Mauaji ya RPC yaibua mapya, kampeni za CCM zarindima msibani, 15 wakamatwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya RPC yaibua mapya, kampeni za CCM zarindima msibani, 15 wakamatwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Informer, Oct 14, 2012.

 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,223
  Likes Received: 2,434
  Trophy Points: 280
  Published on October 14th, 2012

  SIKU moja baada ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza (RPC), Liberatus Barlow (52), kuuawa na kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, taarifa zinasema polisi wa kimataifa watashirikishwa kufanya uchunguzi na kukamata wahusika wa tukio hilo.

  Polisi mkoani Mwanza wameapa kupambana kuwasaka waliohusika katika tukio hilo la kinyama, huku idadi ya watu waliokamatwa hadi kufikia Jumapili jioni ikitajwa kufikia watu 15.


  [​IMG]
  Kamanda Barlow enzi za uhai wake

  Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zilizopatikana jijini Mwanza zinaeleza kwamba, idadi hiyo ya watuhumiwa waliokamatwa huenda ikaongezeka maradufu kuanzia kesho Jumatatu, baada ya marehemu Barlow (pichani), kuagwa jijini hapa kesho kisha kusafirishwa hadi nyumbani kwake Dar es Salaam, na baadaye Jumanne kusafirishwa nyumbani kwao mkoani Kilimanjaro tayari kwa mazishi.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo baadaye Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Lily Matola pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba walikataa kutaja idadi halisi ya watuhumiwa waliowakamata, zinadai kwamba upelelezi wa kina na wa hali ya juu unafanyika kote nchini, ikiwa ni pamoja na maeneo ya mipakani ili kuwanasa watuhumiwa wa mauaji hayo.

  "Kazi ya kukamata watu wanaoshukiwa inaendelea. Na hadi leo Jumapili zaidi ya watu 15 wameshakamatwa… na upelelezi wa kina unafanyika kila kona ya nchi hii na hadi maeneo ya mipakani.

  "Kuuawa kwa Kamanda Barlow si tukio dogo. Inahitajika nguvu ya ziada kuwanasa watuhumiwa, ndiyo maana IGP Said Mwema amemtuma haraka sana kuja Mwanza DCI Manumba. Ninyi subilieni tu mtasikia…wote waliohusika tutawakamata tu", kilisema chanzo cha habari kutoka ndani ya jeshi la polisi mkoani Mwanza (jina tunalihifadhi).

  Kuhusu ripoti ya madaktari
  Alipoulizwa na FikraPevu iwapo uchunguzi wa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), ya jijini Mwanza juu ya mwili wa marehemu Barlow, Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa, Matola alisema jopo la madaktari bado wanaendelea kufanyakazi yao ya uchunguzi.

  "Suala la ripoti ya madaktari kuhusu mwili wa RPC Barlow bado wanaendelea huko hospitalini Bugando. Subilieni tutawaambia tu ndani ya siku chache!", alisema Kaimu Kamanda huyo wa polisi mkoani hapa, Matola.

  Kufuatia taarifa hiyo ya Matola, habari za awali zilizopatikana kutoka kwa vyanzo vyetu Bugando zinadai kwamba, hadi kufikia leo alasiri tayari jopo la madaktari walikuwa wameshamaliza uchunguzi wao juu ya marehemu Kamanda wa polisi mkoani hapa.

  Inadaiwa kwamba, miongoni mwa risasi zilizompata kamanda huyo, risasi moja ilimpiga shingoni kisha kuvunja na kuharibu kabisa shingo pamoja na mfumo wa damu, hali iliyosababisha kuvuja kwa damu nyingi.

  Makachero wa Interpol kusaidia
  Inadaiwa kwamba ili kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa wa mauaji hayo ya RPC Barlow, jeshi la polisi limeomba ushirikiano kutoka Kitengo cha upelelezi cha Interpol.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jijini Mwanza, zinadai kwamba baadhi ya askari kutoka vikosi hivyo vya Interpol hapa nchini na nchi jirani vimeshaanza kuwasili kisha kusambaa katika maeneo tofauti Ukanda wa nchi zote za Maziwa Makuu, na kwamba watuhumiwa wote lazima wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

  "Polisi imeshaomba msaada wa kikosi cha Interpol ili kusaidia kuwanasa wauaji hawa. Hapana shaka lazima watu waliohusika kummiminia risasi na kupoteza uhai wa RPC Barlow watakamatwa tu. Achana na kazi ya Interpol, maana hata mtu amejificha kwenye handaki atapatikana tu", kilisema chanzo kingine cha habari.

  Katika hilo, Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Matola alipoulizwa na FikraPevu iwapo ni kweli wameomba msaada na nguvu ya kiupelelezi kutoka kwa askari wa Interpol, alishindwa kukubali wala kukanusha, bali alisema:

  "Naomba mambo mengine mtuachie sisi, maana bado tunaendelea kufanyakazi hii ya upelelezi. Na tunachokiamini ni kwamba wahusika wote wa mauaji ya RPC Barlow lazima wakamatwe".

  Aidha, Kamanda Matola aliwaomba wananchi wote kulisaidia jeshi hilo la polisi katika kuwabaini wahusika wakubwa wa tukio hilo la kuuawa kwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, na kwamba waandishi wa habari nao ni sehemu na nguzo muhimu katika kulisaidia jeshi hilo kufikia malengo yake ya kupambana na wahalifu ndani na nje ya mkoa huo.

  DCI Manumba anena
  Katika mahojiano yake na mwandishi wa habari hizi jioni hii, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba alisema kazi inayofanywa na jeshi hilo la Polisi lazima itawanasa watuhumiwa wote wa mauaji hayo.

  "Nina uhakika wahusika wote wa mauaji ya Kamanda Barlow tutawakamata. Kwa sasa kazi ya upelelezi bado inaendelea kufanyika, lakini tutahakikisha sheria inachukuwa mkondo wake kwa watuhumiwa wote", alisema DCI Manumba kwa njia ya simu yake ya kiganjani.

  Alipotakiwa kutaja idadi ya watu waliokwisha kukamatwa tangu mauaji ya Kamanda huyo wa Polisi mkoani Mwanza, DCI Manumba ambaye amejichimbia jijini hapa kwa lengo la kuongeza nguvu ya kiupelelezi alisema:

  "Hilo la idadi siwezi kusema. Naomba mtuache kwanza tutawaambia mara baada ya kazi kukamilika. Vuteni subira, kazi bado inafanyika".


  Msiba wageuzwa siasa
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa baadhi ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, wameugeuza msiba huo kama sehemu ya kufanyia kampeni dhidi ya wagombea wanaowahitaji wao ndani ya CCM, baada ya kampeni kuanza kulindima msibani hapo.

  Hali hiyo ilijitokeza jana nyumbani kwa marehemu Barlow maeneo ya Pasiansi, ambapo baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa baadhi ya wagombea nafasi ya uenyekiti wa CCM kuanza kupenyeza maneno ya kampeni wakati walipokuwa wameenda kuhani familia ya marehemu huyo.

  Baadhi ya watu waliiambia FikraPevu kwamba, wapo baadhi ya wana CCM waliofika nyumbani kwa marehemu Barlow walikuwa wakipiga kampeni kwa ajili ya wagombea wao, na kwamba kampeni hizo zilikwenda sambamba na kuwapaka matope baadhi ya wagombea wasiofungamana na makundi yao.

  "Ama kweli dunia imeisha. Watu wanakuja msibani tukidhani wamekuja kuhani, lakini cha ajabu wanaanzisha kampeni za wagombea wanaowataka CCM. Ni kitendo kibaya sana.

  "Watu wana machungu na wengine wanalia, halafu mtu anaibuka kuanza kukueleza mambo ya uchaguzi wa CCM ngazi ya mkoa. Huu ni uendawazimu kabisa", alisikika mwombolezaji mmoja.

  Uchaguzi wa uenyekiti wa CCM ngazi ya mkoa wa Mwanza, unatarajiwa kufanyika Oktoba 16 mwaka huu, ambapo wanasiasa watato wanaochuana katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo, Clement Mabina, Zebedayo Athumani, Hussein Mashimba na Joseph Yared.

  Alisikika Juzi Oktoba 13 mwaka huu majira ya kati ya saa 7 hadi saa 8 usiku, RPC Barlow alimiminiwa risasi kadhaa maeneo ya shingoni na kundi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza, wakati alipompeleka nyumbani kwake mwanamke mmoja Doroth Moses ambaye pia ni mwalimu wa shule ya msingi, Nyamagana jijini hapa.

  Katika tukio hilo la kinyama, inadaiwa kabla ya RPC kukumbwa na mauti alikuwa amekwenda kuhudhuria kikao cha harusi cha mtoto wa dada yake, aliyetajwa kwa jina la Sembeli Mareto kilichofanyika Frolida hoteli maeneo ya Kitangiri jijini hapa, na kwamba baada ya kikao hicho marehemu aliwasha gari lake binafsi kisha kumpeleka nyumbani kwake Mareto.

  Inadaiwa kwamba, baada ya kumfikisha nyumbani mpwa wake huyo, RPC Barlow aliyekuwa akiendesha gari lake binafsi, akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake maeneo ya Pasiansi alikutana na mwalimu Doroth Moses ambapo aliombwa lifti ya kumpeleka nyumbani kwake Kitangiri, na bila ajizi Kamanda huyo alimpatia msaada huo hadi nyumbani alikokwenda kuuawa kinyama na watu wanaodaiwa waliwakuta getini nyumbani kwa mwanamke huyo.  Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma – FikraPevu, Mwanza | Mauaji ya RPC yaibua mapya, kampeni za CCM zarindima msibani, 15 wakamatwa! | Fikra Pevu
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Ujinga mtupu kuanzia kwa mwandishi hadi vyanzo vyake vya taarifa, Leo polisi mmeona Roho ya RPC ni mali sana kuliko ya mwangosi na wengineo mliouwaua, mwisho tu niwape ujumbe maharemu huwa hafukuki.
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bwana ametoa na Bwana Ametwaa!
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Ujinga mtupu, inaonekana hata hao Interpol hawana kazi ndio maana wanaweza kujishughurisha na mambo ya kijinga kama haya. Kamanda Barlow ndio Mtanzania wa kwanza kuuwawa kwa risasi?
   
 5. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Kama walimpenda sana mwema, kamuhanda na shilogile wafanye maombi afufuke.
   
 6. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Mmmhhh, tarifa za awali zilitueleza kuwa walitoka wote kwenye kikao na mwalimu Doroth, mara mambo yamegeuzwa walikutana njiani (usiku saa 8 huyo mama alikuwa anatembea peke yake, makubwa!!).

  Moyo wangu unakataa kuamini hii new twist. Nyie badilisheni na kunyumbulua tu, time will tell.
   
 7. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Labda polisi ndio ana thamani zaidi anapokufa kuliko Mwangosi na wale wahanga wengine waliouawa na polisi, wamwache apunzike kwa amani.

  Labda na hao interpol wakachunguze pia mauaji ya Mwangosi ntawaelewewa na sio kutumia kodi zetu kwa maslahi ya wachache
   
 8. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu aina ya uandishi wa Huyo mwandishi aliyeandika hiyo makala ndugu sita tuma ndio ukanjanja wa hali ya juu, hivi yeye kakutana lini na marehemu akaambiiwa mwalimu Dorothy alimuomba lift , Wakati taarifa za kuaminika ni kuwa walikuwa pamoja toka hotelini. Hii habari yake ni ukanjanja tu anasaidia polisi kuficha ukweli wa tukio, waandishi wa tanzania wangeungana kufichua uovu wa viongozi badala baadhi yao kutumika kuficha uovu huo
   
 9. p

  politiki JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  sasa nafikiri mmeona kuwa ni chama gani kinachoubiri siasa misibani ......NI CCM
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Umeona eeh!!! hawa Polisi magamba wanataka kuufanya umma wa Watanzania hauna uwezo wa kuchanganua mambo...watasema uongo hata pale ambao ukweli umedhihiri!! wacha wadharauliwe na jamii ya Watanzania.

   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Hivi fikiria hawa paolisi ndio wangekuwa JWTZ .Yaani wakawa ndio walinzi wa Nchi?
   
 12. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hivi akina Shilogile na Kamuhanda wanahamishiwa lini Mwanza?!
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Wanatesa watu bure tuu wakati alichomwa na kitu chenye ncha Kali kilicho chomoka kwenye gari
   
 14. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  tukio ni kubwa. msaada wa interpol ni lazima ili kama wauaji wamekimbilia nje wadakwe.
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,898
  Trophy Points: 280
  Nilijiuliza swali hilo baada ya kusikia kwamba ni mmojawapo wa watu wanaoshikilia,sasa kipengele hicho hapo juu ndicho kinaonyesha wazi kwanini wanamshikilia kwa mahojiano zaidi,nadhani wanataka kujuwa kama ni nani mwingine aliyekuwa akijuwa kuwa kamanda atampeleka nyumbani,kwasababu inaonekana kama vile alikuwa akisubiriwa na hao watu.Hata mimi nilidhani waliondoka naye kutoka kwenye hicho kikao cha harusi.

  Kuna vitu vingi sana havi add up,kwa mfano kuna habari iliyokuwa ikisema kwamba haikuwa mara ya kwanza kwa kamanda huyo kumpeleka nyumbani,however kuna habari nyingine inayodai tena kwamba alimpelekea nyumbani ili apajue anapoishi.Sasa imeshageuka tena kuwa aliombwa lifti wakati akielekea nyumbani kwake Pasiansi.

  Wanataka waandishi wawasaidie kwenye uchunguzi na huku wanatoa habari zisizo add up.
   
 16. Offline User

  Offline User JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 3,768
  Likes Received: 1,460
  Trophy Points: 280
  mbona hapa kamati/tume haiundwi badala yake wanaleta eti 'interpol'....
  Au RPC ana thamani kuliko watz wengine? #absurd
   
 17. K

  Konya JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  sasa sijui nani mkweli coz hizi taarifa za kifo cha kamanda zinakachanganya kiasi flani kila mtu na lake
   
 18. S

  Setuba Noel JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njia ya mwongo fupi. Hadithi kamili anayo huyo mama mrembo Dorothy. Hatujajua kwa uhakika nani anayeipindisha kati yake na polisi. Yeye anaweza kupindisha kujiondoa hatiani, polisi pia wanaweza kupindisha kuficha aibu ya mwenzao (ambayo ni ya kwao pia). Na kwa bahati mbaya ndiyo wao wanaofanya huo uchunguzi.
   
 19. anjnr

  anjnr JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 483
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nahisi kaka MWANGOSI, kama kweli kuna kukutana hukotuendako, ameweka tick ya kwanza kwenye diary yake - kwa kuona tu MAGWANDA ya wale wabaya wake.
   
 20. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  E bwana nimekupa 100%. Yaani wewe ni kama kamuhanda/shilogile.
   
Loading...