Mauaji ya Pwani, ni mbinu ya kuwachonganisha wananchi na Serikali

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Kwa mtu mwenye fikra pana atagundua yanayotokea katika Mkoa wa Pwani ni mwanzo tu wa makusudio makubwa ambayo watenda mauwaji wanatarajia kuyafanya.

Kinachotafutwa kwa sasa na wauwaji ni mbinu ya kuichonganisha serikali na wananchi wengi ili watenda mauwaji wapate nafasi ya kupenyeza hoja zao/malengo yao.

Wanafahamu serikali itatumia jazba na kuanza kufanya operesheni za kijeshi ambazo madhara yake yatakuwa kwa wananchi wengi halafu hicho kikundi kitaanza kuwaambia wananchi ‘’mnaona tuliwaambia kuhusu udhalimu wa serikali’’.

Kwa maana nyingine wanatumia mbinu ambayo kama serikali haitakuwa makini itajikuta inakisaidia hicho kikundi katika kutimiza malengo yake ambayo msingi wake ni kuwajengea wananchi chuki kwa serikali kwa malengo ya kutengeneza ombwe (vacuum) kati ya serikali na wananchi huku kikundi hicho kikijaza ombwe kama watetezi wa wananchi lakini malengo yao makuu ni kuhakikisha wanatawala maeneo hayo. Historia inaonyesha hata Boko Haram kule Nigeria ilianza hivi hivi.

Kinachofanyika katika Mkoa wa Pwani hakihitaji operesheni ya kijeshi/JWTZ bali kinahitaji fikra pana ikisaidiwa na technologia ya kisasa.

Kufanya operesheni ya kijeshi/JWTZ haitakuwa tofauti na mtu mjinga anayetumia rungu kumrushia nzi aliyeko ndani ya nyumba yenye vyombo vingi vya udongo. Gharama ya kumuua nzi itakuwa ni kubwa pamoja na kwamba unaweza kumuua huyo nzi mwenye mazalia.

Wataalamu wa saikologia wanabainisha kuwa wauwaji huwa wanapata uzoefu wa kiwango cha juu na kujiamini zaidi kadri wanavyozidi kufanikiwa katika mauwaji huku pia wakipunguza umakini wa kuwawezesha kutogundulika/kukamatwa.

Kujiamini kwao kuwa hawawezi kugundulika/kukamatika huwa kunawafanya waanze kutochukua tahadhari katika nyendo zao na hii ndio huwa ni anguko lao.

Wanaofanya mauwaji katika Mkoa wa Pwani watakapomaliza ‘’soft target’’, wataanza kwenda kwenye ‘’hard target’’ ambako kunahitaji mbinu zaidi lakini ninaamini hili ndilo litakuwa anguko lao kama serikali itatumia akili nyingi zaidi ya nguvu kwa sababu kujiamini kwao kutawafanya wasichukue tahadhari zaidi.

Wanaotaka serikali ipeleke jeshi/JWTZ ili kukabiliana na wauwaji watakuwa wanajidanganya kwa sababu kufanya hivyo itakuwa ni kuucheza mchezo ambao wauwaji wanataka serikali iucheze.

Ieleweke kuwa wauwaji mpaka sasa ni ‘’invisible enemy’’ wakati JWTZ lina mbinu na ueledi tu katika kupambana na ‘’visible enemy’’.

Kinachotakiwa sasa kwa serikali ni kutumia mbinu inayoitwa ‘’winning hearts and minds’’ ambayo mwanzilishi wake ni Mfaransa ambaye alikuwa Generali, Louis Hubert Gonzalve Lyautey ambaye alifanikiwa katika mapambano kusini mashariki mwa Asia(Indochina) mwaka 1895. Hii mbinu itasaidia sana kuwabaini wauwaji kwa sababu wako miongoni mwa jamii lakini pia haitatoa mwanya wa kuwepo na ombwe (vacuum) kati ya wananchi na serikali.

The government must remember, the two most powerful warriors are patience and time.
 
Nimesoma baadhi ya komenti za watu ''wanafurahia'' kila mauwaji yakifanywa huko mkoani Pwani lakini kitu wanachoshindwa kuelewa ni kuwa hawa jamaa waki-‘’graduate’’ wataanza kuzitafuta ‘’hard target’’ na hapo ndipo kutakuwa na uwezekano wa kuona wakifanya mauwaji katika ofisi za halmashauri, Mkuu wa Wilaya na Mkoa, Makanisa, Misikiti, bunge, Supermarkets na viwanja vya michezo.

Time is of the essence...
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom