Mauaji ya watu 17 Musoma: Watanzania Tunajifunza nini?

kalikenye

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
1,649
372
Tangu nilipopata taarifa za mauaji ya watu 17 wa Ukoo mmoja yaliyotokea huko Musoma, nimekuwa nikiangalia hatari iliyopo mbele ya watanzania. Nasema hatari kwa sababu kitendo hicho licha ya kuwa ni cha ajabu na kisichoweza kutegemewa kutokea katika jamii ya leo lakini ukweli ni kwamba kimetokea na hatuwezi kugeuza matokeo yakawa vinginevyo.

Lakini kwa maoni yangu, tukio hilo ni changamoto kwetu kama Taifa na tuna sababu zote za kulifanyia kazi kwa lengo la kubaini chanzo na kiini chake ili tukiondoe na kuhakikisha kuwa tukio kama hilo halitokei katika jamii ya watanzania wa leo na hata kesho.

Wakati nasoma maoni ya Jaydee, nilikumbuka mjadala mmoja uliyojitokeza huko Mbeya ambapo watu waliokuwa kwenye kilaji katika Baa moja iliyopo Soweto, walikuwa wakitoa maoni yao juu ya tukio hilo la Musoma ambapo wengi wao walikuwa wakiwatuhumu watu wa Mkoa wa Mara kuwa ni WAKATILI waliopindukia.

Katika kundi lile wengi walikuwa ni makabila mchanganyiko ya Mkoa wa Mbeya na jamaa mmoja ambaye nilikuja kumfahamu kuwa kati ya wazazi wake, mmoja ana asili ya Mkoa wa Mara.

Licha ya ukweli kwamba makombora yaliyokuwa yakirushwa yalikuwa yakielekezwa kwa yule jamaa mwenye asili ya Mara, lakini cha kushangaza ni kwamba Mtetezi wake alikuwa ni jamaa kutoka kabila la Kinyiha lililoko Mbeya na ambaye alishawahi kufika Musoma.

Katika maelezo yake, alidai tusiwanyoshee vidole watu wa Mara kama watu pekee wakatili, bali tujiangalie katika jamii zetu. Je tuna amani kama tunavyofikiria? Je hakuna mauaji yanayotokea katika jamii zetu bila kujali mauaji hayo yanatokea kwa namna gani. Akatolea mifano ya namna wanavyoogopa kwenda kwao Mbozi kwa sababu za ushirikina.

Lakini si hivyo tu, hebu tujiulize: Ni mauaji mangapi yanayofanyika kwa kisingizo cha wananchi wenye hasira kali? Huo ujasili wanautoa wapi

Je ni mauaji mangapi yanayofanywa kwa njia za kishirikina? Je hawa nao sio tatizo?

Ni mara ngapi tumesikia katika jamii zetu familia zikiteketezana au kuharibiana mali kwa njia za kishirikina. Je huo pia sio ukatili?

Tuna mifano mingi ambayo kama tukianza kuitaja hatutaimaliza kwani naamini hata humu JF kuna watu hawakanyagi vijijini kwao kwa hofu ya kutekezwa kwa njia za kishirikina.

SOMO LA KUJIFUNZA.

Baada ya mifano niliyoitaja hapo juu, ni wazi kuwa waliofanya mauaji yale ya Musoma walikosa njia mbadala ya kulipiza kisasi kwani naamini kabisa kuwa wangekuwa wanaujuzi wa kutumia njia za kishirikina wangezitumia na wala leo hii tusingekuwa tunajadili hapa.

Lakini huenda walishajaribu wakashindwa ndio maana wakatumia njia ile. Usukumani baada ya kuwashindwa watu waliokuwa wakituhumiwa kuwa wachawi walitumia njia ya Mapanga kama njia mojawapo ya kulipiza kisasi au kuwatekeza watu hao na naamini kabisa kila mtu hapa JF alishasikia habari za mauaji ya Vikongwe katika Mikoa ya Mwanza na Shinyanga.

Yote haya ni mauaji aidha mbele ya Sheria za Binadamu au za Mungu.

Naamini ni wakati muafaka sasa kwa sisi watanzania kujiangalia na kujiuliza maswali. JE TUKO SALAMA KIASI GANI KATIKA NCHI YA AMANI NA UTULIVU katikati ya mauaji yanayofanyika bila kujali yanafanyika kwa kutumika kwa njia gani.

Nawasilisha.
 
Na hata wanasiasa ambao huaminika ndio Cream ya Jamii wamakuwa wakitekezana kwa njia za kishirikina. Je nao sio wakatili?
 
WanaJF naombeni maoni yenu hasa ikizingatiwa kuwa suala hili ni nyeti.
 
Back
Top Bottom