Mauaji ya Songea; IGP - Said Mwema aomba radhi

IGP anasema iwapo itabainika kuwa polisi walitumia nguvu nyingi kupita kiasi watachukuliwa hatua za kinidhamu. Ni nani wa kuchunguza na kubaini hilo? Ni Chagonja huyu huyu?
 
pamoja na kuomba msamaha lakini tume aliyoiunda imekosa integrity.ni sawa na kesi ya mbuzi kumwachia chui unategemea nini hapo?
 
Tatizo sio tume kinachokera ni utekelezaji wa kile kitakachobainishwa baada ya uchunguzi je kitatekelezwa? Nchi hii zimekwishaundwa tume kibao linapokuja swala la utekelezaji wa ripoti ya tume hamna kinachofanyika. Kuhusu msamaha IGP alisubiri kamati ya bunge ndo apate sehemu ya kuonesha kuguswa na mauaji hii mi naona sio sawa....
 
Radhi iendane na hatua za kuchukua, simamisha kazi RPC Kwanza ndiyo Uchunguzi ufanyike, RPC anaweza kuathiri uchunguzi huo kwa kuwa na yeye ni mtuhumiwa.
 
Hawa wanafiki tu,hawa askari kama wangekuwa wanadibishwa kutokana na kufanya mambo kama haya sidhani kama wangekuwa wanarudia...Mbeya ilikuwaje? Arusha ilikuwaje? na sehemu nyingine nyingi.Asitufanye sisi matahaira tusiojua kinaendelea nini,askari wanatimiza amri ya mkuu wao,na mkuu wao anapata amri toka juu...watuambie tu wanaifanyia kazi ilani ya chama tu....
 
"hivi ninavyozungumza nina kidonda moyoni mwangu,"
Angepata vidonda walipouwawa watu wasio na hatia Arusha na Tarime labda tungekuwa na IGP mwingine bora kuliko huyu 'bora IGP'. Amechelewa sana kupata kidonda moyoni.
 
Angeanza kumuomba samahani Dr. Mwakyembe amabye ni kiongozi mwenzie then kistaarabu angeomba kwa Baba Mwanaasha ili ajiuzulu kuficha hii aibu. Yule RPC ni wa kupeleka Mahakamani tu akale ugali wa bure.
 
Kwa mauaji ya Arusha, JK aliomba radhi kwa wafadhili na kudai ni bahati mbaya; hayatatokea tena. Hakufanya hivyo kwa wana-Arusha na kwa wa-Tanzania. Tulisikia tu Polisi wakipongezwa kwa kuepusha nchi yetu na vurugu na machafuko yanayochochewa na CDM. Mwema sasa anaomba radhi kwa kamati ya Bunge. Sijui kama atafikisha hayo "maumivu" yake kwa wana-Songea. Tena huyu jamaa mjanja sana; kauli yake nadra sana kusikika akiamrisha vipigo. Tunasikia tu makamanda wakiletewa amri za dharura toka makao makuu kufanya vitu vyao. Wasemaji/wapayukaji wanakuwa akina Manumba, Chagonja na malofa wengine jeshini.

Hebu tuamke. Kuna mwelekeo (pattern) ya viongozi kutaka kutumia polisi kuvunja kabisa ujasiri wa wananchi kudai haki zao dhidi ya Serikali na vyombo vyake vya dola. Wako tayari hata kwa mauaji katika hilo. Kinachowatisha tu ni kuchafuka mbele ya wafadhili (US, UK, n.k.). Huko ndiko wako tayari kuomba radhi haraka haraka. Kauli zao tata baada ya maafa kutokea zinatosha kuwatahadharisha wa-Tanzania kwamba tuna serikali katili. Kazi inahitajika kudhibiti hali hii kabla hatujafika "kuzimu" kama asemavyo Johnson Mbwambo wa Raia Mwema.
 
Atauambie ukweli kwanini ma RPC wameasi wanaamlisha Polisi wauwe watanzania wasio na hatia waliokuwa wakitoa kilio chao cha mauaji yaliyokuwa yakiendelea mjini Songea ,Karibu kila wilaya,mkoa ,Polisi wanaua wananchi kwa risasi,hao wabunge wa CCM majambazi kwa nini wasimdodose kitu gani kimetokea katika uongozi wa Jeshi Kwa nini Jeshi limekosa nidhamu badala ya kulinda usalama wa raia na mali zao limekuwa jeshi la Kuua na kupora mali za wananchi
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema, amesema amesikitishwa na kusononeshwa sana na mauaji ya watu wanne yaliyofanywa hivi karibuni katika mji wa songea na vijana wake askari wa jeshi la polisi, ndiyo maana amepeleka kikosi maalum toka makao makuu ili kubaini ukweli wa hali halisi iliyojiri. Said Mwema, ameyasema hayo hivi punde, wakati alipokutana na kamati ya kudumu ya bunge inayoshughulika na maswala ya ukimwi, inayoongozwa na mhe. Lediana Mng'ong'o.

Akiongea kwa upole na unyenyekevu, hata kabla hajaulizwa, IGP, alifafanua kuwa yeye binafsi ameumizwa sana moyoni mwake na mauaji ya raia wasio na hatia. "hivi ninavyozungumza nina kidonda moyoni mwangu," alisema IGP akisisitiza kuwa, "mimi [said mwema] binafsi ninsingependa kuona hali hii inaendelea."

Kufuatia hali hiyo, mbunge wa Ludewa, mhe. Filikunjombe, alimtaka IGP aombe radhi, kuthibitisha kauli yake kwamba ni kweli ana 'kidonda moyoni' kinachosababishwa na mauaji ya watendaji wake wa chini.

Pamoja na kukubali rai ya Mhe. Filikunjombe, IGP Mwema, amesema askari waliofanya yale mauaji, ikibainika wametumia 'nguvu ya ziada', watachakuliwa hatua za kinidhamu. Na hivyo IGP amewataka wabunge wasubiri ripoti ya uchunguzi.

My take: Ni jambo la busara kwa IGP Mwema kuomba radhi kwa makosa yalosababishwa na askari wake. Huu ni uungwana. Hata hivyo, Mawaziri nao wajifunze kuwajibika kwa makosa ya walio chini yao.

Ni sawa kuomba radhi ni uungwana tena sana na nampongeza sana IGP Mwema kwa kufanya hivo na iwe ni tabia endelevu isiishie Songea tu na iwe pia kwa viongozi wengine wa kitaifa na hata wa chini.

Ila tuangalie uzito wa jambo lenyewe. Hapa inahusu vifo vyo watu...maisha ya watu yamekatishwa (terminated!) kinyama.. na haiishii tu kwa waliouawa bali je wale ambao walikuwa wakiwategemea kwa matunzo na hata kwa ushirikiano wa mambo fulanifulani wamepata pigo kwa kiasi gani, wamesumbuiwa kiasi gani. Hili la kwanza

La pili: Kuomba radhi ni sawa ila je tuko serious kiasi gani na hiyo radhi iliyoombwa? Unajua haihusu labda watu wameibiwa bidhaa (mahindi, ngup, ngombe, n.k) bali watu wamekufa..vifoooo!!!

La tatu: Uchunguzi: Hapa napata wasiwasi kuwa uchunguzi huu utawahusu tu askari walioshika bunduki na kufyatua risasi kama walikuwa wamefanya hivo kwa nguvu ya ziada au nao walizidiwa na waandamanji. Hapa jamani suala siyo aliyebeba bunduki na kufyatua tu!! Inaenda mbali zaidi ya hapo. Kijeshi mtu/askari hawezi fyatua risasi bila ya amri kuto kwa wa juu yake na wa juu yake hawezi kutoa amri ya piga pasipo na yeye kupewa ruhusa kutoka kwa wa juu yake, na wa juu yake pia hawezi ruhusu kuua kama mfumo haumpi ku-ua. Sasa utakuja kuona uchunguzi huu unawahusu wengi...kuanzia askari aliyefyatua/triger risasi na kumpata aliyeuawa au kujeruhiwa, aliyetoa amri piga!!, aliyeruhusu matumizi ya silaha za moto kutoka stooo, Mkuu wa polisi wa mkoa, wilaya, na Mkuu wa mkoa naye, hadi IPG pia anaweza husika hapo kutokana na mfumo unavyofanya kazi... na kwa mbali utaweza ona hata rais...amiri jeshi mkuu anawezaguswa kimfumo kuwa naye anaweza husika... so is a chain of people and events...

Ila kwa kuwa tunaanza kutaka kuwa wa kweli na makini na kwa mazingira ya tuko hili la huko Songea ngoja tu itoshe kusema kuwa watu hawa wachunguzwe kwa umakini na kwa undani sana
  • Mkuu wa mkoa: Watu walitaka kwenda kumwona kwa nini asimwambie mkuu wa polisi wa mkoa waacheni watu waje wanione tuongee nitawasikiliza....wapeni tu ulinzi ili maandamano yao yafike na hali ya usalama iimarike???
  • Mkuu wa polisi wa mkoa na wilaya: Kwanini wasiwe wepesi wa kujua maandamano ya hatari na ya amani kiasi cha kutoa amri ya piga/ua au waacheni waandamane wakamwone mkuu wapeni tu ulinzi???
  • Askari walioshika silaha na kufyatua: Wasionewe na wakawa kondoo wa kafara...wapo waliotoa amri au wapo waliopelekea hawa kufyatua
  • Mtoa silaha kule amara: Ilikuwaje silaha za moto zitolewe kule stoo kama mawazo ya kuua yalikuwa yapo mapema hata kabla ya waliofyatua silaha kufanya hivo na kuweza kua na kujeruhi??? Wahusika hapo ni wengi kuliko hao wachache
  • n.k
Naomba haki itendeke na pia kuwepo na fidia ya wahanga wa mauaji na waliojeruhiwa
 
assa von micky said:
uzuri wa sinema za bongo ni kama zile za hollywood ,utofauti ni kwamba za bongo zinaongozwa na siasa.....

Umesema kweli kaka, hili nalo litaisha kimya kimya na watu wote tutaendelea na maisha yetu kama kawaida kama vile wanaokwenda katika ukumbi wa sinema si ikiiisha (the END) kabla hata hatujaambiwa tutoke tunaanza kusukumana kutoka hata kama ulichoona hakifanani na pesa yako. Sijui watanzania tumerogwaaa! tutaendelea kufa hadi lini ! Waziri kwa nini asiwajibike kwani nafasi yake ni ajira ya kudumu? na huyo IGP, ni mnafiki tu antuma watu wa chini yake ili yeye apate nafasi ya kutuliza munkari wananchi lakini hafanyi lolote ndo kwanza atawasaidia kwa kuwahamishia kwingine.
 
Wameshazoea kuua hao, hana lolote ni unafiki tu!!
mkuu wangu Limbani ni kweli wamezoea kuua na huwa hawaombi msamaha lakini juzi wameua ktk jimbo linaloongozwa na mbunge wa CCM na waziri ktk serikali ya JMT. Bila shaka umenipata mkuu wangu.
 
kusema samahani au naomba radhi mdomoni wakati rohoni kwake hatujui, sisi haitusaidii wala hajatuaminisha kwamba ameguswa. Sisi tunachojua kwamba haya ni maksudi. Huu ni upumbavu mkubwa wanafanya. Kuhusu uchunguzi, zimefanyika chunguzi nyingi sana majibu yanajulikana kabla kama hivi. HUU NI UPUMBAVU MKUBWA BORA ANGEKAA KIMYA kwasababu waliokufa hawarudi tena.
 
ya kama ni kweli basi amefanya vyema ila tume tushachoka nazo kwani huwa kinachojiri baada ya tume kuundwa

Hajaunda 'tume' bali kikosi. Hata hivyo, kwa nini asiwajibike kama Ali Hassan Mwinyi alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani?
Hawa tumewachoka.
 
Radhi itaponyesha vp kidonda cha wanandugu walio ondolewa ndugu zao bila kosa lolote?igp cha msingi ni kuhakikisha haki inasimamiwa na wahusika wote wanahukumiwa kwa kuua kwa kukusudia la sivyo itakua ni hadith inayojirudia na jesh kuzidi kupoteza imani kwa raia wake,hawa wahusika inabidi iwe fundisho kwa askari wengine wenye kujichukulia sheria watakavyo
 
Sasa aombe radhi au awajibike kwa kujiuzulu?


Ni kweli. Miaka ile ya 70 akina RPC Ihuya na wengine walijiuzulu kwa masuala kama haya. Nadhani mnakumbuka vifo vya akina Mazegenuka na wenzake kule Shinyanga. Labda hawa ni malaika wanaendelea kula nchi.
 
Back
Top Bottom