Mauaji ya Watanzania Afrika Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya Watanzania Afrika Kusini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by waukae, Jun 18, 2008.

 1. waukae

  waukae Member

  #1
  Jun 18, 2008
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  vijana wa kitanzania waliopo south afrika hali zao zinasikitisha sana wana jf juzi nilipigiwa simu na mmoja wao akiwakilisha wenzie 51 alinambia kwamba maisha ya kule yamewashinda na walikuwa wako uwanja wa ndege wa johernesberg walipopelekwa na maofisa wa ubalozi wa tanzania ili kurudishwa makwao na wengine kwa maelezo yao kwamba walishachanga baadhi ya fedha zao lakini cha kushangaza baada ya kufika uwanja wa ndege wakatelekezwa na hao waliojiita mafisa wa ubalozi wa tanzania, na hivi ninavyoandika wanasema wamerudi tena mitaani kwenda kujisalimisha polisi lakini polisi nao wamewakataa sasa wana jf hebu tutafakari tuwasaidie vipi hawa watanzania wenzetu ambao wanakimbia machafuko huko south afrika? je serikali ya tanzania inashindwa nini kuwasaidia kurudi hawa watanzania mbona kenya wameweza?
   
 2. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Bwana Waukae Kwanza karibu JF

  Huyo aliyekupigia simu kwa nini asikupe list ya majina ya watanzania waliokwama airport kama kweli wanataka kurudi nyumbani ili wenye ndugu zao watapata taarifa na watatafuta njia za kuwasaidia warudi.

  Pili hao maofisa wa ubalozi hawana majina?? Majina yao yawekwe hapa tutauliza ubalozi wetu wa SA kwa nini wamefanya huo utapeli kama ni kweli unayoyasema.

  Cha muhimu mwambie mtoa habari akupe list ya watu wote 50 wanaotaka kurudi iweke hapa naamini wenye ndugu watayaona na kuwasaidia.
   
 3. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimepokea kwa majinzi makubwa mauaji ya ndugu zetu wa Zanzibar waliokuwa wanajitafutia maisha Afrika Kusini kupigwa risasi kama kitoweo. Ninaishauri serikali kwa kushirikiana na ubalozi wetu ufanye uchunguzi wa kina.

  Pili ninaulaumu ubalozi wa Tanzania nchini AfriKa Kusini kushindwa kuwa-mobilize watu na yenyewe kutoa support ya kuleta miili ya marehemu hao nchini. Je wajibu wa balozi zetu ni upi?
   
 4. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #4
  Sep 19, 2008
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Wanandugu,

  NIna hakika kwamba nyote mmesikia na kusoma taarifa mbali mbali kwenye vyombo vya habari, zinazohusiana na kampeni chafu ya uendeshaji wa chuki, ubaguzi na mauaji, ya raia wa nchi za kigeni nchini Afrika Kusini.

  Mpaka sasa, taarifa rasmi zinasema ni takriban Watanzania 36 ambao wamepoteza maisha yao nchini humo, lakini hao ni wale tu ambao wanajulikana, yaani, wamesajiliwa kwenye ubalozi wetu nchini humo. Kuna wengi zaidi, kwa kuhofia kugundulika kuwa wao si raia, wamekataa kujisajili na wengi wanaishi nchini humo kama wazawa, yaani, wenye uraia wa Afrika Kusini.

  Sina mengi zaidi ya taarifa rasmi ambayo ninaiambatanisha hapa, ikiwa ndiyo Tamko la Dar es Salaam, kuhusu udhalimu huo ambao wenzetu - ambao tuliwapigania kwa hali, mali na maisha - wameamua kutugeuka na kutugeuza asusa.

  Nawaombeni, kila mmoja, mlisome Tamko la Dar es Salaam (the Dar es Salaam Declaration), kisha mtoe mchango wenu nini kifanyike kuhamasisha hii Kampeni, ili tuweze kufanikiwa kupata na kufikia malengo yetu.

  Asanteni,

  ./Mwana wa Haki
   
 5. D

  Darwin JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kama hawataki na nchi yao kwanini mnaenda huko?

  Watanzania baada ya kwenda kuiga wenzetu wamefanya nini mpaka wameendelea mkifika huko wengine mwajihusisha na wizi au kufungua mashina ya CCM.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  jamani wa south wamechoka na kuvamiwa na kuchukuliwa kazi zao zoooote....zooote kabisa na wageni...duuu ukienda jo burg.....utashanga a wa TZ hadi wanauza charge za simu jamani..kweli???wamachinga wa bongo kibaoo SA...hadi huelewi wamefuata umachinga au wanafanya uhalifu?...kwa kweli hizo kazi labda ilikuwa zamani...maana siku hizi hata hao wazawa wenyewe hawana kazi....wamebakia kuwa walinzii tuu..kama huna shule /huna mtaji wala hakulipi kabisa....sasa masela wa tandika,migomigo,manzese wanaenda tafuta connection z a meli....muda kusubiriaa "zali"ndio wanakaba na kuiba...kwenda mbele.....
   
 7. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Eboo, sawa tuone yatakapoishia haya!!

  Na hawa waMalawi wetu, waChina nk tunaogombea watimuliwe itakuwaje??
   
 8. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,600
  Likes Received: 6,767
  Trophy Points: 280
  ondoa hilo jina kwanza kwa sababu unataka hii iwe ni movement ya watu na si movement yako

  kisha vipengele vinavyofuata ondoa pronoun "I" weka pronoun "We", kwa sababu ya sababu nilizoziweka hapo juu. then baada ya hapo ninakuunga mkono kwa movement hii. maana hatuwezi kuendelea kukaa kimya kwa huu unyama unaofanywa na binadamu kwa binadamu wenzao!
   
 9. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #9
  Sep 19, 2008
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Jambo mnalosahau ni kwamba, Wazawa, Waafrika Kusini, WALIPEWA nafasi za kusoma BURE, elimu madaraja yote, kuanzia chekechea hadi chuo kikuu! Walikataa! Wakaona bora waendelee kupeta, kufurahia UHURU wao! Nafasi pia za ajira ya upendeleo kwa Wazawa, zilitolewa. This is documented, Google it and you will find... Start with South African Affirmative Action Programmes.

  Sasa, nafasi hizo ziliishia kati kati ya muda wa utawala wa Mbeki. Serikali yake iliona, kama watu wanapewa nafasi na wanazikataa, sasa waendelee kutumia pesa za walipa kodi kuendelea kutoa matangazo ya kuhamasisha bila response ni waste of time and much needed financial resources. Ni mfano wa utawala mbaya, kutumia fedha ambazo huoni matokeo yake. Wakaacha kutangaza, wakasitisha mipango hiyo miwili.

  Sasa Wazawa wamejikuta, (i) hawana elimu na (ii) nafasi za kazi za upendeleo zimesitishwa. Walie na nani? Wageni!

  Wameamua kuhamisha lawama za uzembe wao, kwa wageni, na kudai kwamba wageni ndio wamevamia ajira zao. Huo si ukweli hata kidogo!

  Kumbukeni, hizi chuki dhidi ya wageni hazikuanza jana wala juzi. Zimeanza tangu miaka ya 90. Mimi nina kesi ambayo rafiki yangu mpendwa alipatwa na msiba, baada ya kaka yake (ambaye alikuwa ameishi RSA kwa takriban miaka 7) kuuwawa, baada ya kugundulika kuwa ni Mtanzania. Kaka yake huyo, kwa kuhofia kwamba angekuja kuuwawa kwa kujulikana kuwa si raia wa kule, aliamua kubadili jina, na kwa kuwa Wangoni ni kabila moja sawa na Wazulu, hakutofautiana kilugha na kwa matamshi, akawa anakubalika kama Mzulu.

  Vijana fulani kule Capetown walimwonea wivu yeye na mchumba wake, ambaye alikuwa Mzulu Mzawa. Wakaanza kumpeleleza, wakagundua kwamba ni Mtanzania. Walimvamia usiku, wakamteka nyara, wakamsiliba kwa kumchoma visu na kumpiga, kisha wakamwashia risasi saba (risasi moja kwa kila mwaka alioishi RSA), na kuutupa mwili wake kwenye mojawapo ya fukwe za Capetown!

  Baada ya siku tatu toka kupotea kwake, mwili wake ulionekana, na hatimaye maiti ikasafirishwa hadi nyumbani, akazikwa hapa Dar.

  Sasa mnadhani kwamba sisi hatuna haki ya kuishi kule kwao? Mbona wao wako hapa, tena wengi, kila mkoa, na sisi hatuwafukuzi wala kuwafanyia fujo? Au na sisi tufanye kama wao wanavyofanya?

  Mimi nimesema, TUWASUSIE! Vodacom, Shoprite, Game, Truworths, W Store, 4u2, Stanbic Bank, Tanzania Breweries, na kila kampuni inayojulikana ni ya Afrika Kusini, tusinunue bidhaa zao na tusitumie huduma zao. Nimesahau, kuna Blue Finance na Bayport Finance, labda Platinum Credit, lakini wamekuja pia hawa Instant Credit (www.instantcredit.co.za), ambao nao wanastahili KUSUSIWA!

  Hakuna jambo linaloweza kubadilisha fikra na maoni ya watu, kama kuwanyima mapato yao halali. Tukianza sisi, wapo wengine watakaofuatisha mwenendo wetu, hatimaye inaweza kuwa a GLOBAL CAMPAIGN! Think locally, act globally, for maximum effect!

  Na ni TUSI kusema kwamba ndugu zetu waliopo RSA wanajihusisha na vitendo vya uhalifu. With WHAT FACTS? No research, no right to speak! Waje na concrete data, si uzushi!

  A luta continua!

  ./Mwana wa Haki
   
 10. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #10
  Sep 19, 2008
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Gamba la Nyoka,

  I concur with you. The Declaration has been revised!
   

  Attached Files:

  Last edited: Sep 19, 2008
 11. D

  Darwin JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mwanahaki jiulize hao watu walipata uhuru wa haki mwaka gani kutokana na data zako.

  Nimesema kama hawatutaki basi hatuna haja ya kwenda huko.

  Hayo makampuni uliyosema tuyasusie ndio yanawasaidia watangayika wengi kupata ajira ukilinganisha na kwamba sisi wenyewe hatuna uwezo wenyewe wakufanya vyetu imara.

  Unafikiri mimi sichukii kuona babu zetu kule Lushoto biashara zao za ma apple zimeshuka thamani kutokana na kuingizwa ma apple ya SA?
  Nachukia lakini sasa nitaamua lipi? wakati kule Lushoto wazalishaji wa matunda hawana mtetezi bungeni.
  Njia zakwenda kuyapata hayo matunda mvua ikinyesha tu basi ndio kila kitu kwisha hakuendeki tena.
  Viko viwanda vingapi kwa ajili ya mboga na matunda?
  Cha kulaumu ni serikali yetu, kwani najua kama tungekua na mwelekeo na hatuna ufisadi bali kuliendeleza taifa letu kwenda mbele ili iwe mfano kwa nchi nyingine sijui kama vijana wetu wangepita mapori na mapori hata wengine kuliwa na simba kwenda SA.

  SA ilichotuzidi ninini? kama ni ardhi tunayo, madini tunayo, bahari tunayo, kila kitu tunacho.

  Umasikini wetu umezidishwa na viongozi wetu wachache wanaojali maslahi yao kuliko maslahi ya watanzania.

  Ahadi za ajira kwa vijana ziko wapi?

  Nafikiri pia kwamba kama Tanzania ingekua imeendelea basi huko SA watu wangeenda tu kama watalii.
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,570
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Wape darasa mkuu...
   
 13. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tupo pamoja,sio kuchonga tu,sasa tunataka utendaji
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ina maana hii petition sisi naturalized citizens hatuna nafasi? Hata kama mmoja wa wazazi wangu ni raia mzaliwa?
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kukataa kunywa Safari kutamstua nini Mbeki? Au kufanya shopping Shoprite?
   
  Last edited: Sep 21, 2008
 16. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Just a little bit curious about this pettition.

  Je pettition hii ni kutokana na mauaji yanayofanyika huko SA?

  Au pettition hii ni kutokana na Watanzania kuchoka "kunyonywa" na SA kutokana na mfumo wa kiuchumi tulioukimbilia wa Soko Huria na Utandawazi?

  Kama unaunganisha yote mawili, utatoka kapa!

  Suala la uhai wa mtu, ni muhimu na Serikali yetu ni lazima iwajibishwe kulinda na kutetea uhai wa Mtanzania yeyote popote pale alipo.

  Hata ikiwa kana kuwa Mtanzania huyu kafanya uhalifu, ni wajibu wa Serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa Mtanzania huyu anapewa kinga na huduma zote kufuata mkondo wa haki na sheria katika kumuadhibu, hii ikiwa na kufikishwa mahakamani, kupewa uhuru wa kupewa dhamana kama ana uwezo, kupewa wakili wa Serikali ya nchi husika au wakili binafsi kama Mtanzania huyu ana uwezo na zaidi kuliko yote ni kwa Mtanzania huyu kuwekwa katika mazingira sawa na wazawa na wenyeji wa nchi husika ambao ni wahalifu.

  Ikiwa Mtanzania kaingia kwenye matatizo yoyote, ni wajibu wa Serikali kulishughulikia jambo hili na kutumia vyombo vya masuala ya haki za binadamu au mahusiano yetu na nchi mama aliko Mtanzania huyu. Kuna baadhi ya mambo tunajua Serikali haiwezi kufanya kwa kila kitu, mfano nikiugua nikakosa fedha za tiba, Serikali ya Tanzania inaweza nipa mkopo au kuiomba Serikali ya nchi niliko inipe msaada wa kiafya na si kuachwa nife.

  Mfano wa wanafunzi Ukraine, ni uzembe wa Serikali kusimama kidete kulinda uhai wa Raia wake.

  Mifano ya Watanzania walioko jela na kupewa mateso makali kutokana na Uraia wao juu ya uhalifu wao huko Pakistan, Afghanistan, Ugiriki, Uturuki hata Guantanamo Bay, ni dalili kuwa Serikali yetu imejitenga nasi.

  Tukirudi kwenye suala la kiuchumi, ni SISI Watanzania ambao tumeruhusu na kuwaachia SA wajitwalie na kumiliki Uchumi wetu. Ni SISI Watanzania wa kulaumiwa kwa kuona ni bora bidhaa za SA kuliko zetu. Ni SISI ambao tumekimbilia ajira katika mashirika yao kwa kuwa tutalipwa mishahara minono kuliko mashirika ya ndani. Ni SISI ambao tumeruhusu kuwa na Serikali ambayo imekimbilia Sera za Kuzalisha mali na Kiuchumi ambazo hazimsaidiii Mtanzania bali zinamnufaisha mgeni na mwekezaji.

  Badala ya SISI kusimama kidete na kudhamiria kuboresha ubora wa bidhaa zetu, kuongeza uzalishaji mali, kuwa na usimamizi mzuri na utendaji fanisi wa uzalishaji mali iwe ni kilimo, viwanda, biashara au huduma, kuimarisha pato la Mtanzania kwa kuongeza mishahara kukidhi makali ya Maisha, Watanzania tumekimbilia kutafuta Asprin kutoka kwa Wageni, wawe SA, China, India, UK, Canada, USA, Kenya au Lebanon!

  Tunachotakiwa kufanya si kususia hawa Wageni tuliowakaribisha kwa mikono miwili na kuwaundia kamati na tume za mapokezi na kuhakikisha wanafanikiwa katika kazi zao.

  Tunatakiwa na inatupasa kuisusia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

  Tunapaswa na ni haki yetu kuisusia Serikali ya Tanzania kwa kushindwa kuboresha maisha ya Mtanzania na kumfanya Mtanzania aendelee kutegemea misaada, aendelee kuwa mnyonge na mdhaifu wa kuzalisha mali, huku kipato chake kikichechemea na kukimbilia kumfanya Mtanzania huyu aikimbie nchi yake na kwenda nchi nyingine kufanya kazi japo apate kipato cha kumpa tumaini kuwa ataiona kesho!

  Nafasi ya kuisusia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakuja tena katika kipindi cha miezi takribani 24 kuanzia leo hii. Tujiandae kuisusia Serikali yetu na Chama kilichotupa Serikali mbovu, CCM!

  La mwisho, kuhusiana na SA, kama Serikali yetu ingekuwa inaheshimika jinsi ilivyokuwa miaka ya harakati za mapambano ya kung'oa ukoloni, haya yasingetokea ya Watanzania kuuwawa. Watu 36 ni wengi kuuawa kwa siku chache na Serikali yetu na ya SA kukaa kimya.

  Kama Serikali yetu ingekuwa inaheshimika kwa kuwa na uchumi huru na viongozi makini wenye kusimamia haki na utu, yaliyotokea SA majuzi hata wakati majambazi walipovamia nyumba ya Balozi wetu Emmanuel Mwambulukutu yasingetokea.

  Tatizo kwa upande wetu si SA bali ni Serikali yetu wenyewe!
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Naona Mbeki amesikia juu ya hii petition ndiyo maana ameamua kuachia ngazi. Go JF!!
   
 18. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Fundi, umeniacha mbavu zinavunjana zenyewe Mkuu..... That will be a clip for my weekend!!
   
 19. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #19
  Sep 27, 2008
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Na bado! Chupi zitabana tu! Uzi ule ule!

  Tusipokunywa Safari na kufanya shopping Shoprite tutawanyima KODI! Inyime Serikali kodi yake, halali, ndipo uone utamu wake. Wimbo mzuri wataimba!
   
 20. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Yeah naona declaration inabagua naturalized citizens, rekebisha.

  Tatizo kubwa ni ukosefu wa alternatives za hizo kampuni za south africa, ukiamua kuzitosa zote sijui utaishi vipi.
   
Loading...