Mauaji ya RPC yaibua mapya, kampeni za CCM zarindima msibani, 15 wakamatwa!

Taarifa za POLISI wa kileo zinatia shaka sana naona kabisa kuna sababu ya kufanya marekebisho makubwa katika kutoa taarifa za kipolisi katika nchi hii nyingi ni za kupotosha ukweli, Tukianzia na taarifa hii ya kuuwawa kwa kamanda Barlow taarifa inadai eti alimkuta njiani Mwl.Doroth akampa lift hiyo lift gani ya saa nane za usiku? hata mjinga hadanganywi na taarifa kama hii,sema waliondoka nae,na huenda anawajua wauaji sasa Interpol wa kazi gani.Pili kupigwa kwa ulimboka walitoa taarifa ya kukamatwa kwa mtu sijui mkenya kwa kuhusika na kipigo cha Ulimboka,sijui walidhani kuwa atakufa? hivyo kuficha ukweli wa kipigo? sasa karudi na anadai anawajua fika watesi wake,yule mtuhumiwa habari zake zimekufa ghafla hatusikii kama anapelekwa mahakamani.tatu kifo cha mwangosi eti kauwawa na bomu lililotupwa umbali wa mita 100 wakati picha zinaonyesha kitendo kilichosababisha kifo chake,HIVI UONGO WOTE HUU WA NINI KATIKA TAASISI KUBWA KAMA HII YA SERIKALI TENA YA USALAMA WA RAIA,KUNA HASARA GANI KUTOA TAARIFA ZA HAKI NA UKWELI?.SISI RAIA HATUPENDI KUSIKIA TAARIFA ZA UONGO KILA SIKU ZINAZOGANDAMIZA RAIA ZINATUCHEFUA NA KUTOKULIAMINI KABISA JESHI HILI NI UOZO MTUPU,HILI LAZIMA LIINGIE KATIKA KATIBA MPYA LA HILI JESHI MAVIMAVI LA SASA LISAFISHWE KABISA WAJE WATENDAJI(VOTED OFFICERS) KULIONGOZA JESHI HILI SIYO KUPEANA VYEO KIUSHIKAJI NA KINDUGU,HATUTAKI TENA HABARI ZA UONGO NA HATUDANGANYIKI.:embarassed2::embarassed2::A S 465::A S 465::embarassed2::embarassed2:
 
Poleni sana, Mungu ni mwenye haki anajua yote. Poleni familia, Poleni polisi, Jina la bwana libarikiwe.
 
nilichogundua ni kuwa habari za ngono zinaaminika na kuhusishwa na mambo mbalimbali ya umwagaji damu. Na hata kama tukio limetokea tu katika mazingir ya kawaida, basi itatafutwa habari inayohusiana na ngono kuhalarisha tukio hilo.

Inabidi watanzania tupeane pole

rubbish!
 
hahaha si unajua tena labda huyu mwalimu alikua na jamaa mwingine hawakuelewana jamaa akaamua kumtelekeza barabarani kabla "msamaria mwema kamanda hajatokea kumrescue" matukio kama haya yapo Smile au hutaki lol
Na huyo kamanda alikuwa anatokea wapi muda huo?na kwanini yeye na sio mtu mwingine
 
Published on October 14th, 2012

SIKU moja baada ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza (RPC), Liberatus Barlow (52), kuuawa na kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, taarifa zinasema polisi wa kimataifa watashirikishwa kufanya uchunguzi na kukamata wahusika wa tukio hilo.

Polisi mkoani Mwanza wameapa kupambana kuwasaka waliohusika katika tukio hilo la kinyama, huku idadi ya watu waliokamatwa hadi kufikia Jumapili jioni ikitajwa kufikia watu 15.


barlow-enzi-uhai.jpg

Kamanda Barlow enzi za uhai wake

Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zilizopatikana jijini Mwanza zinaeleza kwamba, idadi hiyo ya watuhumiwa waliokamatwa huenda ikaongezeka maradufu kuanzia kesho Jumatatu, baada ya marehemu Barlow (pichani), kuagwa jijini hapa kesho kisha kusafirishwa hadi nyumbani kwake Dar es Salaam, na baadaye Jumanne kusafirishwa nyumbani kwao mkoani Kilimanjaro tayari kwa mazishi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo baadaye Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Lily Matola pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba walikataa kutaja idadi halisi ya watuhumiwa waliowakamata, zinadai kwamba upelelezi wa kina na wa hali ya juu unafanyika kote nchini, ikiwa ni pamoja na maeneo ya mipakani ili kuwanasa watuhumiwa wa mauaji hayo.

“Kazi ya kukamata watu wanaoshukiwa inaendelea. Na hadi leo Jumapili zaidi ya watu 15 wameshakamatwa… na upelelezi wa kina unafanyika kila kona ya nchi hii na hadi maeneo ya mipakani.

“Kuuawa kwa Kamanda Barlow si tukio dogo. Inahitajika nguvu ya ziada kuwanasa watuhumiwa, ndiyo maana IGP Said Mwema amemtuma haraka sana kuja Mwanza DCI Manumba. Ninyi subilieni tu mtasikia…wote waliohusika tutawakamata tu”, kilisema chanzo cha habari kutoka ndani ya jeshi la polisi mkoani Mwanza (jina tunalihifadhi).

Kuhusu ripoti ya madaktari
Alipoulizwa na FikraPevu iwapo uchunguzi wa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), ya jijini Mwanza juu ya mwili wa marehemu Barlow, Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa, Matola alisema jopo la madaktari bado wanaendelea kufanyakazi yao ya uchunguzi.

“Suala la ripoti ya madaktari kuhusu mwili wa RPC Barlow bado wanaendelea huko hospitalini Bugando. Subilieni tutawaambia tu ndani ya siku chache!”, alisema Kaimu Kamanda huyo wa polisi mkoani hapa, Matola.

Kufuatia taarifa hiyo ya Matola, habari za awali zilizopatikana kutoka kwa vyanzo vyetu Bugando zinadai kwamba, hadi kufikia leo alasiri tayari jopo la madaktari walikuwa wameshamaliza uchunguzi wao juu ya marehemu Kamanda wa polisi mkoani hapa.

Inadaiwa kwamba, miongoni mwa risasi zilizompata kamanda huyo, risasi moja ilimpiga shingoni kisha kuvunja na kuharibu kabisa shingo pamoja na mfumo wa damu, hali iliyosababisha kuvuja kwa damu nyingi.

Makachero wa Interpol kusaidia
Inadaiwa kwamba ili kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa wa mauaji hayo ya RPC Barlow, jeshi la polisi limeomba ushirikiano kutoka Kitengo cha upelelezi cha Interpol.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jijini Mwanza, zinadai kwamba baadhi ya askari kutoka vikosi hivyo vya Interpol hapa nchini na nchi jirani vimeshaanza kuwasili kisha kusambaa katika maeneo tofauti Ukanda wa nchi zote za Maziwa Makuu, na kwamba watuhumiwa wote lazima wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

“Polisi imeshaomba msaada wa kikosi cha Interpol ili kusaidia kuwanasa wauaji hawa. Hapana shaka lazima watu waliohusika kummiminia risasi na kupoteza uhai wa RPC Barlow watakamatwa tu. Achana na kazi ya Interpol, maana hata mtu amejificha kwenye handaki atapatikana tu”, kilisema chanzo kingine cha habari.

Katika hilo, Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Matola alipoulizwa na FikraPevu iwapo ni kweli wameomba msaada na nguvu ya kiupelelezi kutoka kwa askari wa Interpol, alishindwa kukubali wala kukanusha, bali alisema:

“Naomba mambo mengine mtuachie sisi, maana bado tunaendelea kufanyakazi hii ya upelelezi. Na tunachokiamini ni kwamba wahusika wote wa mauaji ya RPC Barlow lazima wakamatwe”.

Aidha, Kamanda Matola aliwaomba wananchi wote kulisaidia jeshi hilo la polisi katika kuwabaini wahusika wakubwa wa tukio hilo la kuuawa kwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, na kwamba waandishi wa habari nao ni sehemu na nguzo muhimu katika kulisaidia jeshi hilo kufikia malengo yake ya kupambana na wahalifu ndani na nje ya mkoa huo.

DCI Manumba anena
Katika mahojiano yake na mwandishi wa habari hizi jioni hii, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba alisema kazi inayofanywa na jeshi hilo la Polisi lazima itawanasa watuhumiwa wote wa mauaji hayo.

“Nina uhakika wahusika wote wa mauaji ya Kamanda Barlow tutawakamata. Kwa sasa kazi ya upelelezi bado inaendelea kufanyika, lakini tutahakikisha sheria inachukuwa mkondo wake kwa watuhumiwa wote”, alisema DCI Manumba kwa njia ya simu yake ya kiganjani.

Alipotakiwa kutaja idadi ya watu waliokwisha kukamatwa tangu mauaji ya Kamanda huyo wa Polisi mkoani Mwanza, DCI Manumba ambaye amejichimbia jijini hapa kwa lengo la kuongeza nguvu ya kiupelelezi alisema:

“Hilo la idadi siwezi kusema. Naomba mtuache kwanza tutawaambia mara baada ya kazi kukamilika. Vuteni subira, kazi bado inafanyika”.


Msiba wageuzwa siasa
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa baadhi ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, wameugeuza msiba huo kama sehemu ya kufanyia kampeni dhidi ya wagombea wanaowahitaji wao ndani ya CCM, baada ya kampeni kuanza kulindima msibani hapo.

Hali hiyo ilijitokeza jana nyumbani kwa marehemu Barlow maeneo ya Pasiansi, ambapo baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa baadhi ya wagombea nafasi ya uenyekiti wa CCM kuanza kupenyeza maneno ya kampeni wakati walipokuwa wameenda kuhani familia ya marehemu huyo.

Baadhi ya watu waliiambia FikraPevu kwamba, wapo baadhi ya wana CCM waliofika nyumbani kwa marehemu Barlow walikuwa wakipiga kampeni kwa ajili ya wagombea wao, na kwamba kampeni hizo zilikwenda sambamba na kuwapaka matope baadhi ya wagombea wasiofungamana na makundi yao.

“Ama kweli dunia imeisha. Watu wanakuja msibani tukidhani wamekuja kuhani, lakini cha ajabu wanaanzisha kampeni za wagombea wanaowataka CCM. Ni kitendo kibaya sana.

“Watu wana machungu na wengine wanalia, halafu mtu anaibuka kuanza kukueleza mambo ya uchaguzi wa CCM ngazi ya mkoa. Huu ni uendawazimu kabisa”, alisikika mwombolezaji mmoja.

Uchaguzi wa uenyekiti wa CCM ngazi ya mkoa wa Mwanza, unatarajiwa kufanyika Oktoba 16 mwaka huu, ambapo wanasiasa watato wanaochuana katika kinyang’anyiro hicho ni pamoja na Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo, Clement Mabina, Zebedayo Athumani, Hussein Mashimba na Joseph Yared.

Alisikika Juzi Oktoba 13 mwaka huu majira ya kati ya saa 7 hadi saa 8 usiku, RPC Barlow alimiminiwa risasi kadhaa maeneo ya shingoni na kundi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza, wakati alipompeleka nyumbani kwake mwanamke mmoja Doroth Moses ambaye pia ni mwalimu wa shule ya msingi, Nyamagana jijini hapa.

Katika tukio hilo la kinyama, inadaiwa kabla ya RPC kukumbwa na mauti alikuwa amekwenda kuhudhuria kikao cha harusi cha mtoto wa dada yake, aliyetajwa kwa jina la Sembeli Mareto kilichofanyika Frolida hoteli maeneo ya Kitangiri jijini hapa, na kwamba baada ya kikao hicho marehemu aliwasha gari lake binafsi kisha kumpeleka nyumbani kwake Mareto.

Inadaiwa kwamba, baada ya kumfikisha nyumbani mpwa wake huyo, RPC Barlow aliyekuwa akiendesha gari lake binafsi, akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake maeneo ya Pasiansi alikutana na mwalimu Doroth Moses ambapo aliombwa lifti ya kumpeleka nyumbani kwake Kitangiri, na bila ajizi Kamanda huyo alimpatia msaada huo hadi nyumbani alikokwenda kuuawa kinyama na watu wanaodaiwa waliwakuta getini nyumbani kwa mwanamke huyo.



Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma – FikraPevu, Mwanza | Mauaji ya RPC yaibua mapya, kampeni za CCM zarindima msibani, 15 wakamatwa! | Fikra Pevu
Interpol intakuja na kula kodi zetu kwa ajili ya mtu mmoja aliyefariki!! Interpol ije na kushughulikia; Mauaji ya Iringa (Mwangosi), Mauaji ya Arusha, Vipigo vya Ulimboka na wabunge wa Mwanza!! If really this is Just society!! Where is Human rights organisations!? where is transparent international! some humans are more humans than others CCMABWEPANDE your curse is now on!!
 
1. Mmeshaambiwa alikuwa kwenye kikao cha harusi ya ndugu yao wote Doro na BARLOW
2. Barlow ndo aliombwa kuwa mwenyekiti wa kikao
3. kikao kilichelewa kuanza na badala ya kuhudhuria na waalikwa 100, walifika 55, kati yao wanawake wawili, Doroth akiwemo.
4. wamemaliza usiku wakaanza kunywa pombe na Barlow ndo alikuwa mlipaji, alizungusha raund na ikamgharimu 40,000 na mhudumu alinunuliwa yake.
5. Baada ya kinywaji sasa wanarudi nyumban, sasa mwenyekiti kumrudisha mmoja wa wajumbe wake kuna ubaya gani?

Kwa nini muanze kulazimisha habari za kingono kuwa ndo chanzo?

hii inadhihirisha kuwa TUNAPENDA UZINZI ZAIDI.

SOMA HAPA http://www.mwananchi.co.tz/componen...story/26596-mshtuko-mauaji-ya-rpc-mwanza.html

Mtake msamaha Mwenyezi mungu, hapo kwenye red, yaani unamwambia maneno hayo hayati kamanda? Lol!
 
Nataka nifuatilie kwa kina ni nini kimemuua huyu mtu, je ni kweli amepigwa na Risasi au ni vitu vizitozito na venye ncha kali kutoka kwa watu wasiofahamika ndiyo vimepelekea kifo chake.
Ni afadhali upate jibu la kuwa kitu chenye inchi kali ndio kimemuua kuliko KAMANDA WA MKOA(RPC) kuuwawa kwa siraha yake mwenyewe ni aibu sana
 
hii movie inafanana kwa mbali na ile ya marehemu Kanumba na mkasa wa Lulu...
Kuna vitu vinafichwa sana, kama hao majambazi walikuwa wanamsubiri Barlow basi ilikiwa ni mpango uliosukwa.
Nijuavyo mimi watu waliokusudia kuua wasingemwacha hai huyo mwanamama au la basi hata kipigo kidogo.
 
Leo magazeti yanadai
Doroth keshafunguka zaidi kuwa wale wauaji walibishana km wamuue na yeye Boss wa wauaji akasema mwacheni kwa hiyo. Mauaji yamepangwa hapo hamna haja ya Interpool
Huwezi linganisha kio cha Mwangosi akutafuta habari kweupe na cha RPC kwenye Maguest eti kalipia vinywaji tu 75,000 usiku wa manane na mke wa mtu mkudanganya dada yake wametoka wote Kirua Vunjo. Hiyo dhambi ni kubwa hata mkimpigia mizinga na kumuaga Dar-Mwanza tofauti na Mwangosi alivyopokelewa MBINGUNI baada ya kushindiliwa bomu tumboni huku kapiga magoti akiomba asiuawe
Mwisho RPC hakufanya haki kutaka kumuua askari wa Uhamiaji na kudai ni jambazi aliyeingia katika Target
 
Hebu kuweni wadadisi kidogo, toka juzi mpaka leo mnajadili kwann kamanda alimpa lift yule dada? Tambua hakuna kikao cha harusi kinaishaga saa saba usiku, pili wewe unaweza kumpa lift stranger mpaka kwake usiku wa manane? hapa cha kujua huyu teacher ni kweli ameolewa? ana boyfriend? ni mjane? ni jambazi? anashirikiana na majambazi? nk, kama tulivyopostiwa picha yake she is really very beautful, so labda kamanda alijitengenezea maadui na akajiamini kwa cheo chake. Jambazi haui mtu, ukiona kaua ni ili acomplish mision yake, what was the mision there? kamanda alikuwa na hela? au je ni kweli ameua majambazi wengi Mwanza kwahiyo wakawa wanamuwinda nayeye wamuue? that obvious na ndo maana anapewa ulinzi 24/7, kwann atumie private transport bila bodyguard? kwanini kusiwe na escort car? najiuliza tu. RIP BARLOW
 
Taarifa za POLISI wa kileo zinatia shaka sana naona kabisa kuna sababu ya kufanya marekebisho makubwa katika kutoa taarifa za kipolisi katika nchi hii nyingi ni za kupotosha ukweli, Tukianzia na taarifa hii ya kuuwawa kwa kamanda Barlow taarifa inadai eti alimkuta njiani Mwl.Doroth akampa lift hiyo lift gani ya saa nane za usiku? hata mjinga hadanganywi na taarifa kama hii,sema waliondoka nae,na huenda anawajua wauaji sasa Interpol wa kazi gani.Pili kupigwa kwa ulimboka walitoa taarifa ya kukamatwa kwa mtu sijui mkenya kwa kuhusika na kipigo cha Ulimboka,sijui walidhani kuwa atakufa? hivyo kuficha ukweli wa kipigo? sasa karudi na anadai anawajua fika watesi wake,yule mtuhumiwa habari zake zimekufa ghafla hatusikii kama anapelekwa mahakamani.tatu kifo cha mwangosi eti kauwawa na bomu lililotupwa umbali wa mita 100 wakati picha zinaonyesha kitendo kilichosababisha kifo chake,HIVI UONGO WOTE HUU WA NINI KATIKA TAASISI KUBWA KAMA HII YA SERIKALI TENA YA USALAMA WA RAIA,KUNA HASARA GANI KUTOA TAARIFA ZA HAKI NA UKWELI?.SISI RAIA HATUPENDI KUSIKIA TAARIFA ZA UONGO KILA SIKU ZINAZOGANDAMIZA RAIA ZINATUCHEFUA NA KUTOKULIAMINI KABISA JESHI HILI NI UOZO MTUPU,HILI LAZIMA LIINGIE KATIKA KATIBA MPYA LA HILI JESHI MAVIMAVI LA SASA LISAFISHWE KABISA WAJE WATENDAJI(VOTED OFFICERS) KULIONGOZA JESHI HILI SIYO KUPEANA VYEO KIUSHIKAJI NA KINDUGU,HATUTAKI TENA HABARI ZA UONGO NA HATUDANGANYIKI.:embarassed2::embarassed2::A S 465::A S 465::embarassed2::embarassed2:

POLISI wanatumia principal ya 'shifting of onus of proof' yaani hata kama wanajua ukweli wanachohamisha kwao ni kukupa wewe mtendewa kazi ya kuthibitisha. Wanajua inahitaji utaalamu na kazi kubwa raia kuthibitisha mashtaka na njiani unaweza kushindwa so wao wanapona-chukulia mifano yote yamauaji ya arusha, moro na mwangosi. Nadhani wamefundishwa kutokukubali kosa moja kaw moja kama wengi wa wahalifu sugu walivyo.
 
"Aidha, Kamanda Matola aliwaomba wananchi wote kulisaidia jeshi hilo la polisi katika kuwabaini wahusika wakubwa wa tukio hilo la kuuawa kwa Kamanda wa Polisi mkoani"
Ivi hao wananchi si ndio ambao mnawapiga virungu sometimes na kuwaua,Jan - Sept mshawaua zaidi ya 24 leo mnataka ushirikiano upi tena Yakhe!
 
upuuzi mtupu lifti saa nane usiku kauli tata na zinakinzana Barlow na mwangosi ni yupi watanzania wanamlilia? Kwa kuuwawa akiwa kazini na si..........
 
Huko ndiko staili yao kabisa ili wakileta za kuleta wakutane na jamaa

Naomba kazi kupeleleza tukio la kifo cha Kamanda.
Am sure ntapata ukweli fasta.Ila lazima ntaanzia Mbeya.moro,Dar then nashuka Mwanza.Ni siku 2 tu chanzo cha vitu vyenye ncha kali vinakoma kuruka na kuua watu.
 
upuuzi mtupu lifti saa nane usiku kauli tata na zinakinzana Barlow na mwangosi ni yupi watanzania wanamlilia? Kwa kuuwawa akiwa kazini na si..........
 
uko sawa ngugu ninchouliza ni kwanini uchunguzi unaohusisha interpol usifanywe kwa wote na sio kamanda peke yao?
nadhani kama sio kamera za waandishi kuwaumbua polisi tungeambiwa Mwangosi aliuliwa na chadema.
umeona polisi walivotaka kuturubuni kuwa ni mauaji ya bahati mbaya na umesikia sakataka la afisa uhamiaji kuwa waliweka mtego wa kumnasa jambazi na walipanga kumuua huyo afisa kama sio Mungu kumsimamia
Kamanda barlo akasema ni tukio la nahati mbaya
nadhani hapa tuseme nae alikufa bahati mbaya pia mistaken identity
ndugu usalama wa raia uko mashakani kwa sasa.
Hapana Lokissa vifo vyote viwili vinasikitisha. Hakuna mtu aliyepewa mamlaka ya kutoa uhai wa mtu. Inasikitisha sana kuona watu tunaona uhai kama kitu kidogo sana. Waliomuua Mwangosi hawakuwa na haki na hata hawa waliomuua RPC hawana na haki. Mbele za macho ya Mungu wote wanamakosa. Wafiwa poleni sana. Mungu atawape faraja.
 
Back
Top Bottom