Mauaji yaliyojaa utata

princewilly

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
259
526
Sehemu ya Kwanza.

Ilikuwa ni taarifa mbaya, iliyoshtua ambayo ilianza kwa kusikika katika sehemu mbalimbali jijini Las Vegas nchini Marekani kabla ya kuwafikia polisi. Kila aliyezisikia taarifa hizo, hakuamini, wengi wakahisi kwamba hazikuwa taarifa za kweli, labda kulikuwa na mtu mwingine aliyetaka kuivumisha habari hiyo ambayo ilimsisimua kila mtu aliyeisikia.
Msichana mrembo aliyeitwa kwa jina la Stacie Lawrence, msichana aliyebahatika kunyakua taji la Urembo wa Dunia, alikutwa amekufa ndani ya chumba kimoja cha Hoteli ya Vikings Hill iliyokuwa Las Vegas, Nevada nchini Marekani alipokuwa amepanga huku akisubiri kuonana na Mkurugenzi wa Tovuti ya Google kwa ajili ya kusaini mkataba wa picha zake kutumika katika programu moja ambayo ingetumiwa katika simu zote zinazotumia system ya android.
Stacie aliyekuwa gumzo kwa kipindi hicho duniani kutoka na uzuriwake, alikutwa amekufa baada ya kujiovadosi madawa ya kulevya aina ya Heroine kwa kujichoma sindano katika mkono wake wa kulia wakati kitandani ndani ya hoteli hiyo.
Hiyo ndiyo ilikuwa habari ya mjini, kila aliyeisikia, hakuamini, swali la kwanza kabisa walilojiuliza watu ni juu ya utumiaji wa madawa ya kulevya. Kila mtu alijua kwamba Stacie hakuwahi kutumia madawa hayo, si kipindi hicho tu, hata kabla ya kutwaataji hilo, hakuwa mtumiaji, sasa ilikuwaje mpaka leo hii akutwe chumbani kitandani akiwa amejidunga madawa hayo? Hilo lilikuwa swali lisilokuwa na majibu.
Waandishi wa habari kutoka katika mashirika mbalimbali ya habari kama CNN, BBC, Sky News na hata wale wa kujitegemea tayari walikuwa nje ya hoteli hiyo, vitendea kazi vyao vyote vilikuwa mikononi mwao, walitaka kupiga picha na kupata habari kuhusu kifo cha msichana huyo mrembo ambaye bado uzuri wake ulikuwa gumzo duniani.
Polisi walitanda kila sehemu nje ya hoteli hiyo, mkanda wa njano ulioandikwa Do Not Cross yaani ‘Usivuke’ulizungushiwa katika hoteli hiyo kwa muda. Magari ya wagonjwa mawili yalikuwa yamekwishafika katika hoteli hiyo, kilichosubiriwa ni kuingia ndani na kuuchukua mwili huo.
Waandishi hawakuruhusiwa kabisa kuingia ndani ya hoteli hiyo, waliambiwa wasubiri hapo nje wakati polisi wakiingia ndani kwa ajili ya kufanya kazi yao, hawakuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri.
Polisi wakaingia ndani ya chumba kile. Huko wakaukuta mwili wa Stacie ukiwa kitandani, katika mkono wake wa kushoto kulikuwa na sindano iliyochoma mshipa wake, aliishikilia kwa kutumia mkono wake wa kulia mbali na hivyo, pembeni yake kulikuwa na noti za Dola, Paundi, Yeni na Euro.
Udenda ulikuwa ukimtoka, pale alipokuwa, hakutingishika, kilikuwa kifo kibaya, kilichozua maswali mengi kwa watu wengi, maswali hayo yote, hakukuwa na mtu aliyekuwa na majibu zaidi ya Stacie mwenyewe ambaye kipindi hicho alikuwa marehemu.
“This is the fifth one, what the hell with the drugs?” (huyu ni mtu wa tano, kuna nini na haya madawa?) alisikika akiuliza mwanaume mmoja huku akionekana kushangaa.
“I don’t know. What the hell with these teenagers, they like to try each and every goddamn thing, why?” (sifahamu. Nini kinaendelea kwa hawa vijana, wanapenda kujaribu kila kitu, kwa nini?) aliuliza mzee mmoja huku akionekana kukasirika.
Kila mmoja alishangaa, huyo hakuwa mtu wa kwanza, supastaa aliyejiua baada ya kujiovadozi kwa madawa ya kulevya, huyo alikuwa mtu wa tano, kijana supastaa ambaye aliamua kujiua kwa kujidunga sindano ya madawa ya kulevya.
Mtu wa kwanza kabisa kujiua kwa kujidunga shindano alikuwa Paul McKenz. Huyu alikuwa mcheza kikapu aliyekuwa akichipukia, mwenye sura nzuri, alijitengenezea jina kubwa katika Timu ya La Lakers, akaanza kupata mashabiki wengi, alipendwa na kila mtu aliyekuwa akiupenda mchezo huo, jina lake likaanza kuwa kubwa, akapata mikataba mingi lakini mwisho wa siku, Paul akaja kujidunga sindano yenye madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine chumbani kwake.
Watu wengi walisikitika kwani ndiye alikuwa kijana aliyekuwa akichipukia katika mafanikio makubwa. Hiyo haikuishia hapo, pia kulikuwa na kijana mwingine aliyekuwa na kipaji cha uigizaji. Katika filamu yake ya kwanza ya Fallen Tree, alishinda Tuzo ya Oscar, Global na nyingine nyingi, huyu aliitwa Todd Lewis.
Bahati ikaanza kuonekana upande wake, akapendwa sana, kila kona alisikika yeye tu. Kadiri jina lake lilivyovuma ndivyo alivyozidi kujitengenezea mashabiki. Wakati akiwa amenunua gari yake ya kwanza ya thamani kabisa aina ya Ferrari Testarossa nyekundu, akakutwa naye akiwa amejidunga madawa ya kulevya ndani ya gari lake nje ya klabu moja huku pembeni kukiwa na noti ya dola, paundi, Yuan na Euro. Watu walisikitika na kulia, vilio vyao, huzuni zao hazikuweza kuwarudisha watu hao duniani.
Mtu mwingine kabla ya Stacie kujiua kwa madawa ya kulevya alikuwa kijana aliyeitwa kwa jina la Carter Phillip. Huyu alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakichipukia katika muziki wa Pop. Alikuwa na sauti kali, yenye nguvu ambapo kila alipokuwa akiitumia katika nyimbo zake, wanawake walichanganyikiwa.
Alikuwa mzuri wa sura, mwili uliojengeka. Kibao chake cha kwanza kabisa cha Come and Get Me Shawty alichokitoa kilitingisha kila kona duniani. Uwezo wake ulionekana, si hapo tu hata kwenye Shindano la American Got Talent, mpaka aliposhinda, watu waliona kipaji kikubwa ndani yake.
Wengi wakatabiri kwamba Carter ndiye angekuwa mrithi sahihi wa Michael Jackson, wengi wakamtabiria mema, njozi njema ikaonekana mapema kabisa kwani ngoma zake mbili alizozitoa, zote zilishika nafasi za juu kabisa katika orodha ya Billboard.
Akatengeneza fedha nyingi huku ndiyo kwanza akiwa na miaka kumi na tisa. Akapendwa, akawa kipenzi kikubwa cha watu ila baada ya kwenda nchini Uingereza kwenye Tamasha la UKIMWI lililokuwa likifanyika katika Jiji la Southampton, akakutwa akiwa amejiua ndani ya chumba alichochukua hotelini baada ya kujidunga sindano iliyokuwa na madawa ya kulevya aina ya Dextromethorphan huku pembeni kukiwa na noti za dola, paundi, yuan na euro.
Hakukuwa na aliyejua sababu ya vijana hao kujidunga madawa hayo ya kulevya, kila mtu aliyepata habari za vijana hao alishtuka. Mpaka katika kipindi ambacho msichana mrembo, Stacie kujiovadozi madawa hayo, bado watu hawakujua sababu ilikuwa nini, ni afadhali kama wangekuwa wamepigika katika maisha yao, ila kilichoshangaza, walikuwa wakianza kupata umaarufu, kupata fedha, na ndipo kipindi hichohicho nao waliamua kujidunga madawa ya kulevya.
Dunia ikatetemeka, watu wakaogopa kuwa mastaa, wengi walisikia kwamba unapokuwa staa, ilikuwa ni lazima kutumia madawa ya kulevya. Wazazi walipowaona vijana wao wanaanza harakati kupitia vipaji vyao, waliwazuia kwa kuona kwamba mwisho wa siku wangejiua kama hao wengine.
Swali kubwa ambalo waandishi wa habari walihoji, mitaani ni sababu gani zilizopelekea vijana hao kujidunga madawa ya kulevya? Kila aliyeuliza swali hilo, alikosa jibu kabisa.

Je, nini kitaendelea?
Nini kilipelekea watu hao, mastaa wakubwa kujimaliza kwa kujiovadozi madawa ya kulevya?
Tukutane kesho hapahapa
 
NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA

Sehemu ya Pili.

“You are a killer,” (Wewe ni muuaji)
“No! I am not a killer officer, I am not,” (Hapana! Mimi si muuaji ofisa, mimi si muuaji)
“You killed them, why? Why did you kill them? Why?” (Umewaua, kwa nini? Kwa nini umewaua? Kwa nini?)
“I killed nobody officer,” (sijamuua yeyote ofisa)
Yalikuwa ni mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ndani ya chumba kimoja katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini New York. Ndani ya chumba kile, kulikuwa na kijana mmoja, kwa kumwangalia, alikuwa na miaka isiyozidi ishirini na tano, alikuwa mtu mwenye mchanganyiko wa rangi, mama yake alikuwa Mzungu na baba yake alikuwa mtu mweusi.
Polisi wanne waliovalia makoti makubwa ambayo nyuma yaliandikwa NYPD yaani New York Police Department walikuwa wakifanya naye mahojiano kwa sauti kubwa, walimuuliza maswali na kumwambia kwamba yeye alikuwa muuaji lakini alikataa, alikataa katakata lakini polisi hawakuacha, waliendelea kumwambia kwamba alifanya mauaji.
Polisi hao walizungumza naye kwa zaidi ya dakika arobaini, neno lao lilikuwa lilelile kwamba mtu huyo alikuwa muuaji. Kijana huyo aliyeitwa Benjamin Saunders hakukubali, aliwaambia wazi kwamba hakuwa amemuua mtu yeyote na katika maisha yake hakuwahi kuua hata siku moja.
Polisi hawakuridhika, waliendelea kumwambia hivyohivyo mpaka baada ya dakika kadhaa walipotoka ndani ya chumba hicho. Benjamin alikuwa kimya, pingu zilikuwa mikononi mwake, alilia, kila alipokiangalia kile chumba, moyo wake ulimuuma mno, hakuwahi kufikiria kwamba kuna siku angeitwa ndani ya jumba hilo kubwa la polisi na kuambiwa kwamba aliua.
Wakati akiwa humo huku akilia, mara mlango ukafunguliwa, wanaume wawili waliovalia suti nyeusi wakaingia ndani, mmoja alikuwa na begi dogo, wakachukua viti na kukaa mbele yake.
Hawakuzungumza kitu kwanza, walibaki wakimwangalia kwa muda, waliporidhika, wakachukua vitambulisho vyao na kumuonyeshea Benjamini, walikuwa ni maofisa kutoka katika Shirika la Kijasusi la FBI(Federal Bureau of Investigation).
“Naitwa Brett Phillip,” alisema mwanaume mmoja.
“Naitwa Ryan Cashman,” alisema mwingine na kunyamaza.
Benjamin akawaangalia wanaume hao usoni, walionekana kuwa makini na kazi yao. Walipoona kijana huyo ameangalia vitambulisho vyao na kujiridhisha kwamba wao walikuwa maofisa kutoka FBI, wakavirudisha vitambulisho vyao mifukoni.
“Tunajua kwamba hukuua, tunajua hilo Benjamin,” alisema Brett huku akimwangalia Benjamin usoni.
“Ndiyo! Sijaua, sijawahi kuua, na kamwe sitoua,” alisema Benjamin kwa sauti ya chini huku akijifuta machozi.
“Ila alama zote zinaonyesha kwamba uliua,” alisema Brett.
“Sijajua nini kilitokea ila sijamuua mtu yeyote,” alisema Benjamin.
“Kweli?”
“Ndiyo! Sijamuua yeyote yule.”
Alichokifanya Brett ni kuchukua begi lake aliloingia nalo humo ndani, akalifungua na kutoa karatasi fulani kisha kuiweka mezani huku akimtaka Benjamin aichukue na iangalie.
“Mungu wangu!” alisema Benjamin huku akianza kulia.
“Kweli mpaka hapo unasema hujaua?”
Benjamin akabaki kimya, kile alichokiona kwenye karatasi ile hakuamini, hakujua kitu gani kilitokea, mbele yake aliona giza na kuona maisha yake yakienda kuisha gerezani kama si kuchomwa sindano ya sumu au kunyongwa.
Mdomo wake ulikuwa mzito mno, hakuamini alichokuwa akikiangalia katika karatasi ile, akawaangalia maofisa waliokuwa mbele yake, walionekana kuwa makini na kazi zao, mtazamo waliokuwa wakiutumia kumwangalia Benjamin, ulionyesha walikuwa na uhakika kwamba kijana huyo alikuwa amefanya mauaji waliyokuwa wakimshuku.
“Una lolote la kujitetea kabla hatujakwenda mahakamani?” aliuliza Brett.
“Sikuwahi kufanya mauaji, sijui nini kilitokea...”
“Lakini alama zako zimekutwa kama ushahidi.”
“Najua, ila sijafanya mauaji......ninaanza kukumbuka, ninaweza kuwatajia aliyefanya mauaji haya, ila si mimi. Nakumbuka niliambiwa nifanye mauaji haya, nikakataa, nililazimishwa sana, niliendelea kukataa, nikaambiwa kwamba kama ninakataa, basi kuna mtu atafanya mauaji, baada ya hapo, nitaonekana mimi ndiye nimefanya mauaji. Mungu wangu! Kwanza mchumba wangu Vivian yupo wapi? Walimuua, kwa nini walimuua msichana ninayempenda?” aliuliza Benjamini huku akilia.
Maofisa wale walibaki wakimwangalia, alionekana kukumbuka kitu, kwa jinsi alivyokuwa akijitetea, hata muonekano wake ulionyesha kabisa kwamba hakuwa amefanya mauaji. Kitendo cha kusema kwamba alimfahamu muuaji, kwa maofisa hao kilionekana kuwa nafuu kwao, hicho ndicho kitu walichokuwa wakikihitaji kwani kwa jinsi mauaji yalivyokuwa yamefanyika, ilikuwa ni vigumu kumgundua muuaji.
“Sawa! Sasa muuaji ni nani?” aliuliza Brett huku yeye na mwenzake wakimwangalia Benjamin usoni.
****
Julai 4, 2010
Washington DC
Zaidi ya watu elfu tatu walikuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya Ikulu ya Marekani, White House kwa ajili ya kusikiliza hotuba kutoka kwa rais wa nchi hiyo, Barack Obama ambaye ndiye alikuwa akitimiza mwaka wa pili tangu aingie madarakani na kuwa rais wa nchi hiyo.
Watu wote waliokuwa hapo, walikuwa na bendera za nchi yao, waliipenda, waliitukuza na kuiona kuwa na thamani kuliko nchi zote duniani.
Siku hiyo ya kusherehekea Uhuru wa nchi yao tangu mwaka 1776 ambapo George Washington aliuchukua kutoka kwa Waingereza, ndiyo siku ambayo Wamarekani wote duniani huithamini kuliko siku yoyote ile.
Wanafunzi hawakwenda shuleni, wanachuo hawakwenda vyuoni, wafanyakazi hawakwenda kazini, yaani kila mtu alitakiwa kukaa nyumbani kwake, kwa wale waliokuwa mbali na Jiji la Washington, walitakiwa kubaki nyumbani na kuangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea huko kupitia runinga zao ila kwa waliokuwa Washington tena waliokuwa na nafasi, walitakia kufika katika uwanja wa Ikulu ya Marekani, White House.
Miongoni mwa watu wengi waliokuwa katika eneo la uwanja wa Ikulu hiyo alikuwepo kijana msomi kutoka katika Chuo Kikuu cha Harvard, Benjamin Saunders ambaye alibakiza mwaka mmoja kabla ya kuhitimu masomo yake.
Benjamin hakuwa peke yake, alikuwa na mpenzi wake, Vivian ambaye alisafiri kutoka Los Angeles mpaka hapo Washington kwa ajili ya kumsikiliza rais wao mweusi ambaye alitaka kuzungumza na Wamarekani wote duniani.
Kama walivyokuwa wengine, hata na wao walikuwa na bendera za nchi hiyo mikononi mwao. Muda wote walikuwa wakishangilia, walionekana kuwa na furaha mno huku wakati mwingine wakikumbatiana, hakukuwa na kitu kilichowapa furaha kama kuwa wote katika kipindi kama hicho.
Walipendana mno, hakukuwa na kitu ambacho kingeweza kuwatenganisha. Japokuwa walikuwa kwenye mafarakano ya mara kwa mara lakini muda mwingi walionekana kuwa na furaha kana kwamba hakukuwa na kitu kibaya kilichokuwa kikiendelea.
“Tukitoka hapa?” aliuliza Vivian.
“Twende nyumbani!”
“Kwako?”
“Kwani unaogopa nini?”
“Siogopi chochote, ila naweza kuchelewa masomo,” alijibu Vivian.
“Wala usijali, utawahi tu,” alisema Benjamin.
Benjamin alikuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Harvard kilichokuwa jijini Cambridge ndani ya Jimbo la Boston hapohapo nchini Marekani, mbali na kutoka katika familia iliyokuwa na fedha, Benjamin alikuwa na uwezo mkubwa chuoni. Alikuwa akichukua masomo ya uuguzi, ndoto yake kubwa iliyokuwa mbele yake ni kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini Marekani.
Hiyo ilikuwa ndoto yake, hakutaka kuiona ikipotea, katika maisha yake, alimuahidi mama yake kwamba kuna siku angekuwa daktari mkubwa wa magonjwa ya moyo nchini Marekani, baba yake alikufa kwa ugonjwa wa moyo, hakutaka kuona watu wengine wakifa na ndiyo maana alisoma sana kufanikisha ndoto hiyo aliyojiwekea.
Mpenzi wake alikuwa akisomea masomo ya uandishi wa habari katika Chuo cha UCLA (University of California, huko Los Angeles). Kama alivyokuwa Benjamin, hata naye Vivian alikuwa na uwezo mkubwa darasani, aliwaongoza wanachuo wenzake na kuonekana kufanya mambo makubwa hapo baadaye kupitia uandishi aliokuwa akiusomea.
“Ngriii...ngriii...ngriii...” ulisikika mlio wa simu ukiita, mbali na kuita, simu hiyo ilikuwa katika mtetemo.
Mlio wa simu hiyo waliusikia kwa mbali kutoka na kelele zilizokuwa mahali hapo lakini baada ya Benjamin kuhisi mtetemo huo kutoka mfukoni mwake, harakaharaka akaichukua simu hiyo.
Alishangaa, haikuwa simu yake lakini aliikuta katika mfuko wa koti lake, si yeye tu aliyeshangaa, hata msichana wake, Vivian alishangaa pia. Walibaki wakiangaliana kwa sekunde kadhaa, hawakujua ni nani aliiweka simu ile katika koti lake na wala hawakujua lengo la huyo mwekaji lilikuwa nini.
“Hiyo simu umeitoa wapi?” aliuliza Vivian.
“Sijui, ndiyo kwanza nimeikuta mfukoni mwangu!”
“Nani amekuwekea?”
“Sijui pia.”
“Hebu pokea.”
Alichokifanya Benjamin ni kuipokea simu ile na kuita. Japokuwa mtu wa upande wa pili alikuwa akizungumza lakini Benjamin hakuweza kumsikia kutokana na kelele zilizokuwa mahali pale.
Wakati akiwa na simu hiyo sikioni, mara wanaume wawili waliovalia suti wakamsogelea, wakaanza kumwangalia na kumshika mkono huku wakimtaka wamfuate.
“Kuna nini?”
“Wewe twende tu,” alisema mwanaume mmoja, Benjamin hakuwa na wasiwasi, akaanza kuwafuata kama alivyoambiwa, hata Vivian naye hakutaka kubaki mahali hapo, naye akaanza kuwafuata huku akionekana kuwa na hofu kubwa, kichwa chake kikaanza kujiuliza mambo mengi kuhusu watu wale, walikuwa wakina nani? Akakosa jibu.

JE, nini kitaendelea?
 
Sehemu ya Kwanza.

Ilikuwa ni taarifa mbaya, iliyoshtua ambayo ilianza kwa kusikika katika sehemu mbalimbali jijini Las Vegas nchini Marekani kabla ya kuwafikia polisi. Kila aliyezisikia taarifa hizo, hakuamini, wengi wakahisi kwamba hazikuwa taarifa za kweli, labda kulikuwa na mtu mwingine aliyetaka kuivumisha habari hiyo ambayo ilimsisimua kila mtu aliyeisikia.
Msichana mrembo aliyeitwa kwa jina la Stacie Lawrence, msichana aliyebahatika kunyakua taji la Urembo wa Dunia, alikutwa amekufa ndani ya chumba kimoja cha Hoteli ya Vikings Hill iliyokuwa Las Vegas, Nevada nchini Marekani alipokuwa amepanga huku akisubiri kuonana na Mkurugenzi wa Tovuti ya Google kwa ajili ya kusaini mkataba wa picha zake kutumika katika programu moja ambayo ingetumiwa katika simu zote zinazotumia system ya android.
Stacie aliyekuwa gumzo kwa kipindi hicho duniani kutoka na uzuriwake, alikutwa amekufa baada ya kujiovadosi madawa ya kulevya aina ya Heroine kwa kujichoma sindano katika mkono wake wa kulia wakati kitandani ndani ya hoteli hiyo.
Hiyo ndiyo ilikuwa habari ya mjini, kila aliyeisikia, hakuamini, swali la kwanza kabisa walilojiuliza watu ni juu ya utumiaji wa madawa ya kulevya. Kila mtu alijua kwamba Stacie hakuwahi kutumia madawa hayo, si kipindi hicho tu, hata kabla ya kutwaataji hilo, hakuwa mtumiaji, sasa ilikuwaje mpaka leo hii akutwe chumbani kitandani akiwa amejidunga madawa hayo? Hilo lilikuwa swali lisilokuwa na majibu.
Waandishi wa habari kutoka katika mashirika mbalimbali ya habari kama CNN, BBC, Sky News na hata wale wa kujitegemea tayari walikuwa nje ya hoteli hiyo, vitendea kazi vyao vyote vilikuwa mikononi mwao, walitaka kupiga picha na kupata habari kuhusu kifo cha msichana huyo mrembo ambaye bado uzuri wake ulikuwa gumzo duniani.
Polisi walitanda kila sehemu nje ya hoteli hiyo, mkanda wa njano ulioandikwa Do Not Cross yaani ‘Usivuke’ulizungushiwa katika hoteli hiyo kwa muda. Magari ya wagonjwa mawili yalikuwa yamekwishafika katika hoteli hiyo, kilichosubiriwa ni kuingia ndani na kuuchukua mwili huo.
Waandishi hawakuruhusiwa kabisa kuingia ndani ya hoteli hiyo, waliambiwa wasubiri hapo nje wakati polisi wakiingia ndani kwa ajili ya kufanya kazi yao, hawakuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri.
Polisi wakaingia ndani ya chumba kile. Huko wakaukuta mwili wa Stacie ukiwa kitandani, katika mkono wake wa kushoto kulikuwa na sindano iliyochoma mshipa wake, aliishikilia kwa kutumia mkono wake wa kulia mbali na hivyo, pembeni yake kulikuwa na noti za Dola, Paundi, Yeni na Euro.
Udenda ulikuwa ukimtoka, pale alipokuwa, hakutingishika, kilikuwa kifo kibaya, kilichozua maswali mengi kwa watu wengi, maswali hayo yote, hakukuwa na mtu aliyekuwa na majibu zaidi ya Stacie mwenyewe ambaye kipindi hicho alikuwa marehemu.
“This is the fifth one, what the hell with the drugs?” (huyu ni mtu wa tano, kuna nini na haya madawa?) alisikika akiuliza mwanaume mmoja huku akionekana kushangaa.
“I don’t know. What the hell with these teenagers, they like to try each and every goddamn thing, why?” (sifahamu. Nini kinaendelea kwa hawa vijana, wanapenda kujaribu kila kitu, kwa nini?) aliuliza mzee mmoja huku akionekana kukasirika.
Kila mmoja alishangaa, huyo hakuwa mtu wa kwanza, supastaa aliyejiua baada ya kujiovadozi kwa madawa ya kulevya, huyo alikuwa mtu wa tano, kijana supastaa ambaye aliamua kujiua kwa kujidunga sindano ya madawa ya kulevya.
Mtu wa kwanza kabisa kujiua kwa kujidunga shindano alikuwa Paul McKenz. Huyu alikuwa mcheza kikapu aliyekuwa akichipukia, mwenye sura nzuri, alijitengenezea jina kubwa katika Timu ya La Lakers, akaanza kupata mashabiki wengi, alipendwa na kila mtu aliyekuwa akiupenda mchezo huo, jina lake likaanza kuwa kubwa, akapata mikataba mingi lakini mwisho wa siku, Paul akaja kujidunga sindano yenye madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine chumbani kwake.
Watu wengi walisikitika kwani ndiye alikuwa kijana aliyekuwa akichipukia katika mafanikio makubwa. Hiyo haikuishia hapo, pia kulikuwa na kijana mwingine aliyekuwa na kipaji cha uigizaji. Katika filamu yake ya kwanza ya Fallen Tree, alishinda Tuzo ya Oscar, Global na nyingine nyingi, huyu aliitwa Todd Lewis.
Bahati ikaanza kuonekana upande wake, akapendwa sana, kila kona alisikika yeye tu. Kadiri jina lake lilivyovuma ndivyo alivyozidi kujitengenezea mashabiki. Wakati akiwa amenunua gari yake ya kwanza ya thamani kabisa aina ya Ferrari Testarossa nyekundu, akakutwa naye akiwa amejidunga madawa ya kulevya ndani ya gari lake nje ya klabu moja huku pembeni kukiwa na noti ya dola, paundi, Yuan na Euro. Watu walisikitika na kulia, vilio vyao, huzuni zao hazikuweza kuwarudisha watu hao duniani.
Mtu mwingine kabla ya Stacie kujiua kwa madawa ya kulevya alikuwa kijana aliyeitwa kwa jina la Carter Phillip. Huyu alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakichipukia katika muziki wa Pop. Alikuwa na sauti kali, yenye nguvu ambapo kila alipokuwa akiitumia katika nyimbo zake, wanawake walichanganyikiwa.
Alikuwa mzuri wa sura, mwili uliojengeka. Kibao chake cha kwanza kabisa cha Come and Get Me Shawty alichokitoa kilitingisha kila kona duniani. Uwezo wake ulionekana, si hapo tu hata kwenye Shindano la American Got Talent, mpaka aliposhinda, watu waliona kipaji kikubwa ndani yake.
Wengi wakatabiri kwamba Carter ndiye angekuwa mrithi sahihi wa Michael Jackson, wengi wakamtabiria mema, njozi njema ikaonekana mapema kabisa kwani ngoma zake mbili alizozitoa, zote zilishika nafasi za juu kabisa katika orodha ya Billboard.
Akatengeneza fedha nyingi huku ndiyo kwanza akiwa na miaka kumi na tisa. Akapendwa, akawa kipenzi kikubwa cha watu ila baada ya kwenda nchini Uingereza kwenye Tamasha la UKIMWI lililokuwa likifanyika katika Jiji la Southampton, akakutwa akiwa amejiua ndani ya chumba alichochukua hotelini baada ya kujidunga sindano iliyokuwa na madawa ya kulevya aina ya Dextromethorphan huku pembeni kukiwa na noti za dola, paundi, yuan na euro.
Hakukuwa na aliyejua sababu ya vijana hao kujidunga madawa hayo ya kulevya, kila mtu aliyepata habari za vijana hao alishtuka. Mpaka katika kipindi ambacho msichana mrembo, Stacie kujiovadozi madawa hayo, bado watu hawakujua sababu ilikuwa nini, ni afadhali kama wangekuwa wamepigika katika maisha yao, ila kilichoshangaza, walikuwa wakianza kupata umaarufu, kupata fedha, na ndipo kipindi hichohicho nao waliamua kujidunga madawa ya kulevya.
Dunia ikatetemeka, watu wakaogopa kuwa mastaa, wengi walisikia kwamba unapokuwa staa, ilikuwa ni lazima kutumia madawa ya kulevya. Wazazi walipowaona vijana wao wanaanza harakati kupitia vipaji vyao, waliwazuia kwa kuona kwamba mwisho wa siku wangejiua kama hao wengine.
Swali kubwa ambalo waandishi wa habari walihoji, mitaani ni sababu gani zilizopelekea vijana hao kujidunga madawa ya kulevya? Kila aliyeuliza swali hilo, alikosa jibu kabisa.

Je, nini kitaendelea?
Nini kilipelekea watu hao, mastaa wakubwa kujimaliza kwa kujiovadozi madawa ya kulevya?
Tukutane kesho hapahapa
Imetulia sana.
But is it true or just a story??!
 
NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA

Sehemu ya Tatu.

Benjamin akaongozana na watu wale mpaka walipofika katika gari moja kubwa ambalo hakujua ndani kulikuwa na nini, akaambiwa aingie na mpenzi wake kisha kukaa katika kiti kimoja, ndani ya gari hilo, kulikuwa na televisheni nyingi zilizokuwa zinaonyesha matukio yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano ule.
Hakukuwa na mtu aliyezungumza lolote lile, kila mmoja alikuwa bize akifanya mambo yake. Benjamin na mpenzi wake, Vivian walikuwa karibukaribu, msichana huyo alionekana kuwa na wasiwasi mno, hakuwa na amani wala furaha, kwake alichokiona mbele yake kilikuwa ni tatizo kubwa.
Huku wakiwa wametulia katika viti, mwanaume mmoja akafika mahali hapo, akawatupia macho, hakuonyesha tabasamu lolote lile, macho yake yalionyesha ni jinsi gani mtu huyo alikuwa siriazi.
“Unaitwa Benjamin Saunders, si ndiyo?” aliuliza mwanaume huyo.
Kabla ya kujibu swali hilo, Benjamin akashtuka, hakujua mtu huyo alikuwa nani sasa ilikuwaje alijue jina lake? Akajiuliza, labda alikwishawahi kuonana na mwanaume huyo sehemu fulani, hakupata jibu, alivuta kumbukumbu zake, zikamwambia kwamba mwanaume huyo alikuwa mgeni machoni mwake.
“Ndiyo!” alijibu baada ya ukimya wa sekunde kadhaa.
“Ulikuwa unawasiliana na nani kwenye simu?” aliuliza mwanaume huyo.
“Mimi?”
“Najua unajua nazungumza na nani!”
“Hata mimi sifahamu!”
“Hufahamu nini?”
“Niliyekuwa nazungumza naye, simfahamu!”
“Kwani hiyo simu ni ya nani?”
“Hata hilo pia sifahamu! Nilisikia simu ikiita kwenye koti langu, nikaichukua na nilipotaka kuzungumza kuna watu wakaja kunichukua, ni watu wako bila shaka,” alijibu Benjamin.
Alichokifanya jamaa yule ni kuichukua simu hiyo na kuondoka nayo huku akiwaambia kwamba kunapokuwa na mkutano wa rais, hakutakiwi mtu yeyote yule kupokea simu hasa kwa namba ambayo haipo kwenye simu yake.
Benjamin akashindwa kufahamu ni kwa sababu gani lakini jibu ambalo alikuwa nalo, inawezekana kwa sababu ya masuala ya usalama ndiyo maana waliamua kumchukua na kuondoka naye.
Huko kwenye mkutano, hakuwa na raha hata kidogo, alibaki akikodoa macho yake huku nakule, hata rais alipokuja na kuanza kuhutubia taifa, hakuwa makini kumsikiliza, macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule.
Baada ya rais kumaliza na kuondoka, yeye mwenyewe akamchukua Vivian na kuondoka naye mahali hapo huku akionekana kuwa na mawazo lukuki. Alipokwenda mpaka sehemu alipoliegesha gari lake, akalifungua mlango na kuingia ndani.
“Hii bahasha ya nani?” aliuliza Vivian mara baada ya kuingia ndani ya gari na kukuta bahasha kwenye dashibodi.
“Bahasha ipi?”
“Hii hapa!”
Benjamin akaichukua ile bahasha na kuifungua ili kujua humo ndani kulikuwa na nini. Alipoifungua, alikikuta kikaratasi kidogo kikiwa kimeandikwa ‘Crowne Plaza 1930’ huku kukiwa na noti ya dola, paundi, Yuan na Euro.
“Hii ni nini?” aliuliza Vivian huku akionekana kushangaa.
“Ni ujumbe...”
“Ujumbe gani?”
“Huyu mtu anataka kuonana na mimi!”
“Nani? Kuonana naye wapi?”
“Sijajua ni nani! Ila anataka nionane naye Crowne Plaza saa moja na nusu usiku,” alijibu Benjamin.
“Na vipi kuhusu hizo noti?”
“Sifahamu chochote kile. Huyu ni nani? Anataka nini kutoka kwangu?” aliuliza Benjamin pasipo kupata kitu chochote kile.
“Tukatoe taarifa polisi,” alishauri Vivian.
“Unahisi itasaidia?”
“Ndiyo!”
Hilo ndilo walilokubaliana kwamba ilikuwa ni lazima wakatoe taarifa polisi. Hakukuwa na cha kujiuliza tena, walichoshauriana ndicho walichokifanya. Benjamin akawasha gari na kuondoka mahali hapo, breki ya kwanza kabisa ilikuwa katika kituo cha polisi hapo New York na kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea.
Walichomwambia polisi hao ni kwenda huko kwenye miadi kama alivyoambiwa na wao wangekuwa nyuma wakifuatilia ili atakapokutana na huyo mtu wamkamate kwani hali ilionyesha dhahiri kuwa mtu huyo hakuwa mzuri hata kidogo.
“Wewe nenda kama alivyokwambia, ukifika hapo, subiri, akija, tutamkamata, umesikia?” aliuliza polisi.
“Sawa!”
Alitakiwa kufanya kama alivyoambiwa, hivyo ilivyofika saa moja kamili usiku akaanza kuondoka alipokuwa akiishi kwenda kwenye hoteli kubwa ya Crowne Plaza ambapo kulikuwa na baa pia.
Polisi walikuwa pamoja naye, hawakuwa kwenye gari moja ila walianza kufuatilia tangu mchakato ulipoanza huku wengine wakiwa tayari wamekwishafika ndani ya baa iliyokuwa katika hoteli hiyo. Alipoegesha gari lake, akateremka na kuanza kuelekea ndani ya baa hiyo.
Macho yake hayakutulia, alikuwa akiangalia huku na kule kama mtu aliyekuwa akimtafuta mtu fulani. Kila aliyekuwa humo alikuwa bize, wengine walikuwa wakinywa na marafiki zao, wapenzi wao na hakukuwa hata na mtu mmoja aliyeonekana kumjali.
Akaifuata meza moja na kutulia, hakuonekana kujiamini, bado alikuwa akiiangalia huku na kule. Muda ulizidi kukatika, saa moja na nusu ikaingia, hakukuwa na mtu aliyetokea, saa mbili ikaingia lakini bado hakukuwa na mtu yeyote kitu kilichoonekana kumshangaza.
“Yupo wapi?” alijiuliza huku akiangalia saa yake.
Mpaka inafika saa tatu na nusu usiku, hakukuwa na mtu aliyemsogelea, hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka huku akiwa na mawazo tele.
Polisi ambao aliongozana nao na wale waliokuwa ndani ya baa ile walipoona hakuna kitu chochote kilichoendelea, nao wakaondoka na kuhisi kwamba inawezekana mtu huyo aliwaona na ndiyo maana hakutaka kabisa kujitokeza.
“Imekuwaje huko?” aliuliza Vivian.
“Hakutokea mtu yeyote!”
“Kweli?”
“Nd...” alijibu Benjamin lakini hata kabla hajamaliza kutoa jibu lake, hapohapo simu yake ikaanza kuita, harakaharaka akaipokea.
“Halo!”
“Kwa nini umekuja na polisi?”
“Wewe nani?”
“Hujajibu swali langu! Kwa nini ulikuja na polisi?” ilisikika sauti hiyo ikiuliza Sali.
“Wapi?”
“Nilipokwambia uje!”
“Sikuja na polisi!”
“Acha kunidanganya. Sasa sikiliza. Nataka tukutane kesho saa mbili asubuhi kwenye mgahawa wa KFC jirani yako, kama utashindwa, nitakutumia mkanda wa msichana wako Vivian akiwa anauawa. Umesikia?” alisema mtu huyo na kuuliza.
“Ila wewe ni nani?”
“Mimi ni Dola, Paundi, Yen na Euro.”
“Unamaanisha nini?”
“Fanya unachotakiwa kufanya. Kama unampenda mpenzi wako, njoo, tena ukiwa peke yako, vinginevyo, tutamuua,” alisikika mwanaume huyo.
Simu ikakatika. Mazungumzo yale, hata msichana Vivian alikuwa akiyasikia, wote wakaogopa, hawakujua mtu huyo aliikuwa nani na alihitaji nini kutoka kwa Benjamin.
Wote wawili wakakosa amani, hofu zikawajia mioyoni mwao, hawakujua ni kitu gani walitakiwa kufanya, kutoa taarifa polisi lilionekana kuwa tatizo jingine kabisa, alitakiwa kufanya kila kitu alichoambiwa pasipo kuwashirikisha polisi kwani vinginevyo mpenzi wake Vivian angeuawa kama alivyoambiwa.
 
Hiyu mwandishi ni nguli haswaa.
1.Dili la Dolla Billion Nne
2.Mauaji yaliyojaa Utata
 
Thanks
 
NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA

Sehemu ya Nne.

Usiku mzima Benjamin hakuwa na furaha, moyo wake ulikuwa na hofu tele, simu aliyoipokea ilimtisha, alitamani kwenda kutoa taarifa polisi lakini maneno aliyoambiwa na vitisho hasa dhidi ya mpenzi wake, vilimfanya kukosa amani kabisa.
Alibaki akizungumza naye, jambo lililokuwa mbele yao liliwatisha wote wawili. Hawakujua hao watu walihitaji nini kutoka kwake, alitoka katika familia ya kitajiri, alifikiri labda watu hao walihitaji fedha kutoka kwake, ila kila alipofikiria hilo, hakupata jibu.
Kama kweli wangekuwa wanahitaji fedha, basi wangemteka mpenzi wake na kisha kumwambia kwamba awapelekee fedha lakini kwa kile walichokifanya cha kutaka kuonana naye, hakikumpa uhakika kama watu hao walihitaji fedha kutoka kwake.
“Watakuwa wanahitaji nini?” aliuliza Vivian.
“Sijui! Haina jinsi ngoja niende...” alijibu Benjamin.
“Lakini wanaweza kukuua!”
“Unafikiri nitafanyaje? Naweza nikagoma kwenda halafu wakaja kukuua. Vivian mpenzi, sipo tayari kuona ukifa, acha niende nitasikia wananiiambia nini,” alisema Benjamin.
Hakuwa na jinsi, alitamani kumuona mpenzi wake akiwa mzima kila siku, alitamani kumuona akiwa na afya tele katika maisha yake yote hivyo kwenda huko katika mgahawa wa KFC wala halikuwa tatizo.
Asubuhi ilipofika, akajiandaa na kisha kwenda katika mgahawa huo huku tayari ikiwa ni saa mbili asubuhi. Alipofika, akasimama na kuanza kuangalia huko na huku, alionekana kuwa na hofu tele moyoni mwake, na hata mhudumu aliyekuja kuzungumza naye kuhusu kifungua kinywa, aliweza kugundua hofu aliyokuwa nayo.
“What can I help you?” (Nikusaidie nini?) aliuliza mhudumu huo.
“A cup of coffee, please,” (Kikombe cha kahawa, tafadhali)
Macho yake yaliendelea kuangalia huku na kule, alihisi kwamba angeweza kumuona mtu yeyote ambaye angekuwa akimwangalia ili agundue kwamba mtu huyo ndiye alikuwa akitaka kuzungumza naye, aliangalia kila kona, kila mmoja alikuwa bize na mambo yake.
Baada ya dakika kadhaa, Benjamin akaletewa kikombe cha kahawa na kuanza kunywa. Aliangalia saa yake, muda alioambiwa akutane na huyo mtu ndani ya mgahawa huo ulipita lakini cha kushangaza, hakuweza kuja mtu yeyote pale alipokuwa.
Huku akiwa anaelekea kumaliza kikombe kile, ghafla akaanza kuhisi maumivu ya tumbo, hali hiyo ilimshangaza kwani alikumbuka kwamba hakuwa akiumwa ugonjwa huo, akashindwa kuvumilia, moja kwa moja akasimama na kuelekea chooni.
“Benjamin...” alisikia mtu akimuita wakati yupo ndani ya choo kile.
Aligeuka na kumwangalia mtu huyo aliyemuita, hakuwa ametoka nje, alimkuta mtu huyo humohumo ndani akiwa anaosha mikono yake katika sinki la maji. Benjamini alibaki akimwangalia, alimuita jina lake, aliimfahamu vipi? Alimwangalia kuhisi kwamba inawezekana aliwahi kumuona kabla, sura yake ilikuwa ngeni.
“Wewe ni nani?” aliuliza Benjamin.
“Tumbo linakuuma, kunywa hii dawa,” alisema mwanaume huyo.
“Wewe ni nani?”
“Kwani simu ilikwambiaje?”
“Kumbe ndiyo wewe...unataka nini kwangu jamani?” aliuliza Benjamin huku akimwangalia mwanaume huyo.
“Sikiliza Benjamin, tumbo linakuuma, kunywa hii dawa nikupe maelekezo mengine,” alisema mwanaume yule.
Benjamin hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kuchukua hiyo dawa na kuinywa. Hata dakika mbili nyingi, tumbo likatulia kabisa. Akakiangalia kikopo cha dawa ile, kikopo kile alikifahamu, kiliandikwa Merthamponic, hiyo ilikuwa ni dawa ya minyoo, aliifahamu lakini ile aliyokunywa, haikuwa dawa hiyo.
“Nisikilize kwanza...” alisema mwanaume huyo.
“Sawa!”
“Najua una akili sana, mimi na wewe, tutakuwa tunawasiliana kwa alama tu,” alisema mwanaume huyo.
“Unamaanisha nini?”
“Kwa sababu una akili!”
Benjamini alibaki akimwangalia mwanaume huyo, sura yake ilionyesha kama alikuwa mchangamfu fulani lakini kwa mbali ilionyesha kwamba mwanaume huyo hakuwa na masihara hata mara moja.
“Unataka nifanye nini?”
“Uue..”
“Niue?
“Ndiyo! Kuna mtu anatakiwa kuuawa haraka sana,” alisema mwanaume huyo.
“Nani?”
“Carter Jackson...” alijibu mwanaume huyo.
“Sijakuelewa...”
“Sikiliza. Nenda nje ya mgahawa huu, utakutana na mwanaume anaendesha baiskeli, mfuate huyo, atakwenda mbele kisha ataipaki baiskeli yake katika mgahawa unaoitwa Bavarian, ingia humo, agizia kikombe kimoja cha kahawa. Mhudumu atakayekuletea, mwambia kwamba unataka simu ya mawasiliano, atakupa, ichukue, toka nje, utaikuta ile baiskeli, ichukue, nenda nayo mpaka kwenye uwanja wa NFL wa Timu ya Buffaroes, ingia humo, nenda mpaka kwenye kiti namba 20 floo ya juu, kaa hapo na usiondoke,” alisema mwanaume huyo.
“Laki...”
“Fanya hivyo,” alisema mwanaume huyo na kutoka chooni mule.
Benjamin alibaki ndani ya choo kile, alikuwa na mawazo mengi, maneno aliyoambiwa na mwanaume yule kwamba alitakiwa kumuua Carter yalimchanganya kichwa chake.
Alimfahamu Carter, alikuwa miongoni mwa wanamuziki waliokuwa wakichipukia kipindi hicho, alikuwa na mashabiki wengi, alipendwa kila kona na watu waliokuwa wakizipenda kazi zake alikuwa mpenzi wake, Vivian.
Kumuua Carter ilikuwa kazi kubwa sana, hakuwahi kuua na wala hakufikiria kama kuna siku angekuja kuua, mbaya zaidi mtu aliyeambiwa amuue katika kipindi hicho alikuwa mwanamuziki aliyependwa sana.
Mbele yake ilionekana kuwa kazi kubwa, alikataa katakata kufanya hivyo lakini kila alipokumbuka kwamba kulikuwa na mpenzi na angeweza kuuawa, hakuwa na jinsi ilikuwa ni lazima kufanya hivyo.
Alichokifanya ni kutoka ndani ya choo kile, hakurudi katika kiti chake, akaondoka na kuelekea nje, kama alivyoambiwa, kweli akamuona mtu mmoja akipita huku akiikokota baiskeli yake, akaanza kumfuata kwa mwendo wa taratibu.
Mwanaume huyo aliyekuwa na baiskeli hakuonekana kuwa na habari yoyote ile kama nyuma alikuwa akifuatiliwa, aliendelea kumfuata mpaka katika mgahawa uleule wa Bavaria ambapo aliipaki baiskeli yake na kuingia ndani, alichokifanya Benjamin, na yeye akaingia ndani na kutulia kwenye meza moja.
“Nikusaidie nini?”
“Nahitaji kikombe kimoja cha kahawa,” alijibu Benjamin, msichana huyo akaondoka, aliporudi, alikuwa na kikombe cha kahawa.
“Unahitaji nini kingine?”
“Simu ya mawasiliano,” alijibu, hapohapo msichana huyo akatoa simu mfukoni na kumgawia simu hiyo, Benjamini hakutaka kusubiri, alichokifanya ni kutoka nje, akachukua baiskeli ile na kuanza kuondoka kuelekea katika uwanja wa Timu ya Buffroes ambao aliambiwa kabla.
Alipofika huko, nje hakukuwa na watu wengi, kulikuwa na walinzi ambao walikuwa wakiwazuia waandishi wa habari na watu wengine kuingia ndani kuiona timu hiyo ikifanya mazoezi, kitu cha ajabu, alipokwenda yeye, hakuzuiliwa na mtu yeyote yule hali iliyoonyesha kwamba watu hao walijua kama angefika mahali hapo.
Akaingia ndani, akaelekea mpaka katika floo aliyoambiwa na kutafuta kiti namba ishirini, alipokiona, akatulia huku akisubiri ninii kingefuata. Wakati akiwa hapo kusubiri, simu yake ikaanza kuita, alipopokea, akaambiwa aangalie chini ya kitu, kuna fedha, achukue na aende akanunue baga katika mgahawa wa hoteli hiyo, hakubisha.
Alipoangalia chini ya kiti kile, akaona noti ya dola mia moja, akaichukua na kwenda kununua baga, alipofika huko, akapewa na kwenda sehemu kula, ghafla, macho yake yakaanza kuona giza, alijitahidi kuyafumbua zaidi lakini yakashindikana, kama mzigo, akajikuta akianguka chini, kilichoendelea baada ya hapo, hakukijua.
Mara baada ya saa mbili, Benjamin akayafumbua macho yake, akajikuta akiwa katika chumba kidogo kilichokuwa na mwanga hafifu, hakujua ilikuwa sehemu gani, aliangalia huku na kule lakini hakuwa akiona vizuri.
Kumbumbuku zake zikaanza kurudi nyuma tangu pale alipokula baga na mwisho wa siku kujikuta akipoteza fahamu. Hakujua ni kitu gani kilitokea, hakujua kama ile baga aliyokuwa amekula ndiyo iliyomfanya kupoteza fahamu au la.
Akasimama kutoka katika kitanda alichokuwa amelazwa na kuanza kuzungukazunguka ndani ya chumba hicho, alitaka kuondoka lakini hakujua ni wapi alitakiwa kuanzia, kulikuwa na mlango mmoja ila alipoushika na kujaribu kuufungua, haukuweza kufunguka.
“Where Am I?” (Nipo wapi?) alijiuliza huku akiendelea kujaribu kuufungua mlango ule.
“Someone help...someone help...” (Nisaidie, nisaidie...) alibaki akipiga kelele tu.
Baada ya dakika kadhaa, akasikia vishindo vya watu vikielekea kule alipokuwa, alichokifanya ni kuupigapiga mlango ili watu hao wasikie na hivyo kumfungulia. Watu hao hawakuwa wakielekea sehemu yoyote ile, walikuwa wakienda katika chumba kilekile, wakaufungua mlango.
“Let me go....let me go, pleaseee....” (acheni niondoke...acheni niondoke, tafadhali) alisema Benjamin huku akiwaangalia watu wale wa miraba minne ambao waliingia ndani ya chumba kile.
“Benjamin, just wait, there is someone wanna talk to you,” (Subiri Benjamin, kuna mtu anataka kuzungumza nawe) alisema mwanaume mmoja.
“Who is that?” (Nani huyo?)
“Dollar, Euro, Pound and Yuen,” (Dola, Euro, Paundi na Yeni) alijibu mwanaume huyo.
“Who is that man?” (Ndiye nani huyo?)
“Wait, he is coming but let’s go somewhere,” (Subiri, anakuja. Ila twende sehemu nzuri,” alisema mwanaume huyo.
Wakamchukua na kuondoka naye ndani ya chumba hicho. Benjamin alibaki akishangaa tu, alikuwa akiangalia huku na kule ndani ya nyumba hiyo, ilikuwa kubwa na ilionekana kuwa ya kifahari sana.
Safari yao fupi ikaishia ndani ya chumba kimoja kikubwa, kulikuwa na meza ndefu mbele yake ambayo ilizungukwa na viti kumi na mbili, akaambiwa atulie hapo, kuna mtu angekuja na kuzungumza naye.
Watu hao wakaondoka na kumwacha peke yake mahali pale. Benjamin hakuwa na amani, alikuwa na wasiwasi tele, hakujua sababu iliyomfanya kuletwa mahali pale lakini pia alishangazwa na jina la mtu huyo aliyekuwa akimuihitaji. Ndani ya chumba kile kulikuwa na kamera ndogo tatu za CCTV ambazo zilifungwa katika kona tatu za chumba hizo ambazo zilihakikisha kunakuwa na usalama ndani ya chumba hicho.
Katika maisha yake hakuwahi kusikia mtu akiitwa majina ya fedha, kwake ilikuwa ni ajabu kubwa mno. Alibaki akijiuliza mtu huyo alikuwa nani, hakupata jibu. Baada ya dakika kadhaa, mlango ukafunguliwa na mwanaume mmoja kuingia.
“Karibu sana Benjamin,” alisema mwanaume huyo huku akionekana kuwa na furaha mno.
Alimwangalia mwanaume huyo, hakuwa akimfahamu kabisa na hakukumbuka kama aliwahi kumuona mahali fulani. Kichwa cha Benjamin kilikuwa na maswali mengi, akaona huo ndiyo muda wa yeye kumuuliza maswali hayo mwanaume huyo.
“Kwa nini nipo hapa?” aliuliza.
“Kwa sababu kuna kazi kubwa ya kufanya...” alijibu mwanaume huyo, sura yake ilikuwa kwenye tabasamu pana.
“Kazi gani?”
“Usiwe na haraka, subiri...” alijibu mwanaume huyo, hapohapo akaondoka na kumwambia kwamba angerudi muda mchache ujao hivyo alitakiwa kusubiri hapo.
Benjamin akabaki akijiuliza juu ya kazi hiyo ambayo alitakiwa kufanya. Hakujua ilikuwa kazi gani na kwa nini alichaguliwa kuifanya kazi hiyo. Wakati akijiuliza maswali hayo, mlango huo ukafunguliwa na mwanaume huyo kurudi tena, akakifuata kiti na kutulia, wakati huu alikuwa na karatasi mkononi mwake.

JE, nini kitaendelea?
Tukutane Jumamosi.
 
NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA

Sehemu ya Tano.

Watu walikusanyika ndani ya uwanja mkubwa wa mchezo wa NFL wa Metroposa ambao ulikuwa ukimilikiwa na Timu ya New York Ville ambayo ilikuwa ikishiriki mchezo huo.
Watu hao walijazana kuliko siku nyingine ambapo mechi kubwa ya mchezo huo zilipokuwa zikichezwa. Siku hiyo watu hawakukusanyika kwa wingi kwa ajili ya kuiona timu hiyo ikicheza, walikusanyika kwa ajili ya kumuona mwanamuziki aliyekuwa akichipukia kipindi hicho, mwenye jina dogo na uwezo mkubwa, aliyekuwa akiimba nyimbo za Pop, Carter Phillip.
Wanawake ndiyo walikuwa kwa wingi mahali hapo, wengi walimpenda Carter, si kwa sababu ya nyimbo zake kali ikiwemo Come and Get Me Shawty bali hata muonekano wake ulikuwa mzuri mno, alikuwa na sura iliyovutia, mwili uliojengeka vizuri kimazoezi huku ndiyo kwanza akiwa na miaka kumi na nane tu.
“I am free tonight, come to me, Carter,” (Nipo huru usiku wa leo, njoo kwani, Carter) lilikuwa bango moja lililoshikwa na msichana mrembo uwanjani hapo.
Mbali na bango hilo, kulikuwa na mabango mengine mengi yaliyoshikwa na wanawake ambayo yalionyesha hisia nzito walizokuwa nazo juu ya mwanamuziki huyo mwenye sauti nzuri na ujuzi wa kucheza.
Muda huo, watu walikuwa wakishangilia sana, hakukuwa na mtu aliyetulia, kelele zilikuwa kila kona. Carter hakuwa amefika jukwaani hapo lakini kila mtu alikuwa na hamu ya kumuona mwanamuziki huyo akitumbuiza jukwaani.
Baada ya dakika kadhaa, Carter akafika jukwaani hapo kwa mbwembwe, uwanja ukalipuka, wale waliokuwa mbali, wakaanza kuwasukuma wa mbele yao ili nao waweze kuona vizuri, hakukuwa na mtu aliyetaka kumwangalia Carter kupitia kwenye televisheni kubwa iliyokuwa uwanjani hapo, kila mtu alitaka kumuona ‘live’
“Come and Get Me Shawty,” Carter alisema kwa sauti kubwa jina la wimbo wake uliokuwa ukivuma kiipindi hicho.
Hiyo ilikuwa ni kama kuwachengua mashabiki zake, kelele zikazidi kusikika mahali hapo, watu wakachanganyikiwa mno, wanawake wakawa kama wamepagawa, wengine wakakosa hewa ya kutosha kutokana na wingi wa watu hivyo kuzimia.
Uwanjani ilikuwa purukushani, wengine wakapanda jukwaani na kutaka kugusa tu Carter kwani walichanganyikiwa mno. Mabaunsa ambao ndiyo walionekana kuwa walinzi mahali hapo wakawawahi watu hao na kuwazuia, hiyo haikutosha, wakawashusha kutoka jukwaani.
“I wanna introduce my new hit, this is How Am I Suppose To Say,” (Ninataka kutambulisha ngoma yangu mpya, hii ni Nisemeje) alisema Carter maneno yaliyowafanya watu uwanjani hapo kushangilia kwa sauti kubwa.
****
Jina la Carter halikuwa nchini Marekani tu, kila kona katika dunia hii, watu walimfahamu huku wengi wao wakimuita kama The ‘New Michael Jackson’ wakiwa na maana ya Michael Jackson Mpya.
Watu walimtabiria makubwa, katika wimbo wake wa kwanza alioutoa, ulikimbiza vilivyo na kumfanya kuwa tajiri mkubwa. Watu wengi walimpenda, makampuni mbalimbali yakajitolea kumfanya biashara kwani watu wengi waliokuwa wakimfuata, walipenda kufanya kile alichokuwa akikifanya.
Kama leo alinyoa hivi, mitaani hiyo ilionekana kuwa fasheni mpya hivyo nao waliiga, leo alivyovaa hivi, kesho asubuhi nao watu wakaiga. Alikuwa nembo kila sehemu aliyokuwa akipita, barabarani, hakuwa na raha, kila alipotembea watu walimfuata kwa wingi na kutaka wasainiwe vitabu vyao, kwa kifupi, maisha ya Carter yalikuwa yenye usumbufu mkubwa.
Siku zikaendelea kukatika, akaunti yake ikasoma kiasi kikubwa, zaidi ya dola milioni mia mbili kwa kipindi kifupi mno. Fedha hizo, kwa umri wake, jina lake zilikuwa nyingi mno ambazo kwa fedha za Kitanzania zilikuwa ni zaidi ya bilioni mia nne.
Maisha yake yakabadilika, hakutaka kuishia hapo, hakutaka kuridhika, alichokifanya ni kuendelea kufanya mambo makubwa, akazidi kutoa nyimbo kali, zilizomfanya kushika nafasi za juu kabisa katika chati ya Billboard kitu kilichomfanya kuwa tajiri zaidi.
“We have the deal on the table,” (Tuna dili mezani) alisema meneja wake.
“What deal?” (Dili gani?)
Meneja huyo akamwambia kwamba kulikuwa na kampuni ya simu za mkononi, Samsung walitaka kuweka naye mkataba wa kuvuna mamilioni ya fedha kwa kuitangaza kampuni hiyo.
Kiasi kilichotolewa kilikuwa ni dola bilioni moja, zilikuwa fedha nyingi mnoambazo zingemfanya kuogelea katika dimbwi la fedha. Pamoja na kupata kiasi kikubwa cha fedha lakini hakubweteka hali iliyomfanya kila siku kujikusanyia kiasi kikubwa cha fedha.
Baada ya kuingia dili hiyo, akaambiwa aelekee nchini China, huko na safari nyingine ilikuwa ni kuitangaza kampuni kubwa ya Samsung na vifaa vyake kitu kilichowafanya watu wengi kununua vitu kutoka katika kampuni hiyo kubwa duniani.
“Nina wasiwasi mpenzi...” alisikika msichana mmoja akizungumza kwenye simu.
“Wasiwasi wa nini?”
“Umekuwa na jina kubwa sana, unahisi nitastahili kuwa pamoja nawe?” aliuliza msichana huyo.
“Kwa nini usistahili?”
“Naona nitaibiwa, naona nitaumizwa hapo baadaye,” alisema msichana huyo.
“Wala usijali, hakuna atakayekuibia, najielewa sana...”
“Ila wanawake wengi wanakupenda.”
“Si tatizo Mariana, unatakiwa kuniamini tu.”
“Kweli?”
“Hakika!”
Japokuwa alikuwa akipendwa na wanawake wengi lakini Carter hakuwa akiwatamani kimapenzi wanawake hao, katika maisha yake, msichana ambaye alikuwa naye beneti alikuwa mmoja tu, huyu aliitwa Mariana.
Alikuwa msichana mzuri, mwenye macho madogo yenye ubluu, umbo zuri, nyonga zake zilijengeka vilivyo hali iliyofanya hipsi zake kuonekana sawasawa, alikuwa mrefu kidogo huku akiwa na nywele nyingi zilizomfanya kupendeza mno.
Lipsi za mdomo wake zilikuwa nene, alikuwa na pua ndefu kidogo, kwa jinsi alivyokuwa, kulikuwa na wanaume wengi waliomtaka lakini kwake, mtu pekee aliyempenda alikuwa mmoja tu, naye ni mwanamuziki chipukizi mwenye jina kubwa, Carter.
Uhusiano wao wa kimapenzi ulianza zamani, wakati walipokuwa wakisoma shule ya msingi. Walipendana mno, walikuwa pamoja na hata wazazi wao walilifahamu hilo.
Alijua kwamba katika kipindi alichopata jina, wasichana wengi wangempenda, wengi wangetamani kuwa naye lakini siku zote katika maisha yake, alimthamini msichana huyo tu, hakukuwa na mwingine katika maisha yake, kumpenda msichana huyo ilikuwa moja ya vitu vya thamani katika maisha yake, kwani hakumpenda kwa kuwa alikuwa na jina, alimpenda tangu kipindi cha nyuma.
“Nilipokuwa na jina, ulinipenda, sasa kuna haja gani ya kukuacha katika kipindi hiki, sidhani kama ni sahihi,” alisema Carter.
Maisha yalikuwa ya raha kila siku, aliendelea kupata mashabiki wengi duniani huku nyimbo zake zikiendelea kushika chati ya juu duniani kote. Vijana ambao walikuwa mitaani, nao wakaanza kujaribu kuimba, kutokana na Carter kuwa muimbaji, vijana wengi waliamini kwamba wangeweza kuwa kama yeye kitu kilichowafanya kila siku kukaa ndani na kujifunza kuimba.
“Kuna dili jingine,” alisema meneja wake mara baada ya kumaliza ziara ya Samsung huko Asia.
“Dili gani?”
“Kampuni ya Smadav Telecom inataka kufanya mazungumzo na wewe,” alisema meneja wake.
“Kuhusu nini?”
“Bila shaka mkataba utakaotufanya tuchume fedha nyingi zaidi,” alijibu meneja wake.
“Hakuna tatizo!”
Kampuni ya Smadav Telecom ilikuwa miongoni mwa kampuni kubwa nchini Marekani ambayo ilijihusisha na mitandao ya simu za mikononi. Ilikuwa miongoni mwa kampuni zilizokuwa na wateja wengi.
Mbali na Nike, Apple ambazo zilikuwa zikiingiza mamilioni ya fedha, nayo Smadav ilikuwa juu kabisa huku ikimilikiwa na mtu aliyekuwa akishika nafasi ya ishirini kwa utajiri duniani, Bwana David Seppy.
Utajiri wa mzee huyo mwenye miaka hamsini ulitisha, kila siku alikuwa akiingiza kiasi kikubwa cha fedha hali iliyomuongezea utajiri mkubwa kila siku. Alifahamu kwamba wasanii ndiyo watu waliokuwa na ushawishi mkubwa katika dunia ya sasa na hivyo kuwatumia katika kuzitangaza kampuni zake.
Masupastaa wakubwa duniani kama Kobe Bryant, James LeBron, Tiger Woods na wengine wengi walikuwa miongoni mwa masupastaa ambao walitumika katika kumuingizia kiasi kikubwa cha fedha.
Mbali na Smadav, mzee huyo alikuwa akimiliki kampuni nyingine nyingi, majengo makubwa ya kupanga, migodi, vituo vya mafuta na miradi mingine mingi. Jina lake lilikuwa kubwa kwa kuwa alikuwa miongoni mwa matajiri wakubwa ambao walijulikana kutoka na ukaribu wake na wasanii hao.
Baada ya kuingia mikataba na watu wengi, aliyekuwa mbele yake alikuwa ni Carter, aliamini kwamba kama angemtumia kijana huyo katika kampuni zake zingewafanya watu wengi kununua bidhaa zake kitu ambacho kingempa kiasi kikubwa cha wateja, hivyo akaanza kumtafuta kwa kuwatuma wafanyakazi wake.
“Amesemaje?” aliuliza.
“Nimezungumza na meneja wake kwamba tuonane, baada ya hapo tutazungumza naye,” alijibu mfanyakazi aliyetumwa.
“Sawa. Naomba ukakutane naye halafu utaniambia kipi kitakachojiri,” alisema Bwana Seppy huku akikenua kwa kuona kwamba mbele yake kulikuwa na mafanikio makubwa kwa kumtumia mwanamuziki huyo ambaye kadiri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo alivyozidi kujulikana duniani kote.
****
Watu wanne walikuwa mezani, walikuwa wakizungumzia mambo ya kibiashara, kiu kubwa iliyokuwa moyoni mwa Bwana Seppy ni kuona akifanikiwa kumsainisha mkataba kijana huyo kuitangaza kampuni yake ili kuwavuta wateja wengi zaidi.
Kiasi ambacho alikiweka mezani kilikuwa ni dola milioni tano. Kilikuwa kiasi kidogo mno hasa kwa mtu kama Carter ambaye siku kadhaa zilizopita alisaini mkataba wa dola bilioni moja.
Alipousoma mkataba huo, Carter akakenua, akamwangalia meneja wake kisha kumgawia mkataba huo na kuanza kuuangalia. Kiasi cha fedha ambacho kiliwekwa, kilikuwa kidogo mno kulinganisha na jina lake.
“Hii fedha ndiyo ya mkataba?” aliuliza meneja wake aliyejulikana kwa jina la Smith.
“Ndiyo!” alijibu Bwana Seppy kwa kujiamini.
“Huu ni upuuzi...”
“Upuuzi?”
“Ndiyo! Kiasi gani hiki? Unamchukuliaje Carter? Unadhani nyuma yake kuna watu wangapi? Ana mashabiki zaidi ya bilioni moja duniani kote, halafu leo umeweka kiasi cha dola milioni tano! Hebu kuweni siriazi kidogo,” alisema Smith huku akionekana kuchukizwa na mkataba huo.
“Ila yeye ni msanii mchanga!”
“Mchanga! Yaani mpaka leo unamuita Carter msanii mchanga! Acheni zenu.”
Hakukuwa na maelewano, kiasi cha malipo ya mkataba ambacho kiliwekwa kilikuwa kidogo mno kulinganishwa na jina lake. Bwana Seppy alionekana kukasirika, kwake, japokuwa Carter alikuwa na jina kubwa lakini bado alionekana kuwa msanii mchanga.
Alichokifanya ni kuongeza mpaka kufikia dola milioni ishirini, bado Carter alikataa, alichokiangalia yeye ni idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa nyuma yake, hakukubali kuona akinyonywa, hivyo aliwaambia wazi kwamba asingesaidi mkataba mpaka iwekwe dola milioni mia tano mezani.
“Unasemaje?”
“Ufanyieni marekebisho mkataba wenu, milioni mia tano mezani, nitasaini, chini ya hapo, mtanisamehe,” alisema Carter kwa kujiamini kabisa.
Kutoka dola milioni ishirini mpaka mia tano ilionekana kuwa kiasi kikubwa mno, ni kweli alikuwa na fedha nyingi lakini Bwana Seppy hakutaka kutoa kiasi hicho cha fedha.
Walibaki wakibishana na mwisho wa siku, msimamo wa Carter ukabaki palepale kwamba mkataba hausainiwi na hivyo kuondoa zake bila kugeuka nyuma.
Bwana Seppy akakasirika mno, hakuamini kama kweli msanii huyo, tena mdogo kiumri alikataa kusaini mkataba huo uliokuwa na fedha alizoziona kuwa nyingi.
Akaondoka huku akiwa na hasira tele, nyumbani kwake hakukukarika, alipokuwa akimuona Carter katika magazeti na televisheni, alishikwa na hasira mno, hakumpenda hata kidogo. Aliamini kwamba kupitia msanii huyo angeweza kujikuanyia wateja wengi lakini mwisho wa siku mtu huyo alikataa.
Kipindi hicho ndipo akagundua kwamba pombe hazikuwa tamu, zilikuwa chungu, mawazo yalimjaa na kila alipokaa, alikuwa akipiga mikono yake kwa hasira hasira.
Roho mbaya ikaanza kumuingia na kuona kwamba mtu huyo alitakiwa kuuawa, kama yeye alikuwa kiburi, sasa yeye alikuwa jeuri na alitaka kumuonyeshea kwamba alikuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao, hapo ndipo alipoanza kusuka mipango.
“Kwa hiyo unataka afe?” aliuliza kijana wake mwenye sura mbaya, huyu aliitwa Dragon na ndiye aliyekuwa akihusika kwa matukio mengi ya mzee huyo, hasa kwenye kuwaua maadui wa mzee huyo.
“Ndiyo! Tena haraka iwezekanavyo.”
“Sawa! Nitafanya kazi hiyo!”
“Hapana! Hautakiwi kuifanya wewe...”
“Sasa aifanye nani?”
“Hii ni kazi inayotakiwa kufanywa na watu wenye akili nyingi sana, kama ukifanya wewe, niamini kwamba utakamatwa tu kwani huyu si mtu mdogo, ni mtu mwenye mamilioni ya watu nyuma yake, hivyo ni lazima tumtume mtu mwenye akili nyingi,” alisema mzee huyo huku akimwangalia Dragon.
“Ni nani sasa?”
“Subiri, nitakupa jibu!”
Hiyo ilikuwa kazi kubwa, alichokiangalia ni wingi wa watu waliokuwa nyuma ya Carter, kulikuwa na watu wengi, kila alipokwenda kulikuwa na watu wengi hivyo kumuua kwake ilitakiwa kuwa kwa ufundi sana, yaani hata watu watakapojua kwamba amekufa, wasihisi kama aliuawa.
Alichokifanya ni kuingia katika mitandao na kuanza kumtafuta mtu mwenye akili nyingi. Alihangaika sana, alikiamini Chuo Kikuu cha Harvard kwamba kulikuwa na wanafunzi wengi wenye akili, sasa alitaka kuona ni nani aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi hao wenye akili, chaguo lake likatua kwa Benjamin, mwanaume aliyeaminika kuwa na uwezo mkubwa mno kipindi hicho.
“Huyuhuyu! Ni lazima apatikane,” alisema Bwana Seppy huku akikenua, alimhitaji mtu huyo kwa gharama zozote zile. Hivyo wakaanza kumtafuta kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Jumatano.
 
Back
Top Bottom