Mauaji yaliyofanywa na CCM na Kikwete Arusha, wamepata nini cha kujivunia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji yaliyofanywa na CCM na Kikwete Arusha, wamepata nini cha kujivunia?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyota Njema, Jan 13, 2011.

 1. N

  Nyota Njema Senior Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Toka kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010 zilipoanza, CCM wamekuwa na wakati mgumu wa kuwaaminisha watanzania kuwa bado wana uwezo wa kuendelea kuliongoza Taifa hili kutoka kwenye lindi la umaskini ambao sehemu kubwa ya umaskini huo umesababishwa na sera na uongozi wao mbovu ulioandamana na rushwa, uwezo mdogo wa kiuongozi, wizi, tamaa pamoja na ajira za kufahamiana na kulindana.

  Pamoja na udanganyifu mkubwa kwenye uchaguzi huo, CCM imejikuta ikipoteza maeneo mengi muhimu katika nchi kama majiji makubwa na hata baadhi ya sehemu za vijijini. Inafahamika kuwa watu wengi wenye upeo na uelewa mkubwa wa mambo ya kisiasa wanaishi sasa sehemu za mijini, hivyo jambo hili linawasumbua sana viongozi wa chama hiki kinachopoteza mwelekeo na mvuto kwa watanzania.

  Katika kujaribu kunusuru kupoteza ushawishi kwenye miji mikubwa, wamejaribu kwa kila njia kuhakikisha wanapata uongozi sehemu hizo ikiwa ni kwa kutumia rushwa kama ilivyo kawaida yao, na pia matumizi ya nguvu kama ilivyotokea Arusha. Lawama za mauaji ya Arusha kwanza zilianza kutupiwa kwa CHADEMA, walipoona jambo hilo halina mshiko kwa watanzania, sasa hivi kosa limerudishwa kwa polisi waliohusika kama alivyonukuliwa Membe. Ukweli bado unafichwa kuhusiana na nani hasa ni kiini cha uhalifu huu mkubwa kwa Taifa.

  Ninajojiuliza mara kwa mara kuhusiana na chanzo cha uhalifu huu ni kuwa, kama kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha aliyaruhusu maandamano hayo, na huku akijua kuwa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA watayaongoza, je hakumshirikisha IGP na kupata baraka zake kweli? Na kama ni hivyo, ni nini kichosababisha IGP abadili mawazo katika hatua za mwisho kabla ya kuanza maandamano hayo?

  Jibu ninalolipata ni kuwa, kwa upande wa polisi makao makuu, jambo hili halikuwa na tatizo lolote, na maandamano waliamini (na ndivyo ingekuwa kama ilivyo tokea wakati wa mazishi jana) yatakuwa ya amani bila uhalifu wowote kutokea, lakini amri ya mwisho ya kuyazuia ilikuwa ya kisiasa na ilitolewa na mwanasiasa mwenye nafasi kubwa serikalini. Mwanasiasa pekee mwenye nguvu hiyo kisheria ni rais wa jamhuri ya muungano ambaye ndiye amri jeshi mkuu wa majeshi yote ya Tanzania. IGP hawezi kupewa amri na Makamba, bali Kikwete mwenyewe hata kama alishauriwa na Makamba!

  Wana JF, kinachonishangaza ni kuwa, sisikii mtu yeyote akimzungumzia Kikwete kuhusika na hili, na hii ni hatari sana katika kutafuta chanzo cha suala hili ambalo limeleta kilio kisicho na sababu kwa watanzania wapenda haki, pamoja na wapenda haki wote duniani. Rai yangu ni kuwa Kikwete awajibike kwa tukio hili maana ndiye mhusika wa jambo hili kimantiki, na kama IGP ndiye aliyehusika, basi amwajibishe haraka iwezekanavyo, vinginevyo awajibike mwenyewe! Asipofanya hivyo, umma utawawajibisha wote.

  Naomba kuwakilisha.


   
 2. M

  Meshacky Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walichopata cha kujivunia ni UGAIDI WA KIMATAIFA maana sasa dunia nzima inajua Tanzania kuna ugaidi wa Kipolisi!
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kwa hapa nadhani cdm ndio wamenufaika zaidi kwa damu ya hao marehemu, maana wameongeza umaarufu kwa kukataa kutii amri halali ya polisi na kutaka kwenda kuvamia kituo kulikopelekea mauaji ya wapendwa wawili.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  People's souls!
   
 5. N

  Nyota Njema Senior Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walivamia kituo? Walikuwa na silaha gani wakati wanavamia hicho kituo? "Wapendwa" huwa wanavamia vituo? Pole sana ndugu yangu!

  Siku mtakapokosa madaraka mtatumia nini kuwalazimasha wananchi kutii ujinga wenu? green guard? sungusungu?
   
 6. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Kwenye red, ni amri haramu, siyo halali.
   
 7. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Wamepata aibu na huo ndo mwanzo wao wa kushindwa Arusha na sehemu nyinginezo nchini
   
 8. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Miji mikubwa tanzania ni mali ya upinzani, hili linawauma sana, ukimwona makamba nundu la usoni karibia linashuka chini kwa woga wa chadema.
   
 9. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,568
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  hivi ni kweli kwamba hata wale vijana wa makumbusho kwenye mlima walikuwepo kama Ma FFU ?
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  walifanya haya haya Pemba, and Pemba is no more ccm, japo wamemweka rais was SMZ mpemba, bado wameshindwa kuirudisha pemba.
   
 11. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  ccm inazidi kujichimbia kaburi lake. Kama lilikuwa tayari foot 6, sasa limeshakwenda 9.
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwa hili la Arusha wakalaumiwa ni wale walioamrisha maandamano yafanyike. Haiwezekani kikundi cha watu au hata chama cha siasa kizuwiew na serikali halafu chenyewe kijifanye kipo juu ya sheria na hakijali serikali. Mkong'oto tu, haya kafanyeni mengine sasa.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kaburi hilo ni la Chadema wala usijidanganye kuwa ni la Chama Cha Mapinduzi.
   
 14. L

  Leornado JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Maneo ya Baba mkubwa wa marehemu Denis wakati wa mazishi ya mwanaye:
  Alisema damu ya Denis itaendelea kudai 'ukweli, haki na amani'. Alisema damu ya Denis ikiachwa kupotea bure kesho itakuwa damu yako au yangu. Alisema atamwandikia barua Rais Kikwete ameueze Denis alifanya kosa gani na alihukumiwa na mahakama gani hukumu ya ya kupigwa risasi? Alisema kifo cha Denis kisifanye turudi nyuma katika kupigania 'ukweli, haki na amani'. source John Mnyika.

  Inauma sana tusiache damu hii ipotee bure.
   
 15. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  ccm chamacha upinzani,arusha ,mwanza,natanzania kwa ujumla,jk na gagbo wa magharibi hawana tofauti,tofauti nitume huru kule na hapa tume ya ccm
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nasema ni la ccm wala usitie shaka RIP ccm na zomba
   
 17. N

  Nyota Njema Senior Member

  #17
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sishangai sana kwa comment yako, maana naona picha yako na rafiki yako mpendwa! Tunajua mpo wenye mawazo hasi na maslahi ya nchi kwa sababu ya njaa na kujipendekeza kwa wakoloni wa kiafrika. Siku inakuja, na tena imefika, unafiki wenu utakapofikia ukomo! :A S 39:
   
 18. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Walikuwa mamevalia kombati za kijeshi huku wakikimbia mchaka-mchaka na kuimba nyimbo za kivita, baadhi mikononi walishikilia mawe na virungu!

  Inawezekana kabisa POLISI WALIPOONA KOMBATI NYINGI ZINAELEKEA KITUO CHA POLISI BAADA YA LILE TANGAZO LA MKUTANONI WAKAJUA VITA IMEKAMILIKA.

  Inabidi kujiuliza je baada ya mtu kuvaa nguo za kijeshi nini kinafuata? (maana sare za kijeshi hazikamiliki mpaka na silaha ziwemo ndipo zinapendeza!) Je haiwezekani ule kuwa mpango wa kwanza kuteka kituo na kupata baadhi ya silaha na kuonesha kwamba nchi haitawaliki? (kuna mambo mengi yanahitaji majibu... hivi hakuna sare zingine kwa vyama ila hizo za kijeshi-jeshi? Mbona ni CCM, CDM na kile chama cha yule kamarade Dovutwa pekee ambavyo viongozi na wanachama wake wana sare za kijeshi? Hivi MNA AJENDA GANI NA WATANZANIA?
   
 19. m

  mamtaresi Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwaujumbe huu mzuri na shida iko hapo hawamhusishi kikwete katika uhalifu huo wa arusha wakati inaonekana wazi source ni kikwete ambaye ndo mwenye kauli ya mwisho ya kuamrisha uhalifu ufanyike . ameona haitoshi ameamua kurusha matukio hao kwenye televisheni ya taifa kuwafanya wananchi waone kuwa cdm ndo walikuwa na shida sisi hatudanganyiki tena kwa kuonyeshwa picha ambazo tunaweza kuzitengeneza kwenye computer.ccm ndo wanaotaka vita na wameshaianza arusha bado mwanza hakuna amani ya maneno ni lazima watu wafe na damu zimwagike ndo amani ikae sawa keep it up chadema poples power aluta continue mapambano bado yanaendelea arusha hadi kieleweke.raia watakufaa na polisi kama ilivyokuwa japo hamkutoa idadi ya kweli ya walokufa arusha.
   
 20. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  na kwa waliobahatika kumuona raisi siku akiwa na mabalozi ikulu hata kama hujui kusoma sura za watu ilionekana dhahiri kuwa ni hadaa. Nchi imefika pabaya na bora haya yangetokea wakati elimu, matibabu na huduma nyingine za jamii zikiwa katika kiwango cha kuridhisha. Hivi mzee Mwinyi alivyojiuzulu wakati akiwa waziri hakuacha hata funzo!!!!!???? maana tumeona kijana wake (aliye kwenye mbeleko) pale mbagala aliendeleza madharau yake badala ya kuwajibika! NA IWEJE KWELI KATIKA MAUAJI HAYA YA ARUSHA ASIWAJIBIKE HATA MTU MMOJA???, KUSIWE HATA NA TAMKO OFFICIAL LA SERIKALI???? NA MEYA WAO (AKIANA MAKAMBA) AENDELEE KUWEPO OFISINI???? ...itabidi kubadili jina la nchi basi ndipo watu wake waweze kubadilika pia!
   
Loading...