Mauaji ya Rais wa Haiti Jovenel Moise na funzo kwa Katiba yetu bora ya mwaka 1977

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
12,077
12,756
Ubora wa Katiba yetu ya mwaka 1977 na yaitwayo madaraka makubwa ya Rais.

Funzo kwa wenzetu nchi ya haiti na kumpunguzia rais wao madaraka.

Je, watungaji (constitutional framers) wa katiba ya 1977 ya JMT walikosea kumpa rais wetu madaraka makubwa?

Kufuatia mauaji ya rais wa nchi ya Haiti Jovenel Moise kumetokea funzo kubwa hasa kwa Chadema na wote wanaotaka katiba mpya hapa nchini, kwa kigezo cha kumpunguzia rais madaraka yake makubwa.

July 5, hayati Rais wa Haiti Jovenel Moise alimteua waziri mkuu mpya baada ya kumuondoa waziri wake mkuu aliyekuwepo kipindi chote cha uongozi wake.

Bunge lilivunjwa na waziri mkuu mteule alikuwa bado kuapishwa.

Mgogoro mkubwa wa kikatiba.

Kwa katiba ya haiti, bunge ndilo lenye mamlaka ya kusimamia nchi pale ambapo rais atafariki ama kuondolewa madarakani kwa sababu tofauti.

Bunge halipo baada ya kuvunjwa na rais ameuawa baadaye.

Hali hiyo imepelekea kwa mawaziri wakuu wawili (aliyeondolewa na mteule ambaye hajaapishwa) kugombea madaraka ya kuwa rais.

Kufikia leo jioni, waziri mkuu aliyeondolewa madarakani amekichukua kiti cha urais (acting president) na kuzua sintofahamu kubwa kupita kiasi.

Kwetu Tanzania

Kwa funzo hili, nawapa kongole waliotuandikia katiba yetu ya 1977 kwa kule kumpa nguvu kubwa rais wa nchi, kwa kuzifikiria tabia zetu wanadamu.Tabia zetu Waafrika, za kuweza kuyagombea madaraka kwa uchu mkubwa kupelekea kuibua mgogoro mkubwa na kuitia nchi katika mizozo, vurugu na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Binafsi nitaendelea kuwasifu waliotunga Katiba yetu bora kwa kutuepushia na matatizo yaliyowapata haiti na baadhi ya nchi nyingine.

Kiukweli kwetu tanzania wala hakuna haja ya kufanya makosa eti tumpunguzie rais wetu madaraka.

Wako watu wasioliona hili ima kwa kutokujua hatari hiyo ama kufanya kusudi ili kutuondolea utulivu wa nchi na kutuchafulia sifa njema ya amani tuliyonayo na inayopigiwa mfano afrika nzima na dunia kwa ujumla.

N.B: Shime tumuunge mkono rais wetu Mh. SSH katika kuujenga uchumi wetu kipindi hiki cha mtanziko wa corona na kuzikataa hila zote za wapenda chokochoko na ukosefu wa utulivu wa kinchi.

#KatibaMpyaSiHitajiLaWatanzaniaWote
#KatibaIliyopoNiBora
#UchumiKwanza
#KaziIendelee
#UchumiKwanza
#DieHardFanOfCCM
 
Ukikua utaelewa. Kwani ikitungwa katiba mpya itanyima fursa Rais ya kupokezana madaraka?
 
Yaani apo ndio umeandiika kwaiyo unafikiri katiba yetu itakua kama ya Haiti. Ndio maana mkibanwa mnakimbilia kutoa mifano ya nchi zenye migogoro lakini mbona hamtuambii kuhusu elimu duni, huduma zisizokidhi za afya, mazingira magumu ya biashara, ukosefu wa ajira, UMASIKINI uliokidhiri toka tupate uhuru
 
Ni hivi, hili la katiba mpya hata mdhikiri mchana uchi hapo uwanja wa Mkapa hamlikwepi. Uzuri wa takwa la muda ukifika umefika. Mtatoa mifano yote, na kufanya upotoshaji wote, lakini kwenye hili lazima muelekee kibla fullstop.
Mkuu Tindo umenikumbusha ile nyimbo "utatoa hutoi ,utatoa hutoi" 🤣

Kipimo chako cha "huo muda usemao" kuwa umefikia ni nini?

Mbona hakuna upotoshaji bali uhalisia tu, litazame kwa makini hilo hitaji lenu la Kumpunguzia madaraka Rais. Je, halitokuja kutuletea mifano ya HAITI?

#KaziIendelee
 
Yaani apo ndio umeandiika kwaiyo unafikiri katiba yetu itakua kama ya Haiti. Ndio maana mkibanwa mnakimbilia kutoa mifano ya nchi zenye migogoro lakini mbona hamtuambii kuhusu elimu duni, huduma zisizokidhi za afya, mazingira magumu ya biashara, ukosefu wa ajira, UMASIKINI uliokidhiri toka tupate uhuru
Wale maadui wakuu 3 tunaendelea kupambana nao kwani changamoto zao zi kila siku. Ujinga, maradhi, na umaskini.

Mkuu hebu kuwa mkweli. Unataka kusema mazingira ya usafirishaji mazao kipindi cha uhuru yako sawa na sasa ambako karibu mikoa yote imeunganishwa kwa kiwango cha lami.

Mkuu kipindi cha uhuru, kulikuwa na barabara moja ya kiwango cha lami.

Kuhusu afya na elimu mifano iko tele ya kupiga hatua kubwa.
 
Ukikua utaelewa. Kwani ikitungwa katiba mpya itanyima fursa Rais ya kupokezana madaraka?
CHADEMA wanataka katiba MPYA yenye madaraka madogo kwa Rais wa JMT hilo likitimia, huko tuendako kutatokea SINTOFAHAMU tu.
 
Ukikua utaelewa. Kwani ikitungwa katiba mpya itanyima fursa Rais ya kupokezana madaraka?
Umemjibu vyema. Mfano alioutoa hauendani na kichwa cha habari. Katiba ya Haiti haikuwa na tatizo,bali Rais wake. And it was coincidence kuwa kabla bunge kuamua, Rais akauwawa!

Mfano! Uchaguzi Mkuu 2020, ulitakiwa kuhojiwa Mahakama namna alivyopatikana Rais kwa idadi ndogo sana ya waliojitokeza kupiga kura. Kuna mambo yanazungumzwa sana kuwa it was a" tabled election". Katiba yetu inakosa kifungu cha kuhoji Tume ya uchaguzi wa Rais ili Mahakama iweke wazi mambo yanayonungunikiwa.

Ukisema mambo yakae yalivyo, iko siku mbeleni ya Haiti yatakuja kwetu.
 
We mchawi, umeangalia mfano mmoja tu, tena umeenda mbali sana, ungeshuka tu bondeni kwa Madiba, uone Katiba mpya na nzuri inavyomshughurikia Rais wa zamani Jackob Zuma, kwa ufisadi aliofanya, sasa hivi anaenda jera.

Na nchi ipo shwaari.
 
Mkuu Tindo umenikumbusha ile nyimbo "utatoa hutoi ,utatoa hutoi" 🤣

Kipimo chako cha "huo muda usemao" kuwa umefikia ni nini?

Mbona hakuna upotoshaji bali uhalisia tu, litazame kwa makini hilo hitaji lenu la Kumpunguzia madaraka Rais. Je, halitokuja kutuletea mifano ya HAITI?

#KaziIendelee
Dunia ina nchi zaidi ya 200, ww unatoa mfano wa nchi moja tu! Mbona nchi nyingine zilizopunguza mamlaka ya rais hazina unachotaka kupotosha hapa?
 
Kwan katiba mpya yote ilikuwa imelenga kubadiri kipengele kimoja tu?
 
Kwa lilichokuwa likitufanyia lile lisanamu la Chato madaraka ya Rais lazima yapunguzwe
 
CHADEMA wanataka katiba MPYA yenye madaraka madogo kwa Rais wa JMT hilo likitimia, huko tuendako kutatokea SINTOFAHAMU tu.
Unapoambiwa unapotosha angalia umepotosha nini? Hapo madaraka ya Rais yamepunguaje kama kilichokatisha mchakato ni kifo? Burundi walikuwa na scenario kama hii kwa Rais aliyeko madarakani kufa huku akiacha Rais mteule kabla ya kuapishwa. Walisolve jambo lao maisha yanakwenda. Kwa mtazamo wako hata Burundi Rais alikuwa naadaraka pungufu? Yaani unataka katiba ambayo maiti ana mamlaka?
 
Kwa lilichokuwa likitufanyia lile lisanamu la Chato madaraka ya Rais lazima yapunguzwe
Akili yako ni ndogo sana unaongea na kuthibitisha kuwa madaraka ya rais lazima yapunguzwe unanafasi hiyo ya kuyapunguza au unaropoka tu?
 
Back
Top Bottom