Mauaji ya watanzania wenzetu yanafanywa na nani?

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
Gazeti na Tanzania Daima la Tarehe 30 Aprili, 2012 liliandika kwamba wafuasi wa CHADEMA 15 wameuawa . Habari hii inaungana na kauli ya JOHN Mnyika kwamba wafuasi 15 wa Chadema wameuawa.

Madai haya yanatisha kwa sababu CCM imetawala muda wote tangu uhuru hatujasikia kuwa ni chama cha wauaji, lakini inatisha zaidi kupata majibu kutoka CCM kwamba mauaji hayo yanafanywa na CHADEMA na kusingizia CCM kwa lengo la kujiimarisha kisiasa na kujenga chuki ya wananchi dhidi ya CCM.

Hizi tuhuma ni nzito si vema kuzisambaza bila kuchukua tahadhari ya kutosha. Kutupiana Tuhuma za mauaji au kuua si nyepesi na haziwezi kutangazwa bila ushahidi wa kutosha. Hadi sasa tuhuma hizi zimetugawanya hapa JF wako wanaoona kuwa hii ni mbinu ya CHADEMA kuongeza umaarufu na wapo wanaosema ni mbinu ya CCM kuwatisha wafuasi wa CHADEMA. Hakuna aliyejaribu japo kwa dots mbili tatu kuthibitisha kauli zake.

My take: Ni wapi tunakoelekea?
 
ccm ndo wauwaji, wanatumia jeshi la polisi kuficha uovu wao, kumbuka kijana wa Igunga waliyemmwagia Tindikali halafu wakasema ni Chadema.
 
CCM juzi tu walimwua Mwenyekiti wetu wa USA RIVER.
Tena baada ya hapo wakatuma sms kwa Nassari kuwa sasa itakuwa zamu ya Mwenyekiti wa Sing'isi.

Ni mambo ya Intelijensia MAMA POROJO lakini ukifukua fukua kiundani unakuja kupata ukweli kuwa magamba wanawatuma green guard kuwaua watu wetu (Watanzania Wenzetu).
 
siasa ina mbinu nyingi kutangulia kutangaza kwamba CCM ndio wauaji hakuondoi ukweli kwamba hata Chadema wanaweza kuua ili kupata umaarufu
 
CCM juzi tu walimwua Mwenyekiti wetu wa USA RIVER.
Tena baada ya hapo wakatuma sms kwa Nassari kuwa sasa itakuwa zamu ya Mwenyekiti wa Sing'isi.

Ni mambo ya Intelijensia MAMA POROJO lakini ukifukua fukua kiundani unakuja kupata ukweli kuwa magamba wanawatuma green guard kuwaua watu wetu (Watanzania Wenzetu).

Kama hivyo ndivyo tuwataje wauaji kwa majina
 
Mara zote mchawi ndiye analia sana msibani,

Chadema wanalia mno kulikoni? Machozi mengi kuna namna.
 
Gazeti na Tanzania Daima la Tarehe 30 Mei, 2012 liliandika kwamba wafuasi wa CHADEMA 15 wameuawa . Habari hii inaungana na kauli ya JOHN Mnyika kwamba wafuasi 15 wa Chadema wameuawa.

Madai haya yanatisha kwa sababu CCM imetawala muda wote tangu uhuru hatujasikia kuwa ni chama cha wauaji, lakini inatisha zaidi kupata majibu kutoka CCM kwamba mauaji hayo yanafanywa na CHADEMA na kusingizia CCM kwa lengo la kujiimarisha kisiasa na kujenga chuki ya wananchi dhidi ya CCM.

Hizi tuhuma ni nzito si vema kuzisambaza bila kuchukua tahadhari ya kutosha. Kutupiana Tuhuma za mauaji au kuua si nyepesi na haziwezi kutangazwa bila ushahidi wa kutosha. Hadi sasa tuhuma hizi zimetugawanya hapa JF wako wanaoona kuwa hii ni mbinu ya CHADEMA kuongeza umaarufu na wapo wanaosema ni mbinu ya CCM kuwatisha wafuasi wa CHADEMA. Hakuna aliyejaribu japo kwa dots mbili tatu kuthibitisha kauli zake.

My take: Ni wapi tunakoelekea?

Tarehe 30 Mei 2012? We bimkubwa nadhani bado uko njozini. Hebu amka asbhí ishapita. Hiyo tarehe haijafika bado. Acha kutizungua
 
Tanzania Daima linamilikiwa na Mbowe wapi ajabu ya kutangaza kwa kuinyooshea kidole CCM?
 
thibitisha kila mtu anasema lake
kada aliyemwagiwa tindikali ni wa ccm, hao hao ccm wenye dola na polisi wakasema wahusika ni chadema halafu mpaka leo hawajaweza kuthibitisha si kwa kufungua kesi wala kuwataja kwa majina watuhumiwa, wameishia kumpeleka kijana India, kwanini hawakuwashtaki hao watuhumiwa?
 
Back
Top Bottom