MAUAJI ya Polisi; CHADEMA presses JK-one step to demonstrations | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAUAJI ya Polisi; CHADEMA presses JK-one step to demonstrations

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Oct 13, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI[/FONT]

  [FONT=&quot]Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa ufafanuzi kwa umma kwamba pamoja na kauli ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya kusudio la kuwasilisha ripoti tatu zilizotolewa kuhusu mauaji ya Mwanahabari Daudi Mwangosi kwenye Baraza Kivuli la Mawaziri kwa ajili ya hatua za kibunge kuchukuliwa na Kambi Rasmi ya Upinzani; CHADEMA kitaendelea kuchukua hatua zingine nje ya Bunge kwa kuzingatia maamuzi ya Kamati Kuu ya kutaka hatua kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Iwapo Rais kwa niaba ya Serikali hatazingatia, CHADEMA kiliamua kwamba kitachukua hatua ya ziada ya kuwaongoza wananchi kwa njia za kidemokrasia ikiwemo maandamano ya amani kushinikiza hatua za haraka kuchukuliwa kwa maslahi ya taifa.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Itakumbukwa kwamba tarehe 9 Septemba 2012 Kamati Kuu ya CHADEMA ilifanya kikao maalum cha kujadili hali ya siasa nchini kufuatia mfululizo wa mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika shughuli za kisiasa za CHADEMA na mipango ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya kudhibiti vuguvugu la mabadiliko (M4C) kwa mbinu haramu.

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Kamati Kuu ilizingatia masuala mbalimbali na kupitisha maazimio nane na kuamua kumuandikia barua Rais kwa lengo la kumtaka achukue hatua za utekelezaji kwa mujibu wa mamlaka yake na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, CHADEMA bado kinamtaka Rais Jakaya Kikwete kueleza hatua alizochukua na kujibu barua ya CHADEMA.

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Itakumbukwa kwamba baada ya kuwasilisha barua hiyo ya tarehe 10 Septemba 2012 iliyoandikwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe (Mb) ambayo pamoja na hatua nyingine CHADEMA ilitaka Rais achukue hatua ya kuwafukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Emmanuel Nchimbi, IGP Said Mwema, Kamanda Mkuu wa Operesheni Paul Chagonja, RPC wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shigolile, RPC wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda na Mkuu wa FFU Mkoa wa Morogoro, kwa kutowajibika kufuatia mauaji yaliyotokea mkoani Morogoro na Iringa; ikulu ilinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari ikieleza kuwa majibu yatatolewa baada ya Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani kutoa ripoti yake.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Rais Kikwete anapaswa kuchukua hatua kwa kuzingatia barua ya CHADEMA na kwa kurejea pia Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambayo imeeleza uvunjwaji wa haki za binadamu, ukiukaji wa sheria na uvunjaji wa misingi ya utawala bora uliofanywa na wahusika wakuu ambao tayari CHADEMA iliwataja kwenye barua yake kwa Rais na kutaka wafukuzwe kazi.[/FONT]

  [FONT=&quot]Hata hivyo, Rais Kikwete na umma uzingatie kuwa barua ya CHADEMA haikuhusu mauaji ya Mwangosi pekee bali mfululizo wa mauaji yaliyotokea katika mazingira ya kisiasa na pia ifahamike kwamba pamoja na Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kueleza uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukaji wa sheria na misingi ya utawala bora uliofanywa katika matukio ya Iringa; muktasari wa ripoti unaashiria tume haikufanya uchunguzi mpana wa mtandao mzima uliohusika kupanga operesheni haramu na kusababisha mauaji na kupendekeza hatua kali kwa wahusika wote ikiwemo za kisheria.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Hivyo, CHADEMA bado kinasubiri kauli ya Rais na majibu kuhusu barua ambayo pamoja na hatua zingine ilitaka aunde tume ya Kijaji/ Kimahakama ya uchunguzi wa vifo vilivyotokea katika mikusanyiko, mikutano, maandamano au mazingira ya kisiasa yaliyohusisha CHADEMA. Vifo hivi ni vile vilivyotokea Arusha (05/01/2011), Igunga (Novemba 2011), Arumeru Mashariki (Aprili 2012), Iramba (Julai 2012), Morogoro (27/08/2012) na Iringa (02/09/2012).

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Itakumbukwa kuwa katika maandamano yaliyoitishwa na CHADEMA tarehe 05/01/2012 watu watatu walipoteza maisha baada ya Jeshi la Polisi kutumia nguvu na risasi za moto kutawanya waandamanaji.[/FONT]
  [FONT=&quot]Katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga pamoja na matukio mengine yaliyojitokeza na yaliyohusisha vurugu kinyume cha Sheria, Ndugu Mbwana Masoud mwanachama wa CHADEMA aliteswa na kunyongwa katika mazingira ya kutatanisha. Mpaka sasa hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa kufanya uchunguzi kuhusu kifo hicho.

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mara baada ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, kiongozi wa Kata wa CHADEMA Ndugu Msafiri Mbwambo alichinjwa na chanzo chake kudaiwa kusababishwa na masuala ya kisiasa na hivi karibuni baadhi ya watuhumiwa wa mauaji hayo wametoroka

  kutoka wakiwa mikononi mwa polisi katika mazingira yenye kuashiria njama za kutoroshwa.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hivi karibuni yalitokea mauaji katika Kijiji cha Ndago, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida ambapo kikundi cha watu kilivamia mkutano wa CHADEMA kwa mawe Polisi wakiwepo bila kuchukua hatua na baada ya mkutano kumalizika na viongozi wa CHADEMA kuondoka eneo la mkutano kijana mmoja anayedaiwa kuwa kiongozi wa Kata wa UVCCM alikutwa katika kijiji hicho akiwa amepoteza maisha.

  Tayari taarifa za ziada zimeanza kujitokeza kuhusu maelezo ya baadhi ya vijana wa UVCCM kwamba tukio hilo lilipangwa na kigogo mmoja wa CCM (vyombo vya habari vilivyoandika habari hizo vimeeleza kuhifadhi jina lake kwa sasa) huku polisi wakishindwa kufanya uchunguzi huru na kuchukua hatua. [/FONT]

  [FONT=&quot]Hivi karibuni tena katika maandamano ya mapokezi ya viongozi wa CHADEMA Mkoani Morogoro Polisi walimshambulia Ndugu Ally Zona na kupoteza maisha, na baadae Polisi wakatoa taarifa kuwa aligongwa na kitu kizito.

  [/FONT][FONT=&quot]Mkoani Iringa wakati wa kufungua matawi ya Chama kwenye kata ya Nyololo, Polisi walimlipua kwa bomu Mwandishi wa Habari Ndugu Daudi Mwangosi. Pamoja na Polisi kuhusika na mauaji hayo bado Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP Said Mwema, Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja, RPC wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shigolile na RPC wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda hawakuchukua hatua yoyote ya kuwajibika kwa kuhusika moja kwa moja na matukio haya au kiutendaji katika Jeshi la Polisi kwa ujumla.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Mauaji yote haya hayajafanyiwa uchunguzi wowote wa Kimahakama/ Kijaji kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu kinyume na ahadi ya Waziri Mkuu Bungeni wakati akihitimisha hoja yake katika Bunge la Bajeti la mwaka 2011/2012. Hakuna uchunguzi wa kifo “inquest” uliofanyika na hakuna Mahakama ya korona “coroner’s court” iliyoanzishwa ili kuchunguza vifo hivi.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Irejewe kwamba kufuatia hali hiyo, Kamati Kuu ya CHADEMA ilifanya kikao maalumu siku ya Jumapili Tarehe 09 Septemba 2012 katika Hoteli ya Blue Pearl Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilijadili hali ya siasa nchini kufuatia mfululizo wa mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika shughuli za kisiasa za CHADEMA na mipango ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya kudhibiti vuguvugu la mabadiliko (M4C) kwa mbinu haramu. [/FONT]
  [FONT=&quot]
  Katika majadiliano ya kina kabla ya kufikia maazimio na maamuzi hayo, Kamati Kuu ilizingatia kuwa hali ya siasa nchini ni tete, Serikali inayoongozwa na CCM imeshindwa kusimamia vizuri rasilimali za nchi ikiwemo kudhibiti mfumuko na ongezeko la bei na kuchangia katika ugumu wa maisha kwa wananchi na migogoro ya kijamii na ufisadi nchini.

  Taifa limegubikwa na tuhuma za vyombo vya Serikali kutenda kinyume na haki za kikatiba na kutumiwa kudhibiti mabadiliko kwa njia haramu ikiwemo kuteka na kutesa (Mf. Tukio la Dr Ulimboka), kulifungia gazeti la Mwanahalisi na kufanya vurugu na mauaji katika shughuli halali za kisiasa za CHADEMA.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Pamoja na hali hiyo, Kamati Kuu iliazimia kuwa Operesheni ya M4C iendelee na kazi zake kwa kufuata kikamilifu ratiba iliyopitishwa na Baraza Kuu na Kamati Kuu katika vikao vya awali kiwa ni sehemu ya kutimiza dhima yake ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Imetolewa tarehe 12 Oktoba 2012 na:[/FONT]

  [FONT=&quot]
  John Mnyika (Mb)[/FONT]

  [FONT=&quot]Mkurugenzi wa Habari na Uenezi[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kaka makene, uoni lakini ktk hii kinachofanyika ni kuchukua kesi ya nyani na kumpelekea ngedere kwani mimi binafsi naamini hata hiyo kamati liyoundwa na nchimbi maagizo hayo yametoka kwa jk ili ajfiche nyuma ya kamati ya nchimbi kwani style ya uongozi wa jk inafahamika ya kutumia watu wengine kuficha udhaifu wake ili baadaye akiulizwa na wazungu au vyombo vya nje awe na mahala pa ku point kuwa kuna uchunguzi unafanyika huku hali akijua kuwa uchunguzi huo ni BOGUS kwahiyo naomba kujua kuwa kulikuwa na busara gani ktk kuamua hili huku mkijua wazi udhaifu wa jk???

  mifano hai ya style ya jk.
  1.Maamuzi ya Luhanjo ktk sakata la jairo, alimtanguliza jairo ambaye yuko ofisini mwake kumsafisha jairo halafu akamgeuka baadaye.
  2.swala la katiba alimtanguliza waziri wa katiba kutoa msimamo wa kupinga katiba alipoona hali mbaya akamgeuka na kukubali katiba.
  3.katika zoezi la kuvua gamba alitangaza zoezi hilo halafu wakina nape bila kufikiria usanii wa jk wakaingia kichwakichwa yeye akakaa mbali nao alipoona wahusika wamegoma akawaita na kutangaza wao ni marafiki wakubwa wamejuwana toka mbali wakina nape wakabakia kuwa maadui wa kina lowassa na wenzake.
  4. kwenye tume ya mwakyembe aliwatanguliza mbele wakafanya kazi yao kabla ya kuwageuka na kuwasimamisha wahusika kwy majukwaa
  huku akiwaita viongozi safi??
  jk ni kiongozi mmoja wa ajabu sana na inabidi ukubali mnafiki mkubwa kuweza kuelewana na jk hakuna mtu serious anaweza kufanya kazi na kiongozi mwenye style hii
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Itakuwaje akisema kuwa hatia yoyote itakuwa premature kwa vile kuna kesi mahakamani? Au akisema hawezi kulazimishwa kuchukua hatua yeyote? Au akikubali kuwa amewasikia na atachukua hatua mjda "muafaka ukifika"?
   
 4. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Na vipi CDM wangekaa kimya kabisa???
   
 5. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  There are only two ways to live your life. One is as though nothing is a miracle. The other is as though everything is a miracle.
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Then ni matumaini yetu kuwa hilo hapo chini litafuatia...
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  yeah nimesoma... kumbuka mauaji yalitokea Septemba 2, 2012 na leo ni Oktoba 12, 2012...
   
 8. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,802
  Trophy Points: 280
  Msimamo wowote atakao uchukua huyu dhaifu tofauti na kuwawaqjibisha wahusika wote kwa kuwafukuza kazi, wajibu wa CHADEMA ni kuishitaki serikali yake kwa wananchi kupitia M4C.kuendelea kuijulisha dunia ya wapenda haki juu uovu na ukandamizaji wa demokrasia unao fanywa na serikali ya kikwete.KWASASA CHADEMA IJIZUIE KUITOA MADARAKANI SERIKALI DHAIFU YA KIKWETE KWA MAANDAMANO KWANI KUNA KILA DALILI KUWA 2015 LAZIMA ITOKE KWA KURA.WANAINCHI WAMEDHAMIRIA TENA KWA DHATI YA MIOYO YAO.
   
 9. MLUGURU

  MLUGURU JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 818
  Likes Received: 386
  Trophy Points: 80
  mkuu,Rais wetu ni kiongozi ambaye hashauriki,akishaurika basi atekelezi,akitekeleza basi cvyo inavyotakiwa,hivyo nashauri cdm kuendelea na harakati za m4c kwani wananchi mikoani bado wananjaa ya kushibishwa sera mbarimbari kuhusu namna ya kuikomboa nchi na rasilimali zao.
  m4c ilivyosimama na viongozi mbalimbali wa chama tawala na serikari ndo wanapata usingizi.
  go m4c go for wana tz
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ila sasa tunakwenda patamu. Ole ole ole. Hakuna mungu mtu. Viongozi rudisheni mioyo yenu kwa wananchi wenu, cheo ni dhamana. Wachukulieni hatua hao waliowatuma maborisi kutumiwa. Nahisi hata hawa maborisi ni kondoo wa kafara, kuna waliojificha nyuma yao. TISS mkooooo.

  Hivi kwanini borisi wasitumie gazeti la mwanahalisi kama chombo cha upelelezi?
   
 11. p

  propagandist Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema si walikuwa hawamtambui kikwete? vipi leo mnapiga magoti mbele ya kikwete nanyi mlisema hatamaliza miaka 5? CHADEMA WAMEISHA TIWA KIDOLE CHA ******, wamechemsha mapema namna hii.
   
 12. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kheri ya aliyekuwa malaria Sugu kuliko wewe ambaye unajidhalilisha kupindukia!!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  CHADEMA wameshasema wataongoza maandamano ya amani. Nafikiri cha mhimu katika taarifa hii ambacho naona kimekosekana ni timeframe ya maamuzi wanayotaka Rais ayafanye. Maana anaweza kuyafanya mwaka 2015. Bado atakuwa ametekeleza walichomtaka afanye.
   
 14. WamLola

  WamLola JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 346
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  ni ajabu kwamba hata kabla ya tume kutoa majibu ya mauaji picha za mauaji yalivyotokea zinaonekana ila ajabu mh nchimbi anawaambia watanzania askari hawajahusikahv kweli kwa mtindo huu tutaendelea kweli manake hata mtoto mdogo ukimueleza majibu aliyoyatoa waziri na kamati yake atakasirika sana manake ni ya uongo!!!!!!!real our leaders is very ignorant na hata huu udokta wa nchimbi sijui kautoa wapi:spy:
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Matamko ya Chadema yamekuwa kama mchezo wa kuingiza kila mtu anakuja na tamko lake, Chadema kila siku wanasema hawamtambui rais Kikwete leo tena wanamuomba.

  Mnyika kila siku anasema rais Kikwete ni dhaifu leo tena unamuomba awafukuze kazi mawaziri ni kichekesho.

  Chadema kama kweli nyie mnakubalika kwa wananchi itisheni maandamano nchi nzima sio kutoa matamko ambayo hayana tija.
   
 16. N

  NAMI Member

  #16
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sura yako mbaya sana halafu unafikiri kwa kutumia nini?
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,626
  Likes Received: 4,728
  Trophy Points: 280
  Ritz ukiacha unafiki na kusema ukweli JK siyo dhaifu?
   
Loading...