Hawakukigusa kioo hicho, waliishika simu kwa tahadhali kubwa, walipofika katika chumba ha wataalamu wao, zile alama zikaanza kutolewa kifundi na mwisho wa siku kufanikiwa, wakawa nazo na hivyo kuziweka kwenye nailoni, yaani hapo popote pale ambapo wangefanya kitu chochote, wangeweka kile kinailoni katika sehemu yoyote, alama za mikono za Benjamin zingeonekana.
“Fanyeni hivyo, ni lazima dunia ijue kwamba yeye ndiye aliyehusika,” alisisitiza Bwana Seppy.
“Sawa mkuu!”
“Na kingine msisahau kuacha fedha, hiyo ni kwa ajili ya kuwachanganya FBI,” alisema mzee huyo.
“Sawa mkuu!”
Hicho ndicho kilichotakiwa kufanywa. Kinailoni ambacho kilikuwa na alama za vidole vya Benjamin (Fingerprints). Walipoanza kuingia ndani ya hospitali hiyo, wakajigawa, isingekuwa rahisi kufikiri kwamba watu hao hawakuwa madaktari kwani mavazi yao, muonekano ulionyesha kabisa kwamba walikuwa madaktari.
Waliwekeana muda kwamba ndani ya hospitali hiyo kubwa wangetumia dakika ishirini na kisha kuonana nje, wangeingia ndani ya gari lao na kisha kuondoka pasipo kugundulika, wakaelewana.
Muda ulikuwa ni saa moja usiku, muda ambao si watu wengi waliokuwa hospitalini hapo. Ndugu wa Carter walikuwepo mahali hapo, si ndugu bali hata polisi nao walikuwepo kuhakikisha ulinzi unafanyika, asiingie mtu yeyote ambaye si mhusika.
Wakati Dracula anapiga hatuia kuelekea katika chumba kile, hakuonekana kuwa na wasiwasi wowote ule, hata ndugu zake Carter walipomuona akisogea kule walipokuwa, hawakuwa na hofu hata kidogo, walijua kwamba naye huyo alikuwa daktari kwani hospitali kubwa kama hiyo, ilikuwa na madaktari wengi mno.
“Poleni sana jamani...” alisema Dracula hata kabla ya kuingia ndani ya chumba hicho. Kwa kumwangalia tu, usingejua kama alikuwa muuaji, na kama ungeambiwa umpe kazi, harakaharaka ungempa uchungaji au upadri, alijiweka katika sura ya kipole mno.
“Asante sana...”
Hakutaka kubaki hapo nje, kila mtu aliyemwangalia, alikiri kwamba hospitali hiyo ilikuwa na daktari aliyekuwa na huruma kuliko madaktari wote duniani. Kabla ya kuingia ndani ya chumba kile, akaonyesha alama ya msalaba kama wanayofanya Waroma, yaani kwenye paji, kifuani na mabegani.
Alipofanya hivyo tu, watu wote wakajawa na tabasamu pana, mbali na kuwa daktari, wakagundua kwamba Dracula aliyekuwa na kichuma kilichoandikwa Dr. Kevin kifuani alikuwa mtumishi wa Mungu, hivyo walikuwa na uhakika kwamba mambo yangekwenda salama.
“Unajisikiaje Carter?” aliuliza Dracula mara baada ya kuingia ndani ya chumba hicho, Carter alikuwa kitandani akisubiri muda wa kuona wagonjwa ufike ili ndugu zake waingie.
“Najisikia vizuri kidogo...”
“Sawa! Ngoja nipime mapigo ya moyo,” alisema Dracula na hapohapo akatoa mashine ya kupimia mapigo ya moyo, stethoscope na kuanza kumpima.
“Mapigo ya moyo yapo vizuri kidogo,” alisema Dracula na kumwambia Carter ageuke, mgongo uwe juu.
Carter hakubisha, alimwamini Dracula na kuona kwamba alikuwa daktari wa ukweli hivyo akageuka. Hilo lilikuwa kosa kubwa sana kulifanya, hapohapo Dracula akaanza kumkaba Carter palepale kitandani.
Carter alijitahidi kuitoa mikono ya Dracula, akashindwa, alijitahidi kupita kelele, sauti haikutoka kabisa. Alihangaika na kuhangaika lakini hakufanikiwa hata kidogo.
Dakika moja nzima bado Dracula alimkaba mahali pale vilivyo. Nguvu zikaanza kumuisha Carter, akachoka na hapohapo pumzi ikaanza kukata, mbele yake akaona giza, hazikupita sekunde nyingi, akafa hapohapo kitandani.
Dracula hakutaka kuchelewa, akachukua kile kinailoni, akakiweka shingoni mwa Carter, akakikandamiza vilivyo na alama zile kubaki shingoni mwa Carter, alipomaliza, hakutaka kubaki, akatoka nje ya chumba kile, akawaambia ndugu zake Carter kwamba mgonjwa wao aliendelea vizuri hivyo wasubiri, wote wakamshukuru Mungu, Dracula akaondoka zake huku akiwa amekwishakamilisha kazi yake.
“It’s done,” (Kazi imefanyika) alimwandikia ujumbe mfupi Bwana Seppy ambapo alipoisoma, tabasamu pana likajaa usoni mwake.
****
Kila mtu alikuwa na uhakika kwamba Carter alikuwa amepona na hivyo alitakiwa kurudi nyumbani. Watu walimkumbuka, kazi zake alizokuwa akizifanya zilimfurahisha kila mmoja na hivyo kutamani kuona mwanamuziki huyo akirudi tena nyumbani na kuendelea kuwabuirudisha.
Hakukuwa na mtu aliyejua kwamba kulikuwa na kitu kimetokea ndani ya chumba alicholazwa Carter, hata madaktari na manesi wa hospitali hiyo hawakuwa wakijua chochote kile.
Baada ya dakika kadhaa tangu Dracula aondoke ndani ya chumba kile na kufanya mauaji, Dk. Rafael akatokea na kwenda ndani ya chumba kile, kama kawaida aliwakuta ndugu zake Carter wakiwa nje, nyuso zao tu zilionyesha furaha tele, mioyo yao ikajazwa na nguvu.
Dk. Rafael akawasalimia na kisha kuingia humo ndani, kwanza jinsi alivyomkuta Carter kitandani pale, akashikwa na wasiwawasi kwa kuhisi kulikuwa na kitu kimetokea, akasoegea na kumwangalia vizuri, hakuwa akipumua, macho yalimtoka na muonekano wake tu ulionyesha kwamba alikuwa amekufa.
Akajaribu kuvipeleka vidole vyake karibu na pua ya Carter, hakuwa akipumua, hakuridhika, akachukua mashine yake na kusikiliza mapigo ya moyo ya stethoscope na kuanza kuyasikiliza mapigo ya moyo wa Carter, hayakuwa yakidunda.
“Mungu wangu!”
Hakutaka kubaki chumbani humo, alichokifanya ni kutoka huku akikimbia, ndugu waliokuwa nje walipomuona, wakashangaa, hawakujua sababu ya daktari yule kukimbia hivyo.
Kule alipokwenda, karudi na madaktari wawili ambao wakaingia ndani ya chumba kile, walichoambiwa ndicho walichokutana nacho ndani, Carter alikuwa kimya kitandani, wakampima kila kipimo lakini hakushtuka, dalili zote zilionyesha kwamba alikufa.
“Nani amefanya hivi?” aliuliza Dk. Michael.
Madaktari waliulizana lakini hakukuwa na mtu mwenye jibu, walichanganyikiwa, hawakujua kama kulikuwa na mtu mwingine alikuwa ameingia ndani ya chumba kile au la.
Mbali na mwili ule, pembeni kulikuwa na fedha za nchi tofauti, yaani dola ya nchini Marekani, paundi ya Uingereza, Euro ya Ulaya na Yeni ya China. Hawakujua kwa nini fedha zile zilikuwa mahali pale.
Walichokifanya ni kutoka nje na kuwauliza ndugu wale ni nani alikuwa ameingia ndani ya chumba kile, ndugu wale wakasema kwamba kulikuwa na daktari mmoja aliyekuwa ameingia kabla.
“Yupi?”
“Ni daktari mmoja, mrefu, ana shingo ndefu, ana sura ya kipole sana,” alijibu ndugu mmoja.
Jinsi walivyomzungumzia huyo daktari, hakukuwa na daktari aliyekuwa na sifa hizo hivyo wakajua kwamba kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa ameingia. Hawakutaka kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea ndani bali wakawasiliana na polisi, baada ya dakika kadhaa, polisi wakafika hospitalini hapo.
Kitu cha kwanza kabisa, hawakutaka mwili uguswe kwa ajili ya kutokupoteza alama za vidole kama zipo, madaktari walilifahamu hilo na tangu walipohisi kwamba alikuwa ameuawa, hawakuugusa mwili huo.
Walipoona kwamba mwili haujaguswa, hawakutaka kuchelewa, wakaharakaiisha vipimo vichukuliwe harakaharaka na kama kuna alama za vidole viangaliwe ni vya nani ili muuaji huyo atafutwe haraka iwezekanavyo.
Kilichowashangaza polisi ni kwamba walikuta fedha kitandani, hawakujua zilikuwa na maana gani lakini walipokumbuka, hata siku ambayo Carter alisadikiwa kuwa aliuawa kwa kuchomwa na sindano, pia palepale kitandani kulikuwa na fedha, hilo likawapa maswali, je kulikuwa na mtu aliyekuwa akifanya hivyo?
“Hivi mmejiuliza kuhusu hizi fedha?” aliuliza polisi mmoja.
“kivipi?” akauliza mwingine.
“Siku ile taarifa ziliposema kwamba Carter alijidunga sindano, pembeni kulikuwa na fedha kama hizi, leo ameuawa, pia kuna fedha, hamuhisi kitu chochote hapa?” aliuliza polisi huyo.
“Mmh!” Polisi wengine wakaishia kuguna tu.
Kama Carter kuuawa, aliuawa, mtu wa kwanza kabisa aliyeshukiwa ni mlinzi ambaye aliwekwa mahali hapo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kila kitu kinakuwa sawa, akachukuliwa na kupelekwa kituoni kwa mahojiano maalumu.
Ndugu zake waliokuwa nje, wakaambiwa kweli kile kilichotokea, kwanza hawakuamini, inakuwaje ndugu yao auawe na wakati muda wote wao walikuwa nje ya chumba kile na hakukuwa na adui yeyote aliyeingia zaidi ya madaktari tu?
“Mmoja wa watu walioingia hawakuwa madaktari, alikuwa muuaji,” hilo ndilo jibu alilolitoa daktari hivyo kuibua vilio mahali hapo.
Taarifa zilitolewa kwamba mwanamuziki Carter alikuwa ameuawa ndani ya chumba cha hospitali, kwanza watu hawakuamini, walihisi kwamba taarifa hizo zilikuwa ni uongo kwani kipindi cha nyuma, taarifa zilitoka hivyohivyo kwamba alikuwa amejichoma sindano na kujiovadozi madawa ya kulevya.
Katika kuuchunguza mwili ule wakagundua kwamba muuaji wa mauaji hayo hakuwa amevaa glavu kitu kilichoifanya alama za vidole vyake kubaki shingoni mwa mwili wa Carter.
Walichokifanya madaktari ni kuwasiliana na polisi ambao wakafika mahali hapo na kuchukua alama zile na kurudi nazo ndani ya kituo chao. Huko, kwa msaada wa mashine walizokuwa nazo, wakaziscan alama zile na kisha kuziingiza katika kompyuta zao, kilichoendelea ni kuanza kutafuta Marekani nzima juu ya mtu aliyehusika katika mauaji yale.
Picha zilipita nyinginyingi na tena kwa haraka mno, zilikwenda na kwenda, kama dakika kumi na tano hivi na ndipo picha moja ikasimama huku neno 100% MATCH likionekana kuonyesha kwamba picha ya mtu aliekuwa akionekana na alama alizoziweka wakati akisajiri kitambulisho cha taifa, alama zile alizokuwa nazo ndizo zilizoonekana katika mwili wa Carter.
“Anaitwa nani huyo?” aliuliza ofisa wa FBI.
“Benjamin Saunders.”
“Yupo wapi?”
“Cambridge, Boston ni mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Harvard,” alijibu ofisa mmoja.
“Ni lazima twende huko, ni lazima huyu muuaji apatikane. Wasiliana na polisi wa Cambridge, inawezekana hayupo huko ila ni lazima tuweke mitego, mbali na hivyo, pelekeni picha zake kila kona, kwenye vituo vya habari na sehemu nyingine. Gideon, hakikisha mtu huyu anapatikana,” alisema mkuu wa FBI, Bwana Solomon Kane, hivyo picha zake kuanza kutumwa sehemu tofautitofauti, kila mtu akajua kwamba Benjamin ndiye aliyemuua Carter
 
Back
Top Bottom