Mauaji ya profesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya profesa

Discussion in 'Celebrities Forum' started by bongisa, Jul 17, 2011.

 1. b

  bongisa Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana nilikuwa kunduchi salasala kwenye kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha profesa jwani mwaikusa aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika mazingira ya kutatanisha nyumbani kwake kama mnakumbuka wadau. Katika maongezi ya hapa na pale nikapata kuambiwa kuna watuhumiwa walikamatwa wamewekwa ndani, na kesi inaendelea. Cha kushangaza tokea wakamatwe na kesi kuanza sasa ni mwaka mmoja, hiyo kesi hata mahakama kuu haijafika, bado ipo kisutu kwa hivyo inatajwa na kuahirishwa tu hata kusikilizwa bado haijaanza kwani kesi za mauaji husikilizwa mahakama kuu. Hii inamaana upelelezi bado haujakamilika sijui, hivi katika mazingira haya kuna haki kweli au maigizo? Na sababu ya mauaji yale mpaka leo ni giza nene kwa mujibu wa wanafamilia. Wadau hebu tuchangie mawazo kwenye hili.
   
 2. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mhh! jamani nchi hii!!!!!!!!!!, kwa kweli inasikitisha sana.
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Unataka tuchangie nini?
  We nenda kafuatilie usaidie kuipush forward bana.

  Mawazo mawazo!
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  Waache hao wauaji waendelee kusota knako mahabusu mpaka wazeeke ndipo kesi ianze kusikilizwa. Huo ndio utawala wa haki na sheria hapa bongoland.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Oooo,kweli alifariki last year........nakumbuka mwili wake uliagwa NKRUMAH HALL UDSM,sijui familia yake inajiskiaje??????
   
 6. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mambo mengine ni mazito sana ndugu yangu. Solution ni kuyaacha kama yalivyo na kumshuluru Mungu!
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  r i p mwai..
   
 8. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Mauaji ya prof. kwa kweli yanasikitisha sana....................................................
  ....................................................................................................................
  ........................................................................................................
   
 9. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Justice will be served! Hata kama c hapa duniani.. Yaani late prof. was an amazing person kwa tuliofanikiwa kumjua kiasi. May his soul rest in peace.
   
 10. b

  bongisa Member

  #10
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua kilichonisukuma kuandika thredi hii ni baada ya kusoma thredi moja kwenye jukwaa hili kuhusu ile kesi ya babu sea, sina uhakika lakini naona kama kesi yao ilikwenda haraka sana kulinganisha na hii, naomba mdau anayefahamu ile kesi ya wakina babu seya ilitumia muda gani atujuze, au hawa wakubwa wanapanga kulingana na matakwa yao?
   
 11. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Amen....!
   
 12. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Ni kweli wakati mwingine ukifuatilia fuatilia haya mambo hasa ya case za mauaji unapoteza muda na pengine hutafanikiwa. Ni vyema wakati mwingine kumwachia mungu pekee ambaye aliona kila kitu na walio muua ni viumbe vyake vile vile. Atahukumu hapa hapa duniani kama tutakuwa hai tutasikia tu......
  Poleni sana ndugu wa marehemu profesa
   
 13. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Sasa ndugu unataka tuchangie nini?, wajua kifo hiki kinasikitisha sana, wewe mtu wa karibu wa familia na kama memba wa JF tupe in black and white kile ambacho wanafamilia wanasema juu ya chanzo cha kifo cha prof, hii itasaidia kwa baadhi ya watanzania kuepuka vifo vya aina hii where possible. Pili tueleze ni kipi hasa kinachoendelea juu ya uendeshaji wa kesi ili members wazoefu watupe uzoefu wao bcos huenda mwenendo wa kesi niwa kawaida. Na mwisho tetesi za vijiweni zinasema kuwa prof aliponzwa na utashi wake wa kukataa uhuni na ubabaishaji ulioko kwenye uendeshaji wa mahakama ya ICTR hivyo Rais wa Rwanda akaona atakuwa amevuliwa nguo- akaamua kumu....................... Mwenye ukweki atujuze.
   
 14. b

  bongisa Member

  #14
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwakweli mwenyewe ni hivo juzi ndiyo nimesikia kuna watu walishakamatwa na wapo ndani, kesi inaendelea lakini ndio kwa mwendo wa kutajwa tu hivyo. Kuhusu chanzo cha kifo wanafamilia hawajui pia, sijaweza kufukunyua sana kutokana na mazingira ya tukio lenyewe lakini inaonyesha wazi kutofahamu ukweli wa nini kilichosababisha kwao kinawatatiza sana, na katika mazingira hayo hata kuwahoji inakuwa ngumu. Ndio maana nilikuwa naulizia mwenendo wa hiyo kesi je ni sawa? sababu kama kuna watuhumiwa na kama ni wenyewe basi ukweli upo mahakamani sasa kwanini uzidi kuahirishwa kila siku?
   
 15. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Huyo Prof si aliuwawa na system chini ya uratibu wa jk..unataka nani amshtaki nani?
   
 16. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 3,335
  Trophy Points: 280
  hebu elaborate fresh mkuu.
   
 17. b

  bongisa Member

  #17
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusihukumu tu jamani, labda kama una lolote la kutwambia, aliuwawa na system kwa uratibu wa jk kwa faida ya nani? Huyo jk ana maadui wangapi na wangapi amewaua kwa kutumia hiyo system? Kumbuka prof mwenyewe alikuwa na msaada mkubwa kwa serikali, je alikosana nini hasa na jk mpaka aamue kumhukumu umauti?
   
 18. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  R.I.P Jwani Mwaikusa, mashairi yako bado yanaendelea kusomwa.
   
 19. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  nyie munaongelea Mahakama!!!! Nani kakuambia kuna mhimili wa mahakama Tanzania? Zile ni kangaroo courts tu ambazo zinawalenga watu dhaifu na ambao hawana nafasi kwenye jamii. Profesa Juani Mwaikusa alikuwa eliminated na nguvu za Paul Kagame ambazo tumeona zikivuka mipaka ya Rwanda na kuwafuata watu huko huko waliko kama akina Generali Kayumba aliye nusurika kufa baada ya kupambana na paid assassins. Jiulize kwa nini Profesa mwingine wa USA alivyokataa kuja Kigali kumwakilisha mteja wake kwa kuogopa kupatwa na yaliyompata Profesa Mwaikusa. Fuata link hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-sheria-the-law-forum/123461-wakili-peter-erlinder-na-kifo-cha-prof-juani-mwaikusa.html
   
 20. b

  bongisa Member

  #20
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mdau, kuna uwezekano mtu mwenye umuhimu kwa serikali kama alivyokuwa prof mwaikusa akauwawa na serikali ya nchi jirani bila ya serikali yetu kupitia vyombo vyake vya usalama kupata fununu?
   
Loading...