Mauaji Ya Vita kati ya wakristo na waislam Nigeria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji Ya Vita kati ya wakristo na waislam Nigeria

Discussion in 'International Forum' started by ZionTZ, Jan 25, 2010.

 1. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Maiti 150 zimetolewa toka kwenye visima vya maji katika mji wa Jos uliopo ukanda wa kati wa Nigeria.

  Jumla ya watu 450 wanahofiwa kufariki kufuatia mashambulizi baina ya waislamu na wakristo katika mji huo.

  "Hadi sasa tumefanikiwa kuziopoa maiti 150 toka kwenye visima vya maji lakini watu wengine 60 hawajulikani walipo hadi sasa", alisema Umar Baza, mkuu wa kijiji cha Kuru Karama kilichopo karibu na mji wa Jos.

  "Hadi sasa tuna miili ya watu 150 waliopatikana toka kwenye visima kuanzia siku ya alhamisi. Tunaendelea kutafuta miili zaidi ya watu kwenye misitu inayotuzunguka".

  Umar alisema kuwa watatafuta miili ya watu kwenye misitu kwa kuwa watu wengi waliuliwa walipokimbilia misituni kukimbia mapambano kwenye kijiji cha Kuru Karama.

  "Tunaamini kuna maiti nyingi zaidi kwenye visima lakini kutokana na jinsi zilivyoharibika vibaya tumeamua kuvifukia visima vyote kwa michanga", aliongeza Umar.

  Serikali ya Nigeria haijatoa idadi kamili ya watu waliofariki kwenye vurugu hizo za kidini ambazo zilianzia kwenye mji wa Jos na kusambaa kwenye miji ya jirani.

  Viongozi wa dini na watoa huduma za afya walisema kwamba hadi kufikia jumatano walikuwa wameishahesabu jumla ya maiti 300.
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hivi ni dini ipi iliyo chokozi?
   
 3. bht

  bht JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hii habari niliisikia juu juu tu, ZionTZ unaweza kunihabarisha zaidi as nini kilikuwa chanzo cha mapigano hayo???
   
 4. B

  Bull JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  A US-based rights group has urged Nigeria's vice-president to order an immediate criminal investigation into "a massacre of at least 150 Muslim residents" of a town in central Nigeria.

  In a statement, Corinne Dufka, Human Rights Watch's (HRW) senior West Africa researcher, said the killings in Kuru Karama, 30km south of the city of Jos, required "the authorities to act now".

  Several villagers told our correspondent, Andrew Simmons, that they members of the armed groups to be Christians and showed him charred corpses, including those of young children and babies, in addition to dozens of bodies stuffed down wells.

  The three main mosques of the town were burned and destroyed as well, according to HRW


  http://english.aljazeera.net/news/africa/2010/01/201012434859704908.html
   
 5. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  It seems and looks that there is a serious religious issues down there. I don't know if it is another 21st century biafra civil war of the sixties which causes the self-proclaimed Republic of Biafra.
   
 6. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Nigeria ina historia ndefu ya mapigano ambayo ni ya kika bila na pia ya kidini maana pande zote mbili zinaingiliana huko.
  Siwezi kujua "nani alianza" au kama yuko aliyeanza kwa maana hiyo...

  Ila tu naona aibu kama mkristo nikisoma taarifa hizi za kuhuzunisha ya kwamba kijiji kile wauaji walijiita "wakristo". Bila shaka hawakuwa washambulizi wa kwanza waliona walipe kisasa lakini aibu kwangu ni kubwa.

  (tena nasoma mauaji yalitokea baada ya viongozi wa wakristo na waislamu wa kijiji kile kukutana na kupatana eti wajaribu kuachana fitina hii nje wajitete pamoja lakini hao vijana walifika mapema maandalizi hayakukamilika...)
   
 7. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  i got this from Nigerian buddy:

  IN NIGERIA CHRISTIANS ARE THE ONES WHO SUFFER GENOCIDES IN THE HANDS OF MOSLEMS. I THINK THE CHRISTIANS ARE NOW WAKING UP, NOT LETING THIER LIVES ERADICATED WITHOUT SOME KIND OF DEFENCE THIE TIME. SINCE THEY ARE USED TO BEING ATTACKED BY THE ISLAMIST NORTH AT WILL, THEY´RE LEARNING TO FIGHT BACK WHEN ATTACKED UNLIKE IN THE PAST YEARS! NIGERIAN MOSLEMS HAVE BEEN FOR YEARS RADICALIZED BY AL-KAIDA AND TALIBAN. FOR CHRISTIANS FORCED INTO THE NORTHERN NIGERIA SHARIA LAWS LIFE HASN´T BEEN THE SAME! YET THE ISLAMIST WON´T LET THE CHRISTIANS WHO ARE DEFINITELY OF DIFFERENT CULTURE AND GEOGRAPHY HAVE THIER INDEPENDENCE!! THE FIRST CIVIL WAR IN NIGERIA STARTED BY THE SAME MOSLEMS KILLING CLOSE TO A MILLION CHRISTIANS OF SOUTHERN NIGERIA. AS THE SOUTHERNERS DECLEARED THEIR INDEPENDENCE, THE ISLAMIST SAID "NO". THE NEED "INFIDELS" TO DOMINATE! MAY BE IT´S TIME FOR EACH SIDE TO DEPART NOW FOR GOOD!!
   
 8. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145


  Kaka kwa nini unapeleka yale hapa?
  Nani alijitetea hapa katika mfano wa kijiji hiki??? Walishambuliwa hovyo na wakorofi waliojiita Wakristo. Aibu kubwa!

  Labda wale wakorofi awali hawakuwa wakorofi labda walikuwa vijana wa kawaida. Labda mioyo yao ilijazwa chuki, labda walibadilishwa baada ya kuona jinsi ndugu zao walichinjwa.
  Halafu?? Haki gani kupeleka ukorofi kwa watu wengine??
   
 9. Nostradamus

  Nostradamus JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dalili nyingine ya utumwa wa kifikra..MaxShimba, you dont belong here.Here is the home of great thinkers and you are not among us.
  Unataka kujua ni dini gani chokozi ili uchangie nini?? na kama dini unayoiamini wewe ndio itakuwa chokozi,mchango wako utakuwaje?
  No one deserve to die,thats what i beleave
   
 10. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  What a stupid reason to fight! Yaani mijitu inauana sababu ya hizi dini za wageni wakoloni wa kizungu na kiarabu? Mnapigania mungu? Stupid! Mungu anayetaka nimpiganie mimi simtaki kabisa, siyo mungu huyo. Mungu anapaswa atetee watu wake, sio wao wamtete yeye ilhali ndiye mwenye nguvu zote. Very illogical and nonsensical! Mungu asiyeweza kukutetea, anataka wewe ndio umtetee, siyo mungu huyo, hakufai, achana naye! Mtadanganywa sana, mtalipishwa mafungu mnadanganywa yanakwenda kwa mungu kumbe wanakula wajanja, mnadanganywa mnapigania mungu kumbe mnapigania wajanja wapate utawala! Hovyo sana!
   
 11. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Katika wale waliouana, kuna jamaa wawili mmoja muislam, mmoja mkristo walifika kwa Malaika aliyewapeleka mpaka mbele ya Mwenyezi Mungu kisha Mwenyezi Mungu akawaita kwa Majina yao Kama ifuatavyo:

  Mwenyezi: ''Juma Bin Ozechukwu Bin Rashid''

  Juma: ''Naam Mwenyezi Mungu Subhanahu wa-ta'ala"

  Mwenyezi: ''Joseph Obina Okerekwo ''

  Joseph: ''Naam Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu"

  Mwenyezi: ''Pamoja na tofauti hizi za kiimani mlizo nazo, sitawahukumu
  Kwa kuwa mmezaliwa mkazikuta na hamkuwahi kuniona na
  kuujua ukweli kwa macho yenu, hivyo mngestahili kuingia
  katika mema yangu. Lakini .........................................
  Kosa lenu ni kufanya kazi isiyokuwa Yenu...kuhukumu..Mimi
  Peke yangu ndie naweza kuhukumu...sijafundishwa dini mimi
  Mimi ni Muumba wenu...Hivyo mtatupwa motoni kwa kuwa
  Kwa midomo Yenu mmesema kuna Muumba mmoja lakini kwa
  matendo Yenu mmejifanya nyinyi ndio mimi. Mmeuana wakati
  mimi sikuwaua. Kosa lenu ni Hilo tu tangu mzaliwe.

  Juma: '' Mwenyezi Mungu...lakini hawa wanaamini Miungu Mitatu!''
  Mwenyezi: '' Hilo niachie mimi"
  Joseph: '' Mwenyezi Mungu...hawa wanamkataa Yesu Kristo Mwanao"
  Mwenyezi: '' Hilo niachie mimi"
  Juma: '' Mwenyezi hawa wanagawa pombe kwenye Ibada zao
  wanasema Pombe ni damu yako''
  Mwenyezi: '' Hilo niachie mimi"
  Joseph: '' Mwenyezi hawa wanaabudu na mashetani na Majini
  wanasema wewe umeagiza waabudu pamoja.
  Mwenyezi: '' Hilo niachie mimi"

  Joseph na Juma: '' Mwenyezi kama ni hivyo naomba utusamehe na sisi kwa
  hiyo tumeshasameheana"
  Mwenyezi: '' Mngefanya hivyo huko huko duniani, kwa sasa mnasubiri
  Moto"
   
Loading...